Haka karafiki kangu kataniletea matatizo soon....!!!!!

Haka karafiki kangu kataniletea matatizo soon....!!!!!

Eiyer anahitaji Mchumba fake amsaidie kumtimua Mama King'ang'anizi.
Sasa nikakukumbuka wewe Rafiki kama mmoja wa watu Makini wanaoiweza hii kazi.


Huoni kuwa huyu Jamaa ako vere Msweet mpaka tutoto tudogo tunafolu kwake?
TANMO ningeweza kumsaidia kabisaa..kut vikwazo viwili vitasumbua. Moja distance hatuishi mji mmoja so it is a prolem. Mbili hata nikisakrifaisi nikaenda aliko afu niakifekisha, then nikamind alivo msweet km ulivyosema hapo juu, afu nikanogewa na mimi si nitakuwa king'ang'anizi.
Naogopa kuwa mtuhumiwa namba mbili katika kesi hii lol
 
Last edited by a moderator:
Nikae mabli na rafiki yangu au mama ake?

huyo mama take! namwona ana genye zake na unavyozidi kuchelewa na yeye anajenga chuki. siku ya siku anakuitia polisi unakatekenya katoto shauri yako
 
TANMO ningeweza kumsaidia kabisaa..kut vikwazo viwili vitasumbua. Moja distance hatuishi mji mmoja so it is a prolem. Mbili hata nikisakrifaisi nikaenda aliko afu niakifekisha, then nikamind alivo msweet km ulivyosema hapo juu, afu nikanogewa na mimi si nitakuwa king'ang'anizi.
Naogopa kuwa mtuhumiwa namba mbili katika kesi hii lol

Hahahahaa
Rafiki umenifanya nicheke Bana.
Ila Kikwazo cha nauli tutakisovu, tutaitisha Donee kwa Friends of Eiyer..
Usiogope kuwa king'ang'anizi, manake hata yeye anahaha sana kumpata wa ukwee kama wewe.
 
Last edited by a moderator:
We huoni anavyobabaika?
Au hujapitia ule uzi wanapoelezea sifa za mwanaume aliyefolu halafu anashindwa kusema?

Ha ha ha haaa, kwa hiyo Eiyer kafall kwa nani tumsaidie kusema?
 
Last edited by a moderator:
Eiyer anahitaji Mchumba fake amsaidie kumtimua Mama King'ang'anizi.
Sasa nikakukumbuka wewe Rafiki kama mmoja wa watu Makini wanaoiweza hii kazi.


Huoni kuwa huyu Jamaa ako vere Msweet mpaka tutoto tudogo tunafolu kwake?

ndio ako msweet lakini mie nko occupied bana, huo ufake stauweza mie, habby wangu mkali kama pilipili
 
Vijana wa JF nawaasa sana na nnawaomba mjifanyie ka research chenu kadogo nyinyi wenyewe kwa watu kama huyu anaependa kucheza na watoto, watu kama hawa ni hatari sana kwa jamii.

Tulioishi na kulea watoto zetu nje ya Tanzania tunaelewa haya mambo kwani hupata darsa mara kwa mara za "child abusers" na "pedophiles". Najuwa kliniki za Tanzania huhusisha afya ya mama na mtoto lakini kliniki za nje huhusisha pia namna ya kuhami mtoto na majanga ya ma "pedophiles".

Huyu mtu anaejiita "Eiyer" kwa maandiko yake, ameonesha "symptoms" zote za hayo matatizo na nimewawekea link mjisomee wenyewe.

nimesoma link uliyoiweka na pia nimesoma maelezo yako yote humu ndani

nachoona hapa unachosisitiza ni kuwa wakutakiwi kuwa na mazoea kati

ya mkubwa na mtoto(yani hakuna urafiki kati ya watu hawa yani mtoto

na watoto wenzake na mkubwa na wakubwa wenzake) si ndio
 
Hakuna mtu asiyependa watoto lakini kuna mipaka ya urafiki wa mtoto na mtu mzima, kumbuka hilo.

