Uchaguzi 2020 Lema: Msafara wa mgombea Urais, Tundu Lissu washambuliwa vibaya katika Ofisi ya CHADEMA Wilayani Hai, Kilimanjaro

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,833
23,135
Aliyekuwa Mbunge Arusha Mjini, Godbless Lema kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Twitter amesema msafara wa Tundu Lissu umevamiwa katika Ofisi za Chama hicho Wilayani Hai

Amesema "Msafara wa mgombea Urais Mh Tundu Lissu umevamiwa na kushambuliwa vibaya katika ofisi ya CHADEMA HAI,magari yame haribiwa. Mgombea Uraisi na Team yake wako salama. Polisi wako lakini wana shuhudia, mkutano umevunjika. Taarifa kamili kuwajia"

1.PNG
 
Hii ni hatari kwa mstakabali wa Taifa,vipi upande wa pili wakiamua kujibu mashambulizi.

Wote kwa pamoja tukemee bila kujali vyama vyetu, maana hali ikibadilika haiangalii ulishiriki ama hukushiriki.
 
Duuuh, inamaana makamanda wameshambuliwa na migambo au imekuajee!

Kuna wale tuliokua tunawaambia kuwa adui wa Chadema ni Mlevi mkuu Mbowe wakawa wanabisha na kutoa lugha za kejeli.
Oooh, Mbowe ndiye anayeijenga Chadema ma wengine ni Wasaliti. !!! Imekuaje ameshindwa kujenga Chama nyumbani kwake mpaka vibaka wanawashambulia?

Kama hii ishu ni kweli Mbowe ajitathimini mana atakua ameandaa hayo magenge nyumbani kwekwe. Hakiwezekani ngome ya Chama itekwe na wahuni na vibaka na kumsumbulia Mgombea urais. Aibu kubwa kwa Mbowe wala si vinginevyo.
 
Back
Top Bottom