Gharama ya kujenga chumba na sebule master

Gharama ya kujenga chumba na sebule master

Inategemea unataka chumba cha ukubwa gani na ubora gani. Hiyo hela hata kwa udongo unamaliza hicho unachotaka
 
Inatosha na chenji inabaki hata Kama huna kiwanja.

1.Nunua kiwanja cha 1m vipo 15 kwa 15.

2.Chimba karo moja tu laki 1 na nusu,kulijengea na kulipiga zege kwa juu utaongeza laki 3 itajumiasha kokoto za elfu 80,cement 50k,mchanga yebo ya 50 na ufundi 120k.

3.utanunua tofali 700 sh 700k kuzijenga zote Hizo ni 250k gharama ya kuchimba msingi ni 40k.

4. Nunua bati 20 kwa 240k nunua mbao 20 za 4 by 2 na 20 za 2 by 2,gharama za mbao ni 240k na vifaa vidogo waya,misumari jumla 20k na ufundi 100k.

5.Nunua Dirisha 3 kwa 240k na mlango mmoja tu wa mbele kwa 150k na ufundi kuweka 40k.

6.Nunua yebo mbili kwa 100k na cement mifuko 10 kwa 120k kwa aioli ya floor na plasta ndani.

Kuna chenji Kama 1m imebaki kwa ajili ya nyavu dirishani,plaster nje,kuweka wiring,kununua pipe za chop,kununua sink la chop etc......Chenji inabaki bado.

Savimbi Jr wapi kuna kiwanja cha 1m dar es salaam?
 
Last edited by a moderator:
Inawezekana .Mimi ni Fundi ujenzi . Nipatie hilo dili.
 
Kwa ufupi haitoshi ndugu! Bt unaweza anza kidogo kidogo. Nunua material weka site au wekeza kwenye duka la vifaa vya ujenzi kidogo kidogo ukihakikisha una material zote tafuta hela ya fundi anza ujenzi.
Kujenga inawezekana na hakuna muujiza ktk kujenga. Usiogope unaweza kujenga zaidi hata ya chumba sebule.
Ukitaka fundi muaminifu nipm kuna fundi mzuri alinifanyia kaz zangu kwa uadilifu na uaminifu sana
 
nyumba ni kitu cha kudumu mkuu, hupaswi kukurupuka!tafuta raman nzuri unayoipenda then anza kujenga msingi kwa kutumia hyo 5m. Kikawaida kwa standard residential house 5m yatosha kumaliza foundation kabsa. Then endelea kuchapa kaz kwa juhudi na kila sent utakayopata sasa waeza peleka tofal kidogo kidogo site na mwsho wa siku utajikuta zishatimia za kufikisha mjengo wako kwenye lintel. Give yourself time, usichoke kulipa kodi, lipa tu ila mwsho wa siku wahamiakwenye nyumba nzur inayoeleweka.
 
hii point nzuri, naona hata mimi itanifaa tu!!
 
mie nilikua na gofu, nikalipaua weka bati , gypusm tiles umeme , bafu ndani kwa 6 mil

so approx apo unaweza ,,,kama una kiwanja utafanikiwa
 
Back
Top Bottom