Je, unafahamu ngoma ya Forever Young ya Jay Z alikuwa na maana gani?

Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
11,450
12,317
Nadhani watu wengi wanajua kwamba wimbo wa Forever Young, Jigga alimaanisha kwamba hazeeki, still ana muonekano wa ujana. Yes hii ndio maana inayojulikana na wengi sana huko mtaani, hebu tusome wote hapa;

IMG_20230623_084148.jpg


Jay Z ajitangazia kuishi milele

☆ Naomba niwakumbushe tu kuelewa Kingereza,na kuelewa Jay Z kaimba nini ni vitu viwili tofauti (kweli iliyo tupu).

☆ Tungo za Jay Z huwa hazitatuliwi na dictionary tofauti kabisa na rappers wengine.

HOV, ni miongoni mwa wasanii wachache sana ambao wamebarikiwa kuwa na witty lyrics (mistari inayohitaji akili ya ziada sana kuing'amua).

☆ Tungo nyingi za Jigga, shinikizo lake/zimeathiriwa sana na mapito pamoja na maisha yake ya nyuma kiujumla. Hivyo basi, kama wewe siyo mtu ambaye umefuatilia safari ya Izzo ya kimaisha na muziki wake kwa ujumla inaweza kukupa shida sana kumuelewa na hapo utabaki kusikia badala ya kusikiliza kazi zake.

Marafiki na ndugu zake wa karibu wanasema kuna wakati hata akiwaita kwa majina yao mtu anapata mashaka, unahisi kuna kitu kingine kamaanisha au vipi, alisema dada wa Jefe.

Pengine una maswali au pengine tayari ushawahi kujijibu, au uliamua kuacha ili usijichoshe kuwa alimaanisha nini katika huu wimbo "It is fine (ni sawa)."

Kwa maana, moja ya mstari katika wimbo huu anasema, nanukuu;

"Fear not when, Fear not why, Fear not Much, while we are alive,
Life is for living, not giving up tight, till you are somewhere up in the sky."

Akimaanisha usiwe mtu wa kujiuliza sana kupambana na yasiyo wezekana, mengine si ya wewe kuamua. Utajiumiza sana halafu mwisho wa siku utakufa tu (wewe ishi tu kadiri unavyoweza).

Ukweli ni kwamba El Padrino katika wimbo huu wa Forever Young, hakumaanisha kuwa anatamani kuwa mdogo/asizeeke miaka yote kama ilivyo tafsiri ya wengi katika vichwa vyao.

Katika wimbo huu amejaribu kuonesha wapi alipotokea, wapi alipo na wapi anaelekea, na maisha baada ya yeye kutokuwepo tena yaani, Past, Present and future ni sawa sawa na Legacy. Hivyo anaamini kuna siku itafika hatokuwepo (kifo).

Tukianzia katika Past (alipopita)

Niggas thought I lost it, they be talking bullshit,
I be taking more shit,t he nauseous (hold up).

Hapa alikuwa akilenga vijembe na kejeli alizozipata 2006 baada ya kuachia album yake ya Kingdom Come mbayo kitakwimu ndiyo album yake iliyokuwa na mapokeo duni kuwahi kutokea katika career yake, lakini pia anasema pamoja na vijembe hivyo bado album ilifika nafasi za juu kabisa katika charts za billboard na iliuza nakala zaidi ya million 3 kwa US pekee. Anaona haters wake wanatapatapa mafanikio kama hayo kwao ni jambo kubwa

Album kufanya hivyo lakini kwa Young Hovito wanaona ni madogo, kitu ambacho kwake anaona mafanikio, pamoja na kuwa walihisi kapoteza (Niggas thought I lost it), ndiyo kwanza album zilizofuata
American Gangster na The Blueprint 3 yenye huu wimbo.

Zilipokelewa kwa ukubwa sana, na kushika namba moja katka nyakati tofauti. Pia Sanatra katika wimbo huu amejaribu kuelezea wakati uliopo (present) japo si kwa mapana kwakuwa anajua kila mtu anajua maisha aliyoyanayo na kilakitu kuhusu records zake.

Amegusia 👇
"slamming Bentley doors, hopping outta Porsches
Popping up on forbes lists, gorgeous."

Maisha ya kifahari anayoishi, ndinga kali kuorodheshwa katika orodha za matajiri duniani, hayo yote ni kitu ana urahia, lakini je, ndicho kitakachomfanya awe Forever young?

Mpaka hapa utajiuliza mbona hiyo Young kwa maana ya ujana huioni ikileta maana yoyote kwenye nyimbo, kama umegundua hilo (tunaenda sawa).

Yes Jay Z hakumaanisha Young ya udogo, ujana au kwa ujumla rika la umri, la hasha! Na pia toka mwanzo wa uzi huu nadhani kuna baadhi ya majina umeona nikitaja na hujaelewa yanatoka wapi (it's ok).

Lengo lilikuwa ni jibu maswali hayo hapa, ni hivi Jay Z ni rapper mwenye nickname nyingi, zaidi ya 60+ na chache katika hizo ndizo nilizotaja hapo juu kama; Jefe, Jigga, Izzo, Young Hov, Hovito, El Pedrino, Samatra na kadharika, yote ni yake, lakini kila jina amelitumia kwa nyakati na kazi tofauti, wanamfuatilia watanielewa, lakini Young pia ni jina lake pendwa Young Slung kama ilivyo Young Hov.

Sasa tunapata mwanga wa tafsiri halisi ya wimbo wa Forever Young ni sawasawa na useme Forever Jay Z (Jay Z Forever). Sasa Jay z Forover kwa maana ipi, tumeona katika mstari wa kwanza kunukuu ya kuwa anatambua kuna kifo sasa kwanini aite wimbo Jay Z ni wamilele?👇

Ndiyo tunarudi kwenye Legacy au kiswahili (alama chanya) duniani ambazo zitaishi kwa niaba yake milele
Je ni zipi? 👇

"Fear not to die, I will be alive For million years,byebye's
Are not for Legends , am forever young my name shall survive "

Elewa hapo anamaanisha👇

*Fear not to die ~ siogopi Kifo

*I will be alive for million years ~ kusema nitaishi miaka million ni sawasawa na milele

*Byebye is not for legends ~ hata akifa hakuna haja ya kusema kwaheri maana

*Am forever young, my name shall survive ~ jina lake Young/Jay Z litaendelea

Pia YOUNG Katika mstari mwingine Anaendelea kwa kusema;

"Reminisce talk some shit, forever young is in your mind, leave the mark they can't erase neither space no time."

Atakumbukwa kwa mengi, jina lake litabakia katika vichwa vya waliobakia, kwakuwa ameacha alama katika game ambayo kimsingi haiwezi kufutika, siyo muda wala nyakati zitaweza kufuta kumbukumbu hizo. Nikukumbushe tu Young Album 13 katika album zake 20 nimeshika namba 1 katika billboard charts, je, ni jambo dogo hilo?

Hakuishia hapo Young/Young Slung, anaongeza mstari na kusema;

"Through the darkest brock, over kitchen, storves over pyrex pots," hapa akijaribu kuelezea ni kwa namna gani atakumbukwa na watu wa aina zote kuanzia wa chini kabisa wanaojishughulisha na madawa katika mapagala, kwani atasimama kama mfano kwakuwa, ametokea huko na amebadilika na kuwa kioo, hivyo ni kielelezo tosha kwa drugs dealers and users kuwa wanaweza kubadilika na kuwa watu bora
kwa umuhimu kabisa ili tuelewe anathibitisha hayo katika mistari hii;

"Young Slung, hung here showed that nigga From here
With a little ambition, just what we can be ome here."

Sote tunaelewa Jay Z ni mnufaika wa ile Marcy Project, ambayo kwa lugha rahisi ulikuwa moja wapo ya miradi ya nyumba za shirika, kama ilivyo NHC hapa bongo. Unaweza sema ni kota, hivyo watoto wote wanaokulia maeneo yale wataambiwa haya 👇

*Young slung = Jay Z
*Hung here = Aliishi hapa
*With a little ambition = Kijana mdogo alliyekuwa hana matumaini kama ninyi, leo hii.
*Just what we can become - ni mtu mkubwa na hivyo ndivyo yeyote ana weza kuwa kama jayz hakuna linalo shindikana

Hayo yote jayz alikuwa akijaribu kupima ikiwa kama hayupo tena utamkumbuka kwa lipi?

Nadhani sasa tutakuwa tumeelewa kwa pamoja, maana kitaa watu wanapingana kuhusu hili goma.

Credit kwa Mwanetu Chizzo Drama twiter.
 
A

aah kwaiy n kam kupga str za zamani ambas zinakuhusu ww muhusika au hat kam hazikuhusu je inakaa kama umbea hv au kuna utofauti
No, zinazokuhusu wewe.

Jamaica ipo sana, watu unakuta wamewasha moto wanapiga story zao, maisha walopitia, kila mtu anasimulia moments anazohisi kushare. Siku hz hata ukiwa na wadau mnapiga gambe ukaanzisha hizo story wakitoka hapo wanakusema unajidai, kumbe ndo namna maisha yanavyobidi kuwa
 
No, zinazokuhusu wewe.

Jamaica ipo sana, watu unakuta wamewasha moto wanapiga story zao, maisha walopitia, kila mtu anasimulia moments anazohisi kushare. Siku hz hata ukiwa na wadau mnapiga gambe ukaanzisha hizo story wakitoka hapo wanakusema unajidai, kumbe ndo namna maisha yanavyobidi kuwa
Aaaah hapo nimekupata sana mkuu maana hili neno nilianzaga kulionaga kwa msanii wa nigeria ndo alikua anajiita hvo
 
Naomba kwa heshima na taadhima unitafsirie muziki wa tupac HELL FOR HUSTLERS na MADE NIGGAZ
 
Back
Top Bottom