Ipi ni bora kati ya hizi

mabasso

JF-Expert Member
Oct 16, 2022
1,005
1,821
Kumekuwa na news nyingi sana kuhusu single mamaz kwamba siyo watu sahihi sana kuoa labda tu kama wazazi wenzao wawe wametangulia mbele za haki kidogo inaweza kuwa salama kwa muoaji

Lakini niko hapa na mtazamo tofauti kidogo
Kuna wanawake wenye historia ngumu za mahusiano yao yaliyoishia vibaya kwa kutelekezwa na mimba na wengine mimba kukataliwa na wahusika

Jambo lililopelekea mimba kulelewa kwa shida sana na hata mtoto kulelewa kwa shida

Hii matokeo yake mwanamke huyu kumchukia sana baba wa huyu mtoto kiasi cha kutotaka kumuona kabisa au kumuhusisha baba na malezi ya mtoto hata kama ana hali mbaya kiasi gani
Je kukutana na huyu single mama na kumuoa athari hapo ni ipi kutoka kwa mzazi mwenzie?
Ikiwa yeye mwenyewe hataki hata kumsikia

Mimi nafikiri jambo la msingi ni kujua historia ya hayo mahusiano yao yalikuwa na mwisho gani na hiyo ndiyo inaweza kuamua kwamba ni salama kuoa au si salama

Turudi kwa wewe ambaye umeoa mwanamke asiye na mtoto lakini huyu mwanamke uliyemuoa alikuwa na mahusiano yake close sana lakini mtu aliyekuwa naye bado hakuwa tayari kuoa kutokana na sababu kadhaa labda kipato,umri au mwanafunzi na sababu nyingine wengine huwenda wana undugu fulani lakini wana mahusiano

Wewe muoaji umekuja umeonyesha nia ya kuoa uko stable na kila kitu demu kakuelewa mmekuwa na mahusiano ndani ya mahusiano sometimes huwenda haujui kama demu ana mtu wake mwingine na wakati mwingine huwa mtu anajua lakini anaamini yeye ndiyo winer mjanja zaidi ya huyo aliyemkuta

Mwenye demu wake anamruhusu demu aolewe kwa kuwa hamna jinsi wanapiga show ya kuagana kwa uchungu maisha yanaendelea

Hawa ndiyo wale hulala(show) na bibi harusi siku moja kabla ya harusi pale mchizi anapolalamikia roho inamuuma ndiyo kwamba wameachana, demu ili kumtoa hofu mwamba anamletea show kudhihirisha bado tuko pamoja usiwe na mashàka

Kumbuka demu labda alikulia Arusha na huko alikuwa na mahusiano yake ambayo baada ya kuhama Arusha na kuja dar au sehemu nyingine umbali uliuwa hayo mahusiano it means waliachana kwa amani tu

Tuseme mkeo ana ma ex watatu sasa ambapo ameingia tu kwenye ndoa tayari ana mchepuko wa uhakika na hawa wengine wawili itakapotokea wamekutana basi stori haziwi ndefu ni kupasha tu kabichi

Lakini yule single mama alitiwa mimba akiwa shule na ex wake huyo tu ambaye ni mzazi mwenzie ambaye hataki hata kumsikia baada ya hapo kawachukiachukia wanaume mpaka kukutana na muoaji
Swali hapo kwamba yupi ni bora kati ya hawa wawili
 
Kuoa ni sawa na kubet tu,

Marriage is a huge gamble

One don't really know someone until that great commitment is made, Some individuals don't reveal their true selves until they are married.
 
Ukishaona mtu anaitwa singo maza,huyo ameshapoteza point ya kuolewa labda wakutane na jibaba lenye watoto 3,walee watoto
Nadhani kwa mtu kama huyu niliyemuongelea hapa tatizo atakalokuwa nalo ni kumpenda sana mwanae ikibidi kulikuko mume lakini kuna namna rahisi tu ya kudeal na jambo hilo na mambo yakaenda sawa zaidi ya hapo sioni kama kuna shida yoyote
 
Wewe umeoa singo maza?,au wewe ni singomaza uliyeolewa? Maana tujue upande wako kwanza
 
Kiuhalisia watu wanaweza kubadilika, either kutoka kuwa mtu mzuri mpaka mbaya au kuwa mtu mbaya mpaka mzuri,malezi,mitazamo na mambo tunayopitia katika maisha ndio hasa yanajenga Imani zetu,nikirudi kwenye swali lako hapo ni bora hiyo single mother
 
Kiuhalisia watu wanaweza kubadilika, either kutoka kuwa mtu mzuri mpaka mbaya au kuwa mtu mbaya mpaka mzuri,malezi,mitazamo na mambo tunayopitia katika maisha ndio hasa yanajenga Imani zetu,nikirudi kwenye swali lako hapo ni bora hiyo single mother

MTU habadiliki.
Ukiona kabadilika jua alikuwa ana-fake.
 
Back
Top Bottom