Godbless Lema avuliwa ubunge

Godbless Lema avuliwa ubunge

Status
Not open for further replies.
Baada ya kuenguliwa ubunge wa Arusha,sasa bwana GODLESS LEMA anakabiliwa na pigo lingine kubwa ambalo wadadisi wa mambo wanaamini linaweza likamfanya ashindwe kutetea kiti chake na hivyo kushindwa kuingia bungeni! PIGO hilo linahusiana na yeye kuwaambia WANAARUSHA tangu achaguliwe miaka miwili iliyopita ameshawafanyia nini wanaARUSHA mpaka sasa? LEMA amekuwa akihaha huku na huko,kushiriki maandamano yasiyo na TIJA baada ya kujikita katika kuleta maendeleo na kutimiza ahadi, inadaiwa mpaka sasa lema hajafanya chochote arusha, utalii umeshuka kutokana na maandamano yake ya mara kwa mara,hili kwa kweli ni PIGO SANA KWAKE NA CHAMA KWA UJUMLA!
MYTAKE: KAMA CHADEMA WANAWEZA WAMSIMAMISHE MTU MWINGINE ARUSHA

Viroba na bangi za chooni zinashida sana.Hata mumfufue sheikh yahaya jimbo la Arusha mjini aliwezi rudi CCM.hayo uliyo yaeleza hapo juu ni mawazo yako binafsi na wanachama wa CCM ambao kura zao hazikumuwezesha mgombea wenu kuwa mbunge.
Tupa kule......
 
Wana JF nimeona nika fukue Katiba ya Nchi hii....

=======================================================================
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi
miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu; au
(d) ikiwa katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu amepata kuhukumiwa na kupewa adhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na utovu wa uaminifu au kwa kuvunja sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
..

Wanasheria hebu nisaidieni hapo juu,kifungu kipi kilimruhusu Aden Rage kugombea ubunge?Tulianzisheni nini upinzani mkachukue jimbo la tabora mjini??
 
Mkuu PakaJimmy,

Nilijua Lema atapigwa chini ushahidi wa wanaCCM ulikuwa mzito sana sijui kama ataruhusiwa kugombea walioko mahakamani tafadhali mtujuze kinachoendelea.

Mahakama imempa options mbili...1. anweza kukata rufaa au, 2. anaweza kuacha kukata rufaa NA KUSUBIRI KUGOMBEA KATIKA MARUDIO YA UCHAGUZI....
 
Hiyo delay tactic watakayotumia CCM sijui wataitumia kwa muda gani.

Hapo hakuna Delay kwani Lema kachaguliwa na wananchi na ataendelea kufanya Kazi za wananchi kupitia CDM, Kama ni Pesa za maendeleo tutatoa sisi kupitia M4C...

Ndiyo maana nimeishauri chama chetu kifanye operation ya kumzungusha Nasari na Lema Nchi nzima wakielimisha watu kuhusu Katiba mbovu na kuchangisha pesa za Maendeleo... I am sure watu tuko tayari kuchangia... Watanzania tuko karibu 40 mil.

Kama CDM watawafikia 20Mil na kwa wastani kila moja akatoa 1000, ni sawa na 20Bil. sasa hii pesa inatosha kabisa kuendeshea Chama na kuwezesha vijana ambao wamekuwa wahanga wa kupigania haki za waTZ kutoka mikononi mwa CCM..

Binafsi mimi nina uwezo wa kuchangia 10,000/= kila mwezi kwenye mfuko wa M4C... maana yake watu kama sisi tupo wengi nchi na lengo letu ni mabadiliko ya kweli ambayo CDM ndiyo imeonyesha itayaleta...

Peoples power...
 
baada ya mahakama kutengua ubunge wa lema na kutaka uchaguzi urudiwe.ni bora kupiga kura ya ndiyo kwa lema peke yake kuliko kupoteza muda na pesa za wananchi,pamoja na pesa za vyama,pale lema kwa upepo wa sasa hakuna wa kumtoa
 
Wastage our shortage resources,nilitegemea mahakama ingezingatia hali ya kisiasa mjini Arusha. CDM inakimbiza mbaya. Nategemea Lema kushinda tena. Katiba mpya izingatie hili kwa makini,
 
