Godwin Gondwe wa ITV asilazimishe fani

nndondo

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
1,251
895
Jamani tuwe wa kweli, huyu kijana ana juhudi ya kazi na nasikia ni msomi wa hivi vyuo vyetu vya kata, lakini hana kipaji cha utangazaji jamani.

Anajaribu kuiga ma cow boy wa movie za kimarekani, kicheko chake ni very artficial he is a bad actor, hata kwenye lile tangazo la promotion alilovalishwa suti mpya, lakini bado kicheko kinachafua, halafu naomba Joyce japo husikilizagi la mtu, msimpange kwenye mahojiano hana technique mtu huyu, anaongea zaidi ya mgeni, hana uvumulivu hayuko organized maana anauliza kila kitu wakati mmoja na maswali yake sio maswali ni maelezo ya anachokijua yeye juu ya hilo swala, anaingilia mszungumzaji anauliza maswali mengi wakati mmoja na hajui kufuatilia kama lipi limejibiwa lipi halijajibiwa. Anawezakana ni mwanahabari mzuri lakini sio mtangazaji mzuri especially kwenye TV.

Kwa nini msimuache aka concentrate kwenye u MC wa BSS na taarifa ya habari? hata ninapoongea sasa yuko kwenye kipindi ch akumekucha anazoza yeye hata mzungumzaji hatujui kamuitia nini studio maana angeongea yeye tu
 
kuna mwingine alikuwaga clouds fm nasikia siku hizi yuko ujerumani kwa msaada wa mpiganaji Abuu Liongo,jamaa alikua akisoma taarifa ya habari au akitangaza kipindi cha michezo nilikua nazima redio halafu alikua mshkaji wake gondwe dizaini maana mara nyingi niliwaona wakiwa pamoja...
 
Hakuna mwenye chuki binafsi hii ni cheap strategy ya watanzania msiopenda kuambiwa ukweli, sisi ndio watazamaji wa TV kwa nini utanakataa tunachokisema, ni bahati tu kwamba bado hatujaingia kwenye pay TV tusingelipia hizi TV ambazo watu wengine mnaziona ndio deal, tunachosema ni kwamba hana kipaji sasa chuki binafsi inatoka wapi wakati sisi hatuko ITV wala kuwania kazi yake, tunamwambia kumsaidia yeye na kituo chake kuangalia upya namna ya kuboresha delivery ya vipindi vyao, ebo!
 
Sijaona kama tatizo la Gondwe limefikia hali ya kulaumiwa kiasi hicho, na kusema analazimisha fani!
Ungekuwa wa msaada sana kama ungemtumia kama ushauri binafsi, na si kumlaumu.

Gondwe ni kijana msomi mzuri wa Saint Augustin University(Japo umesema kwa dharau kuwa ni mhitimu wa vyuo vya kata)ambaye anaweza kupokea maoni na kubadilika muda wowote...man be fair, give him a chance, na si kumkwamisha!
 
Sio tumaini ww, ni saut na siku ya mahafali yke mwezi uliopita tulikua nae pale villa park disco. Ila sijaona tofauti ya kabla na baada ya kupata masters.
 
Umenisemea yoote. Hapa si swala la usomi, kiukweli hana 'talking and listening skills'. Kwa hakika mimi huzima TV au kubadilisha channel kila ninapomsikia. Kinachoniudhi ni yeye kujihisi yuko sahihi na 'bora kabisa' pale anapotangaza. Anayebisha hebu ajaribu kumfuatilia ...
 
Umeongeza chumvi sana ila kuna ukweli kuhusu G.G. Nilikuwa naangalia kile kipindi alichokuwa anahoji watanzaji na waandishi wa IPP Media ,walipokuwa wanafunga mwaka.Kweli wakati anamuhoji Joyce nilishangaa sana,Jamaa ana maelezo mengi na haulizi maswali anatoa ufafanuzi wa jambo ili mgeni aelezee kidogo juu ya huo ufafanuzi wake.Ila anayonafasi ya kubadilika kama atagundua makosa yake.Elimu sio kigezo cha yeye kuwa mwandishi mzuri kwa sababu unaweza ukasoma na usielimike.Pia chuo mtu alichosoma kinaweza changia mtu kutobadilika kutokana na kukosa exposure.
 
kuna mwingine alikuwaga clouds fm nasikia siku hizi yuko ujerumani kwa msaada wa mpiganaji Abuu Liongo,jamaa alikua akisoma taarifa ya habari au akitangaza kipindi cha michezo nilikua nazima redio halafu alikua mshkaji wake gondwe dizaini maana mara nyingi niliwaona wakiwa pamoja...

