Hadithi: "Kivuli cheusi"

Hadithi: "Kivuli cheusi"

HADITHI: KIVULI CHEUSI


SEHEMU YA KUMI



TULIPOISHIA.............

Alijua sasa kilichobaki ni mke wa Raymond. Mwanamke aliyesababisha kifo cha mama yake, Bi furahiya.

"Lazima nimuanze yeye ili huyu mshenzi ajue nipo siriazi"

Moses hakufahamu kuwa hakumaliza kufuta kumbukumbu ya taswira yake ya uzee katika kichwa cha Mfaume.

Akacheka sana kwa furaha alipokuwa akitazama taarifa ya habari akiwa ndani ya bar yenye mazingira machafu katika guest aliyolala huko kigogo mburahati.

Taarifa iliyokuwa ikitangaza tukio la kuuwawa kwa kwa muhudumu wa nyumba ya kulala wageni na muuwaji akihusishwa katika matukio ya mauaji ya wasichana wawili.

ENDELEA...............



Majira ya saa 3:15 asubuhi, ndipo Andrew kiongozi wa wahudumu wa apartment aliyoichukua Moses akakosa uvumilivu. Ilipita siku moja bila mtu yeyote kufungua mlango.

"si mwanamke wake wala yeye mwenyewe" alikuwa Baraka, msaidizi wa Andrew.

"kitu cha ajabu na kushangaza zaidi, kuna harufu kali inatokea chumbani"

Haikuwa kawaida kwa Andrew kupoteza uvumilivu haraka kiasi hicho. Lakini kengele ya hatari ikagonga kichwani mwake. Kengele ya kuhisi kumetokea jambo ambalo si la kawaida. Akavunja masharti ya kazi yake.
Kazi yake haikumruhusu kuingia ndani ya nyumba endapo kuna wateja. Labda kwa ruhusa maalumu au baada ya kutoka na kwenda kufanya usafi. Harufu kali ya uvundo, ikampa wasiwasi kila mfanyakazi wa apartment hiyo.

Andrew alichukua ufunguo wa ziada, akatekenya kitasa nacho kikalegea. Harufu ikawapokea kwa kero na hali ya kutofahamu kitu gani kimetokea ndani ya nyumba hiyo. Andrew akifuatiwa na Baraka walienda moja kwa moja mpaka chumbani. Harufu ikawa nzito hata ikawafanya wazibe pua zao. Wakaingia ndani ya chumba hicho, taswira ya dimbwi dogo la damu lililoanza kukauka likataka kumkimbiza Baraka. Kutokana na kukosa uvumilivu, Baraka akaita Mama kwa sauti ya juu kama vile hakuimeza miaka thelathini na nne duniani. Kiwiliwili kilichogawanyishwa mikono na miguu yake iliyowekwa pembeni kikawaadhibu Andrew na Baraka kwa uoga. Jasho jingi likawatoka hakuna aliyemuongelesha mwenzake.

"kichwa kiko wapi?"

likawa swali la kwanza kwa Andrew tangu wafike katika chumba hicho. Baraka akaona michirizi ya damu iliyoelekea moja kwa moja mpaka kwenye friji ndogo ya chumba hicho. Yeye mwenyewe akalifungua alichokutana nacho, kikamfanya apoteze fahamu.

Dakika chache baadaye Andrew ndiye aliwaita mapolisi baada ya kumtafuta kwa muda mrefu mmiliki wa apartment hiyo McCuthbert bila mafanikio. Simu zake zote ziliita bila kupokelewa. Polisi walikuja huku Inspekta Jafari Hiza akiwemo.

Yakawa mauaji mengine ya kushitua zaidi. Tena huenda haya yalikuwa makubwa kuliko yaliyopita. Akampa taarifa rafiki yake wa karibu Vannesa. Kwa kuwa waandishi wengi walikuwepo, basi Vannesa akaendesha gari, hakika ulikuwa ni mwendo wa mwendawazimu. Dakika kumi tu zikamfikisha hapo.

Wengi walimfahamu Vannesa na walizoea kumuona kwenye matukio makubwa, haswa kama hayo. Akaondokea kuwa mwandishi aliyejulikana na askari wengi kwa kazi ya uandishi bila kufahamu kuwa kulikuwa kuna kazi kubwa zaidi ya hiyo. Wakampa njia alipotaka kupita naUshirikiano alipouhitaji.

Akaelekea moja kwa moja kwenye chumba kilichofanyika mauaji. inspekta Jafari Hiza akamkabidhi picha ya kivuli cheusi iliyokutwa ndani ya friji pamoja na kichwa

"Unasema huyu nae amekatwa kichwa?"

Vannesa alihamaki kwa mshangao wa hasira. Haikuwa kawaida kwa Vannesa kuwa katika hali hiyo. Ni nani ambaye hamjui Vannesa anayependa kucheka hata kwenye misiba? Basi leo Jafari Hiza alimshangaa.

"Naomba kukiona kichwa cha huyo msichana"

Akaletewa kichwa cha Eva. Sura ya Eva haikumpotea hata kidogo. Alikumbuka vyema alivyokuwa akimuhoji katika tukio lile la Bertha kijitonyama. Damu yake ikaanza kuchemka. Ilichemka kwa kuwa alifahamu kuwa muuaji anajua anachokifanya. Akaanza kuingiwa na hisia muuaji huyu labda si mtanzania kamili.

Mtanzania aliyezaliwa Tanzania hawezi kuwa na akili za kuua kiakili kiasi hicho.
Ushahidi wa kwanza ukawa umefutika bila kupata chochote cha maana kutoka kwake. Akamwambia Jafari

"namfahamu huyu msichana aliyeuawa"

"unamfahamu?"

Inspekta hakufahamu kabisa kama huyo ni Eva. Jafari Hiza amekuwa msahulifu katika mambo mengi sana, ndio maana akauliza tena

"ina maana tunaweza kumpata muuaji?"

"kifo chake kinazidi kutupa ugumu wa kumpata muuaji"

Vannesa akaondoka akiwa amechanganyikiwa. Kifo cha Eva kikazidi kumchanganya na kumfanya amchukie zaidi muuaji huyo. Akaelekea bar fulani aliyoipenda huko maeneo ya kinondoni. Alichoamini bila kuushitua ubongo wake kwa kinywaji kikali, basi asingekuwa sawa wala kupata chochote katika tafakuri zake.

Akaingia ndani ya bar hiyo maarufu kwa watu maarufu na kama hukuwa nazo, basi usingeweza kumudu gharama za bar hiyo. Hivyo kwa sababu hiyo, ikafanya bar hiyo ya caribean kuwa na wateja wachache waliopata huduma za hadhi yao. Vannesa akajipachika pembezoni mwa ukuta huku akitazama orodha ya vinywaji

XXXXX

Baada ya kufanya mauaji ndani ya apartment ile, Moses alitoka na kuelekea upanga siku iliyofuata mara baada ya kutoka katika guest aliyopanga kama amekurupushwa. Huko alienda moja kwa moja kwenye nyumba aliyoishi McCuthbert. Mholanzi aliyemiliki apartment nyingi hapa mjini. Moses alifahamu fika endapo askari watakuja kumuhoji McCuthebert, basi angeharibu mipango yake. Mipango ya kulipiza kisasi kwa kumtaja kuhusika na mauaji hayo ndani ya apartment yake.

Hakutaka hilo litokee.

Ndio maana akausaliti urafiki walio nao kwa muda mrefu na kumpokonya uhai wake kwa sumu kali ya nyongo ya mamba. Alitokomea huku akiwa amebadilisha muonekano alioingia nao ndani ya ofisi ya bosi huyo wa kiholanzi.

Alitafakari mengi juu ya Raymond kutokana na bugudha ya kelele kusumbua tafakuri zake, sehemu sahihi aliyoamua kwenda ikawa ni kinondoni katika bar ya Caribean. Aliupenda utulivu wa eneo lile pamoja na huduma zake. Alipofika huko akachagua sehemu pweke ambayo angekaa peke yake huku akitafakari jinsi ya kumuangamiza Raymond.

