Ni kweli kabisa, mahakama kama ilivyo inatakiwa kuwa chombo huru, na kwa kiasi fulani imejitahidi kuwa hivyo, lakini ni ukweli usiopingika kuwa mahakama haipo huru kama inavyotakiwa, fikiria kamati za maadili za mahakama zinakuwa chini ya wakuu wa mikoa ambao ni wanasiasa wateule wa rais, Jaji mkuu mwenyewe alikiri hivyo kuwa serikali inaingilia uhuru wa mahakama.
Hivi kweli kwa mtu mwenye akili timamu, anapoona wabunge wa ccm pamoja na mwanasheria mkuu wa serikali, wanalazimisha wakuu wa mikoa waendelee kuwa wenyeviti wa kamati za maadili, hapo utasema hakuna maslahi wanayoyapata kwa mfumo huu?
Tusisahau pia kuwa idira ya mahakama imekithiri kwa rushwa, kwa wale walikuwa na kesi kadhaa wataelewa suala hili, rushwa si pesa tu, ni pamoja na favor za kujuana, ahadi za vyeo n.k, mahakimu na majaji wanapokea rushwa sana, sasa katika mazingira hayo imani kwa mahakama inatoweka, hata kama hukumu ya haki lakini watu hawawezi kuamini.
Lakini, kwa kuwa suala hili ni la kisheria zaidi, na sheria si ya mtu mmoja, basi ngoja tuwe na subira wataalamu wa CDM wafuatilie mwenendo wa kesi na hukumu yake, kesho tupate majibu.