Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,092
- 43,265
Mwandishi wa Mithali inasema hivi: Haki huinua taifa, bali dhambi ni aibu ya watu wote (14:34). Msemo huu ukiuangalia kwa haraka unaweza kukosa kuelewa una maana gani. Ila ukiangalia kwa karibu unaweza kuona ni kwanini "haki huinua taifa". Nimeandika hivi majuzi nikiendeleza tafakari iliyofanywa na wengine juu ya uhusiano kati ya 'amani na haki'.
Mahali penye malalamiko ya dhulma basi hakuna haki. Ukiwasikiliza sana Watanzania unaweza kuona wengi wanalalamikia kukosa haki siyo kukosa amani. Ukitaka kujua ni kwa kiasi gani dhulma imetawala nenda mahabusu au gerezani. Unaweza kukutana na watu wana visa wakikusimulia unaweza kuona ni jinsi gani tunawatu ambao wamedhulumiwa haki zao mbalimbali kwa sababu tu ama hawakuwa na uwezo wa kuhonga (dhulma ya rushwa) au hawakua na uwezo wa kujitetea vizuri.
Hapa Marekani kuanzia mwaka 1989 zaidi ya wafungwa 3700 wameachiliwa baada ya ushahidi kuonesha kuwa hawakuwa na hatia ya makosa yaliyowatia vifungoni. Miongoni mwao wapo waliokuwa wanasubiria hukumu ya kunyongwa au wanatumia vifungo vya maisha. Ushahidi wa vinasaba (DNA) na ushahidi mwingine umeweza kutumika kuwatetea wafungwa hao na kuonesha kuwa hawakuwa na hatia ya makosa ambayo walituhumiwa nayo.
Sasa kama taifa kama Marekani lina watu zaidi ya 3500 waliofungwa na wengine kutumikia miaka mingi kabla ya kuachiliwa kwenye Taifa kama la Tanzania hii namba inaweza kuwa ngapi. Kwenye sehemu ambayo ushahidi wa DNA hautumiki sana kuthibitisha hatia inawezekana tuna watu kwenye magereza yetu ambao wamekuwa wakilia usiku na mchana kuwa "wamebambikiwa kesi" yawezekana ni kweli? Je, katika mazingira haya "haki" hasa ni nini?
Leo hii ukitaka kujua haki inavyokosekana rejea sana matukio ya Oktoba 29 ambao tuliona watu wanachapwa kama watoto wadogo, wanatendewa kama watumwa kwenye taifa lao kwa kisingizio cha "amani". Je, watu hawa wote waliopigwa au kutendewa udhalimu wana "haki" yoyote? Ni kwa sababu hiyo ni lazima tujiulize kama taifa tunaweza vipi kufanikiwa na kuinuka bila kuweka "haki" kama msingi wa taifa letu. Ukisoma kwenye Katiba yetu ya sasa unaweza kuona kwenye eneo la "haki za msingi" au tunachokiita "Bills of Rights" mojawapo ya haki inayotajwa kwa msingi kabisa ni kuwa "Kila mtu (haisemi kila mwana CCM) ana haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake". Je, wale wote waliouawa (wanoitwa "wapendwa wetu" na Samia) wametambuliwa na kuthaminiwa utu wao kwa namna yoyote ile? Kama tunashindwa hata kuchunguza na kuwawajibisha waliohusika na mauaji yale tunaweza vipi kudai tuna taifa la haki?
Watawala wanaweza kutumia nguvu na mabavu kutawala lakini kinachoinua taifa lolote ni haki. Tunakoenda sasa hasa kwenye mwaka huu mpya madai yetu makubwa ni kutamalaki kwa haki katika taifa letu. Tutadai haki hizo kama mmoja mmoja na kwa pamoja. Tutafanya makosa makubwa sana na vizazi vijavyo havitatusamehe kama tutauza haki zao kwa kisingizio cha kuishi kwa amani. Hakuna mbadala wa haki; na bila haki hakuna amani ya kweli. Kunaweza kuwa na utulivu, kunaweza kusiwe na vurugu, lakini bila haki (kutokuwepo kwa dhulma na udhalimu) basi amani ya kweli haiwezekani.
Kheri ya Mwaka Mpya 2026 Mwaka wa Haki na Amani Kubusiana (Zab 85:11).