General Tyre [EA] Ltd kuanza uzalishaji mwaka 2013 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

General Tyre [EA] Ltd kuanza uzalishaji mwaka 2013

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ngongo, Oct 16, 2012.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Heshima kwenu wanajamvi,

  Wakuu General Tyre inafanyiwa ukarabati mkubwa wa majengo na mashine/mitambo kwaajili ya kuanza uzalishaji mwakani Mungu akipenda.NDC wamekabidhiwa kazi ya kuifufua General Tyre tayari mafundi umeme wameshaanza kazi ya kubadilisha nyaya za umeme chakavu.Jengo la utawala limeshamaliziwa kupigwa rangi na matengenezo madogo madogo yanafanyika kwa kasi ya ajabu.

  Inatarajiwa kabla ya mwakani kati ya mwezi wa tatu hadi mwezi wa tano mitambo mipya na yenye technology ya kisasa itafungwa katika eneo lilojulikana kama New bay.Mitambo iliyokuwa ikitumika zamani na bado ina ubora wa sasa ni ile iliyokuwa ikizalisha tairi ndogo Grabber AP 215 R 15 / 205 R 16 / 31 X 10.5 R 15 LT / 165 R 13 / 175 R 14 / 185 R 15/14.Pia mould za matari size 750 - 16 HCT 8PLY,10PLY & SHCT 12PLY itaendelea kutumiwa kwakuwa tairi zake bado zinahitajika sokoni hasa magairi aina ya Land Rover & Land Cruiser kwa safari za porini[Utalii].

  Naipongeza serekali kwa hatua nzuri ilizoanza kuzichukua naamini ongezeko kubwa la magari Tanzania ni soko la uhakika kwa matairi ya General Tyre.Tusisahau pia soko la EA bado liko wazi sana pamoja na kampuni ya kuzalisha matairi ya KENYA kuiba technology ya General Tyre hasa tyre 750 - 16 HCT 10 ply bado halijafikia ubora wa tairi la Genral Tyre nina hakika siku uzalishaji ukianza YANA ya Kenya watafunga virago Tanzania.

  Nakala: Ritz PakaJimmy TUMBIRI Matola Crashwise sweke34 mayega Mimibaba Jasusi Mtambuzi Mwita Maranya zumbemkuu Dotworld Nyange OSOKONI Mzee Mwanakijiji Richard Molemo BAK Mzee wa Rula Bigirita zomba Nyumbu Pasco Kubwajinga Mchambuzi Nguruvi3 Invisible samora10 Arushaone kitalolo Roulette The Boss MpendaTz Mkusa Mag3 MVUMBUZI na wengine wote

  Naomba kuwasilisha.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Natumai itaendeshwa vizuri this time. Nakumbuka katika miaka ya 70 waendesha magari kutoka Nairobi walikuwa wanakuja Arusha kununua matairi ya General Tyre.
   
 3. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sawa Ngongo ila serikali hii unayoipongeza ndiyo iliua GT husasan Waziri wa sasa Abdalah Kigoda; watu wamekosa kazi miaka 10. Serikali imekosa mapato.
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu Mimibaba walioiua General Tyre ni Bwana Basil Mramba.Ikumbukwe wakati alipokuwa waziri wa fedha aliitumia General Tyre kuchota fedha NSSF kwa kisingizio cha kununua mashine za kisasa hilo halikufanyika Mramba na aliyekuwa CEO Devenrah na baadhi ya maafisa wa NSSF walikwapua u$10 milion na mpaka leo deni hilo bado lipo ingawa fedha zaidi ya 60% hazikufika General Tyre kabisa na zilizofika zilichezewa.

   
 5. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Je,ni mwekezaji gani atashirikiana na ndc maana serikali imekuwa na kauli kuwa haiwezi kuendesha mashirika.tupe data kwa hilo mkuu
   
 6. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Mungu mkubwa!mfu anaanza kupumua taratibu.
   
 7. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #7
  Oct 16, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mgaya D.W ni kweli serekali haiatawekeza ila imeipatia fedha NDC kuandaa mazingira mazuri [Matengenezo] ya kuvutia wawekezaji huku serekali ikibakiza hisa nyingi mikononi mwake.Tayari makampuni ya Ujerumani,Malasia,Brazil na Uturuki yameshatoa offer kwa NDC namna gani watakavyowekeza iwapo watachaguliwa.NDC wapo katika hatua za mwisho za kumpendekeza mbia mwenye kukidhi vigezo wanavyovitaka ikiwemo technology ya kisasa,uwezo wa mtaji.

  Serekali pia itayatoa mashamba ya mpira yaliyoko Tanga na Morogoro kama sehemu ya mtaji wake.


