Askofu Gwajima ni nani Tanzania?

Kwani wanochanjwa hawana akili? Si wamejiridhisha? Huwezi kumtukana hivi raisi wako halafu unaangaliwa tu!!! Eti achanjwe zote milioni moja!!! Who is Gwajima to us? Kwani yeye kuwa ni msemaji wetu watanzania? Is he a scientist? a pharmasist? Ni mtaalam wa nini hasa? Who is he? is he a preacher? He claimed to resurrect, why did he not resurrect our president? Was he there when the vaccine was being manufactured? Huyu ni mjanja fulani tu anayejua kuongea na kupotosha watu!!! Hii theory kwamba wazungu wanataka kutumaliza, hivi mzungu akitaka kutumaliza lazima atumie chanjo itakayompoint moja kwa moja? Tunatumia kila kitu cha wazungu kwanini hawatumalizi kupitia vitu vyao tunavyovitumia? Why all the trouble kutengeneza chanjo when they can finish us in an instant with no hussle!!!!
Na pia ukweli ni kwamba mataifa yote ambayo yametoa chanjo vifo vinapungua.
Corona inakwenda kuwa gonjwa la Africa kwa ujinga wetu kama ambavyo ukimwi unatuhenyesha.
Kuna mdudu kwenye bongo zetu si bure.
Ni kweli ukichanjwa unaugua corona lakini ukali wake ni sawa na ambaye hajachanjwa? Chanjo inasaidia kupunguza ukali wa corona kufikia level ya mafua ya kawaida.
 
Kama hujui tafsiri ya kitu si vema kukitumia utaonekana kituko mbele za watu

LOW MINDSETS DISCUSS PEOPLE, MIDIUM MINDSETS DISCUSS EVENTS BUT HIGH MINDSETS DISCUSSE ISSUES
Naam @mshanajr tuelezeee vizuri, gwajima kuzungumza mawazo yake ni kosa?hivyo basi ww mwenye IQ wasaidie wale wenye ndogo ili kulinda afya wasije potea kwa mawazo ya gwajiboy waiting curiously to be britned
 
Gwajima alieleza uelewa au hisia zake na nampongeza Sana kwa Hilo,

Serikali au watu wanaotofautiana nae walitakiwa kuja na hoja ili kupangua wasiwasi wake na kwa wengine. Shida inaanzia pale tunapoangalia Nani kasema badala ya kuangalia Nini kasema.

Wizara na viongozi wake walitakiwa si kuanzisha marumbano naye ambayo muda mwingine wao ndo wanajidhalilisha. Dk Mollel Nani hajui kiki iliyompa Unaibu kipindi Cha Mwendazake, Nani hajui Dk Gwajima alivyokuwa anatetea kujifukiza kuliko miongozo ya WHO.....!

Gwajima amebaki kule ambako watanzania wengi walipelekwa kipindi kile hivyo naye anahitaji elimu na ufafanuzi mzuri ili naye abadili mawazo kama walivyofanya Dk. Gwajima na Mollel.

Mtu sahihi ambaye anaweza kusimama akaueleza Umma bila unafiki kwa wanasiasa ni Dk Ndungulile, huyu hakukubali kuaminishwa ambacho hakiamini na kilicho tofauti na taaluma yake.
asante sana kwa ufafanuzi mzuri bro, nadhani kwa vile tupo kwenye demo-cratic nation basi kila mtu ana haki sawa, tumsikilize
 
Akijulikana kama askofu wa kanisa la ufufuo na uzima ambaye kwasasa ndio Mbunge wa Kawe si mara ya kwanza kuingia kwenye mitifuano na serikali.

Ana kesi nyingi pia ambazo mwisho wake una utata

Ana kashfa nyingi pia

Ni aina ya mtu ambaye sidhani kama ana mshipa wa soni. Ni kinyonga na hachelei kugeuza maneno

Ni kwanini baada ya yote hayo anapeta tuu?

Jibu ni moja tu. Walimuamini wakamtumia katika shida zao mbalimbali za kijamii, mahusiano, siasa, kiroho na hata kifedha..anawajua nje ndani.

Amebeba siri zao nyingi sana, anawajua na kuwafahamu kwa mengi mema na mabaya. Kamwe hawawezi kumgusa.

