Inaendelea
Kuna kipindi maisha yanakua matamu sana yani furaha kama yote na kuna kipindi maisha hua hayana maana kabisa yani unataman mpaka kufa.
Qilah wangu niseme alikuja kibahati sana ( accidentally ) sikua na mawazo kabisa kama nitakuja kuishi nae cku moja.
Mwaka huu mwezi wa 1 alipata msiba kwao huko Arusha ilikua ni must aende me nilisema siendi nae.Nilijua kabisa harudi tena bush kwetu.
Kwa jinsi alivyo afananii kabisa na wa kukaa bush, alikaa wiki mbili tu nikashangaa mtoto huyo karud tena aliniletea viraba flan hivi vikali sema tu vilinipwaya


.
Wale wadem zangu wa nyuma ckua nimewaacha kwa kuwaambia tofauti na yule
mywangu ndo nilimtema kwa kumwambia.
Mwezi wa kwanza huo huo kipindi qilah alikua msibani Lizy alinitafuta cku hyo akaanza mambo yake sasa kulalamika kuwa nimemtenga wala cmjali kihisia wala kimaendeleo.
Sikua na lamaana sana la kumwambia zaid tu ya kumdanganya.Kuna cku alinitumia text ndefu ya malalamiko ya kutosha akaniuliza kama nipo musoma tuonane nae.Nilimpotezea tu maana me na wadangaji saiv nawakwepa.
Siku moja Qilah alikua kasharud bush sasa cku hyo nilienda bush kuwaona.Niliugua tena yani nilikua natetemeka hatar.Niliamua kwenda zahanati, qilah alinisindikiza.Sasa tumefika Zahanati kulikua na watu wengi sana.So foleni ilihusika niliamua me kukaa chini ya mti ulikua hapo kando ya zahanati.
Qilah yeye alikua mapokez anachukua kadi, alivyorud kwangu alinambia nimuelekeze dukani.Me mwenyewe ckua najua maduka maana bush nilikua sio mwenyeji kabisa.
Alielekezwa na Mmama mmoja hivi, maduka yalikua mbali kidogo.Alipanda boda kwenda kununua daftari ( ilikua ni lazima uwe na daftar ili utibiwe ).kipindi amesepa nilikua tu nimekaa nimeegemea mti najiskia vibaya.Niliamua kutoa simu yngu mfukoni nikaanza kupiga piano.
Yalikua ni mazoea yangu kupiga piano kwenye simu sasa wakat napiga piano kuna jamaa mmoja ni Msimbiti.Alivutiwa na nilivyokua napiga ko alikuja akakaa karbu yangu, sasa alikua yuko so interested na mimi navyopiga piano.
Japokua nilikua naumwa niliamua kuzidisha manjonjo ( nikiona mtu yupo interest na ninachokifnya basi hua najiskia raha )....nili muoshea sana, yaan nilitoa piano nikaweka App ya ORG 21 nikaanza kupiga beat.Jamaa uzalendo ulimshinda akaamua kunisemesha.
Alianza na yeye kujisifia, wakat anaendelea kujisifia Qilah wangu alikua kasharud na daftar, sasa na yeye alikua ana msikiliza huyo msimbiti na sifa zake.Msimbiti aliongea wee mwishoe akaniuliza atapata wapi mtu amtengenezee beat, maana yeye ni mwimbaji wa nyimbo za asili.
Nilimwambia mbn me ni producer ( nilimwambia huku namuangalia qilah wangu usoni )..msimbit alinambia kuwa wimbo mmoja narekodia shngp.Nilimwambia kwani we hua unarekodia shngp,akasema ndo anataka kuanza muziki.
Nilimwambia hutaweza muziki bora heka yako ufanye mambo mengine.Nilimwambia aimbe kidogo tumsikie, alivyoimba qilah ni mjinga alishindwa kujizuia alicheka mpaka na mimi nilicheka japo nilikua naumwa



.
Nilimwambia kurekod ina bei yake na kupiga beat kuna bei zake, nilimwambia me natengeneza beats tu kurekod labda jamaa angu mmoja ndo atamaliza show.Nilimwambia beat ni 100k ila yeye kwa vile kaonyesha nia nitamfanyia 70k tu.Hata hakubisha lakin alinambia hana pesa kwa muda ule, ko akadai nimpe no zangu aje kunitafuta.Nilimpa afu tukaendelea na story nyingine ila yeye ndo alikua muongeaji mkuu akitupa story za madisko ya usimbitini.
Saa nane mchana ilifika ndo tukapata huduma pake zahanati.Niliingia chumba cha daktar na qilah, Dokta aliniuliza kama itakua ni vyema Qilah aendelee kubaki ama atoke nje ili dotka aniulize maswali yake.Nilimwambia ata akiwepo ni frsh tu haina shida maana ni mtu wangu wa karibu.
Dokta alianza ooh eti ni lazima kupima ukimwi pale mtu akienda kutibiwa.Nilimwambia kupima c ni hiari ya mtu.Alitwambia mambo mengi ila sana tu alidai kuwa walikua wanataka kujua ni wanakijiji wangap wanaish na vvu...Nilikubali kupima ckua na hofu sana.Nilienda maabara nikapimwa h.I.v pamoja na magonjwa mengine.
Majibu yalitoka nipo vizur kiafya ( sina ukimwi ) ila tu malaria kama kawaida hua haituachi, nilipewa dawa tukasepa kurud home.
Siku hyo Qilah aliniuliza kama kweli me napiga beats nilimwambia me najua ila sio sana ko nilimwambia atulie time hela.Hakua na usemi zaid ya kuguna tu.
Zilipita cku mbili yule msimbit alinitafuta tens cku hyo ilikua cku ya mnada.tulikutana nae mnadani, alininunulia soda ( Pepsi ) wakat hua nikampa simu yngu ajirekod I'll niweze kumpigia beats.Aliimba wee na watu walkua wanatushangaa.Alivyomaliza nikajarbu palepalee kupiga beats kwenye org 21 nikashindwa ( nyimbo za asili kwangu no ngumu ) nikamshawish kwanini nisimpe beat moja hivi aiimbie, alitaka nimsikilizishe nikamsikilizisha.
Hiyo beat niliitengeneza nikiwa Arusha sasa nilikua nayo tu kwenye simu.Jamaa aliipenda hyo beats akanipa 50k kwanza nyingne akadai atanipa akipata, nilimmaind kidogo kwa kunipa hela nusu ( nilikua nazuga tu )...nilimuaga nikapanda zangu gar kurud home nauli buku tu.
Nilifika home nikampa qilah 20k atumie ( nilikua nampenda )...nili Brock namba ya yule msimbit ckutaka anitafute tena.
Kabla cjasimulia hiki kisa hapa Jf nilimsimulia qilah kwanza lakin ni baadh ya matukio, cku msimulia yote lakin yeye alinielewa hata akushangaa.
nitarejea tena.