Hadithi: "Kivuli cheusi"

Hadithi: "Kivuli cheusi"

Cant wait another episode

Halafu kuna sehemu ilinitatanisha, wakat moses akiwapulizia perfume yenye sumu mke wa curtbert na mwenzake na moses pia si alikuwepo? Na inasemekana hiyo sumu ni kali, ina maana na yeye haikumpata wakat walikuwa wote na alijipulizia kwenye nguo zake chafu?, alifanya hivyo hivyo kwa kina raymond ila yeye perfume haikumdhuru y?
 
Mkuu soma vizur episode za nyuma. Kwa mujib wa msimuliz 'moses hutafuna plastic inayomsaidia asidhurike na sumu hiyo kabla hajaipuliza....
 
Ok, nakumbuka kuhusu plastic ila sikujua kuwa alikuwa akizuia sumu nadhan sikuwa makini kusoma, thanks mkuu

Mkasa mzuri sana
 
Duh! Hiza unatakiwa utafakari kwa kina juu ya maelezo ya venessa kabla hujachua uamuzi wowote

Huyo vannesa si amuue tu huyo hiza maana kashajiingiza pabaya, kashajulikana na yeye anahusika na mauaji, maana solution ya matatizo kwenye huu mkasa ni kuua tu
 
Aluuuu Vanesa, penzi ni kikozi. haya sasa chuma kikoli moto twende kazi mizambwa
 
Last edited by a moderator:
HADITHI: KIVULI CHEUSI

SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA

TULIPOISHIA............

Vannesa hakuona sababu ya kuficha kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Akamuhadithia kila kitu Jafari tangu mwanzo walipokutana katika bar hiyo ya carribean. Habari hiyo ikawa mbaya sana kwa Jafari Hiza. Ile tamaa yake kwa Vannesa ikakatika mara baada ya kusikia kuwa Vannesa alikuwa na mahusiano na muuaji wanayemtafuta.
Hisia fulani zikaingia moyoni mwake.
Hisia mbaya za kudhani huenda Vannesa ana husika katika kumrahisishia muuaji kukimbia mitego yao ya kumkamata.
Akaondoka bila kumuaga Vannesa.

******

ENDELEA...............

Baada ya kuandika ujumbe ule na kuiacha picha ile, Moses akiwa anatoka nje ya hotel hiyo; aliiona gari ya Vannesa. Hakutaka kukutana na Vannesa tena, lakini hakutaka kumuua pia. Mapenzi aliyo nayo kwa Vannesa aliamini ipo siku atakuja kuwa nae tena. Licha ya kumwambia ukweli juu mauaji aliyokuwa akiyafanya, lakini aliamini yeye ni binadamu na ipo siku atamsamehe.

Aliamini hivyo ndio maana akawaza tena. Aliwaza kuwa ni vizuri kuendelea kumfuatilia Vannesa kila siku bila kukutana naye. Alitaka kujua Vannesa anafanya nini na anakutana na nani kwa siku. Kazi hiyo aliianza mara baada ya kujificha na kumtazama Vannesa alipokuwa akiingia kuelekea chumbani. Mara alimuona akirudi mapokezi. Moses alitumia gazeti pana kuficha uso wake.

Vannesa hakumuona.

Alimtazama mpaka alipokuwa akiisoma barua yake. Aliyaona machozi machoni mwa Vannesa. Akatamani kumfuata amwambie ni kiasi gani anampenda, ila hakujua maana ya machozi yale. Akaendelea kumfuatilia kila alichokuwa akikifanya.

Alimuona akiipokea simu.

Hakusimama hata alipomuona akiingia ndani ya lifti, alijua wapi alipokuwa anaenda. Akafungua mkoba wake aina ya briefcase, akayaona mavazi yake ya kizee. Ndevu nyingi zilizochoka. Akacheka kimoyomoyo.
Alielekea chooni kubadilisha muonekano wake.

