Godbless Lema: Samia ni Rais bora ambaye hajawahi kutokea Tanzania

Billal Saadat

Senior Member
Nov 30, 2022
169
356
Kupitia kwenye ukurasa wa Twitter, aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini na Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Kaskazini Godbless Lema ameandika:

“Mh Rais SSH kama akiendelea kujenga Demokrasia yenye sura hii kutoka Moyoni mwake bila hila, bila shaka anaweza kuja kuwa kati ya Rais bora kabisa Tanzania kama sio Africa. Siasa ni ushindani. Katiba bora na Tume huru ya Uchaguzi ndio Majaribu yake muhimu.”

Siku ya leo Umoja wa Wanawake wa Vyama vya Siasa Nchini vyenye usajili rasmi, (ULINGO) waliaandaa mkutano maalum wa kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan katika sherehe zilizofanyika uwanja wa Uhuru Dar es salaam.

A8DDE1DB-3A73-48DC-B33C-EFAA84D8220C.jpeg
 
Sio tuu Demokrasia Bali hata intelligence yake ni kubwa kuliko hao waliokariri mavitabu harafu hawajitambui wafanye nini wapi wakati gani na namna vipi..

Umewahi kuona Rais Samia anavunjika Moyo kisa eti ametukanwa etc? Ana uvumilivu mkubwa ambao hata Mimi nisingeweza maana Kuna watu Wana maudhi kweli..

Mwisho Mwendazake miaka 5 kazalisha bil.400, Samia miaka 2 kazalisha Bil.800.

Magufuli full visingizio mara mabeberu sijui wasaliti mara aseme tunajenga miradi mengine yasubiri ila Samia hakuna visingizio na hakuna kilichosimama.

20230319_204523.jpg
20230319_204426.jpg
20230319_081021.jpg
20230319_175908.jpg
 
Ni vigumu sana kwa Lema kunena maneno mazuri kama hayo kwa Bosi wake mwenyewe Dikteta wa CHADEMA.[chaguo ni lako] ndivyo walivyo.
“Mh Rais SSH kama akiendelea kujenga Demokrasia yenye sura hii kutoka Moyoni mwake bila hila , bila shaka anaweza kuja kuwa kati ya Rais bora kabisa Tanzania


Hakika kama alivyosema SSH akiwa na wanamama+19, kiunagaubaga 'wamesha kubaliana yeye ndiye wa kuwavusha wananchi 2025'

Lema yuko sawa, Hakuna Demokrasia CHADEMA, CCM ndiyo demokrasia inavotakiwa kuonekana.
 
Hayo ni yao wanasiasa ambao bodaboda kwao ni laana, ugali kwao ni umaskini, pengine amesahau kusema kusomesha watoto St. Kayumba ni uchuro

Hawa ni wale ambao wakiugua anaweza kwenda hata SA kujitibu mafua.

Wao hata kitunguu kikiuzwa 1000 kwao bado ni affordable.

Kuna mama na watoto hadi muda huu hawajauona usiku. Mwingine mama yupo barabarani kwenye kituo anauza karanga na pipi apate buku ya kununua vidagaa akawapikie wanawe ugali hiyo saa sita usiku akirudi.

Maisha magumu, vitu bei juu. Mtu wa kawaida kusikiliza maneno ya wanasiasa haramu ni sawa na mbwa kumuachia msikiti.
 
Kupitia kwenye ukurasa wa Twitter Aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini na mwenyekiti wa Chadema kanda ya Kaskazini Godbless Lema
Ameandika
“Mh Rais SSH kama akiendelea kujenga Demokrasia yenye sura hii kutoka Moyoni mwake bila hila , bila shaka anaweza kuja kuwa kati ya Rais bora kabisa Tanzania kama sio Africa.Siasa ni ushindani.Katiba bora na Tume huru ya Uchaguzi ndio Majaribu yake muhimu.”

Siku ya Leo umoja wa Wanawake wa vyama vya Siasa nchini vyenye usajili rasmi. (ULINGO) waliaandaa mkutano maalum wa kumpongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika sherehe zilizofanyika uwanja wa Uhuru Dar es salaam.
Naunga mkono hoja
P
 
Kwa sasa lazima wanasiasa mumpongeze Samia kwa sababu wanasaidiana kuimaliza hazina!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom