Hadithi: "Kivuli cheusi"

Hadithi: "Kivuli cheusi"

sasa hapo hata jafari hiza naye akae chonjo maana moses keshamjua 😡😡😕😕😕😡😡
 
Aiseee, wasiwasi wangu ni kwa vanessa tu jamani, Mungu na amuoke
 
Duh!
Moses umeanza kuua na wasiohusika sasa, huyo omary kakukosea nini,ungehama tu gesti bila kumuua kijana wa watu

Kwa wauaji wenye akili timamu ilikuwa lazima amuue, aliona mbali, hata mimi ningefanya hivyo
 
HADITHI: KIVULI CHEUSI

SEHEMU YA KUMI NA TISA

TULIPOISHIA....


Jafari Hiza akazungumza "Hiyo sumu ndiyo ile niliyokuambuia Vannesa" akamwangalia Vannesa kisha akagota kwenye uso uliomvimba Raymond kwa kulia "Huyu muuwaji ndiye huyu huyu aliyemuua mwanao Bertha na wote niliokupa taarifa juu ya vifo vyao. Huyu ndiye aliyewaua wamiliki wa apartment aliyofanyia mauaji ya shahidi namba moja aliyekuwa akimfahamu kule masaki kwa sumu hiyo hiyo" akawaeleza aina ya sumu ambayo aliitumia kwa kuichanganya katika chupa ya manukato. Habari hiyo haikumfanya Raymond kuacha kulia. Alilia kama mtoto.

Jafari Hiza akaeleza kuwa "hewa hiyo yenye sumu hudumu kwa dakika tano tu hewani, hivyo hakuna shaka kama tukiingia"

Wote wakaingia na kukuta miili ya watu kumi na moja ukiwemo wa bi Furahiya, Majura, walinzi sita na wafanyakazi watatu. Walikuwa wamefunikwa katika mifuko maalumu ya maiti.

******

ENDELEA...........


Wakati ambao walikuwa wakizungumza pale nje, ni wakati ambao Vannesa alimuona tena yule mtu aliyemuona kule hotelini kwa Raymond. Hakuwa amebadili shati lake jeupe, alifunga tai ya pink na suruali nyeusi juu akiwa amehifadhiwa na koti jeusi. Alipendeza sana.

Ila kwa Vannesa ikawa ni tatizo.

Akajiuliza kuhusu kumuona sehemu mbili zote zikiwa ni sehemu za ajabu. Alipatwa na wasiwasi sana juu ya Moses. Akaamua kumpigia simu baada ya kujitoa pembeni kidogo katika maongezi ya Raymond, mama koku na Jafari Hiza.

"Uko wapi Moses?.. Upanga.. Na mimi nipo hapa.. Hallo.. Hallo.."

Simu ikawa imekatwa na alipojaribu kupiga mara ya pili ikawa haipatikani. Akaamua kumtafuta mwenyewe.
Akawa haonekani.

Kulikuwa na umati mkubwa wa watu. Hivyo haikuwa rahisi kumuona.

Alirudi kwa Raymond kumuuliza kuhusu kufahamiana kwake na Moses. Aliamini fika kulikuwa na uhusiano fulani kati yao. Yeye hakuwa akijua kuwa Moses ndiye muhusika mkuu wa mauaji hayo, lakini kwanini Moses awe mtu kama anayeficha jambo kila anapomuona katika mazingira ya himaya ya Raymond? Raymond alikuwa tayari yupo ndani akilia juu ya maiti ya mke wake. Alimuacha kwa muda mpaka atakapopata nafasi nzuri ya kuzungumza.

Wakati ukafika, walikuwa wawili tu majira ya jioni ndani ya gari ya Raymond. Ilikuwa ni baada ya kutoka hospitali.

"Naomba nikuulize jambo Raymond"

Raymond akaitika kiunyonge "Sema chochote Vannesa"

"Unamfahamu mtu anayeitwa Moses?" Raymond akapiga breki ya ghafla na kutumbua macho juu ya uso wa Vannesa, akamuuliza kwa mshituko "Umemfahamu vipi Moses? Umemuona? Namtafuta sana, umemuona wapi huyo kijana tafadhali niambie nitampata vipi?"

