Anaeamua kipi kibaya na kipi kizuri ni nani?
Wewe au Nani.
Matsunani na matetemeko yana amuliwa na nani?
Pharmaceutical companies wanatamani magonjwa yaongezeke wapate kuuza dawa.
Na hospital binafsi zinatamani wagonjwa waongezeke ili biashara iwe nzuri.
Kwaiyo kwa matakwa yao ya watu wachache kunaondoaje dhana ya mabaya ambayo yanawakumba watu wengi eti kisa tu wao wanatamani wagonjwa waongezeke??
Unaweza kumuacha muuaji aliyeteketeza familia yako unayoipenda kwasababu alitamani misiba iwe mingi ili apate sehemu ya kula?
Kama wanatamani wagonjwa waongezeke ili wapate kuuza dawa mbona kuna dawa zinatolewa bure? Huoni hapa nia yao si tu kuuza dawa bali ni kusaidia kupunguza magonjwa ambayo hata wao hawapendi yawakumbe raia??
Mashirika na watu binafsi yanayoshughulikia Habari za VIFO na Mazishi na wao wanatamani Vifo viongezeke wafanye Biashara.
Hao watu wanaoendesha hayo mashirika nao wanatamani wote wafe?
Tsunami na matetemeko yanafaidisha wengi mno tofauti kabisa na wewe unavyoelewa.
Hujaelezea ni kwa namna gani yanafaidisha, na hata ukielezea haitaondoa ubaya wake na ndio maana hakuna mtu anatamani kua mhanga wa tsunami na matetemeko
Watengeneza Silaha wanatamani vita visiishe ili wauze Silaha.
Kwani hao watengeneza silaha wao wanatamani wafe waache kazi yao pendwa ya kutengeneza silaha ili wauze??
Sasa nani mwenye kuamua kipi kizuri ktk Hii Dunia ? Na nani apewe hicho anachotaka?
swali la "nani" halitakua na mantiki kwenye mabaya yanayoletwa na tetemeko pamoja na tsunami
Au hujasikia msemo usemao "kwako kilio kwangu sherehe?
pia kuna msemo usemao "leo kwangu kesho kwako" anefurahia kilio cha mtu siku naye atakuja kufiwa atapata machungu kama aliyopata mwenzake. Msemo huu unamaanisha kilio ni jambo baya na sio jambo la kufurahia pindi linapomkuta mwengine
Kazi ya kipi kizuri kwetu na kipi kibaya ni KAZI YA MUNGU.
Kama mabaya ni kazi ya mungu sasa kwanini mseme shetani ndiye chanzo?
Wewe funga mkanda ujiandae tu chochote utakachopangiwa.
Hata kwenda haja kubwa wewe huna hiari kweli utaweza kujua kipi kibaya au kizuri kwako?
Haja kubwa nayo ni imperfection kuonesha sijaumbwa na mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.