Gharama ya kujenga chumba na sebule master

Gharama ya kujenga chumba na sebule master

Kabla sijajua hata ukubwa wa nyumba, haiwezekani

Weka mchanganuo wa gharama
1. Paa(mbao,bati,fundi)
2. Madirisha,milango
3. Gypsum,tiles

sipo hapa kukupa mchanganuo..kama unataka breakdown ni watsapp 0712 507060 niku screen shot daftari la mchanganuo
tusichoshane
 
Au sijaelewa,anauliza sebule na chumba (master room) lkn comment zinaongelea nyumba zima.
 
Nimechoshwa na haotoshi zenu! hebu wekeni sawa kwa nini haitoshi kimahesabu hapa!

Itawekwaje sawa wakati yeye hajaonyesha hata vipimo vya nyumba yenyewe?!
Kila mtu akikisia vipimo vyake ndiyo itazidi kumchanganya..
 
mimi ni quantity surveyor nafany uthaman wa majengo na ukadiliaji wa majengo nicheki kwa 0753757303 nikusaidie hiyo hela namna ya kukadilia na ntakuandalia boq kabisa na yeyote mwingine nachora na michoro

Mmmmmh Qs na kuchora wapi na wapi?
 
Kujenga chumba na sebule ya kawaida bila mbwebwe za aluminium ,tiles unamaliza. Ila hutakuwa na shimo la choo.
Choo peke yake kuchimba, kujenga na kufunika si chini ya 3m.

Mkuu hicho choo unakichimbia wapi mwanza au mbona unadanganya sana
 
Maghufuri NA lowasa waseme kama watashusha bei ya cement had I sh.4000 mfuko halo utajenga
 
Mmmmmh Qs na kuchora wapi na wapi?
Unaweza ukawa na uwezo wa kufanya vyote ila ukajikita upande mmoja Zaidi! mfano hai mimi nipo katika biashara ya utalii lakini ni professional artist in my spare time(wa uchoraji)vileveile! yaani nafanya vitu viwili tofauti kimoja kinataka nikimbie na wakati (tourism industry)kingine kinakula all the time you have (painting /sketching needs patient).
 
1- Tofali1800 @ 1000/= Tshs 1,800,000/=
2- Cement 30bags @13,500/= Tshs 405,000/=
3- Mchanga 5 lories @ 150,000/= Tshs 750,000/=
4- Chuma/Nondo 30pcs ya12mm @ 16,000/= Tshs 480,000/=
5- Zege 13.2 cubic metre @ 225,000/= Tshs 2,970,000/=
6- Labour charges = Tshs 1,000,000/=
7- Gharama nyinginezo = Tshs 500,000/=

Jumla ni 7.9...milioni


Huo ni mchanganuo wa gharama za ujenzi wa msingi tu peke yake na ikizingatiwa nyumba ni msingi usije jidanganya ukalipua ujenzi wa msingi itakugharimu sana baadae. Ok fikiria mpaka hapo...sasa tunafikia milioni 7.9

Msingi unaotumia mchanga lori tano ni wa ghorofa?
Jamaa kauliza gharama za kujenga master bed room,acheni kumtisha hiyo hela inatosha kabisa
 
Kuna kampuni moja iliwahi kujenga kakibanda ka mlinzi ka getini na walitumia milioni arobaini... Sasa mpaka hapo nakata tamaa ya kukushauri...
 
Umetumia ramani gani mkuu!!?

Chumba kimoja cha master nimetumia tofali 500 za block, bati 21, mbao 40, mifuko ya simenti 17, nondo 2, mchanga trip 4, ukijumlisha na vitu vingine vidogo vidogo kama maji, misumali, nk imetumika 3.7 mil pamoja na fundi. kwa hesabu hiyo choo hesabu yake haimo, lakni kama anajenga mbao za kwake, maji ya kwake, mawe ni ya karibu, mchanga ni wa karibu, anaweza kumaliza au kuongeza kidogo.
3.7 inaweza kueleweka ila mchanganuo wake una mushkeli. mchanga trip 4 za lori au guta???? haiwezekani unless hicho chumba ni size ya madarasa mawili kwa viwango vya serikali. Nondo 2 au 20? msingi unahitaji nondo pembe zote na linta nayo inahitaji nondo.
 
wadau niaje?

naombeni msaada kwa bajet ya milion 5.. unaweza ujajenga chumba (master) na sebule mpaka kikakamilika kila kitu

KIWANJA NINACHO TAYARI. HELA HII NI UJENZI TU
mwaka na miezi kadhaa imepita toka post yako hii. Naomba mrejesho ulifanikiwa au ndio ulikatishwa tamaa? nategemea mrejesho wako ili na mimi nifanye maamuzi kama yako.
 
1- Tofali1800 @ 1000/= Tshs 1,800,000/=
2- Cement 30bags @13,500/= Tshs 405,000/=
3- Mchanga 5 lories @ 150,000/= Tshs 750,000/=
4- Chuma/Nondo 30pcs ya12mm @ 16,000/= Tshs 480,000/=
5- Zege 13.2 cubic metre @ 225,000/= Tshs 2,970,000/=
6- Labour charges = Tshs 1,000,000/=
7- Gharama nyinginezo = Tshs 500,000/=

Jumla ni 7.9...milioni


Huo ni mchanganuo wa gharama za ujenzi wa msingi tu peke yake na ikizingatiwa nyumba ni msingi usije jidanganya ukalipua ujenzi wa msingi itakugharimu sana baadae. Ok fikiria mpaka hapo...sasa tunafikia milioni 7.9
Jibu Kutokana na swali mkuu acha upoyoyo
 
Unajenga, ila unatakiwa wewe ndio uwe msimamizi. Vifaa unaenda kununua wewe mwenyewe au pamoja na fundi.
Usimwachie fundi peke yake.
Anapojenga simamia vifaa na material kuhakikisha hakuna kinachopotea.

Kuna mafundi wasio waminifu, endapo hakuna usimamizi wanatoa hesabu za uongo ili wapate cha juu.
Au wanapojenga wanapunguza viwango halafu vifaa vinavyobaki wanauza. Sehemu ya kuweka nondo nne wanaweka mbili.
 
Back
Top Bottom