Vannesa akaonesha tabasamu tu la kutoridhisha wala kuonesha kama alikuwa anafahamu chochote kuhusu Moses. Yeye mwenyewe akajisuta kuwa hakuwa akimfahamu Moses zaidi ya kumfahamu Moses wa kitandani, alimfahamu Moses wa chumbani, juu ya kitanda cha hoteli aliyekuwa akioga naye bafuni. Hakujua kazi ya moses wala hakuwahi kumuuliza. Hakujua nyumbani kwa Moses wala ndugu zake, ndio sababu hakujibu kitu mpaka Raymond alipozungumza kwa sauti iliyoonesha kukata tama "Moses ameshakufa siku nyingi" akawasha gari na kuanza safari ya kuondoka

"Amekufa!?"

Mshangao wa Raymond akawa ameupokea Vannesa mapigo ya moyo yakamuenda mbio na jasho likamtiririka kiasi cha kutoonekana umuhimu wa kiyoyozi. Akaropoka kwa nguvu licha ya kuwa alikuwa anawaza tu "Ina maana"

*****

Baada ya moses kushindwa kuingia katika hoteli ya Raymond, kuna nafsi ikamsukuma kuelekea nyumbani kwake, Raymond. Ilikuwa ni kama alivyotarajia. Umati mkubwa wa watu wakizungumza kila jambo.
Alichokisikia katika vingi walivyovizungumza ni kile alichokijua.

Jambo lile lile la watu wawili kufa kwa hali ya kushangaza. Lakini sasa hawakuwa wawili tena, waliongezeka watu tisa. Ikamshangaza sana lakini hakupenda kustaajabu sana kwakuwa alifahamu ulikuwa ni uzembe wa mtu yeyote ambaye angekuwa hafahamu kuhusu hila zake. Akajitenga na watu ambao walionekana si aina yake. Watu ambao walionekana ni waswahili na wafupi wa elimu.

Akatazama huku na huko, akavutiwa na kikundi kimoja. Kikundi hicho kilikuwa na watu wa rika lake. Watu walioonekana wenye elimu pamoja na jambo alilokuwa akilidadisi, alikuwa na hakika wao wangekuwa na majibu yake.

Akakisogelea taratibu akajiunga nao.

Ulikuwa ni wakati wa simanzi, hivyo hakuna ambaye alijali ongezeko la mtu kati ya kikundi chao kilichobeba watu sita kabla ya Moses.

"Raymond amepatikana"

Kijana aliyeukaribia uzee, akasema kwa upambe. Mwingine na mwingine wakaendelea kudakia bila kuwa na hakika na chochote. Alichokuwa akikitafuta akawa amekipata. Mmoja kati ya wale waliokaa kwenye kikao akaropoka

"Kwani nyinyi hamfahamu biashara haramu anazozifanya Raymond?" Akanyamaza kwanza. Aliwakagua kila mmoja bila kujali ugeni wa Moses kati kati yao. "Inawezekana amewadhulumu wenzake ndio maana wanamlipizia"

Mwingine akadakia kwa udaku "Unachosema kinawezekana" huyu aliyekuwa anaongea akainama kabisa "walianza kwa mtoto wake Bertha huko kijitonyama sasa wanaendeleza mauaji zaidi"

Kabla hajamaliza kuzungumza, yule ambaye Moses alimkuta akiongea akakohoa.

Moses akamtazama kama wengine walivyokuwa wamefanya. Akamkuta naye akimtazama. Yule kijana aliyetawaliwa na ufukara na shida aliyekonda kwa mawazo, akauliza "Sijuhi wewe ni nani mwenzetu?"
Alikuwa akimuuliza Moses. Moses akajichekelesha pale bila kujibu chochote. Alipoona wote wakimtazama, akapata la kuongea

"Mimi ni mgeni katika mtaa huu ila nimeshitushwa na habari za vifo vya watu hawa" aliwatazama watu wale na kuonyesha waliridhika na majibu yake.

