Hadithi ya kweli ya maisha yangu

Hadithi ya kweli ya maisha yangu

Mafanikio mema kaka tunashukuru kwa kutushirikisha mikasa uliyopitia katika maisha yako mengi ya kujifunza mazuri,hatuishi kuwa bora ila tunakuwa bora kwa kuyaona yale tuliyopitia yapo kwa ajili ya kutujenga. Cha mwisho si kila mtu anaweza kuthubutu kama wewe kuwa muwazi. Ni kwa neema tu mkuu Mungu aliyokujalia na kutumika kuwa baraka kuokoa wengine.
Nashukuru sana mkuu tuzid kuombeana tutende mema.
 
Asante Sana mkuu holy holm kwa kuhadithia Mikasa na matukio ya maisha yako.
Nimefurahi Sana kuisoma story. Ila daah bado najiuliza hivi kumbe kwenye makambi ya kiroho Kuna wengine mnatongozana na mnanyanduana fresh!!
Sana tu, watu wananyanduana fresh tu maana si unakuta tupo maporini huko ko kunyaduana sio shida.

Ila me cjawai kufanya hicho kitu
 
Inaendelea


Nawashukuru sana tena wale tuliyokua pamoja kwenye huu uzi.Nilikua nasita sana kuelezea haya maisha yangu, asanteni kwa mlio nitia moyo Pm na hata hapa kwenye comment, bila kuwasahau wale mlio nivunja moyo pm na hapa ila chakuwaambia ni kuwa MAISHA NI HAYA HAYA.


Wazazi na ndugu zangu licha ya kuwaaibisha lakini bado huwaambii kitu kuhusu mimi ( wananipenda), kuna watu nilikua siwapendi yani siwapendi bila wao kujua kama siwapendi.Hicho kitendo kilikua kinasabisha nawachukia na nikikuchukua lazma nikulie njama yoyote ile, mfano mwalimu wangu wa piano enzi hizo nilikua simpendi nikimuona anavyoimba na jinsi watu wanavyopenda kipaji chake nilikuwa nachukia mpk cku moja nilimchomesha kwa muhuni wangu ( saiv ni marehemu ) akamteka simu mbili kali.

Mwingine nae ni jamaa fulani hivi sahiv ni jamaa wa faida kwangu kabisa nae nilikua cmpendi sema huyu ckumfanyia baya lolote.Nakumbuka cku nimeongea nae cku hyo hyo tukawa marafiki wakubwa sana.Tena huyu bila hiyana alinipa Xbox yake aliyopewa na Mama yake kutoka Uingereza, Alinipa bure kabisa bila hiyana na ninayo mpk saiv ila ni mbovu.

Nilisha nusulika kifo kwenye ajali ya pikipiki niliipata pale kona ya baruti, nilikua mwenyewe kwakweli Mungu mkubwa sana na alikua ananipenda sana.


Yule rafiki tuliye kuwa tunateka nae watu simu, mwaka 2012 yeye saivi ni marehemu.Alikufa mwaka 2014 kwa ajali ya pikipiki, walikufa wawili yeye na swahiba wake, nasikia walikua wametoka kupiga tukio sasa speed waliyokua nayo ilikua kubwa sana, pikipiki iligongana na land kruza, japo cjui nitakufaje lakin jamaa angu alikufa vby sana.


Mwaka jana kipind najiandaa kwenda Arusha niimpoteza tena rafiki angu kwa ajali ya pikipiki, cku hyo ilikua jumapili majira ya saa tano alikuja ofisin kwangu ( Ps ), alikua yupo yeye na rafiki zake wawili.Walicheza ps mpk kwenye saa kumi jioni wakasepa.Neno lake la mwisho alinambia "Hakikisha tunaonana leo usiku we fala" akimaanisha kuwa usiku huo tuwe wote kwenye happy birthday ya mdada mmoja hivi ilikua inafanyika palm Beach ( jirani na bwalo la police ).

