Hadithi: "Kivuli cheusi"

Hadithi: "Kivuli cheusi"

Tupe vitu mkuu.. yani ata nikiwa na usingiz nkishaanza kuisoma hii stor usingiz unakata... ni kama muv yaani.. Respect sana mh. mizambwa
 
HADITHI: KIVULI CHEUSI

SEHEMU YA KUMI NA TANO

TULIPOISHIA....


Wakakumbatiana tena, Vannesa akasema kwa sauti ya huba
"Nakupenda mpenzi" Kutoka moyoni Moses akajibu kwa dhati "Nakupenda sana Vannesa"

Walipoachiana, Vannesa akaifuata mojawapo ya glass ya juice.

"He! Kumbe kuna juice hapa"

Moyo ukamlipuka Moses. Alipomuona Vannesa akiichagua juice ileile aliyoimwagia unga wa sumu, akashindwa kujizuia.


ENDELEA...........



"Mpenzi hiyo ya ukwaju ninmeichagua mimi"

"Lakini mpenzi"

Bila Vannesa kumalizia alichoanza kukisema, hakutegemea kilichotokea. Mkono wake ulipigwa kikumbo na glass ya juice ikamponyoka. Ikawa kama bahati mbaya na Moses ndivyo alivyoigiza.

Sumu iliyo ndani ya juice ikamwagilka, hivyo roho ya Vannesa ikapona.

Moses aliingia bafuni akaoga kisha wakajiandaa na Vannesa kwenda kupata chakula katika mgahawa wa hoteli hiyo.
Wakiwa huko majira ya saa nne usiku, simu ya Vannesa ikapata uhai.

Mpigaji alikuwa Jafari Hiza.

*****

Baada ya upimwaji wa vifaa ambavyo vilikutwa ndani ya nyumba ya McCuthbert. Ili
pimwa ile sumu iliyowekwa ndani ya chupa ya manukato. Sumu ambayo ni hatari sana kwa binadamu. Sumu iliyotengenezwa kwa kuchukua mate ya nyoka aina ya kobra anayejulikana kwa jina la egyptian cobra.
Sumu ya nyoka huyo inajulikana kwa jina saikrotiki.

Sumu hii huaribu mfumo mzima wa ubongo wa kati na kusimamisha mfumo wa upumuaji. Historia ya nyoka huyo hata kuitwa jina hilo ni kwa sababu alimng'ata malkia wa misri aliyeitwa Cleopatra.

Daktari mkuu katika idara ya upelelezi akatoa ripoti ya kifo kilichosababisha watu wale wawili kufa. Ikapimwa pia ile plastiki ambayo Moses aliitema pale mlangoni. Ikagundulika ni dawa ambayo ilizuia sumu hiyo. Mtafunaji wa plastiki ile aliitafuna ili tu sumu ile isimdhuru. Jafari Hiza alimpigia simu Vannesa kumpa taarifa hiyo.

"Tunaweza kuonana?"

"Hapana Hiza. Kuna nini tena" Vannesa alijibu upande wa pili wa simu, huku Moses akimkodolea macho kwa umakini.

"Kuna ripoti juu ya chanzo cha kifo cha yule mke na kibaraka wake waliokufa kule masaki"

Macho yakamtoka pima Vannesa, lakini akajizuia kutojionesha hofu yake mbele ya Moses.

Akajibu kiutulivu "Tunaweza kuonana pale pale kwenye meeting point yetu"

Simu ikakatwa Jafari Hiza akachukizwa na tabia mpya aliyoianzisha Vannesa. Tabia ya kutojali kabisa kazi tofauti na zamani. Si kweli kwamba Jafari hiza alichukizwa tu na tabia ya Vanessa pia alitamani kesi hii isiishe mapema ili imuweke karibu na mwanamke huyu. Ilikuwa ni hatari kugundulika kama Jafari hiza alikuwa akimtumia mtu mwingine tofauti na aliyeajiriwa katika kitengo cha usalama wa taifa, lakini yeye hakujali kwa kuwa alimuhusudu sana Vanessa.

*****

Baada ya kumaliza chakula mgahawani, Vannesa na Moses waliongozana pamoja mpaka chumbani. Vannesa hakukaa zaidi kitandani akiwa macho. Usiku ulikuwa mnene uliomlevya, akalala fofofo.

Moses hakulala wala usingizi haukuonekana kuwa karibu na kope zake. Akajiegesha kwenye kiti kilicho pembezoni mwa meza ndogo ya duara. Aliiacha whisky iliyomuunguza koo, akachomoa kasha lake la sigara nene. Aliiwasha ya kwanza huku akiuvuta moshi wake taratibu.

Tafakuri zake zikaingia huruma. Aliwaza ni damu za wangapi zimeingia katika mkondo usiofaa. Mkondo wa kulipiza kisasi kwa ajili ya damu ya baba yake aliyemlea kwa muda mrefu. Alimlea akidhani kuwa ndiye baba yake mzazi. Alimuua kwa mkono wake bila kufahamu kuwa alikuwa akitoa uhai wa mtu muhimu katika maisha yake. Alitoa roho ya pamela kwa hila zake za kutoa siri kutokana na mauaji ya Bertha.

Wa pili akawa Omary aliyefuatiwa na Eva kabla hajaitoa roho ya McCuthbert hatimaye za wawili ambao ni mke wake McCuthbert kisha Andrew.

