Godbless Lema avuliwa ubunge

Godbless Lema avuliwa ubunge

Status
Not open for further replies.
hii sio Breaking newz! Kila mtu alijua itatokea hivyo!
 
naomba jina la hakimu aliyehukumu kesi hiyo......
 
NI nani huyo?????

Ngoja uchaguzi mdogo ndo utadhihirisha ukweli wa Jaji na waliopinga matokeo ya Lema! Majaji watatengua nyingi za Chadema ili kuiabisha Ccm bado ya Lissu.
 
Mahakama zetu
zinatumiwa na ccm
haki ya mtu
haitapotea, Mungu
yupo.
 
Nadhani ccm wanachoyafuta watakipata, haya picha bado linaendelea tusubili tuone sasa kifo cha magamba rasmi
 
HII NI KAMA MOVIE YA KINAIGERIA MASHETANI YANANYANYASA SANA LAKINI MWISHO WA SIKU YANAKUJA KUPIGWA VIBAYA SANA NA NGUVU YA MUNGU.SAUTI YA UMMA =NGUVU YA UMMA=SAUTI YA WATU=SAUTI YA MUNGU
WIZI,UMWAGAJI DAMU,UZINZI NA UWASHERATI,UFISADI,RUSHWA,TAKRIMA,MATUSI,UONGO N.K=UFALME WA GIZA=UFALME WA SHETANI aka LUCIFER.SASA UAMUZI NI WA KILA MMOJA WETU, KUWA UPANDE WA SHETANI AU UPANDE WA MUNGU.CCM WANATEGEMEA SILAHA ZA SHETANI SISI TUNATEGEMEA NGUVU YA UMMA
 
UBUNGE.jpg
Hapo Chacha...
 
Mbona CCM wanajivua nguo hadharani jamani hata wakimweka JK na Lema bado Lema atashinda
 
Ni wazi lema atashinda ila matusi na sera toto za ccm nisingependa kuendelea mkoani mwangu arusha.
 
Tuende mbele..turudi nyuma....

Mara baada ya mahakama ya Arusha leo kumvua rasmi ubunge Comrade Lema, chama cha Magwanda kimepata pigo kubwa, kwani ujasiri na uhodari wa mbunge huyo ni kivutio cha wananchi wengi wanfuatilia siasa za Tanzania. Hii inakuja siku chache baada ya Joshua Nassari kutangazwa kuwa mshindi kupitia jimbo ya Arumeru Mashariki.

Nimewasikia baadhi ya wanachama wa chama cha Magamba, wakisema kuwa wao wamepoteza Arumeru Mashariki na CDM wamepoteza Arusha Mjini..kwa hiyo ngoma droo...maumivu yao ya kushindwa kule Arumeru Mashariki yameshapoa.

I am forced to believe Dr. Batilda Buriani is the next MP ( Conspiracy Theory) :yell::yell:
 
Hii ni aibu kubwa kwa CCM, inaonesha wazi kwamba kuna upendeleo wa hali ya juu unaofanywa na mahakama za Tanzania ambazo ni chombo cha CCM. Hakuna demokrasia ya kweli ndani ya Tanzania. Kuna kesi kama hizo Kigoma mjini na Segerea ambako wagombea wa chadema wanapinga matokeo lakini zinapigwa danadana ila hii ya Arusha imechukuliwa maamuzi mara moja.

Sasa kama issue ni Lema kutumia maneno machafu na kejeli wakati wa kampeni Lusinde mbunge wa Mtera ambaye ametukana live atachukuliwa hatua gani na lini?.

Ushauri kwa CCM, Chadema tuna nguvu ya umma (People power) hata mfanye hujuma lakini bado haki itatendeka na tutachukua tena jimbo la Arusha mjini.
 
Mahakama zetu zinatumiwa na ccm. Kila kitu kina mwisho.
 
This is ridiculous judgement baada ya ile ya case ya Mtikila 2,
mahakama imejiingiza kwenye siasa.
Sasa tunapiga kura za hasira njema.
 
Lema kavulia ubunge rasmi...

Hii ni taarifa rasmi toka hapa mahakamani!

Habari kutoka Arusha zinasema wako tayari kulipa jiwe ubunge kuliko magamba CCM, But serikali inaingia gharama bila sababu za msingi kwani matusi kwenye kampeni ni ya kawaida kabisa
 
Sijui ni na nani anaongoza hii nchi kwa sasa hivi maaan chama chenye serikali (CCM) kiko busy na chaguzi. Mawaziri walifunga ofisi na kuhamia Arumeru Mashariki, sasa watahamia Arusha Mjini, ni lini wanafanya kazi? Miaka 5 itaisha bila kufanya chochote, sjiui 2015 watasema nini hawa CCM?
 
Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kupitia CHADEMA, amepoteza kiti hicho kwa kuenguliwa na Mahakama katika kesi iliyokuwa inamkabili ya kupinga ubunge wake.


UPDATE: Audio imepachikwa hapo baada ya maneno yafuatayo...


Kesi hiyo iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM, Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Mollel (44) ambao walikuwa wanamtuhumu Mbunge huyo kwa kutoa kauli za udhalilishaji, matusi na kashifa kwa aliyekuwa mgombea wa Ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Dkt. Batilda Buriani.


Hukumu hiyo iliyosomwa na Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila.


Katika hukumu hiyo, Lema hakuondolewa haki ya kugombea ubunge huo kwa kuwa kosa lililomtia hatiani ni matumizi mabaya ya lugha tofauti na ilivyodhaniwa kuwa ni vitendo vya rushwa. Uamuzi wa kugombea ama kutokugombea kiti hicho tena utatokana na maamuzi yake mwenyewe na ridhaa ya chama chake ikiwa kitamteua na kumpitisha kugombea.


Taarifa za watu wa karibu zinasema kuwa Lema hatakata rufaa mahakamani juu ya hukumu ya kesi hiyo, bali atakata rufaa kupitia kura ya wananchi wa Arusha Mjini wakati wa kugombea kiti hicho.


Hivyo tutarajie uchaguzi mpya ndani ya siku 90. Tanzania, nchi ya uchaguzi kila uchao...!


Kweli tunahitaji Katiba Mpya yenye kukidhi haja na inayoendana na wakati.


Source: UPDATED: Habari mpya muda huu: Jimbo la Arusha halina mbunge! - wavuti.com 
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom