a. Mahakama imejuaje kuwa Batilda alidhalilishwa? - Bila kumuuliza yeye wanajuaej kuwa alijisikia kudhalilika. Vipi kama aliona ni ujinga tu wala haikumdhalilisha? Hivi mtu mwingine anaweza kwenda kusema "x ameibiwa" wakati yule ambaye anadaiwa kuibiwa anaona kila kitu chake kipo salama?
Sheria ya uchaguzi ya mwaka 1985 inasema kuwa kesi ya uchaguzi inaweza kuletwa mahakamani na:
1. Mtu ambaye kisheria alipiga kura au alikuwa na haki ya kupiga kura kwenye uchaguzi unaohusu hiyo kesi.
2. Mtu ambaye anadai alikuwa na haki ya kuwa nominated au kuchaguliwa kwenye huo uchaguzi.
3. Mtu ambaye anadai kuwa alikuwa mgombea kwenye huo uchaguzi.
4. Mwansheria Mkuu wa Serikali
Kwa hiyo, ilikuwa sio lazima Batilda akafungue kesi mwenyewe. Nimeona watu wengi mpaka wanasheria wana-question inakuwa a thirdy party akafunge kesi. Lakini sheria ya uchaguzi inamruhusu mpaka mpiga kura kufungua kesi bila kuwepo kwa aliyeshindwa uchaguzi. Na hiki ndicho kilichofanyika kwenye kesi ya Lema.
b. Imethibitishwa nini kuhusu alichosema Lema ambacho ni cha udhalilishaji? Alisema maneno gani, lini na wapi na ni ushahidi gani kuwa aliyasema hayo? Kwa mfano watu watatu wakija na walikuwepo kwenye mkutano wakasema hawakusikia maneno hayo na watu wengine watatu ambao walikuwepo kwenye mkutano huo wakasema walimsikia mahakama inaamua vipi kuwa hao watu watatu wanaosema walisikia wanasema kweli?
Well, hapo inabidi mpaka kusoma huku yenyewe. Kuhusu mahakama itaamua vipi kama watu watatu walikuwepo kwenye mkutano wakasema hawakusikia maneno hayo na watu wengine watatu ambao walikuwepo kwenye mkutano huo huo wakasema walimsikia, issue ipo kwa ambao hawakumsikia. Inawezekana alisema lakini wao hawakumsikia. Unaweza ukawa kwenye mkutano wa hadhara na usisikie wanayosema waongeaji. Kama wangesema Lema hakusema kabisa basi hapo pande zote inabidi wadhibishe wanayoyasema. At the end of the day mahakama itaamnua on the balance of probabilities kulingana na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili.
c. Binafsi kwa kweli sijashtushwa sana na Lema kuvuliwa ubunge - kama kuna ushahidi wa kutosha sidhani kama mahakam ailikuwa na uchaguzi mwingine- kilichonishtua zaidi na kinachonisumbua ni kuwa inaonekana hukumu ilishajulikana mapema zaidi almost a week kabla. Hili ni geni sana kwenye mahakama zetu. What happened?
Inawezekana pia kwenye upande wa Lema hawakutilia maanani sana kama angeshindwa kesi hasa kwa sababu haikufunguliwa na Batilda mwenyewe. Yeye na timu yake were over-confident kuwa watashinda kesi, which I don't blame them really. Hata wewe si ulisema una uhakika kuwa Lema atashinda kesi? Lakini kuwa over confident inaweza kusabisha kutowa-scrutinize vizuri mashahidi. Hili ni fundisho kwa wengine. Whether kesi ni ndogo au kubwa kunahitaji umakini mkubwa sana hasa kwenye ushahidi unaotolewa.
Nimeona hata kwenye kesi ya Mnyika alipokuwa cross-examined kulikuwa na baadhi ya maswali alikuwa anajibu ovyo as if anajua zaidi mpaka jaji akamtahadharisha. Otherwise, hii inaweza kuwa moja ya sababu kwenye kwenye popular cases jaji anakuwa na humu mbili, halafu moja inakuwa leaked kupima upepo. Ikionekana poa, inasomwa hiyo hiyo. Taarifa kuwa Lema atashindwa kesi zilisambaa mitaaani kwa muda mrefu na hata Lema mwenyewe anadai aliambiwa na watu wa juu wa CCM na usalama wa taifa, lakini alichukua hatua gani?