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ngongo hivi nani tunatakiwa tumpongeze kwa hili ni kweli serikali tunapaswa kuipongeza...?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Yaani katika bandiko la Ngongo nilipo ona pongezi kwa serikali nikajua kashaanza ningeungana nae 100% kama angeipongeza JF na Lema na Zitto...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. W

  Wimana JF-Expert Member

  #10
  Oct 16, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 2,453
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 145
  Ngongo, hao Wajerumani sio wale wa Continental ambao waliweka menejmenti ya Mnepal aliyshirikiana na Mramba kuiua GTEA?
   
 11. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #11
  Oct 16, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Mkuu Crashwise kwa maoni yangu naipongeza serekali walau imekumbuka ilichoshindwa kukisimamia.Serekali ingeweza kukaa kimya baada ya General Tyre kuuwawa yamkini imeelewa imefanya kosa kubwa sana hasa iliposhindwa kuwafikisha mahakamani wahusika wakuu.

  Kitendo cha kumtafuta mwekezaji mwenye sifa nilizozitaja ni hatua kubwa pia.


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #12
  Oct 16, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Mkuu Wimana hapana Continental walishajitoa siku nyingi.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Sioni sababu ya kuipongeza serikali hata kidogo nakushangaa wewe mwenye umekuwa msitari wa mbele kulipigia kelele swala hili na baadae iliundwa tume ambayo ilikuwa chini ya zitto na kubaidi uozo wa hali ya juu hivyo serikali haikuwa na namna..kama watu walikuwa wameuziana gari kwa US$100 na mkurugenzi anachukua Us$ 2000 kwenda kupumzika na familia yake serengeti ulitaka serikali licha ya kuumbuliwa wafumbe macho...haya hiyo hapo NMC hawajui kama iko hai napo utakuja kuwapongeza..hahahah
   
 14. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #14
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Alieiua GT anapongezwa na serikali na kupamba maneno kama ni mtu mzuri sana, ni mtu safi leo tuwapongeze...
   
 15. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #15
  Oct 16, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Mkuu ngongo tuombe mungu yana wasije na kibiriti pale kabla ya 2013.
   
 16. peri

  peri JF-Expert Member

  #16
  Oct 16, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  big up serekali na wadau wote wanaohusika, wasiishe hapo waende kwenye viwanda vingine kama machine tools kilichopo njiapanda ya machame.
   
 17. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #17
  Oct 16, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Yeh mkuu nimepita pale na nimeshuhudia ukarabati ukiendelea ni jambo jema kwa hatima ya ajira kwa Taifa.
  Ni matumaini kuwa sio siasa bali kazi itapigwa, nilikuwa nashaa kila mara kwa kiwanda kikubwa kma kile kufungwa ilihali soko la tairi likiwa kubwa haswa ukizingatia idadi ya magai yalioko nchini. Hii naamini itasaida si pamoja na ajira tu bali hata bei ya tairi inaweza kuwa nafuu kidogo kwani inaweza kupunguza baadhi ya gharama na haswa utapeleli wa baadhi ya wafanyabiashara kujiwekea bei za juu kweny bidhaa kwa visingizio mbalimbali ikiwemo sehemu wanapotoa tairi pamoja na kodi kubwa.

  Thanks kwa Taarifa endelea kutujuza
   
 18. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #18
  Oct 16, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Soko lipo na hakika GT ilikuwa kiboko EAC. Nakumba matairi yalivushwa mpakani kwa magendo.
  Tatizo ninalo liona ni ushindani katika bei. Hili litasababishwa na nishati ghali na isiyo na uhakika.

  Umeme wetu ni ghali katika kanda hii, lakini pia ili kiwanda kifanye kazi kwa ufanisi kwa shift kama ilivyokuwa ni lazima umeme wa uhakika uwepo. Kukosekana kwa umeme kutaongeza gharama za uzalishaji na mtumiaji atabeba mzigo.
  Ikifika hapo bado mitumba na cheap products zitatawala. Ni hofu yangu tu!

  Pili, management na akina nani? Kama ni ya kisisa basi hapo kuna tatizo bado.
   
 19. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #19
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ngongo kwanza nashukuru kwa kunimention ili nisipitwe na habari hii ambayo kwangu mimi naona kama ni nzuri. Naomba tu serikali itambue wapi ilifanya makosa ili isirudie tena manyanga baada ya kushindwa kuwafikisha wahusika mahakamani.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #20
  Oct 16, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Ngongo,

  Ni habari njema, ila nitakwazika sana kama ubinafsishaji wa GT utakuwa kama wa NBC!! Hivi kwa nini tusiajili management to run the company? Haya mambo yakuuza uza hisa yanavutia watu kuja na mipango mfu!!!

  Tumeshaliwa sana, I hope this time kuwa somo toka katika makosa yetu ya nyuma!
   
Loading...