Utiaji Saini Mikataba ya Miradi ya Maji Mkoa wa Dodoma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,906
945

WAZIRI DKT. ASHATU KIJAJI ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA YA MIRADI YA MAJI KWA HALMASHAURI ZA MKOA WA DODOMA

Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara (Mb) Mh Dkt Ashatu Kijaji tarehe 12 Juni, 2023 alishuhudia tukio la utiaji saini Mikataba ya Miradi ya Maji katika Mkoa wa Dodoma.

Tukio hili la utiaji saini limefanyika Kimkoa katika Kata ya Salanka Wilayani Kondoa huku Miradi hiyo ikijumuisha Halmashauri za Kondoa DC, Bahi, Kondoa Mji, Dodoma Jiji na Chamwino.

Kadhalika Miradi yote ina thamani ya jumla ya Shilingi Bilioni 5.98.
Akiongea na Wananchi wa Salanka waliojitokeza katika hafla hiyo Mh Dkt Kijaji aliwaasa Wakandarasi waliopatikana kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi ili thamani ya fedha iliyotolewa ionekane na Wananchi waondokane na adha ya upatikanaji wa Maji.

"Wakandarasi watumieni Vijana wa Maeneo ilipo miradi hii ili kuinua vipato vya Wananchi kwani wapo Vijana wenye Taaluma na wanaweza kufanya baadhi ya kazi katika Miradi hii ya Maji" Aliongeza Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.

Pia Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alisisitiza kuwa Mh Rais anafanya kazi kubwa sana ya kutafuta fedha hivyo ni jukumu la kila mmoja kuilinda na kuisimamia Miradi hii ili ilete tija iliyokusudiwa.

Hata hivyo Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji aliwaasa Wananchi kuwa makini na Wanasiasa wenye nia ovu na Taifa letu na kusisitiza kuendelea kumuombea Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili aendelee kuchapa kazi na hatimae nchi yetu ipige hatua zaidi za kimaendeleo.

Idara ya Habari na Mawasiliano kwa Umma
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Kondoa

WhatsApp Image 2023-06-14 at 10.42.56.jpeg
WhatsApp Image 2023-06-14 at 10.42.56(1).jpeg
 
Back
Top Bottom