Atafanya atakavyo, atasema atakavyo lakini watafunika kombe tu mwanaharamu apite. Amewafanya kama mateka wake. Anawatumia atakavyo, Dr. Slaa anamjua vema huyu.

Kama ukweli ni tofauti na huu. Basi naamini atachukuliwa hatua walau za kupewa karipio la wazi. Hebu msikize hapo

View attachment 1872360

Kuna mtu mmoja tu ndio alikuwa na uthubutu wa kumsema waziwazi. Naye si mwingine bali ni Mzee Makamba
Gwajima sometimes use unatumia Akili kubisha Vitu usivyo na Ujuzi navyo. Unawakosea Viongozi adabu. Yaani Maza kachanja Fake? Kwa hiyo adungwe zote? Unajidai wajua kila kitu kumbe Mfufua Misukule na Wafu fake. Mbona doctrine yako ya kufufus Wafu imekushinda🙄🙄
 
Naam @mshanajr tuelezeee vizuri, gwajima kuzungumza mawazo yake ni kosa?hivyo basi ww mwenye IQ wasaidie wale wenye ndogo ili kulinda afya wasije potea kwa mawazo ya gwajiboy waiting curiously to be britned
Main point kwenye mada yangu sio ishu ya chanjo bali mtiririko wa matukio hasi kumhusu ambayo kwayo, mengi kati ya hayo angeshakuwa lupango..lakini hayuko huko
Kuna kitu kinaitwa conflict of interest... Uchungaji na uanasiasa... Aina ya mahubiri yake daima kama sio kusimanga watu basi ni kuaminisha waumini wake na wote wanaomsikiliza kuwa anachokisema ni halisi na kinawezekana
Sasa ni mbunge hii sio nafasi ya kiimani ni ya kisiasa.. Hivyo anatumia mamlaka mbili kwenye jambo moja... Na inawezekana kabisa Gwajima hajajitambua nafasi yake kisiasa, miiko na mipaka yake kwenye kuwasilisha hoja na mawazo yake kwenye jambo fulani
Ishu ya chanjo Gwajima anatafuta cheap political mileage..ATACHANJWA na hii ni pale atakapotaka kusafiri nje ya nchi ama ule waraka wa serikali utakapoanza kufanya kazi
Kama kweli chanjo ni mbaya kama anavyoielezea basi aachane na ccm kabisa, na afute mawazo ya kusafiri nje ya nchi JAMBO AMBALO HALITAWEZEKANA...
Hulka ya Gwajima ni kupenda kuabudiwa.. Refer mtifuano wake na Makonda....Hapo anataka serikali imuite waongee kisha arudi kivingine kuisifia chanjo
 
Gwajima naye atakuja kuwageukeni kama huyu
Screenshot_20210729-192118.jpg
 
Na pia ukweli ni kwamba mataifa yote ambayo yametoa chanjo vifo vinapungua.
Corona inakwenda kuwa gonjwa la Africa kwa ujinga wetu kama ambavyo ukimwi unatuhenyesha.
Kuna mdudu kwenye bongo zetu si bure.
Ni kweli ukichanjwa unaugua corona lakini ukali wake ni sawa na ambaye hajachanjwa? Chanjo inasaidia kupunguza ukali wa corona kufikia level ya mafua ya kawaida.
Ameandika Pastor Dr.Zakayo Nzogere (PhD), Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la MICC Mwanza.

Pamekuwa na matamko mengi yanayokinzana kutoka kwa watumishi wa Mungu kuhusu UVIKO19.

Wapo wanaosema ni maandalizi ya “Mpinga Kristo” na alama ya Mnyama 666; na wengine wakisema ni mlipuko wa kawaida usio na uhusiano wowote wa kiimani.

USHAURI WANGU KWA WATUMISHI WENZANGU;

1. Kuwa Mtumishi wa Mungu haimaanishi tuna majibu ya kila jambo kila wakati.

2. Kuwa Mtumishi wa Mungu haimaanishi kila unachokiamini, unachokisema, au kukifiria basi kimetoka kwa Mungu. Mambo mengine ni utashi binafsi unaotokana na taarifa ulizonazo.

3. Kuwa Mtumishi wa Mungu haikupi mamlaka ya kuwafanyia wafuasi wako maamuzi binafsi. Hata Mungu mwenyewe anatutaka tuchague kati ya uzima na mauti; hatulazimishi (Kumbukumbu 30:19).