Vifo vyao visingemtia uchungu Raymond ndio maana akaona ni vifo visivyo na thamani katika mipango yake. Alikumbuka jinsi ambavyo alimfahamu Raymond. Kipindi hicho alikuwa bado mtoto sana.

Alikuwa ameimaliza elimu yake ya msingi akisubiria majibu ya kumpeleka shule ya sekondari.

Mama yake alishindwa kupumua kwa kutumia mashine akiwa mgonjwa mahututi, mauti ukampokonya roho yake.

“Inasemekana aligongwa na gari kwa makusudi” Mashuhuda ajali hiyo walisema.

Haikujulikana ni nani alimgonga hivyo hakukuwa na mtu wa kumuhukumu. Kwa kuwa mzee Carlos alikuwa na urafiki wa karibu na Raymond, hata katika msiba wa mke wake Carlos alikuwepo pia. Huko ndipo alipofahamiana na Raymond. Hapo ndipo zile siku mbaya anazozichukia mpaka leo ndio zilipojizaa.

Raymond alijiweka karibu na familia ya Moses kama rafiki wa Carlos, mzee tajiri aliyemlea Moses tangu akiwa mdogo kipindi hicho Bi Tunu mama yake Moses amekataliwa mimba na kufukuzwa nyumbani na mwanaume. Mwanaume ambaye Carlos alimfahamu fika na Bi Tunu hakumueleza Moses hata alipokuwa mpaka anakufa.

Hivyo ikamfanya Moses kuamini Carlos ndiye baba yake.

Aliendelea kuishi huku akimuona Raymond kama rafiki wa karibu na Carlos. Ikafika ile siku Raymond alimtembelea shuleni na kumuomba afanye naye biashara

"Baba"
Alimuheshimu na kumuita hivyo kwa kuwa alikuwa mtu wa karibu na Carlos "mimi bado mwanafunzi nitafanya biashara gani na wewe mzee wangu?"

Raymond alicheka na kumwambia "mimi huwa sikosei katika maamuzi yangu ndiyo maana nimekufuata wewe. Kama upo tayari kuungana na mimi katika biashara yangu nitafurahi ukinijuza mapema"
Raymond akaondoka huku akimuachia kitita cha pesa ambazo hakuwahi kutegemea kuzishika licha ya utajiri mkubwa alio nao Carlos, baba yake.

Zilikuwa ni shilingi milioni moja.

Wakati akiendelea kukumbuka yaliyopita, sigara ikawa imezima ikiwa mdomoni kwake. Akachomoa kasha na kuiwasha nyingine. Akaendelea kuzama zaidi katika mawazo yake. Alikumbuka jinsi alivyojiingiza rasmi katika biashara haramu za madawa ya kulevya bila Carlos kufahamu. Biashara hiyo ikaendelea mpaka alipokuja kufahamu kuwa hata makampuni ya baba yake Carlos, pamoja na utajiri wake wote ni kutokana na biashara hiyo hiyo pia. Hakufahamu kuwa biashara hiyo ndiyo iliyowaweka kwa ukaribu Raymond na Carlos. Moses akaendelea na shule huku akisambaza madawa ya kulevya.

Ni ile siku alipotumwa kuua. Raymond alimtuma Moses kuua mtu. Si mtu wa kwanza kumuua kutokana na kazi alizokuwa akizifanya, lakini kwa Moses mtu huyu alimfanya hana hatia ya kumuua. Kwanza jinsi ya kumuua ilikuwa ni tofauti na watu wote ambao alitumwa kuwauwa. Mtu huyu alifungwa uso kwa kuvalishwa kitambaa fulani na ilikuwa ni usiku. Moses akaichomoa bastola yake kiunoni kila alipotaka kubonyeza kitufe cha kufyatulia risasi, moyo wake ukawa mzito.

Hakujua kwa nini.

Lakini kutokana na roho ngumu huku akihaidiwa dau kubwa la kuitoa roho ya mtu huyo na Raymond, akafanya kile kitu ambacho nafsi yake fulani ilimnong'oneza asifanye, akampiga risasi ya kifua mtu yule. Raymond na jopo lake likaondoka eneo hilo huku wakimuacha Moses akiwa anamfuata yule mtu aliyempiga risasi.

Moses hakuaamini alichokiona baada ya kumfunua kitambaa mtu yule. Alikuwa ni mzee Carlos, baba yake. Carlos alikuwa akiongea kwa shida sana huku akimueleza ukweli wote kuhusu maisha yake. Alipomaliza kumueleza roho yake nayo ikapaa.

Tafakuri hizo za Moses zilikatishwa ni kikohozi kikavu kilichomvamia Vannesa. Naye akaitupa sigara katika kasha la kuhifadhia jivu na kupanda kiutandani kulala.

*****

Raymond hakuishi kwa amani licha ya kuhisi hali ilianza kuwa shwari. Bado aliamini kuwa Kivuli cheusi alikuwa pahala fulani kajibanza akipanga jambo baya zaidi la kumfanyia. Binafsi hakujua sababu ya huyo mtu aliyejitambulisha kama kivuli cheusi kumtafuta kwa uchu kiasi hicho, lakini aliamini ni mmoja kati ya wabaya wake.

