Inaendelea
Nawashukuru sana tena wale tuliyokua pamoja kwenye huu uzi.Nilikua nasita sana kuelezea haya maisha yangu, asanteni kwa mlio nitia moyo Pm na hata hapa kwenye comment, bila kuwasahau wale mlio nivunja moyo pm na hapa ila chakuwaambia ni kuwa
MAISHA NI HAYA HAYA.
Wazazi na ndugu zangu licha ya kuwaaibisha lakini bado huwaambii kitu kuhusu mimi ( wananipenda), kuna watu nilikua siwapendi yani siwapendi bila wao kujua kama siwapendi.Hicho kitendo kilikua kinasabisha nawachukia na nikikuchukua lazma nikulie njama yoyote ile, mfano mwalimu wangu wa piano enzi hizo nilikua simpendi nikimuona anavyoimba na jinsi watu wanavyopenda kipaji chake nilikuwa nachukia mpk cku moja nilimchomesha kwa muhuni wangu ( saiv ni marehemu ) akamteka simu mbili kali.
Mwingine nae ni jamaa fulani hivi sahiv ni jamaa wa faida kwangu kabisa nae nilikua cmpendi sema huyu ckumfanyia baya lolote.Nakumbuka cku nimeongea nae cku hyo hyo tukawa marafiki wakubwa sana.Tena huyu bila hiyana alinipa Xbox

yake aliyopewa na Mama yake kutoka Uingereza, Alinipa bure kabisa bila hiyana na ninayo mpk saiv ila ni mbovu.
Nilisha nusulika kifo kwenye ajali ya pikipiki niliipata pale kona ya baruti, nilikua mwenyewe kwakweli Mungu mkubwa sana na alikua ananipenda sana.
Yule rafiki tuliye kuwa tunateka nae watu simu, mwaka 2012 yeye saivi ni marehemu.Alikufa mwaka 2014 kwa ajali ya pikipiki, walikufa wawili yeye na swahiba wake, nasikia walikua wametoka kupiga tukio sasa speed waliyokua nayo ilikua kubwa sana, pikipiki iligongana na land kruza, japo cjui nitakufaje lakin jamaa angu alikufa vby sana.
Mwaka jana kipind najiandaa kwenda Arusha niimpoteza tena rafiki angu kwa ajali ya pikipiki, cku hyo ilikua jumapili majira ya saa tano alikuja ofisin kwangu ( Ps ), alikua yupo yeye na rafiki zake wawili.Walicheza ps mpk kwenye saa kumi jioni wakasepa.Neno lake la mwisho alinambia "
Hakikisha tunaonana leo usiku we fala" akimaanisha kuwa usiku huo tuwe wote kwenye happy birthday ya mdada mmoja hivi ilikua inafanyika palm Beach ( jirani na bwalo la police ).
Hiyo usiku ckuonana nae maana nilikua busy tu na mambo yangu.Kesho yake asubui tu naingia whatsapp naona kawekwa status kuwa kafariki.Niliumia sana yani ila ndo ivo mipango ya Mungu.Alipata ajali pale jirani benki ya crdb majira ya usiku saa saba akiwa anatoka kwenye hyo sherehe.
Mambo ni mengi sana yani kuyaweka yote itabidi tena nianze kusimulia na huku nilishaaga.Mungu mkubwa sana niseme ananipenda maana hebu fikiria kwa hayo yote aliyonitendea bado niko vizuri kiafya na hata kiuchumi (najimudu na nina mmudu Qilah wangu ) ingawa pia wazazi wananivusha nikikwama.
Tutende mema ili tuishi vizur bila hofu yoyote ila sometimes kuwa mgumu kidogo pale unapoona inatakiwa kuwa hivyo.Usipende kuwa dhaifu tu muda wote.Kama kuna Konda mmoja siyo konda msafi


ni hawa makonda wa hiace za kwenda Tarime kutoka musoma.
Ni mwaka huu tu nilikua naenda kijiji fulani hivi kiko karbu na kinesi ( kuruya ) sasa nauli ni 3000 na tulikubaliana na huyo konda kuwa ni hyo bei sasa alikuja kunigeuka kipindi anakusanya nauli, nilimpa hyo buku tatu akadai nauli ni buku nne.Nilimwambia vizur toka saa ngap nauli imepanda. tulibisha sana mpk tulipofika pale darajani kinesi kwenye ile check point konda alimwambia dereva akasimamisha gar alafu konda akanichomesha kwa wale maafande kuwa cna nauli alafu naleta fujo.
Nilikua mpole nikamuanyesha afande mmoja nauli yangu na nikakubali kumlipa konda hyo buku nne.Sasa tulivyofika hapo kuruya gari lilpaki pembeni nikampa nauli konda, kwa vile nilikua na kamzigo kalikua kwenye buti nilimwambia konda anitolee.Napo alivyotoa ule mzigo akadai niulipie tena Buku, nilimwambia nishaulipia maana nauli ni 3k ko hyo 4k niliyompa buku ni ya mzigo.
Konda alinitukana akafu kwa sauti mpk abiria wakawa wanackia pamoja na bodaboda waliyokua hapo pembeni mwa barabara.Neno lililo nikera ni alivyonambia "
Unafikiri hili gari ni la baba yako mpk utupangie nauli" nilimpiga konda ngumi ya mdomo akakasirika zaidi tena nikampiga ngumi yenyewe ya pua mpk damu zilimtoka.Dereva alimpa lichuma flani lilikua ndani ya ile gari eti anipige nalo.Nilikimbia kuelekea kule Center na uzuri ni kwamba huyo konda aliangua chini alivyokua akinifukuza, nilivyoona kaangu niliokota likuni nilimpiga nalo mgongoni.nilivyoona nimempiga kisawa sawa nilichukua mzigo wangu nikadandia boda huyo nikasepa.Dereva hakuamini kama nimeondoka maana alijarbu kunikimbiza lakin holaa.
Huyo konda aliyataka mwenyewe na kiukweli cjutii kabisa kumpiga hata cku nikionana nae akitaka ngumi tutazipga tu.
Saivi Holy ni mtu safie kabisa tena mcheshi mpenda masihara. Tena leo baada ya cku nyingi kutokwenda kanisani nimejumuika na wenzangu na tena nimeimba japo nilianza kusahau baadhi ya note.
Biashara ndo inaniweka mjini na kupiga beat ndo kunaniondolea stress kama nikiwa nazo bila kuwa sahau Ndugu zangu, rafiki zangu wa faida bila kumsahau Mama la Mama Qilah nampenda sana.
mcute tu fanya urudi Musoma unipe visa vyako ulivyonisimulia tukiwa sehemu yoyte nzuri

Asanteni sana najihisi sina Deni kabisa ikiwa kuna mtu anaswali akiniuliza nitamjibu hapa au Pm.
Mwisho