Gwajima wa kanisa la Ufufuo na ving'ora barabarani

ndugu yangu, wakubwa waliingilia kati pamoja na familia wakawa hawataki iyo itokee, lakini kama wasingefanya ivyo, amina chifupa angerudi laivu, ..waliogopa mvurugano utatokea huko kwa wakubwa kwasababu kuna siri nyingi sana kwenye hiyo selikali yenu. hivyo ilibidi waombe jamaa asimrudishe..

Duu hii kali, hivyo ule ufufuo tulioahidiwa ndio basi tena, kama huyu bwana keshaanza hiyo kazi by the time Yesu anarudi kaburini hakuna mtu:mad:
 
mbona una nikoti mimi, kwani nani kakwambia mimi nilikuwa nakuongelea wewe ngoshwe? unajishuku nini mkuu? by the way, nashukuru kunikumbusha huko bush party nilikokuwa nimetupwa na wazee nikajifunze kuishi....

Matogoro+1.jpg

umekichukia king'ora? au umemchukia alibebwa na ham'ma?
sijaona tatizo, ukiona hivyo si lazima uruhusiwe na mtu
kiongozi wa kiroho ni mkubwa kuliko, kiongozi wa kundi la wezi
hata ana kofia ya kuwa raisi, any way hii ni nchi yetu na wananchi ndiyo sisi,
hata mimi hakuna kitu kinachoniudhi kama makelele ya adhana

Kiongozi wa kiroho naye ni mwizi tu.

Kwanza hiyo roho iko wapi? Inakaa wapi katika mwili wa binadamu? Huyo mungu mwenyewe yuko wapi?

Uongo mtupu. Bora hata hao viongozi wa kisiasa wanadanganya kuhusu dunia hii, hao "viongozi wa kiroho" ndio majambazi wakubwa kwani wanadanganya watu kuhusu mbingu ambayo hamna mtu aliyefika.
 
Rafiki, Mbingu ipo na Mungu yupo angalia maneno yako. Usikufuru

Kiongozi wa kiroho naye ni mwizi tu.

Kwanza hiyo roho iko wapi? Inakaa wapi katika mwili wa binadamu? Huyo mungu mwenyewe yuko wapi?

Uongo mtupu. Bora hata hao viongozi wa kisiasa wanadanganya kuhusu dunia hii, hao "viongozi wa kiroho" ndio majambazi wakubwa kwani wanadanganya watu kuhusu mbingu ambayo hamna mtu aliyefika.
 
hahaha, mbona kama namwona bwana komba hapa, sijui mapunda, au ni ndimbo huyo au mbonde...duh...pale kama si mfalanyaki, ni matembo hapo...hahaha. duh!
 
sioshwi dhambi zangu, bila Damu yake Yesuuuu, Hapendezewi Mungu, bila Damu yake Yeeesuuu, haaaakuna kabisaaaa, Dawaaa ya makosaaa, ya kututakasaaa, ila Damu yake Yeeesuu,

sipati patanishoooo, bila Damu yake Yeeesuuu, hukumu yaningojaaa, bila Damu yake Yesuuuu, haaakuna kabisaaa, dawaaaa ya makosaaa, yaaa kututakasaaa, ila Damu yake Yeeeesu...

Njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha,jitieni nira mkajifunze kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu.

mwenyewe Yesu aliyakuchuka magonjwa yetu yote, amejitwika huzuni zetu zote, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona....sisi sote kama kondoo tumepotea, na Bwana ameweka juu yake maovu yetu yote....

Eee Nafsi yangu mhimidi Bwana, Naam vyote vilivyoko ndani yangu vilisifu Jina lake Takatifu, akusamehe maovu yako yote, akuponya magonjwa yako yote, akuponya magonjwa yako yote, akuokoa uhai wako na kaburi....

Last edited by a moderator:
Umenikumbusha hizi vesi nadhani ni tenzi za roho ehe..."sioshwi dhambi zangu, bila Damu yake Yesuuuu, Hapendezewi Mungu, bila Damu yake Yeeesuuu, haaaakuna kabisaaaa, Dawaaa ya makosaaa, ya kututakasaaa, ila Damu yake Yeeesuu,

sipati patanishoooo, bila Damu yake Yeeesuuu, hukumu yaningojaaa, bila Damu yake Yesuuuu, haaakuna kabisaaa, dawaaaa ya makosaaa, yaaa kututakasaaa, ila Damu yake Yeeeesu"...

Last edited by a moderator:
Niko Old Bagamoyo road nasikia ving'ora vinapigwa kutoka kwenye gari inabidi kuweka gari pembeni nikihisi ni Mheshimiwa au mgonjwa anapita nashangaa kuona Hummer nyekundu na msururu wa magari ukipita kwa kasi na hayo magari yamebandikwa Picha ya mheshimiwa askofu anakaribishwa nyumbani.

