Godbless Lema aazimia kuondoa kazi za Diamond YouTube/Facebook

Diamond asingekuwa mkubwa kuzidi chadema viongozi wako wasihangaika kupambana nae.

Chadema ni fungu la kukosa
 
Mbowe ana wakati mgumu sana aisee... huyu ni mjumbe wa kamati kuu pamoja na huu uozo wake. DIAMOND ataiangusha CHADEMA.
 
Ajabu wanaofanya hivi, ni watu wanajitanabaisha kuipigania demokrasia, hivi demokrasia nini.
Nilitegemea wao kuwa mdomo wa kumlainisha huyo kijana kubadili msimamo wake, badala ya kumkwamisha shuguri zake.

Haya ndiyo wanayoyalalamikia wao, kufanyiwa na serikali iliyopo madarakani, kumbe wanalalamika tu sababu wako nje.
 
Mwenye kipande cha track ya Diamond akiimba "wapinzani tunawapiga risasi" tafadhalini,naomba akiweke hapa.
 
Sifurahii mtu afeli mambo yake, ila katika hali ya kawaida kama ni mimi nipo ndani ya familia, vipigo na manyanyaso lakini ndugu yangu hanitetei wala kunitafutia msaada, ila anawasemea na kuwatetea majirani, siwezi kumuelewa.

Japo kua alichofanya ndugu Diamond si uungwana, kama binadamu namuelewa, alikaa kimya kulinda mkate wake, wengi tunafumbia macho madhaifu ya serikalini humu tunakofanyia kazi hata mtaani, maana ukiropoka tutakuokota baharini.

Ila kwa mwenzetu ni tofauti, yupo kwenye spotlight, he had to choose between the people or the government. He made his choice, the price has to be paid. Ni ngumu kuelewa hasira na maumivu ya kina Kigogo na wengineo kama wewe sio victim wa yaliyotokea ndani ya kipindi cha Jiwe.

Mungu atusaidie
 
Hivi tumeishiwa maadui wa kupambana nao ?

Na katika hao maadui simaanishi CCM, bali Ujinga, Maradhi na Umasikini..., nadhani tuwekeze nguvu zaidi huko

Diamond tumpime kwa kazi zake na sio choice yake..., ikiwa hivyo mbona hatupigi kelele kwa Mama Samia Kuwa Rais wakati na yeye alikaa kimya ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…