Kwenu Wabobezi wa Marketing hivi Kupunguza Bei ya Bidhaa ili Uuze nyingi na Utambe kwa Watu ndiyo Mafanikio Kibiashara au Mafanikio zaidi ni Kuuza kwa Bei ya Juu hata kama utauza Chache ile utaingiza Pesa nyingi na pia Utakubalika kwa Ubora ( Quality ) ya bidhaa?
Leo Klabu ya Yanga imeamua Kushusha Bei ya Jezi zake kutoka Tsh 35,000/ mpaka Tsh 30,000/ hali ambayo imetushtua zaidi Great Thinkers wachache tuliobakia sasa Ulimwenguni.
Je, Uongozi wa Yanga SC umeamua haraka sana Kuishusha hiyo Bei ili zinunulike nyingi na waweze Kumlinda Msemaji wao Haji Manara hasa baada ya Wiki Mbili nyuma kusikka akisema kuwa Yanga SC ndiyo Klabu pekee iliyouza Jezi nyingi Afrika Mashariki na Kati?
Shukran nyingi na za dhati kabisa ziende kwa Uongozi wa Simba SC na Mbunifu wa Jezi za Simba SC Fred Nganjiro ( Fred Vunjabei ) kwa Kusimama na Bei ile ile ya Jezi za Simba SC zinazouzwa Tsh 40,000/ na ambazo zimeuzika nyingi na zinaendelea tu Kuuzika huku kila Siku tu zikitolewa za Muundo mpya na anbazo zinapendeza vile vile Mwilini ukivaa ( ukizivaa )
Hivi Mashabiki wa Mpira wenye Akili zao Timamu kabisa waache Kununua Jezi za Klabu ambayo sasa ndiyo Balozi wa Watanzania, wa Rais Samia na wana Afrika Mashariki kisha wanunue Jezi za Timu ambayo haishiriki Mashindano yoyote ya Kimataifa na Kutwa tu inapishana na Malori ya Mkaa, Mafuta na Takataka katika barabara za Vumbi tupu na Milima mingi huko Mikese, Mdaula, Ubena Zomoni, Turiani na Msamvu.