Dakika tano zikawa nyingi akarudi eneo lile la mapokezi. Wakati ambao sasa anarudi pale alipokaa mwanzo, ndipo akagongana na mtu. Mtu yule alikomaa sana, kiasi cha kikumbo hicho kumdondosha mpaka sakafuni. Alipouinua uso wake huku akiugulia maumivu, alimuona mtu huyo. Mtu huyo hakuwa mwingine bali ni Jafari Hiza. Jafari Hiza hakumtambua Moses kwa kuwa hakuijua hata taswira ya muuaji. Akamuinua Moses huku akimuomba radhi kwa heshima kama mzee mwingine. Moses akajua fika Jafari alikuwa akielekea kwa Vannesa. Akamfuatilia alipokuwa anaenda.

Ni katika bar ile ile aliyokutana na Vannesa kwa mara ya kwanza. Jafari Hiza alikuwa mbele Moses nyuma kwa mwendo wa tahadhari. Moses aliziacha meza tano toka alipokaa Jafari Hiza na Vannesa. Huko baada ya muda akaona hali si shwari. Aliona Vannesa akimpatia Jafari Hiza picha ile ya kivuli cheusi. Ghafla Jafari aliondoka bila kuagana kwa heri.

"Kuna tatizo"

Kuna nafsi ikamnong'oneza. Jafari Hiza akampita pale pale alipokaa na kuondoka zake. Alipomuona Vannesa akiwa peke yake, hakuona si tatizo akimuacha na kumfuatilia Jafari Hiza. Alipanga kumfanyia kitu mbaya. Moyoni akajiambia

"Bila kumuua Jafari Hiza atamghiribu Vannesa "

*****

Baada Jafari Hiza kuondoka, Vannesa naye hakuona umuhimu wa kubaki tena; naye akaondoka. Aliamua kurudi nyumbani kwake na kukiacha chumba kilichokuwa kikimkumbusha kumbukumbu mbalimbali za Moses. Alikumbuka kipindi ambacho alikuwa akishikana na moses kila sehemu ya mwili.

Akilikumbuka tabasamu la Moses, chozi likamdondoka tena. Akatoka kinyonge ndani ya hotel ya Carribean. Akaifuata gari yake iliyopo maeneo ya maegesho ya hotel hiyo. Aliufungua mlango na kunyonga ufunguo, injini ikaitika. Aliisogeza gari yake lakini hakuwa amekwenda mbali sana. Alikutana na foleni kubwa ya magari. Bila kujua tatizo lililopo mbele, akaipiga sterling ya gari kwa hasira na kuitusi foleni hiyo. Gari hazikusogea zaidi ya dakika kumi aliyokaa kwenye foleni hiyo. Alichoka kusubiri. Aliamua kushuka na kujaribu kwenda kutazama nini kilichosababisha foleni hiyo.

Aliopishana nao walikuwa wakisema "Huenda breki zilifeli" Wengine wakadai "Ni uzembe bwana, unaweza kukuta alikuwa amelewa si unajua wikiendi hizi" Umati mkubwa wa watu ulikuwa ukishangaa ajali mbaya aliyokutana nayo Vannesa. Ajali hiyo ilitokea katika makutano ya kuiunganisha barabara ya kuelekea mwananyamala na ileile ya Jomo kenyata. Eneo lililoitwa studio. Gari ndogo iliyopondwa vibaya vioo kudondoka chini na kuwa kama unga ndio picha halisi iliyomvuta Vannesa kuzubaa kama mashuhuda wengine.
Akataka kuondoka ageuze gari apite njia nyingine, lakini kuna kitu kikamfanya asite. Kitu hicho ni aina ya gari hiyo iliyokanyagwa vibaya na Kontena lililodondoka kutoka katika gari yake. Gari hiyo aliifahamu vizuri, alikwishaipanda mara nyingi na aliizoea kuiona mara kwa mara. Akaropoka kwa nguvu "Mungu wangu"

Mara kikafuata kilio.