Hakuweza kuwaza kabisa kama Moses angekuwa ni mbaya wake anayeitafuta roho yake usiku na mchana. Yeye pia alimtafuta Moses kuyamaliza yale yote yaliyotokea kumsababishia kifo Carlos ambaye ni baba yake. Raymond akawa amesahau kabisa kama aliwahi kumpa mwanamke fulani ujauzito na kumfukuza nyumbani kwake. Mwanamke yule alizaa mapacha lakini mmoja kati ya watoto wale alifariki. Hakufahamu kuwa Moses ndiye mtoto wa Bi Tunu aliyemgonga na gari kwa makusudi kule maeneo ya kimara baruti na kukimbilia maeneo ya mbezi akikatisha barabara ya maramba mawili na kukimbia kesi ya mauaji hiyo ilikuwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.

Bi Tunu mwanamke aliyebeba ujauzito wake ndiye mwanamke aliyetambulishwa na rafiki yake kuwa ni mkewe. Rafiki yake wa muda mrefu Carlos. Ndiyo!! alimfukuza Tunu kutokana na ujauzito lakini si kwamba alikuwa hampendi. Alimpenda sana lakini kutokana ujana na kazi aliyokuwa akiifanya, hakuhitaji mtoto kwa wakati huo. Roho ikamuuma sana kumkuta Tunu akiwa na Carlos. Akaapa kumuangamiza Tunu na Carlos bila kujali ukaribu wao wa siku nyingi.

Ndiyo sababu alimuingiza Moses katika biashara zake akiamini kuwa Moses ni mtoto wa carlos. Hivyo angemtumia Moses kumuua baba yake. Hakufahamu siku zote hizo kuwa yule Moses aliyemuona tangu akizaliwa mpaka amekuwa ni mtoto wake aliyemkataa tangu tumboni.

Hakujua sababu ya Moses kuwa na mahusiano na Bertha mara walipokutana chuoni. Raymond akawa amelipiza kisasi kwa kuiangamiza familia ya Moses. Moses akawa ameingia katika kisasi cha kuiangamiza familia ya Raymond.


ITAENDELA............
 
Wapenzi wafuatiliaji wa Hadithi hii.

Hadi hapa bila shaka mmepata jibu kwa nini Moses anaitafuta Roho ya Raymond.

Je, atafanikiwa kwani ni VISASI JUU YA VISASI??.

Na Vannesa atapona toka katika mdomo huu wa Simba??

TUENDELEE TUJUE MWISHO WAKE.


See you on Monday...............Have a Nice Weekend



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Wapenzi wafuatiliaji wa Hadithi hii.

Hadi hapa bila shaka mmepata jibu kwa nini Moses anaitafuta Roho ya Raymond.

Je, atafanikiwa kwani ni VISASI JUU YA VISASI??.moses hawezi kumuua vanesa bana

Na Vannesa atapona toka katika mdomo huu wa Simba??

TUENDELEE TUJUE MWISHO WAKE.


See you on Monday...............Have a Nice Weekend



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
moses will spare the life of vanesa for the so called love
 
HADITHI: KIVULI CHEUSI

SEHEMU YA KUMI NA SITA

TULIPOISHIA....


Ndiyo sababu alimuingiza Moses katika biashara zake akiamini kuwa Moses ni mtoto wa carlos. Hivyo angemtumia Moses kumuua baba yake. Hakufahamu siku zote hizo kuwa yule Moses aliyemuona tangu akizaliwa mpaka amekuwa ni mtoto wake aliyemkataa tangu tumboni. Hakujua sababu ya Moses kuwa na mahusiano na Bertha mara walipokutana chuoni. Raymond akawa amelipiza kisasi kwa kuiangamiza familia ya Moses. Moses akawa ameingia katika kisasi cha kuiangamiza familia ya Raymond.

******

ENDELEA............



Moses aliamini kuwa Raymond hatakuwa nyumbani hivyo ugeni wake wa ghafla ungemshitua sana Bi Furahiya. Kupotea kwake muda mrefu kungemshitua sana. Bila shaka angestaajabu na kuduwaa kwa kuwa ni muda mrefu tangu kifo cha Bertha nyuma yake ni zaidi ya miezi nane iliyopita.

Aliichukua bajaji iliyomfikisha moja kwa moja katika nyumba ya Raymond. Nyumba iliyolindwa na mitambo maalumu, getini akiwemo Majura. Mlinzi aliyemfahamu vizuri Moses.

Nyumbani kwa Raymond kukawa na ulinzi mkali uliongezwa ili kuilinda familia hiyo. Ulinzi wa askari maalumu waliolipwa kwa ajili ya kuilinda familia. Majura aliwatambulisha kwa Moses askari hao na kuruhusiwa kupita.

Moses alicheka moyoni kwa kuwa aliamini ulinzi huo ni kutokana na uoga na mtu aliyejiita Kivuli cheusi, ambaye ni yeye. Aliingia ndani kwa mapokezi ya heshima.

Kama alivyotarajia, Bi Furahiya alishituka sana huku akifurahi sana kumuona Moses.

Alimpokea kwa maswali mengi huku akiongea kwa furaha na machozi yakibaki kidogo yamdondoke.

"Ulikuwa wapi Mose jamani? Kaka yako Ray, amekutafuta sana kwenye simu amekukosa"

Ray huyo ambaye Bi Furahiya alikuwa akimuita Kaka, ndiye huyo Moses alikuwa akiitafuta Roho yake. Raymond ambaye ndiye mtu pekee anayemchukia kuliko yeyote duniani. Moses alikaa kochini baada ya salamu za hapa na pale, Alijitia kucheka cheka kumpoteza wasiwasi Bi Furahiya.