Hiyo usiku ckuonana nae maana nilikua busy tu na mambo yangu.Kesho yake asubui tu naingia whatsapp naona kawekwa status kuwa kafariki.Niliumia sana yani ila ndo ivo mipango ya Mungu.Alipata ajali pale jirani benki ya crdb majira ya usiku saa saba akiwa anatoka kwenye hyo sherehe.


Mambo ni mengi sana yani kuyaweka yote itabidi tena nianze kusimulia na huku nilishaaga.Mungu mkubwa sana niseme ananipenda maana hebu fikiria kwa hayo yote aliyonitendea bado niko vizuri kiafya na hata kiuchumi (najimudu na nina mmudu Qilah wangu ) ingawa pia wazazi wananivusha nikikwama.

Tutende mema ili tuishi vizur bila hofu yoyote ila sometimes kuwa mgumu kidogo pale unapoona inatakiwa kuwa hivyo.Usipende kuwa dhaifu tu muda wote.Kama kuna Konda mmoja siyo konda msafi ni hawa makonda wa hiace za kwenda Tarime kutoka musoma.

Ni mwaka huu tu nilikua naenda kijiji fulani hivi kiko karbu na kinesi ( kuruya ) sasa nauli ni 3000 na tulikubaliana na huyo konda kuwa ni hyo bei sasa alikuja kunigeuka kipindi anakusanya nauli, nilimpa hyo buku tatu akadai nauli ni buku nne.Nilimwambia vizur toka saa ngap nauli imepanda. tulibisha sana mpk tulipofika pale darajani kinesi kwenye ile check point konda alimwambia dereva akasimamisha gar alafu konda akanichomesha kwa wale maafande kuwa cna nauli alafu naleta fujo.

Nilikua mpole nikamuanyesha afande mmoja nauli yangu na nikakubali kumlipa konda hyo buku nne.Sasa tulivyofika hapo kuruya gari lilpaki pembeni nikampa nauli konda, kwa vile nilikua na kamzigo kalikua kwenye buti nilimwambia konda anitolee.Napo alivyotoa ule mzigo akadai niulipie tena Buku, nilimwambia nishaulipia maana nauli ni 3k ko hyo 4k niliyompa buku ni ya mzigo.

Konda alinitukana akafu kwa sauti mpk abiria wakawa wanackia pamoja na bodaboda waliyokua hapo pembeni mwa barabara.Neno lililo nikera ni alivyonambia "Unafikiri hili gari ni la baba yako mpk utupangie nauli" nilimpiga konda ngumi ya mdomo akakasirika zaidi tena nikampiga ngumi yenyewe ya pua mpk damu zilimtoka.Dereva alimpa lichuma flani lilikua ndani ya ile gari eti anipige nalo.Nilikimbia kuelekea kule Center na uzuri ni kwamba huyo konda aliangua chini alivyokua akinifukuza, nilivyoona kaangu niliokota likuni nilimpiga nalo mgongoni.nilivyoona nimempiga kisawa sawa nilichukua mzigo wangu nikadandia boda huyo nikasepa.Dereva hakuamini kama nimeondoka maana alijarbu kunikimbiza lakin holaa.


Huyo konda aliyataka mwenyewe na kiukweli cjutii kabisa kumpiga hata cku nikionana nae akitaka ngumi tutazipga tu.


Saivi Holy ni mtu safie kabisa tena mcheshi mpenda masihara. Tena leo baada ya cku nyingi kutokwenda kanisani nimejumuika na wenzangu na tena nimeimba japo nilianza kusahau baadhi ya note.

Biashara ndo inaniweka mjini na kupiga beat ndo kunaniondolea stress kama nikiwa nazo bila kuwa sahau Ndugu zangu, rafiki zangu wa faida bila kumsahau Mama la Mama Qilah nampenda sana.


mcute tu fanya urudi Musoma unipe visa vyako ulivyonisimulia tukiwa sehemu yoyte nzuri

Asanteni sana najihisi sina Deni kabisa ikiwa kuna mtu anaswali akiniuliza nitamjibu hapa au Pm.



