Jamani Ndugu zangu wa ukawa naomba tuweke Silaha chini tumuunge mkono mh. Raisi katika hili, hata kama kuna makosa yalifanywa na ccm siku zilizopita lakini sasa wanayarekebisha hilo ni jambo jema kwa nchi yetu, nchi kwanza siasa baadaye, wazungu wanasema hata kama umetembea umbali gani ukigundua umepotea geuka urudi ulikotoka ili ufuate njia sahihi
Mkuu
MKWEPA KODI, I salute you!
Naomba nianze kwa kukukumbusha kuwa: mtu yeyote mwenye NIA NJEMA na nchi hii, basi ataanza na KATIBA, na sio tu kuirekebisha, bali pia kuhakikisha anaisimamia na hii ikiwa ni pamoja na utawala bora na demokrasia.
Haya yanayolumbaniwa leo, yametokana na udhaifu wa katiba. Waliyoyafanya walijua kuwa 'makaburi hayatafukuliwa' na badala yake watatangaziwa neema ya kupumzika. Kilichotokea ni
watu wachache kuamua VIBAYA kwa niaba ya taifa, na leo tunalumbana na kurusha makombora kwa wawekezaji tukiwaita jina baya. Kumbukumbu zangu zinanikumbusha kuwa UPINZANI ULIPIGA KELELE JUU YA USIRI WA MIKATABA YA MADINI, lakini kwenye bunge letu kuna 'Team Ndiooooo' na Refa ni wao, uwanja ni wao...wanasahau kuwa TAIFA NI LETU. Kwa kipindi kile, mbaya hakuwa ACACIA, wabaya walikuwa WAPINZANI. Nikukumbushe kuwa, kwenye GESI nako Team Ndioooo ilipiga show kwenye HATI YA DHARURA.
Mkuu
MKWEPA KODI, unachoniambia leo ni kuunga mkono juhudi fulani ambazo binafsi sizielewi zinalenga nini. Ikiwa sakata hili ni matokeo ya USIRI na MAAMUZI YA WACHACHE, mbona tunakanyaga mule mule?
BOMBADIER haikuwa hata na hati ya dharura wala kipande cha bajeti. Ikiwa kesho pakatokea msuaguano wa kiufundi kuhusu 'maintenance' ya hizi ndege, napo tutaombwa kuonesha uzalendo kwa kitu ambacho kilifanywa 'kwa nia njema'?
Mkuu
MKWEPA KODI, pamoja na jeuri yooooote ya Trump au rais awaye yote yule wa taifa kuuuuuubwa la Marekani, mbele ya BUNGE ni breki. Bunge likisahau jukumu lake la kuisimamia serikali, kiasi likakubali kuwa hata Naibu Spika atoke Serikalini, basi tumeumia. Nimekua nikiajua kuwa ni bunge la bajeti ndio linaidhinisha allocation of fund na hiyo ni baada ya kuhoji uhalali na yaliyomo katika matumizi ya wizara mbali mbali, lakini si ni juzi tu hapa Waziri wa Afya kasema hajui madaktari wanaoajiriwa Kenya Style watalipwaje?
Wallah kwenye hili ndugu zangu, tunahitaji kuweka itikadi pembeni. Ni haki ndio huinua taifa na sio nyimbo. Bunge liwe bunge.