Sijui huyu bwana karuhusiwa na nani kwa kutupigia ving'ora na kupita kwa kasi kama kiongozi wa nchi. Sasa hata matapeli wanajidai hii nchi sijui tunaenda wapi?

4.jpg

mimi ndugu zangu nashangaa kumuona Kiongozi wa Kanisa kuwa na Hummer nyekundu? Wakati Bwana Yesu Kristo alikuwa napanda Punda!!! Kweli tutakwenda Peponi jamani? Pesa za hiyo Hummer nyekundu Askofu huyu amezipata wapi?kama sio Michango ya Waumini? kazi kweli ipo. Bwana Yesu Kisto alisema (Tajiri hawezi kuingia katika Ufalme wa Mungu mpako hapo Ngamia aweze kuingia katika Tundu ya sindano) Viongozi kama hawa Wenye Ma Hummer nyekundu mimi kwa binafsi yangu siwaamini hata kidogo bora Uswali uwe nyumbani kwako kuliko uende kuibiwa pesa na Maaskofu Matapeli wanaotumia Jina La Mungu na Bwana Yesu Kristo kuwaibia watu Pesa zao.
 
Siku hizi wahubiri wengi wanafanya biashara na waumini, Wanauza injili kwa sadaka. Wanawakamua kondoo (washirika) bila aibu. Hata Benny Hinn ana kashfa kubwa ya kuwa nabii wa uongo. Kwa maoni yangu, watu wasome maandiko yanavyosema na kuyafuata na sio kuwafuata wahubiri matapeli. Ni maoni tu.
 
kitendawiliiiiii......!
Mtumishi yupi hapa dar amezaa na mke wa kaka yake na kumlazimisha kaka yake amuoe?????????
 
mimi ndugu zangu nashangaa kumuona Kiongozi wa Kanisa kuwa na Hummer nyekundu? Wakati Bwana Yesu Kristo alikuwa napanda Punda!!! Kweli tutakwenda Peponi jamani? Pesa za hiyo Hummer nyekundu Askofu huyu amezipata wapi?kama sio Michango ya Waumini? kazi kweli ipo. Bwana Yesu Kisto alisema (Tajiri hawezi kuingia katika Ufalme wa Mungu mpako hapo Ngamia aweze kuingia katika Tundu ya sindano) Viongozi kama hawa Wenye Ma Hummer nyekundu mimi kwa binafsi yangu siwaamini hata kidogo bora Uswali uwe nyumbani kwako kuliko uende kuibiwa pesa na Maaskofu Matapeli wanaotumia Jina La Mungu na Bwana Yesu Kristo kuwaibia watu Pesa zao.

nikiangalia post karibia zote zakwako wewe mzizi mkavu, ni upinzani wa ukristo, nimeona sehemu zingine ulishamtishia mtu kuwa utamkata kichwa...sasa si kitu cha ajabu kwamba hautamwamini kwasababu upo wazi muda wote kuangalia wapi kuna kitu cha kikristo ili upinge...mimi binafsi nilishasali kwenye kanisa lake pindi yupo pale ubungo, ile hummer alipata zawadi toka kwa wajapan, hata ukienda pale leo utakuta kuna wajapani kibao wapo wanasali, ameweka makanis amengi huko japan china na korea...na ninakuhakikishia hakununua...

uyu jamaa hata nyumba yake ya kuishi amepanga...hajajenga yake...sasa akipewa hummer, mnataka akatae? halafu kusema ngamia sijui kupita kwenye tundu la sindano, hauelewi maana yake...sasa kwasababu post yako imekaa kichukichuki na intention ya wewe kuandika hapa ni chuki tu kwa kifupi, sina haja ya kukueleza sana because haupo hapa kwa mazuri.....kama haujui kitu kiundani, ogopa sana kuongea kama wewe ndo unajua kila kitu, inakuwa si fair kabisa kuongea kitu juu ya mtu kumbe si kweli....lets be fair kwa huyu mchungaji, na tuache wivu na fitina vya kidini.havitatusaidia kamwe.
 
Kuna huyo Chris Oyakhilome rai wa Nigeria mwenye Kanisa la Christembassy tunang'anganizwa kununu vitabu vyake vya Rhapsody of Realities hapa ofisini kila mwezi na waumini wake. Huwa najiuliza kwanini asingekuwa anatengeneza nakala moja ya mwaka mzima badala ya kuwafanya waumini wake wawe wachuuzi kila mwezi. bei 2000/=, usiponunua unanuniwa weee na kuonekana unamkana Yesu.
 
wamekulazimisha ununue?, au ni hiari?
 
Back
Top Bottom