Yaani mm mwenyewe nilipokiwa nasoma nikajisemea moyoni, huyu mtu si tu MUNGU amempa kipawa cha mziki lakin ana kipawa cha UANDISHI mzuri, maana jinsi ulivyokuwa ukipangilia matukio, asiee nimependa sana, umejua kuzigusa hisia za watu na kuwashika hisia zao wapate kuendelea kukufuatilia sana kwa ukaribu.
Ni makosa madogo madogo ambayo nimeyaona kweny uandishi wake, kama kuweka nukta na koma, hivi ni vitu vidogo sana kweny uandishi lakin vina thamani sana. Yaani unakuta umeanza sentensi ghafla unajikuta umeshaanza kusimulia kitu kingine, kwahiyo ule mtiririko unapotea kwa ghafla, na hii si kwa sana umefanya lakin kama akipata shule nzuri yeyote ile iwe Youtube au mafundisho yoyote online au hata vitabu akienda bookshop yaan atakuwa ni mtu bora sana, anaweza akawa mtunzi mzuri sana hata akapata ajira ya kuandika makala mbalimbali kwenye magazeti.
Sent from my Redmi Note 3 using
JamiiForums mobile app