Hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba ya Uchimbaji wa Makaa ya Mawe Yaliyopo Ludewa Njombe Kati ya Wawekezaji wa Ndani na Shirika la Taifa la Maendeleo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
944
Serikali imeyataka Makampuni ya Wawekezaji Wazawa ambao wamesaini mikataba ya uchimbaji wa makaa ya mawe Mchuchuma kufanya biashara kwa uadilifu, weledi kwa juhudi ili kifikia malengo yanayo kusudiwa, kuongeza ajira na pato la Taifa hususani dola za Marekani.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji Septemba 12, 2023 wakati wa hafla ya utiaji Saini wa Mikataba ya uchimbaji wa makaa ya mawe yaliyopo Ludewa mkoani Njombe kati ya wawekezaji wa ndani na Shirika la Taifa la Maendeleo, ambapo amesema baada ya miezi sita wawekezaji ambao hawajaanza kufanya shughuli za uchimbaji watanyang'anywa leseni .

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Ligano Wilson amesema uchimbaji wa makaa hayo ya mawe yatawezesha upatikanaji wa nishati muhimu na ya uhakika kwa uendeshaji wa viwanda nchini na maendeleo ya sekta hiyo kwa ujumla.

Naye Kamishina wa Madini na Mkumbe wa Bodi ya NDC Dkt. Abdulrahman Mwanga amesema mradi huo utaenda kuzalisha makaa ya mawe tani 30,000 kwa mwezi, huku wawekezaji hao wakisema watafanya kazi kwa muda uliopangwa ili kifikia malengo yaliyokusudiwa katika mradi huo.

Naye Mkurugenzi Mwendeshaji wa NDC Dkt Nicolaus Shombe amesema Makampuni ya wawekezaji wazawa matano yamesaini mikataba hiyo na kukabidhiwa leseni ya uchimbaji na NDC ambayo ni Kindaini Company Limited, Chusa Mining Company Limited, Sheby Mix Investment Limited, Nipo Engineering Company Limited na Cleveland Mine and Service Company Limited.

WhatsApp Image 2023-09-13 at 19.00.20.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-13 at 19.00.20(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-13 at 19.00.20(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-13 at 19.00.21.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-13 at 19.00.21(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-13 at 19.00.22.jpeg
 
Hii habari ya makaa ya mawe mchuchuma imenisisimua sana hasa pale uchimbaji ukifanyika kweli na watu wa ludewa kupata fursa mbalimbali za kiuchumi. Kongole kwa serikali yetu.
 
Hii habari ya makaa ya mawe mchuchuma imenisisimua sana hasa pale uchimbaji ukifanyika kweli na watu wa ludewa kupata fursa mbalimbali za kiuchumi. Kongole kwa serikali yetu.
Hello mwenyewe nimeliona nawaza pia kwenda huko.
 
Back
Top Bottom