Anaitwa nani?
 
Hakuna mwenye chuki binafsi...........sisi ndio watazamaji wa TV kwa nini utanakataa tunachokisema, ni bahati tu kwamba bado hatujaingia kwenye pay TV tusingelipia hizi TV ambazo...........ebo!

Ndugu much as I respect maoni na mtazamo wako lakini sidhani kama vi vema uka-generalize kana kwamba kila mtu anaona na kufikiri unachokifikiri. What I mean is epuka kuweka pleuralism kwenye statement zako. Wewe semea moyo wako na si ya wengine

Binafsi nampa big up gondwe, anajitahidi sana. Wewe unasema amesoma kwenye shule za kata, so what? Nafahamu amesoma Tumaini-Iringa which is quite a good higher learning institution. Wewe uliyesoma Harvard au Oxford wapi kazi yako? wapi impact yako kwenye jamii? Sishangai ndio nyie mnaokuja na hoja kwamba fulani ni failure kaishia tu darasa la saba au form 4 hivyo hawezi kuongoza wakati mtu anadeliver.....

Ushauri wangu kwako ni kwamba ainisha mapungufu ya gongwe na ikiwezekana toa na maboresho au yeye kama yeye a-build kuanzia hapo otherwise THIS IS PURE CRAP NA UNA CHUKU BINAFSI juu ya mafanikio ya mwenzako
 
Katika kila kipindi cha ITV mwishoni kuna tangazo lisemalo "Toa maoni yako juu ya hiki kipindi." Na wanaweka email address pale chini, sijui mwenzetu ulishawahi kufanya hivyo?

umesema sawa kbs mkuu.
ile ki2 ingetumika ipasavyo kama nia yake ni kutaka kumsaidia kumchana uku duuuh.
 
Fine, kama umegundua hayo mapungufu ya GG nadhani kwa kumsaidia ni vema ungemtafuta ukampa huo ushauri ili abadilike na sio kulalamika kwetu, unatwambia sisi tufanye nini sasa kama sio unafiki wako nadharau eti chou alichosoma heheheeee haitakusaidia hiyo hata kidogo au mwenzetu umesoma Havard au Oxford lol. Tafakari na badilika.
 
wewe unapozungumzia exposure unamaanisha nini? kwani hawa watangazaji wetu hawawaoni wenzao wa CNN,RT,Sky news wanavyofanya kazi zao, ni vichwa vyao vigumu tu na hawataki kujifunza zaidi.period.
 
Kweli kabisa analazimisha fani,yaani sauti hadi aitengeneze weee anatumia force na energy na ikitoka vilevile mvuto hakuna,nawapenda watu kama tido mhando yaani anaongea tu natural daaah yaani unamfeel sauti ya ukweli na tamu jamani vile tu ni mzee ningemmendea
 
Jamani tuwe wa kweli, huyu kijana ana juhudi ya kazi na nasikia ni msomi wa hivi vyuo vyetu vya kata, lakini hana kipaji cha utangazaji jamani, anajaribu kuiga ma cow boy wa movie za kimarekani, kicheko chake ni very artficial he is a bad actor, hata kwenye lile tangazo la promotion alilovalishwa suti mpya, lakini bado kicheko kinachafua, halafu naomba Joyce japo husikilizagi la mtu, msimpange kwenye mahojiano hana technique mtu huyu, anaongea zaidi ya mgeni, hana uvumulivu hayuko organized maana anauliza kila kitu wakati mmoja na maswali yake sio maswali ni maelezo ya anachokijua yeye juu ya hilo swala, anaingilia mszungumzaji anauliza maswali mengi wakati mmoja na hajui kufuatilia kama lipi limejibiwa lipi halijajibiwa. Anawezakana ni mwanahabari mzuri lakini sio mtangazaji mzuri especially kwenye TV, kwa nini msimuache aka concentrate kwenye u MC wa BSS na taarifa ya habari? hata ninapoongea sasa yuko kwenye kipindi ch akumekucha anazoza yeye hata mzungumzaji hatujui kamuitia nini studio maana angeongea yeye tu

sasa inakuhusu nini...mambo ya kishamba hayo...mind your own business
 
Back
Top Bottom