General Tyre [EA] Ltd kuanza uzalishaji mwaka 2013

Srikali hii inafanya vyema zaidi ya Serikali yeyote ya kabla yake. Kama unalo japo moja tu ambalo Serikali hii haijafanya zaidi ya Serikali zote zilizopita, litaje.

Nakuhakikishia utachemsha!

Haipambana na ufisadi na rushwa kama ilivyoahidi
 
Haipambana na ufisadi na rushwa kama ilivyoahidi

Awamu ipi ulisikia kesi za rushwa nyingi kuliko awamu hii zilizopo mahakamani?

Awamu ipi ulisikia taasisi ya kupambana na rushwa ikisambazwa na kufunguliwa ofisi zake wilaya zote za Tanzania?
 
Acha kujikanyaga wewe mtumwa wa mafisa! Ina maana chama cha majambazi haikuwa madarakani?
Ni nani aliyeifanyaga hiki kiwanda iliyokuwa na wafanyakazi zaidi ya 2,000 kufa kama siyo mafisadi waliokuwa madarakani?

zomba! Angalia sana kauli yako ya kufunika uchafu ulioko ndani ya serikali legelege ya jk! Tuna macho na tunafikiri na tunatambua!

Miaka 10 iliyopita "serikali hii" haikuwepo madarakani.

Eti serikali hii haikuwepo madarakani!

Danganya watumwa wenzie unaowajua!
 
Mkubwa! Tunashukuru kwa kuwa makini na yote utujuzayo na bila shaka ni wakati mwingine tena wa vijana kutegemea ajira pale!

Je? Kwa ufahamu wako wa haraka haraka inaweza ikabaki ikiwa kama shirika la Umma kama ilivyokuwaga? Yaani (SU)!

QUOTE=Ngongo;4838242]Wakuu wawekezaji wote tayari wameshatembelea General Tyre na kujionea wenyewe hali halisi.Jambo moja kubwa lililowashangaza sana ni hali ya utunzaji wa thamani na mashine.Computers,printers,photocopy machine,meza,viti,viyoyozi na mashine zote vilikuwa katika hali nzuri.

Mkuu Mchambuzi ni kweli reli ni muhimu katika ujenzi wa uchumi imara lakini gharama za kuifufua ni kubwa mno inabidi serekali ijipange sawa sawa.Gharama za kuifufua General Tyre ni ndogo sana utashangaa sana baadhi ya mitambo mingi itahitaji kupakwa grease tu ?.Mould za kupika matairi za saizi mbali mbali zipo haziitaji matengenezo kabisa zaidi ya kusafishwa,bambari inafanyakazi,boiler zipo mbili zote nzima kabisa,sehemu ya kufunga mashine mpya ipo sana sana itahitaji kuoshwa na kufutwa utando wa bui bui.

Bwana L Mgoyo,Bwana Palangyo ,Bwana Urassa na Bwana Athumani wanastahili pongezi za dhati kwa uaminifu wao wa kutunza kumbukumbu za vifaa vyote bila kuchakachua.
[/QUOTE]
 
Last edited by a moderator:
This is good news, kiwanda kikifufuka na kuweza kuwa competitive kwenye soko. Matairi yamepanda bei sana, Kiwanda cha kenya kinakula shavu kwenye soko la EA.

Kinachotakiwa ni kuweza kuwa kibiashara, management isiwe ya kisiasa. Wanasiasa, hata huyu mkuu wa nchi nae akae Mbali na uendeshaji wa kiwanda. hawakawii kukifanya mtaji wa kuchotea fedha nyingine kwenye mifuko ya kijamii na kisha kutokomea, tukaachiwa majengo yaliyopakwa rangi.
 
Awamu ipi ulisikia kesi za rushwa nyingi kuliko awamu hii zilizopo mahakamani?

Awamu ipi ulisikia taasisi ya kupambana na rushwa ikisambazwa na kufunguliwa ofisi zake wilaya zote za Tanzania?
Mbona unahangaika sana wewe Kichenchede?

Sio kila kitu ni siasa na JK, grow side ways if you cant grow up.
 
Awamu ipi ulisikia kesi za rushwa nyingi kuliko awamu hii zilizopo mahakamani?

Awamu ipi ulisikia taasisi ya kupambana na rushwa ikisambazwa na kufunguliwa ofisi zake wilaya zote za Tanzania?

Serikali hii ni ya CCM ondoa mawazo ya awamu. Mimi sitaki maneno nataka vitendo kesi ipi imehukumiwa kwa manufaa ya taifa na ikapokelewa kwa dhati kuwa haki imetendeka? Ninachokiona mimi:-

1. Maigizo ya kesi hizi ni ya usanii, vinara wa rushwa hawaguswi akiwepo dhaifu JK aliyeingia madarakani 2005 kwa rushwa ya Tshs 20bn toka kwa warabu. (Ushahidi JK kukiri kwenye kipindi cha KitiMoto ITV kilichoendeshwa na Pascal Mayala kabla ya uchaguzi 2005)

2. Rushwa sasa ni taasisi, na hiyo TAKUKURU ni waigizaji kwenye usanii unaoendeshwa na JK kajisemea mwenyewe Hosea "Wanasiasa wanafiki" Na JK ni namba moja yaani ndiye kiongozi mkuu wa rushwa na ufisadi.

3. Kwenye orodha ya Uswizi JK ni namba moja anafuatiwa na Ridhwani. Sasa wewe Zomba unaimba wimbo usio na kina wala waitikiaji kwa sababu wakukuitikia wanajua wimbo huo hauuziki.

Niendelee??
 
Kuna vitendo zaidi ya kutawanywa TAKUKURU nchi nzima? au unafikiri ni uyoga ule unajiotea tu?

1) Utaziona wapi kesi zinazohukumiwa? nawe umeziba macho na masikio hayasikii!

2) Rushwa ililetwa na kuendelezwa na watu kama wewe ambao mnachaguwana kwa kuwa tu umetoka kanisa fulani.

3) Hiyo orodha labda ya uwani kwenu. Ya Uswisi ungekuwa nayo ungelala usingizi?
 
Ngongo hii itakuwa ni re-structuring, new capital structure ikoje? Awali ilikuwa Tanzania I think 70 na Continental 30 lakini kwa upumbavu wetu Watanzania tukawakabidhi wenye hisa kidogo ndio waweke uongozi (executive management) na wenye hisa wakatoa chairman ambaye hana ujuzi wa hiyo biashara
 
Last edited by a moderator:
Kwa jinsi nilivyokosa imani na hii serikali mpaka kikija funguliwa ndo nitaamini ili
Infact serikali ni kupitia bidhaa zinazoongoza kwa matumizi ya forex ili zitengenezwe apa apa nchini ili kuokoa forex ambayo ndo inaipaisha Dola
Ila hili unaitajinmzalendo
Mfano kama wataka create ajira nyingi fufua viwanda vya pamba wakulima watafaidika na raia watapata ajira lukuki na MD anapewa target kila mwaka akifeli piga chini unless ana sababu za msingi na wote lazima kupiga pamba za viwanda vyetu
India wameweza wanapiga pamba zao na magari wanatumia TATA mpaka mawaziri
 
Kuna vitendo zaidi ya kutawanywa TAKUKURU nchi nzima? au unafikiri ni uyoga ule unajiotea tu?

1) Utaziona wapi kesi zinazohukumiwa? nawe umeziba macho na masikio hayasikii!

2) Rushwa ililetwa na kuendelezwa na watu kama wewe ambao mnachaguwana kwa kuwa tu umetoka kanisa fulani.

3) Hiyo orodha labda ya uwani kwenu. Ya Uswisi ungekuwa nayo ungelala usingizi?

Nimeamini wewe ni mtumwa wa fikra. Sahihisho mimi naishi kijijini nafanya kazi za kutoa ushauri wa kitaalam duniani. Silambi viatu vya mtu kama wewe

Natoka kwenye familia ya kiislaam na ni msimamizi wa msikiti wa ukoo si fanatic kama wewe na mwenzio Ponda. Kwa hiyo endeleza upuuzi wa ki Ponda Ponda. Mtabana lakini mtaachia hamna ubavu kwa sababu mtabanwa na HAKI.
 
jamani jamani tukubali tusikubali upinzani wa kichama uwepo ,tu. BIG UP VIONGOZI WA UPINZANI MLIOSHINIKIZA HILI LIFANYIKE PONGEZI SANA
 
Nimeamini wewe ni mtumwa wa fikra. Sahihisho mimi naishi kijijini nafanya kazi za kutoa ushauri wa kitaalam duniani. Silambi viatu vya mtu kama wewe

Natoka kwenye familia ya kiislaam na ni msimamizi wa msikiti wa ukoo si fanatic kama wewe na mwenzio Ponda. Kwa hiyo endeleza upuuzi wa ki Ponda Ponda. Mtabana lakini mtaachia hamna ubavu kwa sababu mtabanwa na HAKI.

Ushauri wa kitaalaam huku wewe mwenyewe huoni wala husikiii, insikitisha sana. Ikiwa Wataalaam wa Tanzania ni kama wewe, basi kazi tunayo na si hasha mpaka leo tuko nyuma hata kielimu, ahsante Kikwete anaefanya kila njia kuwapa elimu kwa kuwajengea mashule na vyuo vikuuu kedekede ambavyo haijawahi kutokea kabla yeke.

Kuwa msimamizi wa msikiti wa ukoo au kanisa la ukoo hakukufanyi kuwa wewe ndiye mjuaji zaidi, tena wala haihusu hapa.

Uponda na upondo unahusu nini hapa? Hapa tunaongelea mafanikio ya Rais mpendwa Jakaya Mrisho Kikwete na anavhohuisha viwanda vilivyouliwa na wanaojiita "watalaam" kama wewe.
 
Poa hakuna haja ya kubishana na mtu kama wewe mwenye upeo unaoishia Sytem at Work.
 