Baada ya kuenguliwa ubunge wa Arusha,sasa bwana GODLESS LEMA anakabiliwa na pigo lingine kubwa ambalo wadadisi wa mambo wanaamini linaweza likamfanya ashindwe kutetea kiti chake na hivyo kushindwa kuingia bungeni! PIGO hilo linahusiana na yeye kuwaambia WANAARUSHA tangu achaguliwe miaka miwili iliyopita ameshawafanyia nini wanaARUSHA mpaka sasa? LEMA amekuwa akihaha huku na huko,kushiriki maandamano yasiyo na TIJA baada ya kujikita katika kuleta maendeleo na kutimiza ahadi, inadaiwa mpaka sasa lema hajafanya chochote arusha, utalii umeshuka kutokana na maandamano yake ya mara kwa mara,hili kwa kweli ni PIGO SANA KWAKE NA CHAMA KWA UJUMLA!
MYTAKE: KAMA CHADEMA WANAWEZA WAMSIMAMISHE MTU MWINGINE ARUSHA
Nimefikiri unaongea point kumbe unaleta porojo hapa.Amepata pigo!!!!! huna jipya wewe,nenda ukalale,hapasio sehemu ya umbea!!!!!!!
 
Baada ya kuenguliwa ubunge wa Arusha,sasa bwana GODLESS LEMA anakabiliwa na pigo lingine kubwa ambalo wadadisi wa mambo wanaamini linaweza likamfanya ashindwe kutetea kiti chake na hivyo kushindwa kuingia bungeni! PIGO hilo linahusiana na yeye kuwaambia WANAARUSHA tangu achaguliwe miaka miwili iliyopita ameshawafanyia nini wanaARUSHA mpaka sasa? LEMA amekuwa akihaha huku na huko,kushiriki maandamano yasiyo na TIJA baada ya kujikita katika kuleta maendeleo na kutimiza ahadi, inadaiwa mpaka sasa lema hajafanya chochote arusha, utalii umeshuka kutokana na maandamano yake ya mara kwa mara,hili kwa kweli ni PIGO SANA KWAKE NA CHAMA KWA UJUMLA!
MYTAKE: KAMA CHADEMA WANAWEZA WAMSIMAMISHE MTU MWINGINE ARUSHA

assume kua hawa wote waliokoment ndo wapiga kura wa arusha.
mpaka hapa ccm mna kura ngapi dhidi ya huyo lema ulosema hana cha kuwajibu wanaarusha??
Pumbaf sako baia naso hukohuko sisiem yenu nna wesi wenzako.
 
nafikiri wananchi wa TANZANIA tunatengenezewa njia yakufanya MABADILIKO hii ni njia tu yakutupeleka kwenye kuiondoa CCM KILEENI maana hizo hujuma zinatufungu bongo zetu na kuzidi kuichukia ccm tusijali bali tuwe nania moja tu kuwashusha na kuwaweka chini HAO CCM ARUSHA CDM CHUO CHA ELIMU KWA UMA
 
Baada ya kuenguliwa ubunge wa Arusha,sasa bwana GODLESS LEMA anakabiliwa na pigo lingine kubwa ambalo wadadisi wa mambo wanaamini linaweza likamfanya ashindwe kutetea kiti chake na hivyo kushindwa kuingia bungeni! PIGO hilo linahusiana na yeye kuwaambia WANAARUSHA tangu achaguliwe miaka miwili iliyopita ameshawafanyia nini wanaARUSHA mpaka sasa? LEMA amekuwa akihaha huku na huko,kushiriki maandamano yasiyo na TIJA baada ya kujikita katika kuleta maendeleo na kutimiza ahadi, inadaiwa mpaka sasa lema hajafanya chochote arusha, utalii umeshuka kutokana na maandamano yake ya mara kwa mara,hili kwa kweli ni PIGO SANA KWAKE NA CHAMA KWA UJUMLA!
MYTAKE: KAMA CHADEMA WANAWEZA WAMSIMAMISHE MTU MWINGINE ARUSHA

Kwa hapa Tanzania nani atahoji???????????? kama hatuwahoji CCM kujua wamefanya nini ndani ya miaka50 sembuse miaka miwili ya Lema??????:nono:
 
Kikwete ameifanyia nini TZ?zaidi ya mfuko wa bei,hali ngumu,ajira duni n.k achana na Lema.
 
