Ghadaffi Alitawala miaka 41 (1967-2011), alikuwa na kitu gani cha ziada?

ward41

JF-Expert Member
Apr 3, 2022
398
1,398
Miaka 10 tu inatosha kupima uwezo wako wa uongozi. Ghadaffi ALITAWALA Miaka 41 ALIKUWA na KITU GANI CHA ZIADA?

Kuna watu wengi wanalalamika kupinduliwa Kwa ghadaffi Kwa madai ETI alikuwa na maono ya kuunganisha Africa, Kweli?

Mambo mengi kuhusu Ghadaffi yalikuwa propaganda. Miaka 41 Kwenye uongozi unatafuta Nini Tena zaidi ya kuharibu tu.

Naamini Libya itatulia na maisha yataendelea vizuri tu
 
Nchi nyingi za Africa zilizobadili viongozi mara kwa mara bado azina unafuu kuizidi Libya ya Gadafi ya miaka 41.
Tatizo kila kiongozi mpya anapoingia huanza na ajenda zake, hataki kuendeleza ya mtangulizi wake.

Na mataifa mengi hayana vipaumbele vya kitaifa hivyo kila kiongozi huamua cha kufanya.
 
Shida sio viongozi shida ni katiba za Africa zipo kwa ajili ya kuwalinda viongozi.Kama kweli tunataka maendeleo tuanze na katiba bora.Akina mgabe na mseveni wapo madarakani kwa miaka mingi lakini maendeleo hakuna.Katiba Bora ndiyo itakua dawa kwa mataifa ya Africa kupata maendeleo.
 
Nchi chache sana za Africa zimekuwa na utamaduni wa kubadilisha viongozi wakuu mara kwa mara, na katika hizo chache bado zipo ambazo huwa zinabadilisha viongozi kwa vurugu na wizi wa kura hivyo kuharibu hata hatua ndogo zilizokuwa zimeanza kupigwa.
Nchi nyingi za Africa zilizobadili viongozi mara kwa mara bado azina unafuu kuizidi Libya ya Gadafi ya miaka 41.
 
uarabuni wanatawala miaka hata 50 tena kwa kupokezana kwa kufata katiba... afrika rais bora kama gadafi haji kutokea kamwee yale maendeleo makubwa yakaja kuzimwa kwa kisingizio cha demokrasia na katibaa upuuzi sanaa..!! Apumzike kwa amani lakini kifo chake ni laana kwa LIBYA
 
Back
Top Bottom