Akamalizia "mnisamehe kama nimeingilia mkutano wenu"

Yule ambaye alikuwa kama kiongozi katikati yao, akamsimamisha Moses mara alipokuwa akigeuka na kutaka kuondoka "Hapana usiondoke" Moses akasimama na kurudi miongoni mwao "tusamehe bwana, unajua hizi habari ni nyeti sana hivyo nilishitushwa na sura yako kwa kuwa wewe ni mgeni katikati yetu"

"Hamna .."

Kabla Moses hajamaliza kuongea, akaiona gari ya Raymond. Akabaki akiwa ameduwaa kuitazama. Kwa nyuma ilikuwa inafuatwa na gari ya Jafari Hiza. Hakufahamu kama ndani yake alikuwepo pia Vannesa. Wote kati yao wakawa wanashangaa alichokuwa akikitazama Moses. Wakaliona gari ya Raymond. Kila mmoja alianza kuaga na mwisho Moses alijikuta amesimama peke yake.

Ni wakati huo alipomuona Vannesa akishuka na Jafari Hiza kutoka ndani ya gari ya jafari. Alipoendelea kutazama kwa muda wa dakika ishirini zaidi, aliyaona macho ya Vannesa yakimtazama.

Alishuhudia mshangao juu ya macho hayo ya Vannesa. Lakini alijizugisha pale na kujiingiza kati kati ya vikundi vya watu kumkimbia Vannesa.

Alipotazama kwa mbali akiwa ameuacha mtaa wa Raymond, alimuona Vannesa akihangaika kumtafuta.

Akacheka kwa kuuzika na kujisemea moyoni

"Hutaniona tena Vannesa"

Akatokomea anapopajua.


*****

ITAENDELEA...................!!!
 
mkuu tiririiiika aseeh niko nawewe sambamba......moses ingefaa akutane na Joram Kiango/Wille gamba sio level za Vannesa kabsaaa jamaa ni nouma sana....hivi mafunzo yakigaidi aliyapata wapi mizambwa
 
Last edited by a moderator:
mkuu tiririiiika aseeh niko nawewe sambamba......moses ingefaa akutane na Joram Kiango/Wille gamba sio level za Vannesa kabsaaa jamaa ni nouma sana....hivi mafunzo yakigaidi aliyapata wapi mizambwa

Kuandika story za akili namna hii, lazima na wewe uwe una akili sana, i wish bongo movie wangekuwa wana upeo mkubwa kama moses na vannesa , nadhan tungekuwa tunalamba tuzo za oscar daily sema kwa wasanii wetu hawa wa kulala na kuamka tayar waigizaji au ma director mbona tutasanda
 
Last edited by a moderator:
HADITHI: KIVULI CHEUSI

SEHEMU YA ISHIRINI

TULIPOISHIA....

Kabla Moses hajamaliza kuongea, akaiona gari ya Raymond. Akabaki akiwa ameduwaa kuitazama. Kwa nyuma ilikuwa inafuatwa na gari ya Jafari Hiza. Hakufahamu kama ndani yake alikuwepo pia Vannesa. Wote kati yao wakawa wanashangaa alichokuwa akikitazama Moses. Wakaliona gari ya Raymond. Kila mmoja alianza kuaga na mwisho Moses alijikuta amesimama peke yake.
Ni wakati huo alipomuona Vannesa akishuka na Jafari Hiza kutoka ndani ya gari ya jafari. Alipoendelea kutazama kwa muda wa dakika ishirini zaidi, aliyaona macho ya Vannesa yakimtazama. Alishuhudia mshangao juu ya macho hayo ya Vannesa. Lakini alijizugisha pale na kujiingiza kati kati ya vikundi vya watu kumkimbia Vannesa. Alipotazama kwa mbali akiwa ameuacha mtaa wa Raymond, alimuona Vannesa akihangaika kumtafuta.
Akacheka kwa kuuzika na kujisemea moyoni

"Hutaniona tena Vannesa"
Akatokomea anapopajua.

****
ENDELEA..........


Vannesa akiwa ameachana na Raymond mawazo juu ya Moses yakazidi kumuumiza nafsi yake. Alijiuliza ni vipi Raymond atamke kuwa Moses amefariki. Moses huyu aliyelala naye chumba kimoja? Kitanda kimoja? Akaoga naye bafu moja? Hapana kuna namna juu ya jambo hilo. Akaamua kumpigia simu.