Muhudumu akaifuata orodha ya vinywaji, huku akiwa amechagua mvinyo kutoka dodoma (dompo) leo hakuhitaji kabisa kulewa. Kabla hajafanya chochote wala ajamimina funda lolote kinywani mwake. Alihisi kusimamiwa mbele yake. Alipouinua uso wake kumtazama mtu huyo hakuwa mwingine zaidi ya Vannesa....

XXXXX


ITAENDELEA!!!
 

HADITHI: KIVULI CHEUSI


SEHEMU YA KUMI NA MOJA.

TULIPOISHIA

Alitafakari mengi juu ya Raymond kutokana na bugudha ya kelele kusumbua tafakuri zake, sehemu sahihi aliyoamua kwenda ikawa ni kinondoni katika bar ya Caribean. Aliupenda utulivu wa eneo lile pamoja na huduma zake. Alipofika huko akachagua sehemu pweke ambayo angekaa peke yake huku akitafakari jinsi ya kumuangamiza Raymond.
Muhudumu akaifuata orodha ya vinywaji, huku akiwa amechagua mvinyo kutoka dodoma (dompo) leo hakuhitaji kabisa kulewa. Kabla hajafanya chochote wala ajamimina funda lolote kinywani mwake. Alihisi kusimamiwa mbele yake. Alipouinua uso wake kumtazama mtu huyo hakuwa mwingine zaidi ya Vannesa....

******

ENDELEA..............


Kifo cha Bertha na muendelezo wa vifo vingine vya ghafla, vilimchanganya sana Raymond. Maswali mengi aliyojiuliza "ni vipi kifo cha Bertha kiungane na vifo vya hawa wengine?"

taarifa za vifo hivyo alizipata kutoka kwa Inspekta Jafari Hiza.

Yeye ndiye aliyempa taarifa za kifo cha Omary yule muhudumu wa nyumba ya kulala wageni, yule msichana muhudumu wa GQ pub na hata mmiliki wa apartment McCuthbert. Hao wote aliambiwa kuwa muuwaji ni mmoja na aliyemuua binti yake, Bertha.

Raymond akawatafakari maadui zake wengi, kati ya wote aliyewaogopa alikwishawamaliza. Aliwamaliza wote kwa mkono wa kijana wake aliyemuamini sana. Kijana aliyependa kumuita simba. Jina la kijana huyu mwenye nguvu na aliyetokea kumuamini sana ni huyu huyu Moses.

Akiwa katika tafakuri nzito huku machozi yakiwa karibu kumtoka, ndipo alipomkumbuka simba wake. Aliuhitaji ulinzi wake, aliamini akilindwa na yeye hakuna baya litakalompata. Alikumbuka vitisho alivyovipata kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kwake kama 'KIVULI CHEUSI' mtu huyo huyo ndiye anayeendeleza mauaji na kuacha picha yenye kuonesha ujumbe wa kivuli cheusi. Akapata tabasamu mara baada ya kutafakari juu ya kijana wake.

Akajisemea "atapambana na simba"

Aiinua simu yake ya kiganjani na kuanza kumtafuta Moses, kijana wake aliyemuita Simba. Alipoipiga simu ya Moses haikupatikana.

"huyu mtoto kwa pombe!" kisha akacheka "nitamtafuta kesho nimkate pombe zake kwa supu ya kuku aipendayo huku tukizungumza biashara mpya"

Wakati huo ulikuwa usiku wa saa 2:20, alipata chakula cha usiku pamoja na mkewe huku akimkumbusha jambo juu ya simba.

"Yule anafaa mume wangu" Bi Furahiya akagongea nyundo juu ya msumari wa tafakuri ya Raymond. Kesho asubuhi bado Simba hakupatikana. Ndani ya wiki mbili na siku zote Simba hakupatikana.
Akakata tamaa ya kumpata Simba.

Raymond hakufahamu Simba ambaye ndiye Moses ndiye alikuwa akiisaka roho yake usiku na mchana. Ndiye kivuli cheusi aliyemuua Bertha. Alimfahamu Moses muda mrefu kutokana na urafiki wake pamoja na Carlos lakini hakumtilia manani, kupitia Bertha akaanza kufikiria kufanya naye kazi. Mwanzo alikuwa haupendi uhusiano wa Bertha na Moses, lakini baadaye aliuridhia. Alimpenda Moses kwa kuwa alionesha ukomavu wa misuli, nguvu pamoja na akili.

Alishitushwa katika kifo cha Bertha kwa kuwa hakumuona Simba msibani. Hilo halikumtisha wala kumtia wasiwasi Raymond. Lakini kutokupatikana kwake siku zote alizomtafuta, zikamfanya ahisi huenda Simba alishauawa. kitu pekee alichokiweka kichwani mwake ni kuwa Simba ameshakufa. Akapoteza tumaini la kumkomoa KIVULI CHEUSI, Akapanga jipya la kufanya kulinda himaya yake.

******

Asubuhi Vannesa alijikuta akiwa kitandani, ndani ya chumba cha hoteli juu ya kitanda chenye mashuka meupe pekee.

"nipo wapi?"

Alitazama kila kona ya chumba cha hoteli hiyo na kuona nguo za kiume.

"Nimelala na mwanaume?"

Jasho likamtoka, jasho la uoga. Akainua shuka zito jeupe alilojifunika nalo, alijikuta mtupu.

"Mungu wangu nimetembea naye?"

Alipokuwa akiendelea kujiuliza alisikia mtu akikohoa kutokea bafuni. Kiwiliwili kilichoongozwa na kifua kipana mbele kikajitokeza mbele yake. Alikuwa ni kijana mwenye mvuto usoni akiwa amepambwa na tabasamu. Alikuwa akimtazama kwa viulizo vingi lakini Moses alikuwa tayari kumjibu yote ambayo angemuuliza.

Moses akaendelea kujifuta taratibu na taulo zito la hoteli hiyo. Tabasamu bado likiwa usoni mwake, alimuuliza

"Umeamkaje Vannesa?"

Alinyanyuka na kumsogelea kitandani alipokaa.

"Nimekuagizia supu ya kukata hangover uliyonayo"

kitu pekee ambacho vannesa alimuuliza mara baada ya kupata sauti yake ni kuwa "Wewe ni nani?"

Moses alicheka kwa kebehi akamwambia

"Vannesa kazi yako ya uandishi wa habari ni mbaya sana" alichukua suruali akawa anavaa "kila kitu unahoji, jana tulikuwa wote kwenye ile bar ya caribean tulizungumza mengi unanishangaza yote niliyokujibu jana leo unaniuliza upya"

Muhudumu wa hoteli aliileta huduma kama alivyoagizwa. Supu ya samaki sato na pilipili nyingi iliyochanganywa na ndimu. Vannesa alishangaa sana, alishangaa kwa kuwa supu hiyo ndiyo ilikuwa pendeleo lake kubwa alipokuwa akihisi uchovu mara baada ya kunywa kiasi kikubwa cha pombe. Akauliza tena

"Umejuaje kama mimi ni mpenzi wa supu ya aina hii?" Tabasamu la Moses halikutosha kuwa jibu. Akamwambia "umeshanieleza yote jana tulipokuwa tunakunywa Caribean huna haja ya kurudia"

Vannesa akajihoji kwa mashaka. "Nimekwisha mueleza yote? Yapi?" ukawa mtihani mkubwa kwa Vannesa kukumbuka vyote ambavyo alikwishaongea mbele ya Moses.

Lakini ukweli ni kwamba, Vannesa hakumueleza lolote kuhusiana na uchunguzi wa mtu anayejiita kivuli cheusi.

Moses alikaa chumbani hapo naye akizimua kwa pombe alizozikuta ndani ya friji dogo la hapo chumbani. Vannesa akavutiwa na huduma aliyoipata kutoka kwa Moses. Ni siku nyingi zimepita bila kuwa na mwanaume, hivyo alijihisi faraja kuwa karibu na Moses.

Hivyo hivyo ikawa kwa Moses.

Penzi alilopata usiku kutoka kwa Vannesa, likamrudisha katika kumbukumbu zake na Bertha. Wakiwa wanatazamana kwa muda mrefu bila huyu kumuongelesha mwenzake na huyu akiendelea kumtazama tu mwenzake bila kuzungumza chochote, ukafika wakati ambao kila mmoja akamuhitaji mwenzake tena. Vannesa akaliweka pembeni bakuli la supu na kumkaribia Moses.

Hakika Vannesa alikuwa ni mtundu aliyefuzu michezo ya mapenzi. Akampagawisha tena Moses kwa kumlamba masikio, mabusu motomoto ya mdomoni na kila sehemu. Moses akaapa kumpenda Vannesa milele. Wakatoka kwenye kochi na kumtupia Vannesa juu ya kitanda, kitanda nacho kikawapokea kwa bembelezo mathubuti.

Walitumia muda mwingi kushikana hapa na pale mpaka kila mmoja aliporidhika kumridhisha mwenzake.
Simu ya kiganjani ya Vannesa ikapata uhai. Juu ya kioo jina la mpigaji alikuwa Jafari Hiza kama alivyomuhifadhi katika kitabu cha namba zake za simu.

Alimuacha Moses kitandani na kuelekea bafuni kuzungumza na simu hiyo. Wasiwasi ukiwa juu ya tafakuri za Moses. Tangu aanze kazi hii ya mauaji akiwa peke yake, hakukiamini hata kivuli chake mwenyewe. Hivyo hakutaka aharibu mipango yake kwa uzembe kidogo.

Alinyanyuka mpaka karibu na mlango wa bafu kusikiliza maongezi ya simu aliyoipokea Vannesa.

*****

ITAENDELEA...................
 
haya sasa patamu hapo mpelelezi Vanessa na muuaji Moses wameanza uhusiano wa mapenzi bila kujuana,sijui itakuwaje huko mbeleni tusubiri tuone.
 
HADITHI: KIVULI CHEUSI


SEHEMU YA KUMI NA MBILI.

TULIPOISHIA

Hakika Vannesa alikuwa ni mtundu aliyefuzu michezo ya mapenzi. Akampagawisha tena Moses kwa kumlamba masikio, mabusu motomoto ya mdomoni na kila sehemu. Moses akaapa kumpenda Vannesa milele. Wakatoka kwenye kochi na kumtupia Vannesa juu ya kitanda, kitanda nacho kikawapokea kwa bembelezo mathubuti. Walitumia muda mwingi kushikana hapa na pale mpaka kila mmoja aliporidhika kumridhisha mwenzake.
Simu ya kiganjani ya Vannesa ikapata uhai. Juu ya kioo jina la mpigaji alikuwa Jafari Hiza kama alivyomuhifadhi katika kitabu cha namba zake za simu. Alimuacha Moses kitandani na kuelekea bafuni kuzungumza na simu hiyo. Wasiwasi ukiwa juu ya tafakuri za Moses. Tangu aanze kazi hii ya mauaji akiwa peke yake, hakukiamini hata kivuli chake mwenyewe. Hivyo hakutaka aharibu mipango yake kwa uzembe kidogo. Alinyanyuka mpaka karibu na mlango wa bafu kusikiliza maongezi ya simu aliyoipokea Vannesa.


ENDELEA............


*&****

Kwa muda mrefu InspektaJafari Hiza alivutiwa na Vannesa. Alishindwa kumueleza ukweli kwa kuwa hakujua pendeleo halisi la Vannesa.

Moyo wake ulisumbuka alipoliona tabasamu la Vannesa mara kwa mara. Kila alipotamani kuweka hoja yake mezani, mdomo ulikuwa mzito. Kuna wakati aliishia kumsifia tu na kumtamani zaidi.

Ila usiku wa leo alichoka kuvumilia. Ulikuwa ni usiku mrefu sana kwa Inspekta Jafari Hiza. Aliota ndoto nyingi nzuri kuhusu Vannesa. Lakini hii iliyomkatisha usingizi majira ya saa 3:15 asubuhi, ilikuwa ni mbaya sana.

Ilikuwa ndoto ambayo inamuonesha Vannesa akiwa njiani kisha vumbi fulani lililokuja mithili ya kisuli suli likammeza. Vumbi hilo likiwa limejigeuza mithili ya nyoka mkubwa mweusi.
Ndoto hiyo ndiyo iliyomfanya aipige simu ya Vannesa asubuhi asubuhi. Maongezi yao yakawa yanasikika na mtu wa tatu. Mtu ambaye hawalali usiku na mchana wakimtafuta. Mtu ambaye anawaumiza kichwa na kujiita kivuli cheusi.

"Habari yako Vannesa?"

sauti ya Vannesa ikawa ya kichovu "Kwanini asubuhi asubuhi" aliongea kana kwamba kuna kitu alichokuwa akihofia. Akaendelea "Kuna tukio? Ameuua tena?" wakati huo Moses hakuwa bado hajasikia chochote. Alipokuja kusikia ni wakati ambao maongezi yalikuwa yamefika tamati. Neno la mwisho alilolisikia ni sauti ya kuhamanika iliyomtoka Vannesa.

"Nipo kwenye hatari!?" sauti ilikuwa imeweka pozi kwa muda "Nitakuwa mwangalifu usijali Jafari"

Jafari Hiza aliikata simu kisha akaibusu huku tabasamu likiwa kwenye papi zake. Akajisemea kwa sauti ya chini "Nakupenda sana Vannesa, leo jioni nitakueleza kiasi gani nakupenda"
akajinyanyua kitandani na kuelekea nje kusafisha kinywa.

*****

Vannesa alipotoka bafuni baada ya mazungumzo hayo, alimkuta Moses akivuta sigara. Moses alijua kuigiza haswa. Akaizima sigara yake na kumpa kumbatio la haja Vannesa. Vannesa akalihisi joto la kimahaba kutoka kwenye kifua cha Moses. Vannesa akaonesha kumuhitaji tena Moses, lakini Moses aliuhitaji upweke. Upweke ambao ungempa fursa ya kutafakari njama zake juu ya kumuangamiza Raymond. Alimsihi Vannesa "Nisikilize tafadhali" penzi la Moses likamchanganya sana Vannesa. Hakusikia chochote alichoambiwa zaidi ya kuhema zaidi kimahaba na kuonesha uhitaji wa penzi la Moses tena kwa mara ya tatu. Moses akajaribu kumzuia Vannesa "Mpenzi sikia kwanza" Vannesa alipoonesha utulivu, Moses akazungumza

"Huu ni wakati wa mimi kuelekea ofisini, tafadhali tukutane jioni bado nakuhitaji pia zaidi."
Vannesa akaonesha kumuelewa zaidi Moses. Baada ya kujiandaa kwa pamoja na kila mmoja kuchukua bajaji moja na Waliachana maeneo ya posta ambapo Vannesa alihamishia ofisi yake hapo.

Moses akaelekea katika hoteli ya new afrika jirani na ofisi ya Vannesa. Hakujua kwa nini aliamua akae jirani na ofisi hiyo. Aliagiza mvinyo mtamu wa st anna. Akainywa taratibu huku akipasha joto mapafu yake kwa sigara kubwa. Tafakuri zake zikazama katika mauhusiano ya ghafla aliyoyaanzisha na Vannesa. Msichana aliye na kila dalili za upelelezi.

"Nipo kwenye hatari?" akaikumbuka sauti ya Vannesa akizungumza na mtu asiyemfahamu akiwa bafuni.
Aliyatafakari mazungumzo hayo kwa muda ndipo akapata jibu kwanini ameamua kuja kukaa new afrika karibu na ofisi ya Vannesa. Mazungumzo hayo ndio sababu ya kutaka kumfuatilia kwa ukaribu Vannesa na kutaka kufahamu nini anachokificha Vannesa katika maisha yake halisi. Akapiga funda moja la kinywaji chake.
Kisha akatabasamu.

Alitabasamu mara baada ya kuyapinga mawazo yake. Mawazo aliyoyatamka kwa sauti iliyosikika "Vannesa hafai kufa mapema. Nahitaji kumjua zaidi"

Ofisini, mawazo ya Vannesa yalikuwa juu ya Moses. Yeye alikuwa ni msichana ambaye aliogopwa na wengi. Wengi waliomtamani Vannesa waliogopa kumueleza hisia zao. Kazi yake ikamfanya kujitenga na mapenzi. Mapenzi yakamchukia na kumkinaisha kwa kuwa alikuwa busy na kazi. Hata alipokuwa akiwaza kuhusu Moses, bado ungedhani alikuwa akitafakari jinsi ya kumkamata muuaji.

Alipotabasamu ndipo aligundua kuwa hayupo peke yake katika chumba cha ofisi aliyopo. Kicheko kikubwa ndicho kilimshitua na kumfanya apoteze furaha yake. Alipotazama mbele ya meza yake ya mstatili, alimuona Naima akiwa anapasuka kwa kucheka yeye pia akacheka kwa tuo kana kwamba hakutaka kucheka.
Naima alizungumza huku bado kicheko kikiwa kimembana. "Dada Vannesa" alishakatazwa kumuita bosi.

Vannesa alipenda kuishi na Naima kama mdogo wake wa kuzaliwa na mama mmoja.

Naima akaendelea kuuliza "vipi mbona umesahau hata kunisalimia? Tabasamu halijabanduka usoni mwako tangu uingie ofisini leo" Ilikuwa ni hali ya kushangaza lakini fikra juu ya Moses ndizo zilimchanua na kuwa mng'avu.

Hakuacha kutabasamu hata alipoambiwa hivyo.

"Niambie basi kama umeshakikamata Kivuli cheusi na mimi nifurahi?"

Naima alijikaribisha katika kiti kilichopo mbele ya meza hiyo. Neno kivuli cheusi, likabadilisha kabisa taswira ya Vannesa. Taswira iliyojizaa upya ni ile ya hasira. Mistari fulani juu ya paji la uso ikajitutumua na kufanya uwe uso unaochukiza.

Hakucheka tena.

Naima akalifahamu hilo vannesa alipozungumza
"umenikumbusha jambo"

Naima naye aliacha kucheka, akaingiwa na shahuku ya kufahamu.

"Jambo lipi?"

"Huyu mshenzi amemuua shahidi mkubwa wa kesi hii"

"Mungu wangu" Naima akaishika midomo yake kwa kustaajabu, akauliza "ina maana yule Eva amekufa?"

"Ndiye huyo"

Vannesa alinyanyuka na kutaka kuondoka. Naima naye alinyanyuka "kwa hiyo umepanga kufanya nini?"

"Naelekea kwenye eneo lake la kazi, pale sitakosa pa kuanzia" vannesa pamoja na Naima wakiwa nje ya ofisi, Vannesa akamalizia "Nitaenda pia katika apartment ambayo huyu msichana ameuawa, niliziona kamera katika nyumba ile, hivyo nitapata chochote kutoka hapo pia"

Naima akastaajabu ufanyaji kazi wa Vannesa. Kifua chake kikapanda na kushuka kwa kuwa ni jambo lilohitaji umakini sana kugundua kamera ndogo ndogo zilizofichwa ndani ya nyumba ile. Ufuatiliaji wa kesi kama hiyo ukahitaji Pia ujasiri na hekima ya kumfahamu muuaji.

Vannesa na Naima wakaagana mara baada ya Vannesa kutekenya ufunguo wa gari na kuligeuza kuelekea kijitonyama. Mwendo ulikuwa wa wastani huku akiendelea kutafakari namna ya kumkamata muuaji huyo. Muuaji aliyemkosesha usingizi. Mauaji yake yalimfanya aone kuwa muuaji huyo alifahamu alichokuwa akikifanya. Alimuona muuaji kama mtu mwenye akili za ziada na aliyehisi kufuatiliwa kwa ukaribu.
Akiwa amekipita kituo cha mwenge akaendelea kutafakari huenda pia kuna anayehusika katika jeshi la polisi
"Ndio" akajinong'oneza "iweje aweze kuua mashahidi ambao wataniwezesha kumpata muuaji?"

akaanza kuuondoa uaminifu kwa jeshi la polisi. Akatafakari mishahara midogo wanayoipokea inaweza ikawafanya kupokea rushwa za kuwarubuni na wao wakazitoa siri zote. Akaendelea kuamini kuwa ni mmoja kati ya mapolisi hao anamfahamu muuaji na kutoa siri zote. 'eva amekwisha uawa. Omary pia ameuawa' hapo akamkumbuka pia na mfaume.

Akaiegesha gari yake pembezoni mwa pub ya GQ, kuna gari aina ya IST nayo ikaegeshwa mbali kidogo.
Vannesa alikwishaiona.

Alihisi muda mrefu ikimfuatilia sasa hakujitia tena uzembe naye akataka kuanza kumfuatilia yeye anayemfuatilia. Akaingia ndani ya pub ya GQ na kuelekea moja kwa moja kaunta. Akapokelewa kwa tabasamu na msichana aliyenyuma ya nondo za kaunta hiyo.

"Naitwa Vannesa"

"Nakukumbuka Afande" alijibu haraka haraka yule msichana "nikupe nini" Vannesa hakupenda kuitwa Afande ndio maana akatabasamu kwa hasira. Akampinga kabla hajaagiza sprite.

"Mimi sio afande ila nahitaji kufahamu jambo"

"Jambo lipi hilo dada Vannesa?"

Msichana yule wa kaunta aliitwa Zainabu. Vannesa akaieleza shida yake juu ya kumtambua muuaji wa Eva. Zainabu alionesha kuna jambo alikuwa akilifahamu, akamueleza Vannesa yote kuhusu Moses wa kikongo aliyezungumza lafudhi ya kifaransa. Alieleza jinsi alivyo, hata kuahidi kumfahamu endapo angemuona mara ya pili.

Zainabu akawa ametimiza furaha ya Vannesa na kumfanya kuondoka. Gari ya Vannesa ilipokuwa ikiipita gari ambayo alihisi ilikuwa ikimfuatilia, alimshuhudia mvulana akibadilishana mate na msichana fulani mwenye asili ya kiarabu. Akairudisha barabarani gari yake na kurudi Masaki kwenye apartment ya McCuthbert.

Huko alifuata mkanda wa video uliorekodi matukio yote ya mgeni aliyeingia ndani ya nyumba hiyo. Japo dhumuni la kamera hizo, zilikuwa kupiga picha za watu ambao walitaka kufanya uhalifu kwa wageni watakaolala ndani ya nyumba hiyo.

Vannesa akaiendesha gari yake kwa uangalifu zaidi. Alifuatilia kuitazama gari ile aliyoiacha pale Gq, haikuwepo.

Wasiwasi huo ukamshitua kuitazama kila gari na chombo cha usafiri. Ndipo vinyweleo vikamsimama alipohisi bajaji iliyokuwa ikimfuatilia kwa muda mrefu, ikiambatana naye kila alipokuwa anaenda mara alipokiacha kituo cha bamaga sheli.

Hata alipofika jirani na apartment aliyokuwa anaifuata, hakushuka. Aliichunguza bajaji ile ilipokuwa inaelekea. Haikusimama kama alivyotarajia. Bajaji ile iliendeshwa na mzee wa makamo aliyesahau matumizi ya kiwembe juu ya kidevu chake. Bajaji ikampita pale pale na kutokomea.

Vannesa alishuka na kuiendea apartment ile. Ikawa rahisi kwa kuwa alikutana na mke wa McCuthbert, alifahamiana naye siku ya msiba wa mumewe.

Akaieleza shida yake na hakukuwa na kikwazo. Kwa kutumia kompyuta ya mapajani, walizitoa cd ndani ya kamera zile na kuzichomeka kwenye deki ya kompyuta. Picha iliyoonekana ndani ya cd ile ikamfanya Vannesa kuhamaki.

