Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

Ndugu zangu watanzania kwanza tupeane pole kwa yaliotukuta na yanayoendelea kutukuta nasema hivi maana inaonekana huu ni muendelezo wa kila sehemu yalipo mabomu ya jeshi
Habari zaidi kutoka jeshi la polisi zinasema mabomu 4 yaliobaki ambayo inasemekana ni hatari zaidi kuliko yalliolipuka na huku mtaalamu wao alielipua mabomu kule mbagala akikataa kushiriki kuyalipua haya yalobaki jeshi la polisi linatazamia kulipua hayo mabomu SAANANE ZA MCHANA local time

Hivyo hivi sasa kuna maandamano barabaran na pembezoni watu wakiondoka maeneo ya gongolamboto na kwingineko wakiwa wanatembea bila kupenda akika ni mazoezi yanayotuonyesha kumbe hata hwa jamaa wa gym wanakula hela zetu bure kama tukiamua kweli kweli..namwona bibi vizee zaidi ya watatu wakitembea kama wako darasa la saba na speed kali hakika ni hali tete ni vizuri rais nae akaja kuona shida wanayopata watanzania badala ya kusubiri CHEKI za DOWANS ZINATOKA LINI AMA LINI MKATABA MPYA UNAANDIKWA KUTUMIA MITAMBO YA DOWANS
 
Maskini jeuri sio Mtanzania nini? manake anasema poleni sana watanzania as if yeye sio mtz, Mimi naona huo ni uzembe wa serikali na wanaohusika na vyombo vya dola....ilivotokea Mbagala wangechukua tahadhari mapema...hapa ni dar...kule Moro ghala liko milima ya uluguru kwenye mahandaki sijui yakilipuka itakuwaje..milima itafunika mji...Serikali ichukue tahadhari mapema
 
Habari za kuaminika ni kwamba ghala hilo huwa linalindwa na askari wenye bunduki ambao hawana redio za mawasiliano. Yaani hata hawa walinzi wa uswazi wanakuwa na vijiredio vya upepo sembuse hawa wa jeshi la ulinzi wa Taifa?

Jiulize chukua tahadhari!
 
Kwa wale wanaotarajia kusafiri hivi karibuni jana tulipokea memo kutoka TAA kusema wamefunga uwanja kwa siku tatu ndugu zetu wa airline mnaombwa kwa heshima na taadhima kuwafahamisha abiria wenu na sikuwaacha waende kujazana kama mahujaji pale airport walipodanganywa ndege yao
Tuna amini mteja mfalme tuwape heshima zao...hakika hilli janga la kitaifa

Haitoshi tuu kufunga bila alternatives. Kwa nini ndege zizielekezwa kutua KIA? au abiria waelekezwe kwenda kupandia Nairobi? Ule uwanja wa Zanzibar una hadhi ya kimataifa au ni kwa ajili ya ndege ndogo tuu? Mipango yetu mibovu ya kutokuwa na alternatives kwa vitu vingi sasa inajidhihirisha tukianzia na uwanja wa ndege!!!!!
 
Nimetaarifiwa na ndugu yangu wa huko Gongolamboto ambaye anasema ameshuhudia mabomu mengi yakipita juu ya nyumba yake. Moja lilipiga nyumba ya jirani yake na kusambaratisha kabisa, bahati nzuri walikuwa wamekwishakimbia. Mabaki ya bomu hilo yamechukuliwa asubuhi. Bomu moja kubwa lilipiga sehemu ya nyumba yake na kwenda kuanguka kwenye choo chake cha nje, hilo halikulipuka. Askari wamekuja mara mbili asubuhi hii lakini wameshindwa kulichukua maana ni kubwa sana, na halijalipuka.

Familia yake yote ilitawanyika usiku, ni yeye pekee yake alibaki hapo nyumbani, akisali usiku kucha. Mmoja wa wanafamilia alikuwa mgonjwa, alikutwa na wasamaria wema njiani akijikongoja wakamsafirisha kwa ndugu zetu huko Mikocheni. MMoja wa wanafamilia kabla ya kukimbia alikuwa ameumia mkono lakini haukukatika. Namshukuru Mungu kwa kuwanusuru, na ninawapa pole sana wale waliopoteza ndugu, kuumia na kuharibiwa mali na nyumba zao.

jamani sasa umefika wakati wa sisi watanzania kukumbuka mambo muhimu kama vile bima za maisha na property zetu ...... tumesahau sana insurance covers .... tena sasa hivi sio gharama kubwa sana ..... tunalamba bia tuu hata kama zinapanda bei
 
Kuzi-direct hizo flights to KIA, au uwanja tuu unafungwa bila ya incentives za kufanya mambo mengine yasiwe at standstill mpk wa Nairobi watusaidie (plus huge revenues)? maana tuangalie pia na measures taken after a disaster! kuufunga bila hatua mbadala ni kuonyesha zaidi upungufu wa kufikiri wa serikali tulionayo! haina tofauti na watu wa Milembe! :sad:
 
.....ajiuzulu........ajiuzulu hebu wana jamii acheni kutaharuki, watajiuzulu wangapi??? Subirini mjue chanzo ni nini, hata huyo mnayemtaka atawale atakuwa na macho ya kuona nchi nzima??? Kuna watu wanajilipua sehemu mbalimbali mbona huko hawajiuzulu na ni nchi ambazo angalau zimeendelea kuliko sisi??? Watanzania kwa maelfu wanakufa kila siku kwa magonjwa yanayotibika mbona hamsemi waziri wa afya/rais ajiuzulu?? Waziri wa Ujenzi nae ajiuzulu maana ajali kila siku zinaua watu, Waziri wa Mawasiliano nae ajiuzulu simu zinaingiliana kila siku, Waziri wa habari,vijana na michezo ajiuzulu Yanga ilifungwa Ethiopia...Waziri wa Maji......nk.nk nk..Hivi matatizo yote yatakwisha siku moja???Huyo....mnayemtaka angeweza kumaliza matatizo yote haya??? Kumbukeni tunajifunza kutokana na makosa.. Acheni hizo....Mmetumwa au mmepatikizwa humu???? Waswahili walisema mfa maji haachi kutapatapa. Subirini 2015 msivizie matukio ili mpate cha kusema. mnakera!!!
 
Explosions at an ammunition depot at Mbagala army base in spring 2009 killed at least three people.

hii yakweli au BBC wanapotosha kuhusu 2009? yaani walikufa angalau watu 3 tu??

mkuu mi naona kama kuna neno "at least" lina maana yake. Ukumbuke siku zile za iraq waziri wa ulinzi na usalama marekan alisema atleast 2military men of USA are killed. Familia za Waliofikwa na mauti wakataka kuandamana kwani maaskari wengi walikuwa wamekufa. Baada ya kuwaeleza maana ya neno "atleast" wakaridhika,ila ingesemwa atmost ndo ingeleta kelele. Kwa ili mkuu sioni tatizo,japo nakasirika kuona idadi ya kweli haitajwi kwa matukio kama haya. Wanasema ni ajali,mbona dereva wa gari anapata ajali anapanda kizimbani? Basi waliosababisha ajali hii wawajibike.
 
PDIDY umezungumza la mana kabisa,badala ya watu kukaa na kudiscuss malipo ya dowans yatalipwaje(sio hayatalipwaje) wangeelekeza nguvu zao kuokoa raia G/Mboto.Sasa hivi akili za hawa DOWANS na mawakala wao zimeganda kwenye mkataba mpya unaondaliwa kuliokoa taifa(kama sio kulihujumu).HIVI NCHI HII IMELOGWA???????
Tunaingia mkataba na mwizi.
 
Hii kweli ni press release kutoka JWTZ??mbona haiko kwenye offical letter??na tena kwenye email ya bure 'yahoo' unataka kuniambia hawana website au?.....
 
Bila shaka nilitegemea waziri mchana huu atangaze kuachia ngazi na sii vinginevyo....
 
Waziri mkuu kasema mawaziri wa ulinzi, manbo ya ndani, mambo ya nje wameenda Dar, ila kanishangaza kwamba hata Mkulo waziri wa fedha nae kaenda maramoja!! kufanya nini? nimejiuliza au kulipa posho vikao vitavyoanza kukaa na kuzidi kuwapatia ulaji wakubwa!!
Kwani kama ni "kompasesheni" baado sana hadi mahesabu yaje yapigwe......
 
pdidy umezungumza la mana kabisa,badala ya watu kukaa na kudiscuss malipo ya dowans yatalipwaje(sio hayatalipwaje) wangeelekeza nguvu zao kuokoa raia g/mboto.sasa hivi akili za hawa dowans na mawakala wao zimeganda kwenye mkataba mpya unaondaliwa kuliokoa taifa(kama sio kulihujumu).hivi nchi hii imelogwa???????
Tunaingia mkataba na mwizi.

...................na aliyeiroga keshakufa zamaaaaaaaaaaaaaani!!!
 
- TBC ILISEMA WALITANGAZA WATU WAONDOKE HARASA SANA
- ITV WATU WAKIMBILIE MABONDENI
- ITV/CHANEL 5 WASIKIMBIE HOVYO
- tv ZINGINE WALIONYESHA MZIKI TUUU!
-TBC GHALA LINALOLIPUKA NI NAMBA 5 LINAUWEZO WA KWENDA 10KM
HALAFU HAWASEMI 10KM ZINAKOVER MAENEO GANI!? NCHI INAMATAAHILA HII!
PUMAVU ZENU SAANA, MNATUCHANGANYA KAMA ILIVYOKUWA DOWANS

Ahsante mkuu kwa kuliweka sawa hili,
Ni kweli media zetu zilikuwa zinachanganya, Chanel ten walisema Kisarawe, wengine watu waende mabondeni, wengine wasema watu waondoke haraka sana! Watanzania sisi ni kondoo
 
Hapa ndipo ninapochoka na TZ Mabomu teba halafu ni kwa mara ya Pili, ndani ya miaka miwili mabomu yanalipuka tena na kusababisha vifo. Haikubaliki....lazima Amiri jeshi mkuu, waziri mkuu, waziri wa ulinzi, na mkuu wa majeshi wakiuzulu mara moja. Wanataka wafe watanzania wangapi ndipo wajue kazi imewashinda, au wanataka maghalamangapi yalipuke ndipo wajue uongozi waliudandia, kama laa basi watuambie kuwa wakifa watanzania wangapi ndipo tujue wameshindwa kuongoza serikali? Watoke natoa wito watoke sasa?
 
Back
Top Bottom