".. Haipatikani"

ilikuwa ni sauti ya mashine kutoka katika mtandao aliokuwa akitumia Moses.

'Kwanini amezima simu? Ni yeye kweli niliyemuona nyumbani kwa Raymond'

Akajiambia mara baada ya kuingia ndani ya gari yake aliyoiacha kazini.

Wakati huo Naima alikuwa tayari ameshatoka kazini. Kichwa chake kikawaza kwenda hoteli aliyokuwa akilala na Moses. Hakutumia muda mrefu mpaka kuifikia hoteli ya Caribean. Alienda moja kwa moja mpaka chumbani. Kitasa kikawa kigumu kufungua mlango. Akagonga hodi bado ukimya ukatawala. Aliamua kushuka mpaka chini kwenda kuuliza mapokezi kama mteja wao ambaye ni Moses amekwisharudi hadi wakati huo.

Msichana wa mapokezi akajibu

"Ndiyo na amerudisha chumba tayari"

"Amerudisha chumba? Hajaacha ujumbe wowote?" Alikuwa akiuliza huku akijipekua pekua kuitafuta simu yake. Yule muhudumu wa mapokezi akatoa bahasha fulani ya rangi ya kaki. "Ameniachia bahasha hii hapa"
Vannesa aliiacha simu ile na kufungua bahasha hiyo kwa shahuku kubwa. Alitamani kufahamu nini kipo ndani ya bahasaha. Alipoupenyeza mkono wake ndani ya bahasha, akagusa vitu viwili. Vyote vilionekana ni kama karatasi.

Kitu alichodhani ni Karatasi kikadondoka.

Nyingine ilikuwa ni karatasi aliyoishika mkononi mwake. Hicho kitu kingine kilichodondoka, kilikuwa ni picha. Picha ambayo alikutana nayo kama ushahidi kwa watu waliokutwa wamekufa. Picha iliyopigwa na mtu aliyejitambulisha kama kivuli cheusi. Picha iliyopiga kivuli cha mtu ambacho ni cheusi. Aliishika bila kuamini kama ni ujumbe alioupata kutoka kwa Moses. Akaitoa karatasi ile iliyo mkononi mwake na kuikunjua kusoma kilichoandikwa ndani ya barua hiyo

Barua hiyo iliandikwa na Moses mwenyewe.

Ilisomeka hivi "Pole sana Vannesa kwa siku zote kukulaghai na kukufanya uniamini kuwa nilikupenda. Katika maisha yangu sikuwahi kumpenda msichana wala sijuhi nini kuhusu mapenzi. Mimi ni muuaji. Mimi ni mwanaume hatari ambaye unahangaika kunitafuta usiku na mchana. Dhumuni la ujumbe huu mdogo, ni kukujuza kuwa nitasitisha kusimamisha uhai wa watu wasio na hatia mpaka nitakapopata nafasi huru ya kuzungumza na Raymond. Na ihitaji roho yake endapo hatonieleza ukweli juu ya ninachokitafuta kwake." Akahitimisha ujumbe wake huo kwa kumwambia "wako umpendaye Kivuli cheusi"

Pumzi za Vannesa zikaongezeka, Kifua kilipanda na kushuka huku asiamini alichokuwa akikisoma. Bila kutarajia machozi yakamtoka. Uchungu ulimshika sana. Donge zito likaikamata koo yake alipojaribu kutaka kunyanyuka akahisi uzito.

Kiukweli nguvu zilimuishia. Hakuamini kama alikuwa akilala kitanda kimoja na muuaji. Hakujua kama aliyekuwa akimtafuta kwa udi na uvumba ndiye aliyekuwa akimwambia anampenda kila siku. Alikaa kwa muda mrefu bila kuchukua hatua yeyote, simu yake ndani ya mkoba ikapata uhai.
Juu ya kioo alikuwa Jafari Hiza.

"Vipi Vannesa"

Jafari Hiza alitamani jioni hiyo kukutana na Vannesa. Tamaa ya mapenzi ilimuwaka kiasi cha kushindwa kuvumilia. Alimuhitaji sana Vannesa. Akazungumza kwa mahaba ndani ya chombo cha simu.