Huo ndio ukawa wakati ambao Moses aliupenda sana. Aliiona glass ya juisi ya machungwa juu ya meza. "Bila shaka alikuwa akiinywa huyu mwanamke" Moses akajisemea.

Hakutaka kufanya kosa. Aliutoa ule unga wake wa sumu ndani ya moja ya mifuko yake ya suruali. Unga wa nyongo ya mamba ambayo imekaushwa juani hatimaye ikasagwa uliobaki na kuumalizia hapo katika bilauri ya juisi aliyokuwa akiinywa bi furahiya.

Dakika chache baadaye Bi Furahiya, alirudi akiwa na Glass nyingine ya juisi. Alimpatia Moses, yeye akaenda kuifakamia ya kwake.

Hakufahamu kuwa anainywa sumu.

Alipotaka kuongea, dakika tatu zilikuwa nyingi. Moyo wake ukapunguza kasi ya kusukuma damu. Mapigo ya moyo yalikuwa yanapiga kwa mbali sana. Jasho jingi lilikuwa likimtoka Bi Furahiya. Moses alinyanyuka huku akijikung'uta kung'uta koti lake. Alitoa picha ya kivuli cheusi, kwenye moja ya mifuko ya koti lake. Akampatia mkononi Bi furahiya.

Bi Furahiya alizungumza neno moja tu ambalo halikusikika vizuri.

"Nakufa"

Moses akacheka kwa kejeli, akaropoka neno la kuudhi zaidi "Labda nikuongezee sumu nyingine uliyoifakamia kwa uroho" Akacheka kwa nguvu kisha akatoka nje.

Nyumba hiyo ilikuwa na wafanyakazi lakini wote walikuwa nje hivyo hakuna ambaye ingekuwa ni rahisi kumshitukia Moses kabla hajatoka nje ya geti kabisa.

Wafanyakazi wote walikuwa katika sehemu zao za kazi. Moses aliwaaga askari wale ambao walionekana kutomjali kabisa mgeni huyo. Akiwa anamfikia Majura huku akitafuna plastiki ile kama dawa ya kuzuia sumu, akalitoa kopo lililofanana na kopo lililohifadhi manukato. Kopo ambalo kama lile ambalo alilitumia kumuua mke wa McCuthbert na Andrew.

Alipomfikia Majura baada ya stori za hapa na pale, wakati anaondoka akajipulizia ile sumu. Baada ya kuhakikisha sumu ile imefanya kazi ya kupokonya uhai wa Majura, aliondoka bila yeyote kushitukia chochote.

Baada ya Moses kutokomea, ni dakika nyingi zilipita mpaka ambapo maiti ya Bi Furahiya kufahamika. Aliyetoa taarifa kuhusu maiti hiyo, alikuwa ni mfanyakazi aliyehusika na chakula. Wakati ambao alikuwa akimfuata chumbani kwake kumuuliza kama alikuwa anahitaji chakula, ndio wakati aliomuona Bi Furahiya akiwa anatema povu kaikumbatia sakafu pale pale sebuleni alipokuwa amekaa na Moses.

Alipiga ukunga, uliowafanya walinzi wa nje kutimua mbio kuelekea sauti ile ya kike ilipotokea silaha zao zikiwa mbele. Waliingia ndani wakiwa wanaangaza huku na kule. Walimshuhudia Bi furahiya akiwa wa baridi, kaikumbatia sakafu juu ya povu lilokuwa likimtoka mdomoni.

Mmoja wa walinzi hao, alitoka nje na kukimbilia getini kwa Majura. Mbio hazikuwa ndefu sana mpaka alipokifikia kibanda cha Majura, alimkuta Majura naye akiwa amelala usingizi kama wa Bi Furahiya, mapovu mdomoni, picha yenye kivuli cheusi pembeni ya kichwa chake.

Mlinzi huyo, hakuamini alichokuwa akikiona.

Alirudi ndani ya nyumba na kuwapa taarifa wenzake wanne waliobaki.

"Majura amekufa?"

Wote walishituka.

Mmoja alitoka bila kuongea chochote mpaka nje ya geti kabisa. Alijaribu kuangaza huku na huko kama anayemtafuta mtu. Akarudi ndani mbio jasho likimtoka pumzi zikipishana kwa kasi.

"Ameshaondoka"

"Nani?" Mmoja wao akauliza

"Aliyefanya mambo haya, ni yule aliyetoka hapa punde"

Wote kwa pamoja walionyesha kuelewa jambo fulani. Wazo la kupiga simu katika ofisi za ambulance. Haikuchelewa kupokelewa

"Upanga mheshimiwa... Tunashukuru sana"

Wote wakiwa hawajui la kufanya, wakiwa katika mawazo mazito. Si mfanyakazi wa jikoni, yule aliyekuwa anafua nguo ndani ya chumba chenye mashine za kufulia wala walinzi wote sita waliokuwa wamekaa pembeni ya maiti zote mbili.

Mmoja wao ndipo akakumbuka kuuliza

"Hivi jina la yule mgeni mnalikumbuka?"

Mwingine akadakia kwa huzuni "Anha! Siunajua umapepe wa Majura?"

Mwingine akajisemea "mimi sikumsikia akimtambulisha yule mtu"

Yule aliyekatishwa akamalizia "majura amezidi umapepe sana alituchekesha chekesha wala hatukumfahamu jina lake"

Yule aliyegundua maiti ya Bi Furahiya aliuliza jambo. "Mmekumbuka kumpigia baba?" Wakashituka kwa pamoja.

Mmoja akakiri kusema "Dah! Sisi ni wajinga tumesahau" Ndipo wakati ambao iliingia simu mbaya kwa Raymond na kumfanya apoteze fahamu.

"Mzee.. Mzee!!?"

Mmoja wa walinzi aliyejitolea kumpigia Raymond, aliishia kuita bila kufahamu
nini kimemkuta bosi wao.

******

ITAENDELEA..................
 
Kazi ipo hapa
Nina wasiwasi na Vanessa jamani, sijui itakuwaje, mosess ameshaanza kumstukia
 
HADITHI: KIVULI CHEUSI

SEHEMU YA KUMI NA SABA

TULIPOISHIA....


Yule aliyegundua maiti ya Bi Furahiya aliuliza jambo. "Mmekumbuka kumpigia baba?" Wakashituka kwa pamoja. Mmoja akakiri kusema

"Dah! Sisi ni wajinga tumesahau" Ndipo wakati ambao iliingia simu mbaya kwa Raymond na kumfanya apoteze fahamu.

"Mzee.. Mzee!!?"

Mmoja wa walinzi aliyejitolea kumpigia Raymond, aliishia kuita bila kufahamu
nini kimemkuta bosi wao.

******

ENDELEA.............


Raymond akiwa ofisini kwake jumanne tulivu yenye manyunyu na umande mande, alipokea ujumbe mfupi uliosema "Bi Furahiya amefariki dunia kwa sumu, kifo kikihusishwa na muuaji yule yule wa Bertha, Kivuli cheusi"

Akili ya Raymond ikawa imeleemewa na ujumbe huo mzito, akapoteza fahamu kwa kuikumbatia meza yake pana yenye umbo bapa.

Baada tu ya jua kuchomoza, Vannesa aliamshwa na simu iliyokuwa ikipiga kelele. Ilikuwa ni simu ya Naima. Katibu muhtasi wake wa ofisi yake ya kuwapumbaza wengine. Kuwapumbaza wasiofahamu kazi yake kubwa ya upelelezi. Alipotaka kuipokea, nayo ikawa imekatika. Kumbe iliita muda mrefu. Alipotaka kumpigia, simu ikaanza tena kuita.

Akaipokea

"Habari yako Naima?.. Yah nimechoka sana aisee.. Vipi mbona asubuhi asubuhi.. Jafari Hiza? .. Amefuata nini asubuhi asubuhi?.. Anha mwambie nakuja .."

Baada ya simu kukatika, alijinyanyua kivivu na kukiacha kitanda. Aliingia bafuni kuoga. Alipotoka, alimkuta Moses amekwishaamka. Alikuwa akiivuta sigara yake taulo kiunoni.

"oh! Mpenzi umeamka?"

uso wa Moses haukuwa na furaha licha ya kuongeleshwa kwa huba na Vannesa. Alipomgeukia Vannesa, Vannesa ndipo alifahamu roho mbaya ya Moses kwa mara ya kwanza. Ile sura iliyokuwa ikimchekea na kumuonesha tabasamu siku zote, haikuwepo. Sura iliyojitutumua mbele yake kwa hasira ikaongozwa na maneno ya chuki ya Moses.

"hivi huyo Jafari Hiza ni nani?" wakati ambao Vannesa alitaka kujibu, alikatishwa "haiwezekani jana wakati tunakula akupigie simu, leo asubuhi asubuhi akupigie simu. Na wewe unakurupuka na kumfuata?"

Vannesa akataka kujitetea,

Moses akamkatisha tena "Sipendi na nabidi uchague moja"

Hilo likawa jambo gumu kwa Vannesa kukubaliana nalo. Alijua jinsi ambavyo serikali ilikuwa ikimtegemea. Bila yeye kumpata huyo muuaji ilikuwa ni ngumu kwa jeshi la polisi kumpata. Muuaji ambaye yupo naye karibu na ndiye huyo anayemtazama kwa hasira.

Vannesa hakujua yeye akawa anatumia akili na nguvu za kibinadamu. Alimtazama kwa hasira, akijuta kwanini aliamua kuwa na mwanaume? Alimuona mwanaume huyo kama ni kizuizi kipya katika kazi yake. Kuna dakika alipokuwa akizitazama ndita za Moses, hakutamani kuendelea kuwa naye.

Akajibu kwa hasira "Moses, mimi na wewe tumekutana tu barabarani. Hunijui vizuri na pia bado sijakujua vizuri, hii ni kazi yangu inayonipa kula siku zote tafadhali naomba uheshimu kazi yangu"

Vannesa aliongea kwa hasira hata Moses akaliona hilo. Vannesa akavaa na kujiandaa kuondoka. Alimuacha Moses akiwa bado anapasha mapafu yake kwa moshi wa sigara..

******

Moses alianza kujihisi mwepesi kutokana na jambo alilolifanya. Kumuua Bi furahiya kwake alianza kuona akikaribia ushindi wa kumaliza kisasi chake. Lakini kabla hajamaliza kumuua Raymond, alitaka kufahamu ni nini kilimpata hata akamtelekeza mama yake. Ni nini hasa kilichomfanya amsababishe yeye Moses amuue baba yake kwa mkono wake? Na kwanini amuingize katika kazi haramu za kutoa roho za watu?