Hasira zikampanda na kumfanya aropoke

"Haiwezekani"


ITAENDELEA!!!!!...........
 
Tupe vitu mizambwa... hii kitu inaelekea kuwa ulevi wangu sasa. Dah.... nomah sanah
 
Tupe vitu mizambwa... hii kitu inaelekea kuwa ulevi wangu sasa. Dah.... nomah sanah[/QUOTE

simulizi inazidi kukolea, though sijaelewa msiba wa bertha umeishaje, pja connectionvya moses huyu muuaji na moses simba aliyekuwa anatumiwa na raymond. big up mizambwa soon muuaji anaenda kukamatwa
 
Tupe vitu mizambwa... hii kitu inaelekea kuwa ulevi wangu sasa. Dah.... nomah sanah[/QUOTE

simulizi inazidi kukolea, though sijaelewa msiba wa bertha umeishaje, pja connectionvya moses huyu muuaji na moses simba aliyekuwa anatumiwa na raymond. big up mizambwa soon muuaji anaenda kukamatwa

Tutaona huko mbele connection yao ilivo... ngoja tumsubir director mizambwa
 

HADITHI: KIVULI CHEUSI

SEHEMU YA KUMI NA TATU

TULIPOISHIA....

Wasiwasi huo ukamshitua kuitazama kila gari na chombo cha usafiri. Ndipo vinyweleo vikamsimama alipohisi bajaji iliyokuwa ikimfuatilia kwa muda mrefu, ikiambatana naye kila alipokuwa anaenda mara alipokiacha kituo cha bamaga sheli.
Hata alipofika jirani na apartment aliyokuwa anaifuata, hakushuka. Aliichunguza bajaji ile ilipokuwa inaelekea. Haikusimama kama alivyotarajia. Bajaji ile iliendeshwa na mzee wa makamo aliyesahau matumizi ya kiwembe juu ya kidevu chake. Bajaji ikampita pale pale na kutokomea.
Vannesa alishuka na kuiendea apartment ile. Ikawa rahisi kwa kuwa alikutana na mke wa McCuthbert, alifahamiana naye siku ya msiba wa mumewe. Akaieleza shida yake na hakukuwa na kikwazo. Kwa kutumia kompyuta ya mapajani, walizitoa cd ndani ya kamera zile na kuzichomeka kwenye deki ya kompyuta. Picha iliyoonekana ndani ya cd ile ikamfanya Vannesa kuhamaki. Hasira zikampanda na ku
mfanya aropoke
"Haiwezekani"

ENDELEA..................



Moses akiwa ndani ya tafakuri nzito, ndipo alipomkumbuka McCuthbert. Rafiki yake wa muda mrefu. Alipotoka katika pub ya Gq, alimfuata katika moja ya casino zake tatu iliyopo pembezoni mwa fukwe ya bahari. Uzuri alimkuta akiwa ameshapata kilaji, hivyo hakutumia pesa yake kumlewesha.

Mazungumzo yalianza kikawaida wakijaribu kukumbushiana baadhi ya biashara zao haramu zilizowakutanisha pamoja. Ni huyo ndiye alikuwa mwenye roho ya mwisho aliyotumwa kuiangamiza na Raymond. Hakuwa akielezwa sababu ya kwanini alitumwa kuitoa roho ya fulani na fulani, alichopaswa ni kufuata oda huku pesa yake ikiwa mezani.

Alipewa kiasi cha shilingi milioni hamsini kuitoa roho ya McCuthbert. Alipewa picha na maelekezo ya namna ya kumpata. Hakujua nguvu na utajiri alionao McCuthbert. Mholanzi mwanaharamu wa madawa ya kulevya.

Siku hiyo alipomtafuta, alimkuta katika moja ya fukwe za kifahari huko kunduchi bichi. Sigara yenye moshi mzito kinywani mwake huku akiwa amezungukwa na warembo kadhaa waliofaa kuitwa walimbwende. Alikaa kistaarabu baada ya kukaribishwa kinywaji. McCuthbert akawafukuza wale wasichana mazungumzo yakaanza.

"Nimetumwa nikuue?"

Ulikuwa ni kama mzaha kwa McCuthbert. Ni nani ambaye hafahamu kiasi kikubwa cha pesa alichonacho McCuthbert. McCuthbert, akamtazama Moses kwa dharau kisha akajifanya kumuonea huruma.

Akamuuliza "kijana unajiamini nini?"

Moses alifahamu hilo hivyo hakupata shida, akamueleza yote. Akamueleza kuwa ametumwa kumuangamiza kwa dau la shilingi milioni hamsini. Akamtaja Raymond kama ndiye tajiri wake. Moses akaingiwa na tamaa ya pesa nyingi, hivyo akataka kubadilisha biashara. Akajitia kunyanyuka, uoga uliomvaa McCuthbert ukamfanya ahamaki.

Akaongea kwa pupa "unaenda wapi sasa kijana?" ikabidi awe mpole "tafadhali nahitaji kufanya biashara na wewe" Uso wa Moses ukachanua kwa tabasamu akamgeukia McCuthbert.

"Shilingi milioni 120 pamoja na kukuletea kichwa chake" Moses akadanganya hakumaanisha alichokuwa akikisema. Kutokana na kukiogopa kifo, McCuthbert akapandisha dau "milioni 150"

Moses akampa akaunti yake ya benki na huo ndio ukawa mwanzo wa kufahamiana. Japo hakufahamu McCuthbert alimtenda nini Raymond ila akamsaliti. Usaliti ule ukazaa upendo wa kudumu kati yao.

Moses akamueleza shida yake McCuthbert licha ya kujali ulevi alionao.

"Ninahitaji nyumba yako ya masaki"

"Hilo halina shaka Moses"

Akiwa anachezea chuchu za msichana fulani aliyekuwa akimchezea kifua chake

"Ngoja nimpigie Andrew akupe ufunguo"

"Hapana nipo njiani kwenda huko" Moses akasema

"Bila shaka una bibi leo" McCuthbert akabeua kiulevi huku akitoa kitita cha pesa "hadi umeshindwa kulipia hela ya hotel" kama pesa McCuthbert alikuwa na jeuri nayo haswa.

Moses akaondoka huku mipango yake ikiwa inaenda sawa. Huko alikutana na Andrew pamoja na wasaidizi wengine. Hakuwa na wasiwasi nao kwa kuwa yeye ni zaidi yao. Yeye alikuwa rafiki wa karibu wa mmiliki wa apartment hizo, amuogope nani ikiwa ufunguo alikuwa nao? Simu ilikwishapigwa kwao na waliufahamu ujio wake, hivyo hakuogopa juu ya maswali ambayo angeulizwa nao.

Alikuwa huru kufanya lolote.

Alipishana nao nje ya nyumba ile baada ya salamu na kuingia ndani. Huko aliutumia utundu kidogo kugundua ulipo moyo wa kamera zote zilizofungwa katika nyumba hiyo. Aliukata waya fulani uliosaidia kuonesha picha na kuacha ule wa sauti.

Akauchomeka waya wake aliokuja nao huo haukuwa na kazi ya maana lakini ulikuwa maalumu. Umuhimu wa waya ule ni kuonesha kivuli peke yake baadala ya picha kamili. Akaujaribu na kutazama. Picha ya nje mara baada ya kuufunga, vilikuwa ni vivuli pekee. Akatabasamu kwa furaha huku akiamini ameupoteza ushahidi wa mauaji kabla hajayafanya.

Akatokomea baada ya kuweka kila jambo sawia ndani ya nyumba hiyo.