4. Kuchukua tahadhari siyo kukosa Imani. Kuna wakati Yesu alichukua tahadhari ya kutoingia Yerusalemu waziwazi kwa sababu kuna watu walitaka kumuua; hivyo akaingia kwa siri (Yohana 7:1-10). Si kwamba aliogopa kufa; bali hakutaka kufa kabla ya kutimiza kazi iliyomleta.

Wayahudi walipotaka kumuua Mtume Paulo alitoroshwa mjini kwa kushushwa na KAPU (Matendo 9:25); hebu fikiria Mtumishi wa Mungu kujificha kwenye kapu.

5. Ni sahihi Mtumishi wa Mungu kuwa na msimamo binafsi kuhusu mambo tofauti, lakini si sahihi KUMUINGIZA MUNGU kwenye misimamo binafsi.

Mtume Paulo anatusaidia kwenye kutoa matamko ambayo sio maagizo ya Mungu moja kwa moja, kwa kuweka wazi mara zote anapotoa mtazamo binafsi juu ya jambo fulani:

1Korintho 7:6 (NEN) “Nasema haya kama ushauri na si amri”

1Korintho 7:12 (NEN) “Lakini kwa wengine nasema (si Bwana ila mimi)..”

MIMI NAAMINI YAFUATAYO:

1. Covid19 ni janga la kawaida na litapita.

2. Chanjo ya Covid haina athari zozote za kiroho kwa Mkristo.

3. Hakuna kinachoweza kututenganisha na upendo wa Mungu wala kugeuza imani yetu.

4. Ni sahihi Wakristo kuchukua tahadhari zote za kiafya kama tunavyoelekezwa na wataalamu.

NB: Mtu akisema tahadhari dhidi ya UVIKO ni kukosa Imani; muulize kwanini anafunga mkanda kwenye gari? Kwanini anavaa kofia ngumu kwenye pikipiki? Au kwanini ameweka chandarua chumbani? Zote hizo ni tahadhari, sio ukosefu wa imani.!
 
Habari zenyewe wanazoshadadia kwamba hata Ulaya hawaitaki chanjo zinatoka kwenye vimedia uchwara huzikuti CNN, BBC and alike mainstream media.
Ukiona dunia ya leo unacheza ngoma tofauti na US, Ulaya na Israel jitathmini
 
Hoja hapa chanjo inazuia nisipate korona? Jibu ni HAPANA unapata! Je chanjo hii inazuia nikiwa na korona nisimuambukize mwingine? Jibu ni HAPANA unawezakumwambukiza! Je nikichanjwa nikapata korona siwezi kufa! Jibu ni HAPANA unawezakufa! Je hayo MACHANJO ni ya nn? JIBU yanazuia maambukizi ya KORONA. Mbona waliochanjwa Ulaya wanazidi kupukutika kwa kasi?🤔 Tuwe na ngozi nyeusi na AKILI iwe nyeusi huo ni upimbi.
Tatizo la wanaopigia debe hii chanjo ni kushindwa kujibu hoja zinazotolewa na watu kama akina Gwajima, na badala yake wanaanza kumjadili yeye badala ya kujibu hoja zake, mfano hizo hoha ulizotoa wewe hapo juu, badala ya kuzijibu mtu anaanza kukujadili wewe kwamba eti akili zako zimeenda na mwendazake, mara ooh sijui nini, yaana hawajibu hoja, wanakera sana!
 
Lakini kaka Mshana Jr hebu tuache kumdiscuss mtu, tuzijadili hoja alizozitoa zina ukweli kiasi gani na uongo kiasi gani!? Mamlaka aliyoitaka itoe ufafanuzi wa alichokitaka imefanya hivyo!?

Na mimi nauliza tena, huyu mama si alikuwa Makamu kipindi cha Mwendazake!? Na alikubaliana na alichokuwa akikifanya mzee Joni!? Iweje leo akengeuke!? Ndio kuifungua Tanzania huku anakotuhubiriakila mara!?
 
Swali la msingi sijajibiwa naona watu wamerukia kwenye ishu ya korona..Je unaweza kwanza kunijibu nilichouliza?
 
Back
Top Bottom