Mwisho

Hatari sana...
Chapter closed...
 
Uzi wako una mafunzo makubwa mno...pole kwa changamoto zote lakini nikupongeze kwa kubadirika...mshike Mungu sana maana kwa matukio hayo,hakika amehifadhi na kulinda uhai wako mno.
 
Uzi wako una mafunzo makubwa mno...pole kwa changamoto zote lakini nikupongeze kwa kubadirika...mshike Mungu sana maana kwa matukio hayo,hakika amehifadhi na kulinda uhai wako mno.
Umenibariki kwa hii komenti
 
Inaendelea

Kuna kipindi maisha yanakua matamu sana yani furaha kama yote na kuna kipindi maisha hua hayana maana kabisa yani unataman mpaka kufa.

Qilah wangu niseme alikuja kibahati sana ( accidentally ) sikua na mawazo kabisa kama nitakuja kuishi nae cku moja.

Mwaka huu mwezi wa 1 alipata msiba kwao huko Arusha ilikua ni must aende me nilisema siendi nae.Nilijua kabisa harudi tena bush kwetu.

Kwa jinsi alivyo afananii kabisa na wa kukaa bush, alikaa wiki mbili tu nikashangaa mtoto huyo karud tena aliniletea viraba flan hivi vikali sema tu vilinipwaya .

Wale wadem zangu wa nyuma ckua nimewaacha kwa kuwaambia tofauti na yule mywangu ndo nilimtema kwa kumwambia.

Mwezi wa kwanza huo huo kipindi qilah alikua msibani Lizy alinitafuta cku hyo akaanza mambo yake sasa kulalamika kuwa nimemtenga wala cmjali kihisia wala kimaendeleo.

Sikua na lamaana sana la kumwambia zaid tu ya kumdanganya.Kuna cku alinitumia text ndefu ya malalamiko ya kutosha akaniuliza kama nipo musoma tuonane nae.Nilimpotezea tu maana me na wadangaji saiv nawakwepa.

Siku moja Qilah alikua kasharud bush sasa cku hyo nilienda bush kuwaona.Niliugua tena yani nilikua natetemeka hatar.Niliamua kwenda zahanati, qilah alinisindikiza.Sasa tumefika Zahanati kulikua na watu wengi sana.So foleni ilihusika niliamua me kukaa chini ya mti ulikua hapo kando ya zahanati.

Qilah yeye alikua mapokez anachukua kadi, alivyorud kwangu alinambia nimuelekeze dukani.Me mwenyewe ckua najua maduka maana bush nilikua sio mwenyeji kabisa.

Alielekezwa na Mmama mmoja hivi, maduka yalikua mbali kidogo.Alipanda boda kwenda kununua daftari ( ilikua ni lazima uwe na daftar ili utibiwe ).kipindi amesepa nilikua tu nimekaa nimeegemea mti najiskia vibaya.Niliamua kutoa simu yngu mfukoni nikaanza kupiga piano.

Yalikua ni mazoea yangu kupiga piano kwenye simu sasa wakat napiga piano kuna jamaa mmoja ni Msimbiti.Alivutiwa na nilivyokua napiga ko alikuja akakaa karbu yangu, sasa alikua yuko so interested na mimi navyopiga piano.

Japokua nilikua naumwa niliamua kuzidisha manjonjo ( nikiona mtu yupo interest na ninachokifnya basi hua najiskia raha )....nili muoshea sana, yaan nilitoa piano nikaweka App ya ORG 21 nikaanza kupiga beat.Jamaa uzalendo ulimshinda akaamua kunisemesha.


Alianza na yeye kujisifia, wakat anaendelea kujisifia Qilah wangu alikua kasharud na daftar, sasa na yeye alikua ana msikiliza huyo msimbiti na sifa zake.Msimbiti aliongea wee mwishoe akaniuliza atapata wapi mtu amtengenezee beat, maana yeye ni mwimbaji wa nyimbo za asili.