XXXXX


Hali ya kuikosa picha ya mgeni aliyeongozana na mwanamke aliyeuawa, ilimchanganya sana. Video ilipoanza, Vannesa macho yalimtoka haswa. Shahuku ya kujua sura ya muuaji, ikawa inampeleka puta pumzi zake. Mke wa McCuthbert naye akajawa na shahuku

huku wakiitazama kwa mara ya kwanza pamoja na Vannesa. Video haikuwa video kama walivyotegemea, bali video iliyokosa uhalisia. Vilionekana vivuli tu badala ya taswira kamili ya
mwanadamu. Hakuna aliyepatwa na wazo lolote juu ya kufahamu au kuyagundua maumbo ya vivuli vile.

Vannesa akahamaki

"Haiwezekani"

Akamgeukia Andrew ambaye pia alikuwa amechanganyikiwa kupita kawaida.

"Mchezo gani huu?"

kigugumizi cha kustaajabu, kikamponza Andrew. Vannesa akaanza kuhisi huenda Andrew anahusika juu ya hilo. 'pesa' akazidi kufikiria uwezo wa kipesa alionao muuaji au wauaji. Harufu ya kuwa makini, ikasumbua fikra zake.

"Sifahamu chochote mimi jamani dada Vannesa"

Andrew akajitetea lakini hakuaminika. Vannesa akampigia simu Jafari Hiza. "naomba uje umchukue huyu kijana hapa kwa McCuthbert Hana analolitoa nikamuelewa.. Ndio.. Kijitonyama hapa hapa"

Baada ya kukata simu, akaaga.

"Sina uwezo wa kukukamata kwa kuwa mimi sio askari lakini nadhani maafisa watafanya kazi yao"

Alipotoka nje, akaelekea kwenye gari yake huku mawazo ya mzee mwenye bajaji yakimyeyuka.
Alipoufungua mlango wa gari yake, simu ikaita. Juu ya kioo mpigaji alikuwa ni Moses, Vannesa akahifadhi namba ya Moses "Honey" Alitabasamu. Akaipokea kwa sauti ya
madeko

"mpenzi... Nipo kijitonyama.. Uko wapi?... Kwa hiyo nikufuate ulipo... Kwanza nimechukia... Kwanini tangu asubuhi hujanitafuta? .. Anha.. Haya ninakuelewa mpenzi. Nakupenda.. Nipo njiani.."
vannesa akaiwasha injini na kuingiza gari barabarani.

XXXXX


Baada ya kufahamu kile kilichomfanya aamue kuingia ndani ya hotel ya New Africa, sasa hata kahawa Aliyoiagiza hakuitaka tena. Alitoka nje kwa mwendo wa kukimbia huku akihisi kama alikuwa anachelewa.
Bahati ikawa kwake.

Mpaka alipotoka nje, ikawa ndio Vannesa anatoka akiwa amesimama na Naima pembezoni mwa gari lake Vannesa. Alifahamu fika Vannesa alikuwa anatoka. Akapiga simu kwa mshirika wake mmoja wanayefahamiana. Yeye aliitwa Chanduru. Alikuwa akikodisha gari zake kwa ujira mdogo. Chanduru hakujali juu ya kazi ambayo gari yake ilienda kufanyiwa. Pesa kamili mezani na masharti ya gari lake kurudi salama. Kwa kuwa Moses na Chanduru ni marafiki wa muda mrefu, wakaaminiana.

Moses akamuomba Chanduru dereva wa kike. Dakika chache kabla Vannesa hajaondoka, gari
ya Chanduru iliingia. Aliyeiendesha ni msichana mrembo aliyetumiwa katika biashara haramu kadhaa. Alikuwa Meriana. Wakati ambao anaingia yeye na ndipo gari ya Vannesa ilikuwa inaondoka. Akaingia ndani ya gari harakaharaka. Hawakusalimiana na Meriana akazungumza kama hayawani

"Ifuate, ifuate" Meriana hakufahamu chochote. Alikuwa akigeuka huku na kule akitafuta gari hili na lile.

Hakuelewa.

Akauliza "Nifuate nini?" gari ya Vannesa ikawapita mbele yao.

Moses akanyoosha mkono lilipokuwa likitokomea kuitafuta barabara ya bibi titi. Meriana akaliacha gari moja likiwa katikati ya gari ya Vannesa na gari yake.

Akamuuliza Moses "lakini tunalifuata gari ile kwa nini?"

"tangu lini ukauliza juu ya kazi isiyokuhusu?" alimgeukia na kumwambia "kazi yako ni kuendesha gari na kufanya ninachokuagiza"

Gari ya Vannesa ilipokipita kituo cha Mwenge, gari zao zikawa zinafuatana. Ni hapo Vannesa alipoanza kuhisi kuwa alikuwa anafuatiliwa. Mpaka Vannesa alipoikunja gari yake na kuingia barabara ya sinza. Moses akaongea usikunje kona kwanza" mwendo wa gari aliyokuwa akiiendesha Meriana ukapunguzwa. Gari ya Vannesa ikakunja kona iliyo pembezoni mwa bar ya Hongera.

Moses akamwambia tena Meriana "Ifuate"

Meriana akaifuata gari ya Vannesa ilipokuwa inaelekea. Moses alikwisha gundua kuwa gari ya Vannesa ilikuwa ikielekea Gq pub. Kwa mbali aliiona ikiwa imesimama sehemu ya maegesho. Mita chache yaani miguu kumi kutoka walipo akamuamuru Meriana kusimama.

Walikaa kwa zaidi ya dakika thelathini, Moses akamuona Vannesa akitoka. Akamvuta Meriana na kuanza kubadilishana naye mate. Kitendo hicho kikamshangaza sana Meriana. Lakini ikawa ni sehemu ya njama za Moses. Moses alifahamu Vannesa asingekuwa mjinga. Mjinga wa kutofahamu alikuwa akifuatiliwa. Hiyo ilitokana na kuwa hakuwa akimuamini tena Vannesa. Wasiwasi ulikuwa kwenye fikra zake kuwa Vannesa alikuwa akimfuatilia yeye. Alikuwa akimtafuta kutokana na mauaji aliyokuwa akiyafanya. Alikuwa na uhakika kuwa Vannesa ni mpelelezi mwenye kunusa hatua zake.

"Hawezi kuharibu mipango yangu ni lazima nimuue Raymond"

Gari ya Vannesa ikatokomea. Wakiwa njiani kumfuatilia Vannesa ndipo Moses akayabadilisha mavazi yake. Gari ya Vannesa ikawa umbali wa magari matano mbele ya gari la Meriana na Moses. Moses akamuacha Meriana mara walipofika posta, Meriana alicheka sana.

"umefanana na wazee kabisa"

Moses alikuwa amejibadilisha muonekano wake na kuwa mzee aliyechoka sana. Akairukia moja ya bajaji zilizojipanga pembezoni mwa bank ya NBC. Dereva wa bajaji hiyo alishangaa kumuona mzee aliyeifuata bajaji yake kwa pupa, Kitita cha noti za shilini elfu hamsini kikamchanganya. Akaenda kila alipokuwa akielekezwa na mzee ambaye alihisi kuwa hana pesa hapo mwanzo wakati anaipanda bajaji yake.

Bajaji aliyoipanda Moses ikaifuata nyuma gari ya Vannesa. walipokipita kibonde kilichokuwa kikiwaletea mihemko wasafiri wengi waliokipita, akatambua alipokuwa akielekea Vannesa.

Akaendelea kumfuata nyuma huku akiamini kuwa Vannesa anahitajika kufa kabla hajapata anachokitafuta. Akaliona gari la Vannesa likiwa linaegeshwa mbele ya nyumba aliyomuua Eva ndani yake.

Akazungumza na dereva wa chombo kile "naomba ushuke" Dereva akahamaki

"Unasemaje wewe?"

kitita cha noti za shilingi elfu kumi zaidi ya saba zikamfanya kumuachia ufunguo wa bajaji mzee yule asiyemfahamu. Alimuachia lakini kwa miahadi ya kuchua taksi ambayo itamfuatilia mpaka atakapomkabidhi bajaji yake kwa shughuli yake binafsi anayotaka kuifanya peke yake.

