Gesi imepanda bei kuanzia leo tar 9/2/2017

Gesi imepanda bei kuanzia leo tar 9/2/2017

Yaani bora hata tusingekuwa na gas kweny hii nchi hakuna cha maana
 
Nami mkaa wangu wa reja reja kipimo napandisha bei,cha buku kuanzia kesho ni 1500,watanunua tu,hawataki waache maana hauozi,
 
Acha ipande tu, kwani hata hicho chakula cha kuipikia kiko wapi!
 
Sasa hivi kula ugali sio kubana matumizi maana dona lipo bei juu zaidi ya mchele
 
Ndio miti itaacha kukatwa namna hii? Huo unga walioukamata watupe tukamuuzie Chid Benz tupate hela ya gesi
 
hiyo haituhusu tunaangalia zile biashara ambazo ni supernormal profit kama cocaine kwani ndio inatuweka mjini.. ngoja nikomae na redio kusikilizia epsode nyingine kwani starling mwenyewe katuhakikishia hii ni tamthilia na sio filamu..

Tatizo kubwa kama la madawa ya kulevya linafanywa kimzaha mzaha hivi.
 
Kama mishahara iko pale pale na gesi imepanda na bajeti ya mama zetu ni ile ile. Tutegemee kukosa msosi siku tatu ndani ya mwezi
Kifo cha kujitakia hakina kilio. Hii ni njia mojawapo ya kuongeza jangwa kwa haraka zaidi. Harafu serikali inasema mkaa upigwe marufuku. Mafuta ya taa na umeme bei juu. Twafwaa.
 
Duu utaambiwa gesi tuliyonayo haifai kwa matumizi ya nyumbani kutuchanganya tuu ila China inafaa kwa matumizi ya nyumbani..
 
Kwa kweli hii nchi kuna watu hawana huruma kabisaa,yani sembe hapa nilipo 1800-2000 mchele 1700-1800-1900 hadi 2000 bado na gesi inapaa du.kweli tunaisoma namba.
 
Thamani ya TZS katika mizani ya nguvu ununuzi sokoni imeshuka (purchasing power) hivi karibuni ingawa hatuwezi pata takwimu kutoka benki kuu..hii inachochea vitu kupanda bei, hapo awali ilikua upande wa vyakula hivi sasa tumeenda katika nishati ya gesi. Hatuwezi kupambanunua kesho itahamia sekta ipi.

Majibu hayapatikani kanisani katika maombi ya mfungo na kulia, wala viongozi waliopo bungeni maana wengi ni viziwi huku wale wanzao ni mabubu. Hata wakiongea hawajui kutengeza hoja, watajikita upande wa maslai ya chama na yao binafsi.

Usiniulize utatuzi ni upi na utatoka wapi, wahusika wanajijua ila hawajitambui.
 
Back
Top Bottom