Hakuna mtu anataka aachiwe, ila aibu wanayokutana nayo hao vilaza wa serekali ni hatari. Tena ilitakiwa huyu shahidi wa sasa adhibitishe utambulisho wake, hapo ndio ingekuwa aibu ya Karne. Nilisema toka juzi, kuwa Lisu aliwashinda hao vilaza wa jamuhuri kwenye mahakama kuu toka mwaka jana, wakaenda kuipack kesi mahakama ya rufaa, na huko kawalambisha mchanga.
Wamerudi mahakama kuu wakitegemea kuchomekea ushahidi uchwara kama watafanikiwa. Lakini ndio imezidi kuwa mbaya maana huyu shahidi ndio wangalau walitegemea anaweza kujibu sunami. Lakini sasa imekuwa aibu zaidi. Na kesho sitegemei wawe na shahidi wa maana zaidi ya blabla na kulazimisha maridhiano uchwara. Na cdm wasikubali kabisa maridhiano ya hadaa bila uwajibikaji. Kesi iende hadi mwisho tuone nani zaidi.