"Unasemaje Jafari?".

Vannesa akaitika kivivu kama aliyetoka kusinzia.

"Ha!! Vannesa umeshalala mara hii?"

"Hapana"

"Okey!! sasa tunaweza kukutana sasa hivi?"

"Sipo sawa lakini ni muhimu mimi na wewe tukutane"

Hakuelewa nini alimaanisha Vannesa lakini tamaa ikazidi kumsukuma kuamini kuwa Vannesa pia alikuwa akimpenda. Hakujua kilichomkuta Vannesa kwa wakati huo.

Vannesa na Jafari Hiza wakapanga wakutane katika bar ya Caribean. Ilikuwa ni night club. Vannesa hakupata shida kwenda mbali kwa kuwa ilikuwa ni hatua chache kutoka ulipo mlango wa kuingia katia vyumba vya kulala. Bar hiyo ilikuwa ghorofa ya pili. Hakutaka kutumia ngazi kutokana na uchovu uliomkamata ukichanganya hasira zilizomjia juu ya Moses. Mwanaume aliyeamini ndiye mwanaume atakayeziba pengo la Amani. Amani aliyemsaliti na kutembea na rafiki yake Martha. Akamuona Moses mwanaume anayefaa kuwa mume wake kabisa.

Akaziendea lifti na kubonyeza kitufe cha namba mbili. Akajisogeza katika moja ya viti vilivyo pembezoni kabisa lakini mwanga ulimmulika. Aliutazama mlango huku bado machozi yakimtoka. Akakumbuka siku ya kwanza alipomuona Moses eneo hilo.

Akaijutia sana siku ile.

Siku ile ya kwanza kuingia ndani ya bar hiyo. Pombe zikamfanya kuangukia kwa Moses. Muuaji aliyeondokea kumchukia lakini kiuhalisia alimpenda sana. Aliitafuta chuki moyoni mwake juu ya Moses, lakini haikuepo.

Alimpenda sana Moses.

Licha ya kugundua Moses ni muuaji, bado alimpenda. Ubaya wa Moses ukajitenga mbali na mapenzi yake moyoni. Lakini usoni alionesha chuki za wazi na aliona ni sahihi kumchukia. Mara akajiuliza atamwambia nini Jafari hata akija? Akiwa katika kuwaza huko, alimuona Jafari akiingia. Jafari alipokuwa akiingia, aliiweka simu sikioni mwake akimpigia Vannesa.

"Nimeshakuona.."

Vannesa akamuelekeza wapi alipokaa, Wakaonana. Jafari Hiza alishangaa sana kumuona Vannesa akidondosha machozi, Akauliza kwa huba

"Vipi Vannesa, una matatizo gani?"

Huku akimpapasa papasa mikononi. Bado vannesa akaendelea kulia alilia akalia wala hakunyamaza. Mwisho Jafari Hiza alipofanikiwa kumnyamazisha Vannesa akaiweka picha yenye kivuli cheusi mezani walipokaa.

"Nini hiki?"

Jafari hiza akauliza kama hakuitambua picha hiyo. Ilikuwa ni picha moja iliyoonekana kila sehemu iliyotokea mauaji. Vannesa akajibu kwa kughadhibika

"Kwani huifahamu picha hiyo?"

"Ina maana kuna mauaji yametokea?"

"Ni heri yangetokea kuliko kilichonipata"

Vannesa hakuona sababu ya kuficha kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Akamuhadithia kila kitu Jafari tangu mwanzo walipokutana katika bar hiyo ya carribean. Habari hiyo ikawa mbaya sana kwa Jafari Hiza. Ile tamaa yake kwa Vannesa ikakatika mara baada ya kusikia kuwa Vannesa alikuwa na mahusiano na muuaji wanayemtafuta.

Hisia fulani zikaingia moyoni mwake.

Hisia mbaya za kudhani huenda Vannesa ana husika katika kumrahisishia muuaji kukimbia mitego yao ya kumkamata.

Akaondoka bila kumuaga Vannesa.

******


ITAENDELEA.................
 
Back
Top Bottom