Nilimwambia mbn me ni producer ( nilimwambia huku namuangalia qilah wangu usoni )..msimbit alinambia kuwa wimbo mmoja narekodia shngp.Nilimwambia kwani we hua unarekodia shngp,akasema ndo anataka kuanza muziki.

Nilimwambia hutaweza muziki bora heka yako ufanye mambo mengine.Nilimwambia aimbe kidogo tumsikie, alivyoimba qilah ni mjinga alishindwa kujizuia alicheka mpaka na mimi nilicheka japo nilikua naumwa .

Nilimwambia kurekod ina bei yake na kupiga beat kuna bei zake, nilimwambia me natengeneza beats tu kurekod labda jamaa angu mmoja ndo atamaliza show.Nilimwambia beat ni 100k ila yeye kwa vile kaonyesha nia nitamfanyia 70k tu.Hata hakubisha lakin alinambia hana pesa kwa muda ule, ko akadai nimpe no zangu aje kunitafuta.Nilimpa afu tukaendelea na story nyingine ila yeye ndo alikua muongeaji mkuu akitupa story za madisko ya usimbitini.


Saa nane mchana ilifika ndo tukapata huduma pake zahanati.Niliingia chumba cha daktar na qilah, Dokta aliniuliza kama itakua ni vyema Qilah aendelee kubaki ama atoke nje ili dotka aniulize maswali yake.Nilimwambia ata akiwepo ni frsh tu haina shida maana ni mtu wangu wa karibu.

Dokta alianza ooh eti ni lazima kupima ukimwi pale mtu akienda kutibiwa.Nilimwambia kupima c ni hiari ya mtu.Alitwambia mambo mengi ila sana tu alidai kuwa walikua wanataka kujua ni wanakijiji wangap wanaish na vvu...Nilikubali kupima ckua na hofu sana.Nilienda maabara nikapimwa h.I.v pamoja na magonjwa mengine.

Majibu yalitoka nipo vizur kiafya ( sina ukimwi ) ila tu malaria kama kawaida hua haituachi, nilipewa dawa tukasepa kurud home.

Siku hyo Qilah aliniuliza kama kweli me napiga beats nilimwambia me najua ila sio sana ko nilimwambia atulie time hela.Hakua na usemi zaid ya kuguna tu.

Zilipita cku mbili yule msimbit alinitafuta tens cku hyo ilikua cku ya mnada.tulikutana nae mnadani, alininunulia soda ( Pepsi ) wakat hua nikampa simu yngu ajirekod I'll niweze kumpigia beats.Aliimba wee na watu walkua wanatushangaa.Alivyomaliza nikajarbu palepalee kupiga beats kwenye org 21 nikashindwa ( nyimbo za asili kwangu no ngumu ) nikamshawish kwanini nisimpe beat moja hivi aiimbie, alitaka nimsikilizishe nikamsikilizisha.

Hiyo beat niliitengeneza nikiwa Arusha sasa nilikua nayo tu kwenye simu.Jamaa aliipenda hyo beats akanipa 50k kwanza nyingne akadai atanipa akipata, nilimmaind kidogo kwa kunipa hela nusu ( nilikua nazuga tu )...nilimuaga nikapanda zangu gar kurud home nauli buku tu.


Nilifika home nikampa qilah 20k atumie ( nilikua nampenda )...nili Brock namba ya yule msimbit ckutaka anitafute tena.

Kabla cjasimulia hiki kisa hapa Jf nilimsimulia qilah kwanza lakin ni baadh ya matukio, cku msimulia yote lakin yeye alinielewa hata akushangaa.


nitarejea tena.
Una brain 🧠 Boss uko sharp sana
 
Imeandikwa maneno ya hekima sana,,,,japo style ya uandishi wako imekua ya kishamba sana.
Aiisee samahani. Mimi si mwandishi. The Word of wisdom as you said is from the Bible. Words were taken from swahil bible version. Sasa hapo ushamba wangu ni upi. Ulitaka niandike vipi mheshimiwa.
 
Back
Top Bottom