Mh.Godbless Lema ndani ya miaka miwili tu, ameweza kufanya mambo makubwa lakini watu wamekuwa wakifikiri tofauti kwakuwa hawajui majukumu ya mbunge ni yapi...!
1.Godbless Lema Kupitia mradi wake wa ARDF ameweza kusomesha watoto na kulipia ada zaidi ya 1000, sidhani kama kuna mbunge ndani ya bunge la Tanzania amefikia rekodi hiyo..! na tena hana hata mfadhili zaidi ya yeye mwenye kujitolea pesa zake za ubunge ambazo alipewa kwaajili ya kununulia gari..!
2.Godbless Lema amekuwa kiongozi wa kwanza kwenda Gerezani na kujua kitu gani kinachoendelea Huko gerezani..,baada ya kusema bungeni manyanyaso wanayopata wafungwa, jinsi hata wafungwa wa kike wanaishi gerezani bila hata kupewa pedi...!
3.Godbless Lema ameweza Watanzania kujua jinsi gani kulivyokuwa na uozo jeshi la polisi, ambako watanzania wengi wemekuwa wakibambikiziwa kesi bila sababu za msingi...!

Jamani ni vigumu GODBLESS LEMA KUTIMIZA AHADI baada ya kufanyiwa mizengwe na CCM kwenye harakati zake za kuwatumikia wananchi..,mfano kwenye uchanguzi wa Meya mh.Mbunge alipigwa kama mwizi na polisi baada ya uchaguzi wa umeya kufanyika bila halali, na vile vile SERIKALI YA MAPINDUZI KWA MAKUSUDI walizuia MAANDAMANO YA CHADEMA ili POLISI KUINGILIA NA KUFANYA FUJO KWA KUPIGA MABOMU WANANCHI...!

CCM NDIO WANAPENDA FUJO NA MATUTSI, KWA KUTUMIA JESHI LA POLISI, NA WABUNGE WAO WAMEKUWA WAKITUMIA PESA KUWALAGHAI WANANCHI TOFAUTI NA MH.LEMA ANAPIGANIA HAKI, KULIKO KUMPA MTU ELFU KUMI ALAFU KESHO HANA KITU, KULIKO HAKI ITAMLINDA MTU MAISHA YAKE YOTE
 
Lema alishajua ni jinsi gani kesi ilivyokuwa imepangwa na dhahiri uhamuzi ulikuwa ni mahakama kumpiga chini kwa vyovyote vile:

Akiongea via Star TV mara baada ya hukumu kutolewa Lema ameeleza yafuatavyo ktk kudhibitisha hilo.

1. Lema amesema; kabla ya kwenda mahakamani asubuhi amepitia ofisini kwake kama kawaida lkn alishangaa kukuta kundi la askari polisi zaidi ya 50 wakizunguka ofisi yake kana kwamba kuna jambazi wanamvizia- swala hilo limemfanya afikilie kwamba hao askari polisi tayari walikuwa na majibu juu ya hukumu na wakiamini kuwa haitawependezesha wapiga kura hivyo kuhamua kuweka ulinzi mkali.

2. Wakati wko Bungeni Lema alimtakia Waziri mkuu kwamba amesema uongo Bungeni; jambo ambalo lilimfanya Mh. Lukuvi amwambie Lema kwamba hana nidhamu na kwa vile kesi yake hiko Mahakamani basi watatafuta namna ya kumwadabisha.

3. Mh. Rais mwaka 2007 alimuita Lema na kumuomba agombee Ubunge jimbo la Arusha mjini kupitia tiketi ya CCM jambo ambalo Lema hakuliafiki na tangu siku hiyo mahusiano hayakuwa mazuri kati ya Lema na viongozi wakuu wa CCM.
4......

Kwa kauli yake Lema anasema hawezi kutishika na huu uhamuzi uliojaa mizengwe; kwa vile mahakama haijamuzuia kugombea tena, nafasi aliyonayo nayo ni kubwa kuendelea kuwatumikia wananchi wa Arusha. Lakini anashangaa kwanini Judiciary Machinery inaingiliwa na State Machinery.
 
Hilo wana ccm wote wanalijua. Hata mkapa, wasira ,lowasa , sendeka na lusinde wanajua ni wajibu wao kuishauri vizuri ccm na mafisadi kuwa cdm moto mwingine.
 
Mbona mnaiaibisha hivi jf? si umalize kwanza ndo uandike, kwan lazma uandikie choon?
Pambaf kabsa
 
Hata kijana wa darasa la saba angepewa ile kesi CCM ingeshindwa tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom