Tangu nianze kusikia habari za gesi ya songo songo nadhani nilikuwa shule ya msingi. Ni takribani miaka 20 na zaidi sasa imepita majuzi juzi ndiyo nikaona mitambo ya kufua umeme inayotumia gesi ikizinduliwa kwa sherehe na nderemo pale Kinyerezi.
Lakini swali langu ambalo limekuwa likinisumbua daima ni kwamba hivi hii gesi sisi wananchi wa kawaida tutanufaika nayo vipi?
LPG bado haijaanza kutengenezwa Tanzania , ndio bado wapo kwenye mpango. Hii gesi tunayoitumia inatoka nje ya nchi.
Leo sasa nimegundua kuwa kumbe tunadanganywa kama watoto wa kuku. Wiki tatu zilizopita gesi ya kupikia LPG ilikuwa inauzwa shilingi 43,000 kwa mtungi wa kilo 15.
Leo nimeenda kununua nimekuta imepanda na kuwa shilingi 52,000 yaani bei imeongezeka kwa shilingi 9,000 ambayo ni sawa na asilimia 21%.
Mpaka sasa sijaelewa kwanini watanzania tunahangaishwa na makumpuni ya kibepari yaliyokuja kuvuna pesa kwa maskini sie wakati tuna gesi yetu ambayo kama tungekuwa na dhamira ya dhati ya kuwasaidia watanzania na kunusuru miti na mazingira yetu basi mtungi wa gesi wa kilo 15 usingezidi shilingi elfu 15,000.
Nimeahirisha kununua gesi naenda kununua gunia la mkaa ambalo kwa mazingira ninayoishi mimi nitalinunua kwa shilingi 45,000 na litatumika kwa mwezi na siku kadhaa wakati kwa gesi huwa natumia mitungi miwili ya kilo 15 kwa mwezi.
Wenye mamlaka angalieni hili suala kwa jicho la tatu. Sina ugomvi na wafanyabiashara wa gesi maana wao wanatafuta faida na siku zote faida hutengenezwa panapofursa.
Masikitiko yangu ni kwa miti maelfu kwa maelfu inayooendelea kukatwa kwa kuwa bado kuna demand kubwa ya mkaa kwa watanzania kuliko gesi. Gesi imeendelea kuwa nishati ya anasa kuipikia kama ilivyo kwa umeme nchi hii.
Ni aibu kwa gesi kuendele kuwa bei juu huku tukijinasibu tuna metric feet trilioni sijui ngapi wakati watanzania tunaumia kwa kununu gesi kwa bei ya ajabu. Siku ikishuka bei mnijuze nitaaanza kunua tena gesi ila kwasasa miti na inivumilie.
Asanteni na siku njema