Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,148
- 10,573
Hivi karibuni kwenye mijadala ya harusi, gumzo limekuwa kadi za mchango. Ukitazama kadi, single unachangia elfu 50, double elfu 90. Hapo mtu anajisikia kama amenunua Tiketi ya Mechi fulani, kumbe unakwenda kuwapiga tafu watu katika harusi yao. Lakini ukifika, unakutana na ujumbe kuwa: “Chakula hakipakuliwi kiholela, kuna catering service waliobobea katika kupakua chakula.”
Sasa mtu anabaki kushangaa, hivi hela yangu niliyoitoa kwa moyo mmoja ni mchango au ni tiketi ya chakula cha kupimwa? Kwanini kwenye harusi watu wanajiona kama wameingia kwenye mgahawa wa five star hotel ya Dubai? Na mbaya zaidi, ukitamka kidogo tu, “mimi leo nataka nyama tu,” unachunguliwa kana kwamba umetukana bibi harusi mbele ya maharusi wote, na wakati mwingine kupewa mifupa.
Jamani, kama mtu hajui, nyama ndiyo kiburudisho kikuu wa sahani. Wali, ndizi na chapati ni wachezaji wa akiba tu. Mchango wangu ni kama mzazi wa mjukuu, siwezi kupewa kipimo cha kijiko kimoja cha nyama eti kwa sababu kuna “uwiano.”
Lakini, tuseme ukweli, hizi harusi zetu zinatufundisha kitu: mchango si bei ya chakula, ni kuunga mkono. Ila basi, wenyeji wakumbuke, ukimpa mtu kadi ya mchango, usimfanye ajisikie kama ameingia kwenye jaribio la kidiplomasia la kula kwa mizani.
Weka ucheshi, acha watu wale mchele, nyama ipate wadau, na watu wabaki na kumbukumbu tamu badala ya kumbukumbu za kuhesabiwa idadi ya nyama.