Alifanya kazi hiyo kwa muda mrefu bila uoga lakini hakuipenda. Alimchukia Raymond lakini hakuwa na jinsi kwa kuwa tayari alishajiingiza kwake. Siku alipotoroka katika himaya yake, ndiyo siku aliyopanga kulipiza kisasi kwa Raymond. Alimchukua Bertha kutoka kwa Yesaya, akifahamu fika ni dada yake wa baba mmoja lakini ikawa ni sehemu ya kisasi chake. Akatembea naye mara nyingi, bila kuwa na mapenzi yoyote moyoni.

Alifahamu kuwa kuna siku atamaliza chuo na kumiliki rasmi miradi aliyoachiwa na Carlos. Kipindi hicho ndio alitaka aanze kwanza kuitoa roho ya Bertha. Aliamini kuwa akiwa na pesa pamoja na nguvu sehemu fulani, basi Raymond asingekuwa tishio kwake. Akamiliki makapuni kwa muda mrefu huku wazo la kuiangamiza familia ya Raymond ikiendelea kumpotezea muda mwingi kuwaza.

Hakujali kuibeba damu ya Raymond ndani ya mwili wake.

Alichotaka ni kuingamiza damu yake kama Raymond alivyoiangamiza ya kwake. Akiwa njiani bila kufahamu alipotaka kwenda, akapata nia ya kwenda ofisini kwa Raymond. Alipanga kuonana na Raymond, amuulize hadithi nzima ya mauaji aliyokuwa akiiyafanya huku akitumia mkono wake kuyaficha maovu yake.

Alitaka afahamu yote kabla ya kumtoa roho yake.

Akaiacha pikipiki aliyokodisha akaiendea taksi iliyompeleka hoteli ya Rayberth hotel. Hotel iliyomilikiwa na Raymond kwa fedha haramu. Hotel iliyochipuka ghafla huko pembezoni mwa ufukwe wa bahari. Hakupenda kulaza damu kabla Raymond hajapata habari za vifo vya mke wake na mfanyakazi wake wa siku nyingi.

Moses alipokuwa chini ya ghorofa ya hotel hiyo akimlipa dereva ujira wake, akaliona gari analolifahamu. Aliliona mara ya kwanza katika apartment ya rafiki yake, McCuthbert. Gari ya Jafari Hiza.

*****

ITAENDELEA............!!!
 
Wera wera....mambo yanazidi kunoga, kumbe moses ni mtoto wa raymond, mimba yake ilitelekezwa na akamuua baba yake wa kambo kwa mkono wake mwenyewe....lol!
Ni haki alipe kisasi ila ndio moses usiue watu wasikuwa na hatia
 
bonge la stori wajameniii nakumbuka zama za wille gamba............eti kivuli cheusi nkaichukulia yakizush.... daah ni movie hatare sanaaa kuwah kusoma humu ndani.....
 
HADITHI: KIVULI CHEUSI

SEHEMU YA KUMI NA NANE

TULIPOISHIA....


Akaiacha pikipiki aliyokodisha akaiendea taksi iliyompeleka hoteli ya Rayberth hotel. Hotel iliyomilikiwa na Raymond kwa fedha haramu. Hotel iliyochipuka ghafla huko pembezoni mwa ufukwe wa bahari. Hakupenda kulaza damu kabla Raymond hajapata habari za vifo vya mke wake na mfanyakazi wake wa siku nyingi.
Moses alipokuwa chini ya ghorofa ya hotel hiyo akimlipa dereva ujira wake, akaliona gari analolifahamu. Aliliona mara ya kwanza katika apartment ya rafiki yake, McCuthbert. Gari ya Jafari Hiza.

*****

ENDELEA..........



Mara tu baada ya kuachana na Moses hotelini, Vannesa alienda hadi zilipo ofisi zake. Huko alikutana na Jafari Hiza akiwa anajiandaa kuondoka.

"Umekula ng'ombe mzima umelishindwa Jicho?" Akamtania Jafari Hiza.

Jafari hakucheka, akataka kutoka bila kuzungumza chochote. Vannesa akamzuia kwa kumshika kifuani
"Unaenda wapi sasa?"

"Mke wa Raymond amefariki" akajibu kwa hali ya kughafirika. Jibu hilo likamshangaza sana Vannesa

"Amekufa!?" Jafari hakujibu kitu, kutokana na bumbuwazi ya kifo cha Bi Furahiya iliyomkumba ghafla Vannesa, akaongozana na Inspekta Jafari Hiza mpaka nyumbani kwa Raymond.

Vannesa akapanda gari ya Jafari kuelekea huko. Wakiwa njiani, Jafari Hiza aliamua kumpigia Raymond. Simu yake ilipopokelewa sauti haikuwa ya Raymond.

"Unasema?.. Basi tunakuja sasa hivi"

Jafari akamueleza Vanessa yote kuhusu taarifa aliyoipokea kutoka kwa mfanyakazi wa Raymond; kuwa Raymond amepoteza fahamu na amezinduka dakika chache zilizopita, hivyo amepumzika.

