Gharama ya kujenga chumba na sebule master

Gharama ya kujenga chumba na sebule master

Watu mnapenda kubanana mjini huko.... Viwanja mlandizi,kibaha,kibamba n.k huko unapata tena kwa bei nzuri kabsaaa
 
Ukiamua kuingia bila kujali finishing labda ila sio uhakika, cha kufanya we anza kujenga uone utakapoishia hiyo hela usile bata. Kupunguza gharama kama eneoni halina maji chimba msingi na simamisha tofali, kisha piga bati na chimba shio la la kupokea uchafu wa chooni, madirishani weka nondo na mapazia, nunua mlano wa nje, uone ikiwa hiyo itatosha kazi hizo, ikitosha ingia, uanze kujikusanya kwa umeme na maji.
 
Umetumia ramani gani mkuu!!?

Chumba kimoja cha master nimetumia tofali 500 za block, bati 21, mbao 40, mifuko ya simenti 17, nondo 2, mchanga trip 4, ukijumlisha na vitu vingine vidogo vidogo kama maji, misumali, nk imetumika 3.7 mil pamoja na fundi. kwa hesabu hiyo choo hesabu yake haimo, lakni kama anajenga mbao za kwake, maji ya kwake, mawe ni ya karibu, mchanga ni wa karibu, anaweza kumaliza au kuongeza kidogo.


Inawezekana ukubwa wa master bedroom yako ndio size ya chumba na sebule ya mtu mwingine....master bedroom nyingine bafu ni kama chumba,kuna walk in closet etc.
 
inawezekana mkuu.ila usimamie kila kitu we mwenyewe na material ununue kwa wingi maduka ya jumla pamoja.it is possible mkuu
 
mimi ni quantity surveyor nafany uthaman wa majengo na ukadiliaji wa majengo nicheki kwa 0753757303 nikusaidie hiyo hela namna ya kukadilia na ntakuandalia boq kabisa na yeyote mwingine nachora na michoro
 
Inatosha mkuu mpaka vyumba viwili ukitaka , kama utakuwa na mkanganyiko na upo Dar nitafute PM nitakudadavulia zaidi na ramani simpo ntakupa. mi nimejenga kwa ngarama ndogo zaidi ya hiyo na nipo Dar .
 
Mil 5 haitoshi hata kidogo acheni kumchanganya na maheasabu yaiso na ukweli wowote
 
Haitoshi jamani! hapo atajenga mpaka kupaua labda na grill za madirisha tu! finishing hapo itakuwa bado, kwa uzoefu wangu, hiyo hela ni gharama ya kujenga choo na shimo lake.
 
Back
Top Bottom