Moses akaipita gari ya Vannesa. Huko alikaa kwa muda mrefu akifuatilia ni saa ngapi Vannesa angetoka.
Akiwa amesubiri kwa muda mrefu, ndipo akamuona Vannesa akitoka, akaamua kumpigia simu. Ndiyo simu ambayo aliipokea Vannesa wakati ule ambao anatoka ndani ya apartment, baada ya kuikosa taswira ya muuaji. Alipomaliza maongezi ya kwenye simu na Vannesa, Akajinong'oneza kwa hasira

"Jioni ya leo" tabasamu la chuki likamponyoka Moses "Roho yako nitaitafuna Vannesa kama ukienda kinyume na mimi"

Baada ya Vannesa kuondoka kichwani akiwa na wazo la kwenda kumuona Mfaume, alichokiwaza Moses; ni muendelezo wa mauaji yake. Baada ya gari la Vannesa kutokomea na kutoonekana kabisa, akajitokeza na kusimama kabisa karibu na gari la Vannesa lilipoegeshwa mwanzo. Taswira aliyo nayo ni ile ile ya kizee. Hakuna ambaye angemfahamu kwa taswira hiyo. Akajipa uhakika wa kuingia ndani ya nyumba hiyo kummaliza Andrew. Kummaliza Andrew ingekuwa ni kuufuta ushahidi wake.

Alikagua ilipo sumu yake ambayo alitegemea kuitumia kwa Andrew na kuipata katika mifuko ya suruali yake. Akatazama huku na huko, kisha akagundua kuwa hakukuwa na mtu; akaingia ndani ya nyumba aliyotoka Vannesa dakika chache zilizopita. Alipogonga akakaribishwa na mke wa McCuthbert.

"Oh! Nani wewe" kabla Moses hajaingi, mke huyo aliuliza.

Muonekano wa Moses haukuonesha hata punje kama alikuwa ni mteja wa kuhitaji nyumba hiyo. Andrew naye aliliacha kochi na kujisogeza mlangoni. Alipomuona Moses, akacheka. "Unataka nini babu?"

Moses alikohoa mfululizo huku akijitia kucheka kizee. Akazungumza kwa sauti ya mikwaruzo
"Nahitaji nyumba ya kulala" akiwa analitafuta kopo lake mfano wa manukato mazuri akawauliza kwa hila "au kisa mnaniona mimi ni mchafu na ndio maana mnadhani sina fedha? Au kwa sababu nguo zangu zinanuka na mnadhani kuwa sina manukato ya kunukia?" akatoa kopo lake na akajipulizia kwenye nguo zake kuu kuu kwa hila.

"Hamnikaribishi ndani?" Akauliza huku tabasamu la ushindi likimponyoka.

Hakujibiwa, kimya kilichokaribishwa na kishindo cha miili ya Mke wa McCuthbert na Andrew ikaisalimia sakafu. Moses akatabasamu baada ya kuona wakidondoka chini kama gunia. Akaitema kitu alichokuwa akikitafuna mfano wa plastiki aliyokuwa akiitafuna tafuna wakati aliokuwa akijipulizia sumu ile iliyo ndani ya kopo la manukato.

Akaiingiza miili ile ndani.

Wakati ambao alikuwa akifunga mlango, aliona magari ya polisi yakija katika mtaa ambao nyumba ile ipo. Akayavua mavazi yale na uzee wake, kisha akarudi katika hali ya ujana. Alikumbuka ndevu za bandia ambazo zingewapumbaza wachache ambao wangemuona ni kijana wa kawaida anayevutia. Akajificha juu ya paa, ndani ya dari kutokana na uzoefu wake ndani ya nyumba hiyo aliijua sehemu gani ya kuingilia.
Akiwa ndio kwanza anafunika tu mfuniko wa kumruhusu kujificha vizuri darini, mlango wa nyumba hiyo nayo ukafunguliwa. Alisikia sauti tu "Imekuaje?" Sauti ya mmoja wa walioingia ndani, ikauliza.

Hiyo ilikuwa ni sauti ya Inspekta Jafari Hiza. Moses akaisikia sauti ya mwingine ikijibu
"Hawapumui mkuu" Jafari hiza akawa ameshika nguo za Moses na madevu yake ya kizee. Akiwa katika kutazama chini ya paa alimojificha kupitia tundu dogo lililoachwa kimakosa na fundi wa paa hilo, Jafari Hiza alikuwa akipiga simu kwa Vannesa.

"Halo Vannesa?" Moses akasikia sauti ya Jafari Hiza japo hakumfahamu, akiliita jina la Vannesa. Jafari Hiza akaendelea baada ta simu kupokelewa "Ndani ya nyumba ya McCuthbert ulitoka saa ngapi?... Kuna mauaji ya utata zaidi yametokea... Kuna mwanamke na yule Andrew tuliyekuwa tumekuja kumchukua.. Vitu.."
Kabla Jafari Hiza hajamaliza kuzungumza, kutoka katika moja ya makoti ya kizee aliyoyaokota chini chupa ile yenye sumu ikadondoka.

".. Jafari.. Jafari"

Ilikuwa ni sauti ya Vannesa ikikoroma ndani ya spika za simu ya Jafari Hiza. Aliita bila kupokelewa upande wa pili mpaka alipoanmua kuikata simu yenyewe. Jafari Hiza akaiokota chupa ile kwa uangalifu huku akiwa amevaa gloves. Alipotaka kuipuliza, mmoja wao ambaye ana aina ya udaktari ndani yake ambae pia ni mpelelezi akamzuia.

"Hatujajua bado kifo cha hawa watu wawili, huenda ikawa ni sumu"

Wazo hilo likapita ndani ya fikra za Jafari Hiza. Kila kitu ndani ya nyumba hiyo kikaokotwa kama kithibitisho na kwenda kupimwa. Miili ya Andrew na mke wa McCuthbert ikabebwa kwenye gari maalumu la hospitali lililoitwa punde na kwenda kuhifadhiwa mochwari. Jafari Hiza pamoja na jopo lake walipotaka kutoka, kuna kijana akawazuia. Alikuwa ni yule dereva wa boda boda.

"wewe ni nani?" Jafari Hiza aliuliza.

"Kuna babu namtafuta ameingia humu mimi ni dereva wa bodaboda"

Mwili wa Jafari Hiza ukamsisimuka, vinyweleo vikamsimama kuhisi kuwa muuaji wanayemtafuta hakuwa mbali. Aliwaamuru askari wake wamsake mtu yeyote ambaye angeonekana kuwa ndani ya nyumba hiyo na kumtia nguvuni.

Msako uliendeshwa kwa dakika ishirini zaidi. Hakuna kilichopatika na zaidi ya kila kitu kutolewa katika mpangilio wake maalumu. Jafari Hiza akaondoka na yule dereva wa boda boda kwa ajili ya kumsaidia yeye katika upelelezi wake.

XXXXX

ITAENDELEA............
 
pokea like hizoo
:thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup::thumbup:
 
HADITHI: KIVULI CHEUSI

SEHEMU YA KUMI NA NNE

TULIPOISHIA....

“wewe ni nani?" Jafari Hiza aliuliza.
"Kuna babu namtafuta ameingia humu mimi ni dereva wa bodaboda"
Mwili wa Jafari Hiza ukamsisimuka, vinyweleo vikamsimama kuhisi kuwa muuaji wanayemtafuta hakuwa mbali. Aliwaamuru askari wake wamsake mtu yeyote ambaye angeonekana kuwa ndani ya nyumba hiyo na kumtia nguvuni.
Msako uliendeshwa kwa dakika ishirini zaidi. Hakuna kilichopatika na zaidi ya kila kitu kutolewa katika mpangilio wake maalumu. Jafari Hiza akaondoka na yule dereva wa boda boda kwa ajili ya kumsaidia yeye katika upelelezi wake.

XXXXX

ENDELEA..................



Vannesa akawa amechelewa zaidi ya dakika nyingi mpaka kufika masaki ilipo nyumba ya kupanga yalipofanyika mauaji mengine. Hakuwakuta wakina Jafari Hiza.