Vannesa akasema "Unaonaje tukapitia ofisini kwake kisha tuelekee nyumbani. Kwa sababu
tunaweza kupata chochote huko"

"Sawa"

Jafari Hiza alikubali ushauri wa Vannesa. Akaligeuza gari yake na kuelekea kawe ilipo hoteli ya Raymond. Kwa mwendo wa speed kali, kutokea zilipo ofisi za Vannesa walichukua dakika ishirini pekee kuwafikisha kwenye hoteli ya kifahari ya Raymond. Hawakutaka kupiga simu kwa kuwa walipafahamu mpaka ofisini kwake.

Jafari Hiza aliongoza mbele akifuatiwa na Vannesa.

Walikuwa wakipanda lifti kuelekea ghorofa ya tatu zilipo ofisi za Raymond. Hiyo ni baada ya kuliegesha gari yao eneo la maegesho. Walikaribishwa ofisini kwa Raymond baada ya kuonesha vitambulisho vyao. Raymond alikuwa akihema kwa uoga akashusha pumzi ndefu baada ya kumuona Jafari Hiza.

"Afadhali umekuja Jafari" Akapata nguvu ya kusimama. Machozi yakiendelea kumtoka, akawakaribisha Jafari na Vannesa. Aliwaondoa wafanyakazi wake waliokuja kumjulia hali.

"Mke wangu Jafari"

Alikuwa ameinamisha uso wake, alipouinua, ulikuwa umelowa machozi.

"Pole sana Raymond"

"Nitapoa vipi wakati amesema anaitaka roho yangu?" Raymond akawa mkali. Lakini hiyo haikumtisha vannesa kuuliza.

"Wewe unadhani ni nani anahusika"

"Wewe mwanamke una kichaa?"

Akavuta kamasi jepesi na kumuuliza kwa hasira "ina maana Jafari mnafanya nini mpaka sasa?"

"Tupo hapa kukusaidia, mzee"

"Mnanisaidia kumtafuta nani?"

"Muuaji wa mke wako"

"Sasa muuaji wa mwanangu ndiye muuaji wa mke wangu." Alinyanyuka akawa anazunguka kila upande wa ofisi "anajiita kivuli cheusi"

Vannesa naye alikuwa amenyanyuka na kwenda upande wa dirishani huku akimuuliza swali Raymond

"Natumaini Raymond hili ni jambo unalolifahamu kuhusu..." Kabla Vannesa hajaendelea kuzungumza, alinyamaza ghafla. Alinyamaza mara baada ya kumuona mtu ambaye anayemfahamu. Alipotazama kwa makini,

"Hapana"

Akajisemea'Inawezekana namfananisha' Bila kujua wote waliokuwepo ofisini humo wakimtazama yeye, alitoka mbio na kuikimbilia lifti ya kumshusha chini. Bila kuelewa Jafari Hiza akaelekea dirishani kuchungulia chini ya ghorofa ya hoteli hiyo hakuona cha maana.

XXXXX

Moses baada ya kuliona gari ya Jafari Hiza, akataka kumfahamu mtu huyo vizuri. Bila shaka alikuwa na hakika mtu huyo yupo katika ofisi za Raymond. Akataka kufahamu uhusiano uliopo kati yake na Raymond pamoja na Vannesa.

Sawa alijua Vannesa kuwa ni mpelelezi, mpelelezi aliyetumia kivuli cha uandishi wa habari kuficha uhalisia wake. Lakini yeye akamuona Vanessa kama shushu mwenye njaa anayependa kufuatilia mambo ya hatari kuiepusha njaa ya siku chache badala ya kifo cha milele.

Akajipa moyo na kuzifuata lift za kumpandisha mpaka juu. Aliifahamu vyema ofisi ya Raymond kwa kuwa haikuwa mara ya kwanza kuingia katika jengo hilo. Lakini alipofika ndani ya lift na kutaka kubonyeza nambari ya kuelekea zilipo ofisi za Raymond, roho yake ikasita. Iliposita hakubonyeza kitufe cha namba na kubonyeza kile cha kufungua mlango.

"Hapana siendi"

Roho yake ilipokataa, akaitii. Alitoka mpaka nje tena, na kuifuata ilipo barabara. Ni hapo ndipo Vannesa akiwa juu ya ghorofa ndani ya ofisi ya Raymond, alimuona Moses. Kwa kuwa alihisi amemfananisha hakutaka kuamini tu kwa kumfananisha.

Alitaka kujiridhisha kwa macho.

Alitaka kumuona huyo aliyefanana na Moses kuanzia utembeaji, nguo alizovaa pamoja hata na umbo lake. Vannesa akawa ameshuka na kumuona Moses akiwa kwa mbali kidogo. Umbali uliowatenganisha kwa miguu isiyopungua ishirini. Akashindwa hata kumuita, lakini alipata uhakika kabisa ndiye Moses anayemfahamu.

Akarudi ofisini kwa Raymond akiwa na mawazo.

Mawazo ya kujiuliza Moses amefuata nini katika hoteli hiyo? Sawa ni hoteli na kila mtu alikuwa na uhuru wa kufika katika hotel aipendayo, lakini si kwa Moses aliyemuacha hotelini kule kinondoni.

Kulikuwa na mtu alikuwa na miahadi naye? Akaitazama saa yake. 'Hapana' akajisemea. Haiwezekani amuache saa nne asubuhi hotelini tena kitandani halafu saa nane awe amefika katika hoteli hiyo. Ni saa ngapi ameshakutana na mtu huyo na kuzungumza naye? Kwanini awe hana gari? Kuna uwezekano ana uhusiano wowote na Raymond?

Akajiondoa hofu na kusema inawezekana alikuwa ni mteja kama wateja wengine waliofuata huduma ya hoteli ya Reyberth kama wengine. Akaufungua mlango wa ofisi ya Raymond. Hata alipoingia ndani ya ofisi ya Raymond, bado alikuwa akiwaza kuhusu Moses.

Lakini hawakukaa sana ndani ya ofisi hiyo, wote watatu walitoka kwa nia ya kurudi nyumbani kwa Raymond. Vannesa na Jafari Hiza walipanda kama walivyokuja, raymond akawa peke yake.

Walipofika tu katika mtaa aliokuwa akiishi Raymond, simanzi ilionekana katika kila nyuso ya mkazi wa mtaa huo.

Ni mmoja tu ambaye alipata nguvu ya kuisimamisha gari ya Raymond.

Alikuwa ni mwanamke wa makamo aliyelowa machozi. Alilia kwa uchungu.

Raymond alimfahamu fika

"Habari yako mama Koku"

"Si nzuri jirani yangu" akajifuta machozi kwa upande wa kanga, "tafadhali usiingie ndani ya nyumba yako kwa sasa"

"Kwa nini?" Raymond alihamaki kwa mshangao. Vannesa na Jafari nao walikuwa wameshashuka kutoka katika gari lao wakisikiliza kilichokuwa kikisemwa na mama huyo aliyekuwa akivukwa na nguo kwa kilio.

"Nipo na Merce nyumbani kwangu, nusu saa zilizopita amekuja na kunieleza kuwa kuna mauaji yametokea nyumbani kwako. Ndipo akanieleza kuwa kuna mgeni aliyekuja nyumbani kwako"

Mwanamke yule akawa anamuhadithia Raymond. Mgeni huyo alifika nyumbani bila mtu yeyote kumfahamu. Ni Majura pekee mlinzi wa getini ndiye alikuwa akimfahamu. Akaeleza kuwa mgeni huyo pia Bi Furahiya alikuwa akimfahamu hivyo alikaribishwa sebuleni na Bi Furahiya kwenda kumuandalia kinywaji. Hakukuwa na mtu sebuleni zaidi ya mgeni anayeshukiwa ni muuaji na Bi Furahiya. Mara Merce alipoenda kuwaandalia chakula ndipo alifahamu kifo cha Bi Furahiya. Hatimaye walinzi waliokuwa wakilipwa na Raymond pia kati yao akaeleza kuhusu kifo cha Majura getini.

Wote walionekana kufa kifo kimoja.

Wote walitoa mapovu na walikufa haraka. Walilala usingizi wa milele kwa aina moja. Hadithi hiyo ya mama koku ikazidi kumtia uchungu Raymond. Akashuka garini na kutaka kuingia ndani kwa jazba.

Mama Koku akamzuia. "Tafadhali usiingie" Raymond akasimama "naomba usubiri nimalize kuzungumza"

Baada ya kufahamika Majura na Bi furahiya wamefariki, kosa lingine likafanyika. Hapo moyo wa Vannesa ukaanza kwenda mbio. Wakasikiliza kwa makini.

Jafari Hiza na Vannesa walikuwa wakisikiliza kwa makini sana. Mama koku akawa anaendelea huku akivuta kamasi jepesi lililokuwa likijipenyeza katika pua zake. Kuna mmoja kati ya wale walinzi sita aliokota kopo la manukato. Macho ya Jafari Hiza yakamtoka pima.

Mama Koku akaendelea. "Akaipuliza ile hewa aliyodhani ni manukato. Kati ya walinzi wale sita hakuna aliyehimili kusimama kwa miguu yake. miongoni mwa wafanyakazi wote wa ndani ya nyumba ya Raymond aliyepata nafuu ya kutoka nje akiwa hai alikuwa ni Merce. Hewa ile ndani ya chupa ya manukato ilikuwa ni hewa ya sumu...Mimi ndiye nilimsaidia Merce kumpa maziwa. Ndiye aliyenihadithia hadithi yote hii"

Mama Koku hakumalizia hapo akaishia kwa kumwambia kama ushauri Raymond "unaweza kuchagua kuingia ama kusubiri taarifa ya wauguzi waliokuja kuchukua miili ya watu wako"

Jafari Hiza akazungumza "Hiyo sumu ndiyo ile niliyokuambia Vannesa" akamwangalia Vannesa kisha akagota kwenye uso uliomvimba Raymond kwa kulia "Huyu muuwaji ndiye huyu huyu aliyemuua mwanao Bertha na wote niliokupa taarifa juu ya vifo vyao. Huyu ndiye aliyewaua wamiliki wa apartment aliyofanyia mauaji ya shahidi namba moja aliyekuwa akimfahamu kule masaki kwa sumu hiyo hiyo" akawaeleza aina ya sumu ambayo aliitumia kwa kuichanganya katika chupa ya manukato. Habari hiyo haikumfanya Raymond kuacha kulia. Alilia kama mtoto.

Jafari Hiza akaeleza kuwa "hewa hiyo yenye sumu hudumu kwa dakika tano tu hewani, hivyo hakuna shaka kama tukiingia"

Wote wakaingia na kukuta miili ya watu kumi na moja ukiwemo wa bi Furahiya, Majura, walinzi sita na wafanyakazi watatu. Walikuwa wamefunikwa katika mifuko maalumu ya maiti.

******


ITAENDELEA............
 
Back
Top Bottom