Uchaguzi 2020 Godbless Lema: Arusha leo kuna Mechi ya Simba bure na Tamasha la Wasanii bure ili kuhujumu Mkutano wa Tundu Lissu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,585
142,884
Mgombea ubunge jimbo la Arusha Mjini Ndg. Godbless Lema amelalamika kuwa CCM inawahujumu kwa kuandaa mechi ya Simba bila kiingilio na Tamasha la Wasanii bure ili kuhujumu mkutano wa mgombea urais wa CHADEMA Ndg. Tundu Lissu.

Hata hivyo Lema ameapa kuwa leo ndio CCM watajua kwamba CHADEMA ni baba lao Arusha.

Lema amesema haya katika ukurasa wake wa Twitter.

My take: Kwani sehemu anayoenda Lissu ni lazima shughuli zisimame?

Maendeleo hayana vyama!
 
Lema hana cha kufanya sasa hivi amebalki kuwa mtu wa kulalamika tu mbona kwenye biashara unakuta maduka yamejipanga mstari mengii tena yanauza bidha moja na kila mtu anauza mboona hawafungi? Hivyo wacha CCM wafanya shughuri yao naye lema afanye mkutano wake akipata watu kumi wanatosha kuwahutubia hao.
 
Mkuu, hili la bure si kweli, jana nlkuwa kwenye game, na usiku gari la matangazo lilikuwa linataja kiingilio. Sababu zingine ni za kitoto kabisa. Kwa hiyo ile siku ya jana ya mwananchi mbona hamkulalamika?

Kama unajiamini, kuna haja gani kuanza kulalama mitandaoni? Your poor campaign strategy, usiwe mzigo Kwa wananchi. Ama kweli kama nilivyosema Chadema haina mathink tanks kwa sasa.
 
Back
Top Bottom