Picha ya Marlyn Monroe yavunja rekodi, yauzwa kwa Bilioni 450. Je, huyu mwanadada alikuwa na kipi cha ziada?

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,634
26,373
New York,Marekani.

Picha ya mwanadada Marlyn Monroe iliyopigwa mnada hapo jana imevunja rekodi kwa kununuliwa kwa dola za kimarekani milioni 195($195 Mil) ambazo ni sawa na Shilingi Bilioni 450 za Kitanzania.

Picha hii pia imevunja rekodi ya kuwa ndio picha ya gharama zaidi kwa picha zilizochorwa katika karne ya 20.

Picha hii ilichorwa na mchoraji Andy Warhol mwaka 1964 ilinunuliwa na Bwana Lary Gagosian katika mnada ambao ulichukua chini ya dakika nne tu.

Marilyn Monroe alizaliwa June 1,1926 na alifariki August 4,1962 akiwa na miaka 36.

Je huyu dada alikuwa na kitu gani cha ziada kiasi cha picha yake kuuzwa ghali namna hii?

Kwa kadri nilivyomsoma inasemekana alikuwa mwigizaji,model na sex symbol(mtanisaidia hapa) na pia inasemekana aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Raisi John F Kennedy na ndugu yake Robert F Kennedy,Je kuna mengine unayajua kuhusu huyu mwanadada?.

Picha ya kwanza ndio iliyovunja rekodi.

Ahsante.
IMG_20220510_141252.jpg
IMG_20220510_141354.jpg
images%20(8).jpg
gettyimages-607384406-2048x2048.jpg
 
I was just watching a new Marilyn Monroe documentary "The Mystery of Marilyn Monroe: The Unheard Tapes" on Netflix this past weekend.

Yani haya maisha yanavyoenda sasa hivi inawezekana watu wameamua kum pump Marilyn Monroe kuuza vitu vyao.

Inawezekana pia ni genuine nostalgia.

 
I was just watching a new Marylin Monroe documentary "The Mystery of Marylin Monroe: The Unheard Tapes" on Netflix this past weekend.

Yani haya maisha yanavyoenda sasa hivi inawezekana watu wameamua kum pump Marylin Monroe kuuza vitu vyao.

Inawezekana pia ni genuine nostalgia.

Ngoja nitaangalia hii,ila nisaidie wanaposema sex symbol wanamaanisha nini?
 
Usishangae sana,
Sisi waafrika wananunua kamba ya mtu aliyejinyonga,
Maji ya maiti,nyuzi za sanda.
Yaani basi tu dunia uwanja wa fujo, wenye kujua zaidi ya maana ndo hugharamikia kununua wavitakavyo,ndio maana wewe unajiuliza picha tu ina nn cha ziada,aliyenunua ndio anajua zaidi.
 
Back
Top Bottom