Lakini Moses pia hakuwa mbali na eneo hilo. Alikuwa sehemu ambayo alijificha mara ya kwanza na boda boda ile ya kijana aliyeondoka na Jafari Hiza. Alikaa hapo baada ya sekunde chache alizotoka juu ya dari alipojificha mara baada ya jafari Hiza na wenzake kutokomea.

Alimuona Vannesa wakati akijaribu kukigusa kitasa cha mlango huo lakini hakikufunguka. Yeye akakumbuka alivyotokea ndani ya nyumba hiyo kupitia dirisha la jikoni. Alimuona akihangaika kurudi kwenye maegesho ya magari.

Akaamua kumpigia simu.

Aliongea kwa upole akijaribu kumchota kujifanya tayari yupo ndani ya chumba cha hoteli.

"Mpenzi uko wapi... Kazini hadi saa moja ya jioni?..

Ni chombo gani cha habari kinakunyanyasa kiasi icho hakikupi muda wa kupumzika na mwenza wako?.. Nakuhitaji bwana sasa hivi.."

Kutokana na tabasamu la Moses alilotoa baada ya simu kukatika ikaonesha kuwa Vannesa alimpa jibu zuri. Akajiambia huku akiingia barabarani kuita taksi itakayomrudisha kinondoni ndani ya hoteli aliyolala yeye na Vannesa

"Vannesa"

Taksi ikawa imesimama kama ndiye Vannesa. Alipofungua mlango na kuufunga akamwambia Dereva

"Nipeleke Kinondoni"

"Shilingi elfu kumi na tano"

"Nitakupa ishirini" dereva alipomgeukia, Moses akamwambia huku akitabasamu "naomba ipae"
Maneno hayo hayakumsumbua dereva yule akaziingiza gia kwa fujo na kumuonesha mteja wake yeye ni zaidi ya madereva wa magari ya mashindano.

Moses akamalizia wazo lake "Lazima nikuue"

Akacheka kifedhuli mpaka dereva akashangaa. Taksi aliyopanda Moses ikafika mpaka kwenye hoteli hiyo. Kwenye maegesho ya magari, gari la Vannesa halikuwepo. Moses akamlipa dereva ujira wake kisha aliifuata lift ya hotel hiyo kivivu. Alibonyeza gorofa namba tatu, kilipo chumba chake. Akaingia chumbani kwake kwa kadi maalumu. Milango ya hotel hii, haikuwa na funguo.... Kadi hiyo hiyo ilitumika pia kuwashia taa.

Ufahari, ufahari haswa.

Akiwa amejipumzisha, akamuwaza sana Vannesa. Kuna nafsi ilimwambia kuwa bado mapema kumuua, kuna nyingine ikamwambia akichelewa kumuuwa basi roho yake ni ya Vannesa. Hakutaka hilo litokee. Akanyanyuka kama amepigwa na shoti ya umeme. Akiwa ndio kwanza anasimama, simu yake ikaita.
Aliitoa haraka kumtazama mpigaji.

Simu hiyo ya mkononi, aliisajili kwa jina la bandia na wala hakuna aliyeifahamu. Ni simu ambayo ameinunua kwa kazi hii nzito ya kulipiza kisasi. Kisasi cha kuitafuta roho ya Raymond pamoja na watu wake wa karibu wanaomuhusu. Alipoitazama simu iliyokuwa inaendelea kuita, juu ya kioo alikuwa ni Vannesa.

"Habari mpenzi.. Upo sehemu gani?.. Sawa nakusubiri mpenzi.."

Kisha simu ikakatwa. Moses akalitoa tabasamu la shetani tabasamu lililoudhi kulitazama. Akaiendea moja ya mifuko katika begi lake alilokuja nalo, akaitoa ile nyongo ya mamba. Ilikuwa inakaribia kuisha, lakini alikuwa na hakika kuwa kwa unga huo mdogo ndani ya juice ingetosha kuupokonya uhai wa Vannesa.
Akiwa amemaliza kuagiza juice kupitia kwenye simu ya chumbani hapo. Aliingia bafuni kuoga. Alipomaliza, mlango nao ukawa unagongwa. Akajifuta maji huku akiwa na taulo kiunoni, akaufungua mlango.
Alikuwa ni Vannesa.

Macho yake Vanessa yakanasa juu ya kifua cha Moses. Ndiyo walikwishalala pamoja, lakini hakupata nafasi ya kukiona sawia kama sasa waliposimama pamoja mlangoni. Vannesa japo alikuwa mchovu, hakujali yote. Alizivamia papi za Moses na kuanza kubadilishana mate. Moses naye alimbeba na kumuingiza ndani. Huko nako mchezo wa kubadilishana mate uliendelea kwa muda mrefu zaidi mpaka Vannesa alipokuwa mtupu kabisa. Moses naye akalitupa taulo pembeni, wakaanza kucheza michezo ya kuchezeana viungo kadhaa katika miili yao. Nusu saa baadaye wote wakawa hoi.

Moses ndiye akawa hoi zaidi.

Kilichobaki akawa anamuhitaji Vannesa, hakutaka tena kusubiri. Alipotaka kumuingilia kimwili, Yule muhudumu wa Juice alikuwa mlangoni akigonga mlango. Moses akajifunga taulo akiwa na hasira kupitiliza. Alizipokea juice zile na kuziweka mezani. Akarudi kitandani alipojilaza Vannesa. Michezo ikaendelea. Safari hii alipotaka tena kumuingilia Vannesa,

Vannesa akamwambia kwa sauti nyororo ya upole "Unaonaje tukioga pamoja kwanza mpenzi?"

Kama mbuzi wa hitima, Moses akakubali. Waliingia bafuni wakaoga, huku wakiogeshana kila mmoja akitumia mikono yake kuchezea kila kiungo cha mwenzake kwa ustadi mkubwa. Hakika kila mmoja akawa hajiwezi tena.
Si Vannesa wala Moses.

Wakaliacha bomba la mvua na kurudi tena kitandani. Moses alikuwa kiboko kwenye nyanja ya mapenzi. Alijua kumdatisha Vannesa mpaka Vannesa akapiga ukunga wa raha. Vannesa naye si kwamba alilala kama gogo. Alijitahidi kukumbuka miaka ya nyuma alipokuwa na mpenzi wake Amani. Yeye ndiye alimfundisha mapenzi, yeye ndiye aliyemfundisha hiki alichokuwa anamfanyia Moses. Moses licha ya ukatili na ujasiri wake mtaani, Vannesa akawa mshindi wa kumtoa chozi. Hakulia kwa huzuni bali kile kilio cha raha.

Saa tatu usiku Moses alikuwa amelala fofofo. Vannesa alijinyanyua taratibu na kuingia bafuni. Huko aliingia kuoga. Bomba la mvua, ikawa limemuamsha Moses. Moses akawa amekumbuka kuwa aliumwaga ule unga wenye sumu kwenye juisi akiwa pale mlangoni bila Vannesa kumuona.

Nafsi yake ikakataa kabisa kumuangamiza Vannesa. Kutokana na penzi zito alilolipokea kutoka kwa Vannesa dakika chache zilizopita, akajiambia

"Hapana" akasimama huku akijifunga taulo "nitamlinda milele aendelee kunipa furaha ya mapenzi"

Vannesa akawa anatoka bafuni.

Wakakumbatiana tena, Vannesa akasema kwa sauti ya huba
"Nakupenda mpenzi" Kutoka moyoni Moses akajibu kwa dhati "Nakupenda sana Vannesa"

Walipoachiana, Vannesa akaifuata mojawapo ya glass ya juice.

"He! Kumbe kuna juice hapa"

Moyo ukamlipuka Moses. Alipomuona Vannesa akiichagua juice ileile aliyoimwagia unga wa sumu, akashindwa kujizuia.


ITAENDELEA............
 
Nooooooooooooooooooooooooo Vanessa!!!!!!!!!!!!!!!!! usinywe you will die, bado hujamaliza kazi mpenzi
 
Back
Top Bottom