Ilikuwa ni gari ya Jafari Hiza. Jafari aliyeachana naye muda mchache uliopita. Akaanza kujilaumu kwa kukutana na Jafari. Alianza kudhani kuwa chanzo cha ajali hiyo huenda ni yeye kasababisha. Alikumbuka vizuri kuwa Jafari aliondoka akiwa na hasira, hakumuaga hata yeye mwenyewe.

Akalia kwa uchungu.

Akiwa katika kulia huko, alishuhudia baadhi ya vijana waliojitolea wakijaribu kuuvuta mwili wa mtu kutoka ndani ya gari iliyoangukiwa na kontena. Kontena lililodondoka baada ya gari hiyo kuigonga gari ya kontena na kusababisha ajali hiyo.

Vannesa alisogea mpaka karibu na mwili ule, alikuwa ni Jafari Hiza kweli. Alikuwa bado anapumua, hata wengi wa mashuhuda waliomtoa walimuona kuwa anapumua.

"Tumuahishe hospitali"

Wenye mioyo ya huruma wakaropoka huku wakishika nafsi zao. Jafari Hiza akawa amemuona Vannesa akajitahidi kutoa sauti huku damu nyingi zikimtoka mdomoni

"Nakufa Vannesa. Gari yangu ilifeli breki wakati..." Hakuimalizia sauti yake, akawa amelala ghafla. Macho yalikuwa yakimtazama Vannesa, moyo ukiwa umeacha mwili. Alikufa kistaarabu, kifo kilichohudhunisha.

Jafari Hiza akapelekwa hospitali kwa msaada wa msamaria aliyejitolea gari yake. Vannesa alipiga simu katika ofisi za Jafari Hiza na kutoa taarifa huku akiomba gari yake kuchunguzwa zaidi.

Alirudi katika gari yake na kuigeuza kuelekea nyumbani kwake. Alipoondoka Vannesa nyuma alifuatwa na gari ndogo ya Moses.

Moses aliyekuwa hapo muda wote katika taswira yake ile ile ya uzee, Alimuona Vannesa wakati akiuacha umati wa watu nyuma na yeye kuupokea mwili wa Jafari Hiza.

Alichukizwa sana na kitendo cha Jafari kutoka mzima na kuamini kuna kitu ambacho jafari Hiza alimwambia Vannesa, akaamua amfuatilie Vannesa ili apajue anapoishi kwanza.

****

****ITAENDELEA!!!!
 
Nilijua tu hiza atakufa , dah sasa vanessa yupo salama na mpenzi wake moses ndo kamuokoa, tumalizie basi scene ya mwisho commandor mizambwa
 
Last edited by a moderator:
mizambwa wewe ni kiboko, I salute you!
Hadi tuone mwisho wa moses......twende kazi
 
Last edited by a moderator:
Gosspcopwarumi, unataka scene ya mwisho, bado sana, moses hajakutana na Raymond, raymond hajafa bado hatujaona hatima ya vanessaa na mosess so bado sana

Nilijua tu hiza atakufa , dah sasa vanessa yupo salama na mpenzi wake moses ndo kamuokoa, tumalizie basi scene ya mwisho commandor mizambwa
 
Last edited by a moderator:
Gosspcopwarumi, unataka scene ya mwisho, bado sana, moses hajakutana na Raymond, raymond hajafa bado hatujaona hatima ya vanessaa na mosess so bado sana

usije kukuta vanesa naye ni mtoto wa raymond mbona patakuwa patamu apo?
 
Last edited by a moderator:
Wapendwa wote msiwe na shaka leo nitarusha sehemu zilizobaki katika hadithi hii zote. kwani kesho sitakuwa hewani hadi wiki ijayo

Hivyo kuna sehemu kadhaa zimebaki napenda nimalizie leo.

TUTAJUA MWISHO WA WOTE

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Poa kamanda tunazisubiri kwa hamu
 
Back
Top Bottom