Watoto zangu mimi niliwatenga sana na watu wanaojidai kupenda sana watoto, na hiyo ni kwa mafundisho kabisa ya namna ya kulea watoto vyema. Sioni hoja wala haja ya jirani kujifanya anampenda sana mwanangu kuliko mimi niliyemzaa.

kikubwa ninachokiona hapa ni utofauti wa kimazingira ...

wewe unazungumzia mazingira ya jumba kubwa wafanyakazi

watatu watatu...mtoto anaanza kwenda shule kuanzia day care

na tuition toka yuko miaka mitatu lakini sisi tunazungumzia maisha

ya watanzania wengi ambayo huwezi kumtenganisha mwanao na jamii

kwani uko uswahilii chumba kimoja au chumba nasebule, msaidizi wa kazi huna

unafikir hapo nani atakayekulelea mwanao kama sio jamii, na hapo


nb: sisime watu wanaowaabuse watoto hawapo na wala siwatetea hao watu na ila napinga kauli yako yakusema eti hakuna urafiki kati ya mkubwa namtoto , wakati mimi nimekulia katika mazingira rafiki zangu wote ni wakubwa ...hivi unajua nikiwa na miaka kumi na sita nilikuwa na rafiki wa miaka 43, achana na na huyu ila rafiki zangu wote ni wakubwa
 
Aisee, we endelea kupenda penda watoto siku hizi watu hawaaminiki unaweza kupewa kesi hiyo hadi ukachanganyikiwa. Mimi pia napenda watoto tena sana tu lakini mazoea yangu yanaishia nje tu tena na mzazi wake akiwepo au kukiwa na kundi la watoto wengi. Lakini sio eti nikae na mtoto wa mtu tukiwa wawili tu eti tunapiga stori!!! Hiyo haipo sio kwa kuwa sijiamini ila siku hizi mambo yamebadilika sana kwa hiyo nafanya hivyo kuepusha matatizo tu.

Kumbuka pia japokuwa watu wanaopenda watoto kwa dhamira safi wapo lakini kuna wengine wengi tu wana dhamira mbovu. Na mbaya zaidi haya mambo yanatokea kwenye jamii zetu. Kwa mfano mimi nakumbuka kuna kipindi tulikuwa tumechangia chumba na jamaa zangu tulipokuwa wanafunzi. Sasa bwana kwenye hiyo nyumba kulikuwa na jamaa mwingine aliyekuwa "single" na hatukuwahi kumwona akija na mwanamke yeyote. Pia huyu jamaa alikuwa mtaratibu sana. Zaidi ya huyo kulikuwa na dada mwingine nesi ambaye kwa kweli alikuwa anavutia sana. Huyu dada yeye alikuwa na katoto ka kike kazuri sana ambako kalikuwa na miaka kama 6 hivi kipindi hicho, kwa hiyo wao walikuwa wanaishi wawili, yeye na katoto kake.

Sasa yule jamaa single alikuwa na mazoea sana na kale katoto ka nesi, yaani walikuwa marafiki wazuri na mara nyingi jamaa alikuwa anakapa vizawadi vya hapa na pale. Pia kuna wakati kalikuwa kanaingia kwenye chumba cha jamaa kanashinda huko. Sisi kipindi hicho tulikuwa bize na shule, saa nyingine kutokana na tamaa zetu za ujana tulikuwa tunamtamani nesi (kiukweli karibia kila mwanaume pale mtaani alikuwa anamtamani nesi). Kwa hiyo akili yetu ilikuwa kwa nesi, sema na yeye alikuwa mgumu kweli hadi tukawa tunajiuliza ilikuwa kuwaje akaachia hadi akazaa!!! Tuachane hilo turudi kwenye urafiki wa katoto na jamaa single, Kumbe bwana yule jamaa ana yake kichwani. Kuna siku tumekaa hatuna ili wala lile kale katoto kakatoka kwenye chumba cha jamaa kanalia, halafu kakakimbilia kwa mama yake. Mama kutaka kujua kulikoni si ndio kakamuonesha huko chini kanavuja damu. Halafu sasa kakawa kanahadithia jinsi jamaa alivyokuwa na tabia ya kukaingiza vidole huko chini na kukapa vipipi ili kasiseme. Kilichofuata ni polisi, na yule dada akawa haamini mtu yeyote katika sisi vijana japokuwa sisi hatuwa na muda na katoto kake. Sijui ile kesi iliishaje, ila utaona kuwa kwa mtu makini, kwa aina ya maisha tunayoishi leo hawezi kuamini mtoto wake wa kike awe na urafiki na mwanaume mtu mzima anayeishi kama mtawa. Ni ngumu sana.

Kwa hiyo mkuu pamoja na kuwa dhamira yako inaweza kuwa njema kabisa, usipende sana hiyo tabia. Inaweza kuja kukugharimu hadi ukashangaa!!
 
Umeshindwa kujibu maswali yangu rahisi tena ya lugha yako mwenyewe unadhani kuna atakaedhania umeelewa hata hiki ulicho kikopi na kepesti hapa??

Mradi wewe umeelewa inatosha kabisa. Nakuasa tena, wacha hiyo tabia, itakupeleka pabaya.
 
Back
Top Bottom