Taasisi zote za Serikali zijitoe katika mtandao wa Twitter X

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,843
9,245
Hili wazo limenijia kitambo ila nilikuwa bado sijapata msukumo wa kuliwasilisha.

Kuna kipindi mtandao wa Twitter ulikuwa ni uwanja unaoheshimika, ukijaa malumbano ya kisiasa na kijamii na kuna kundi fulani la raia ilikuwa imejikita kule katika kukosoa na "kuirekebisha" serikali. Ikafika wakati Serikali nayo ikaona ina ulazima wa kuwa na uwepo wake mule ili kupambana uso kwa uso na hoja zinazotolewa lakini pia kuhabarisha umma kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea nchini maana ilionekana siyo tena mtandao wa kuudharau.

Bahati nzuri au mbaya (kutegemeana na utakayemuuliza) huu mtandao siku hizi umekuwa ni uwanja wa video za porno. Twitter hawana sheria zilizo thabiti kuzuia maudhui ya namna hii. Siku hizi hauhitaji VPN wala nini, unaweza kukutana na kitu kizito katika uzi wowote hata ambao hautarajii. Nadhani ni suala la muda kabla hatujaanza kuona Rais au Ikulu imepost jambo muhimu halafu chini kuna mtu akatupia video ya kugegedana, ikabadili kabisa muelekeo wa post ya mwanzo. Hii itakuja kuleta shida.

Mimi nashauri Serikali ibaki tu katika mitandao ya Instagram, Youtube na Facebook au hata WhatsApp Channel, ingawa huku nako nadhani hakuna ulazima. Hakuna haja ya serikali na taasisi zake nyeti kuwa katika kila mtandao wa kijamii maana wasomaji ni wale wale tu na ni aina fulani ya matumizi mabaya ya rasilimali za nchi.

PS. Pia nahusia taasisi zote za Serikali zijiunge Jamii Forums na wawe active katika kupokea na kufanyia kazi malalamiko, ushauri na mapendekezo ya wadau.
 
Baada ya kubadilisha jina na kuitwa 'X' ndo picha za porn zimeongezeka. Nyuzi nyingi Zina pilao la hatari lisilokuwa na vimiti miti ka la sikukuu ya jana
 
Kudadaki zako tatizo lako una follow watu wa hovyo ndo maana hayo mambo lazima yawepo kwenye account yako. Bata wewe
Hata Shetani mwenyewe nilikuwa simfollow ila kwa jinsi ule mtandao siku hizi ulivyo, si kazi kukutana na feed za vyombo
 
Twitter niliyokua naisikia na content zilizopo saivi ni tofauti mno..

Twitter zamani ilikua official social media, ila kuna wajinga wamegeuza kuwa ni kijiwe cha upumbavu
Isijekuwa ni kampeni ya mfumo kuupotezea uaminifu maana kuna wakati ulikuwa unasumbua sana ule mtandao
 
Hili wazo limenijia kitambo ila nilikuwa bado sijapata msukumo wa kuliwasilisha.

Kuna kipindi mtandao wa Twitter ulikuwa ni uwanja unaoheshimika, ukijaa malumbano ya kisiasa na kijamii na kuna kundi fulani la raia ilikuwa imejikita kule katika kukosoa na "kuirekebisha" serikali. Ikafika wakati Serikali nayo ikaona ina ulazima wa kuwa na uwepo wake mule ili kupambana uso kwa uso na hoja zinazotolewa lakini pia kuhabarisha umma kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea nchini maana ilionekana siyo tena mtandao wa kuudharau.

Bahati nzuri au mbaya (kutegemeana na utakayemuuliza) huu mtandao siku hizi umekuwa ni uwanja wa video za porno. Twitter hawana sheria zilizo thabiti kuzuia maudhui ya namna hii. Siku hizi hauhitaji VPN wala nini, unaweza kukutana na kitu kizito katika uzi wowote hata ambao hautarajii. Nadhani ni suala la muda kabla hatujaanza kuona Rais au Ikulu imepost jambo muhimu halafu chini kuna mtu akatupia video ya kugegedana, ikabadili kabisa muelekeo wa post ya mwanzo. Hii itakuja kuleta shida.

Mimi nashauri Serikali ibaki tu katika mitandao ya Instagram, Youtube na Facebook au hata WhatsApp Channel, ingawa huku nako nadhani hakuna ulazima. Hakuna haja ya serikali na taasisi zake nyeti kuwa katika kila mtandao wa kijamii maana wasomaji ni wale wale tu na ni aina fulani ya matumizi mabaya ya rasilimali za nchi.

PS. Pia nahusia taasisi zote za Serikali zijiunge Jamii Forums na wawe active katika kupokea na kufanyia kazi malalamiko, ushauri na mapendekezo ya wadau.
Well said bro
 
Back
Top Bottom