HADITHI: KIVULI CHEUSI
SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO
TULIPOISHIA............
Hiyo ikawa hadithi iliyomfumua Moses ufahamu wake kwa kiasi kikubwa. Moses alifahamu vizuri kuhusu kaka yake mama yake na alimjua baba yake. Lakini kitu ambacho bado kikawa kitendawili ni kuwa Raymond hakufahamu kuwa Moses ni mtoto wake.
Baada ya hadithi hiyo, ndipo Moses naye alizungumza
"baba"
ENDELEA.......................
Raymond alishituka. Alikuwa amejiinamia wala hakujua kuwa alipokuwa akikukumbuka kila jambo lililotokea hapo zamani, alikuwa akizungumza kwa sauti. Sauti ambayo Moses na Vannesa walikuwa wakimsikia.
Jina hilo la ‘baba' ndiyo lilimshitua.
"wewe ni baba yangu" Moses akajibu huku Vannesa akitabasamu.
"hukufahamu jambo hili kwa kuwa ulimfukuza mama yangu, mimi na kaka bado tukiwa tumboni"
Raymond akashituka "kaka? Kaka yako yupi?"
"Tulizaliwa mapacha ila yeye kaka alifariki wiki chache baadaye"
Moses akamueleza kila kitu huku machozi yakimtiririka. Raymond naye alisikiliza hadithi hizo kwa hisia kiasi cha kumtiririsha machozi yaliyokuwa magumu kumtoka siku zote. Wakiwa wote wanalia yaani Moses na Raymond, Moses alinyanyuka akitoa bastola yake aliyoipachika kwenye kiuno.
Vanessa alipoiona hali hiyo, akamzuia kufanya alichotaka kufanya.
Ikiwa tayari Vannesa alikwishawatumia askari anaofahamiana nao ujumbe kwenye simu zao kisirisiri na kuwaelekeza maeneo hayo. Askari hawakuchelewa sana. Walikuja na silaha nzito za moto kutokana na kumuogopa sana kivuli cheusi.
"naomba unisamehe Moses" Moses alikuwa ametiwa pingu baada ya Kurudishwa mikono yake kwa nyuma. Moses alishangazwa na hali hiyo. Aliduwaa akimshangaa Vannesa huku akijiuliza nini kinatokea? Hali hiyo ikamkumba vile vile Raymond. Hakuelewa kwanini pia naye alitiwa mbingu.
Vannesa akadondosha chozi huku akijifuta kwa kiganja chake. Akasema kwa huzuni.
"Moses naomba unisamehe kwa kukulaghai kuwa nilikupenda sana. Zilikuwa ni njama tu kukuingiza katika mtego wangu. Nilikupenda mwanzo lakini si kabla hujamuua Jafari Hiza. Rafiki yangu wa toka utoto wetu. Nilikuchukia tangu nilipofahamu una sura ya binadamu lakini roho ya mnyama ndani yako. Nitahakikisha wewe na baba nyako mnapata adhabu inayostahili. Kutokana na visasi vyenu, mmepoteza uhai wa wengi wasio na hatia"
…. MWISHO ….
ASANTENI