Heshima kwenu wanajamvi,

Wakuu General Tyre inafanyiwa ukarabati mkubwa wa majengo na mashine/mitambo kwaajili ya kuanza uzalishaji mwakani Mungu akipenda.NDC wamekabidhiwa kazi ya kuifufua General Tyre tayari mafundi umeme wameshaanza kazi ya kubadilisha nyaya za umeme chakavu.Jengo la utawala limeshamaliziwa kupigwa rangi na matengenezo madogo madogo yanafanyika kwa kasi ya ajabu.

Inatarajiwa kabla ya mwakani kati ya mwezi wa tatu hadi mwezi wa tano mitambo mipya na yenye technology ya kisasa itafungwa katika eneo lilojulikana kama New bay.Mitambo iliyokuwa ikitumika zamani na bado ina ubora wa sasa ni ile iliyokuwa ikizalisha tairi ndogo Grabber AP 215 R 15 / 205 R 16 / 31 X 10.5 R 15 LT / 165 R 13 / 175 R 14 / 185 R 15/14.Pia mould za matari size 750 - 16 HCT 8PLY,10PLY & SHCT 12PLY itaendelea kutumiwa kwakuwa tairi zake bado zinahitajika sokoni hasa magairi aina ya Land Rover & Land Cruiser kwa safari za porini[Utalii].

Naipongeza serekali kwa hatua nzuri ilizoanza kuzichukua naamini ongezeko kubwa la magari Tanzania ni soko la uhakika kwa matairi ya General Tyre.Tusisahau pia soko la EA bado liko wazi sana pamoja na kampuni ya kuzalisha matairi ya KENYA kuiba technology ya General Tyre hasa tyre 750 - 16 HCT 10 ply bado halijafikia ubora wa tairi la Genral Tyre nina hakika siku uzalishaji ukianza YANA ya Kenya watafunga virago Tanzania.

Nakala: Ritz PakaJimmy TUMBIRI Matola Crashwise sweke34 mayega Mimibaba Jasusi Mtambuzi Mwita Maranya zumbemkuu Dotworld Nyange OSOKONI Mzee Mwanakijiji Richard Molemo BAK Mzee wa Rula Bigirita zomba Nyumbu Pasco Kubwajinga Mchambuzi Nguruvi3 Invisible samora10 Arushaone kitalolo Roulette The Boss MpendaTz Mkusa Mag3 MVUMBUZI na wengine wote

Naomba kuwasilisha.

Kaka Ngongo nakuaminia. Naomba kifufuke kwani nina jirani yangu aliyekuwa mfanyakazi humo anateseka sana na pia rafiki yangu mwingine yeye ameamua kufundisha na pia sitamsahau Quality Controller R.I.P MC PAP au MC Lema aliyefariki tarehe 2/01/2010 huko Castle Hotel Moshi ambaye alikuwa mfanyakazi pale. Sitamsahau mama yangu Mrs K aliyepoteza kazi ya kutoa huduma ya chakula kwa wafanyakazi pale General tyre. List ya walioathirika ni ndefu naomba wawe hai hadi kitakapoanza kazi nikijua wale waliokuwepo haswa wenye special skills watapewa kipaumbele!!!
 
Mkuu wangu Mimibaba walioiua General Tyre ni Bwana Basil Mramba.Ikumbukwe wakati alipokuwa waziri wa fedha aliitumia General Tyre kuchota fedha NSSF kwa kisingizio cha kununua mashine za kisasa hilo halikufanyika Mramba na aliyekuwa CEO Devenrah na baadhi ya maafisa wa NSSF walikwapua u$10 milion na mpaka leo deni hilo bado lipo ingawa fedha zaidi ya 60% hazikufika General Tyre kabisa na zilizofika zilichezewa.
Mkuu Ngogo, kwanza nitamke tu kuwa ni vizuri tukaipongeza serikali kwa kuona aibu hii kuwa ni yao na inawapasa kuishughulikia japo wamechelewa sana kuchukua hatua stahiki lakini bora kuchelewa kuliko kukosa kabisa.
Serikali yetu inaonekana kujali sana siasa badala ya uchumi wa nchi, maana uchaguzi ukiitishwa mahali sasa hivi mf.huko Igunga Mawaziri wanafunga ofisi kwenda kubwabwaja uwongo, kupanga mikakati ya wizi wa kura nk. huku nchi ikididimia. Lakini jambo kama hili linawachukua miaka kumi kujua la kufanya! Hii ni aibu tena fedheha ya hali ya juu.

Kuhusu aliyesababisha kufa kwa GT, sikubali kutajwa mhusika mmoja na ninaomba katika mambo mazito kama haya watu wasiwe wanadanganya wananchi eti Waziri mmoja kaamua kuua shirika au kampuni muhimu kama hiyo yey peke yake. Yeye ni nani? Wala hakuwa Raisi wa nchi. Kuna baraza la Mawaziri linaloongozwa na Raisi, je maamuzi kama haya anaweza kuyafanya mwenyewe kweli? La hasha! na tuache mzaha kwenye mambo yanayolihusu Taifa. Huu unakuwa mzaha mwingine kama ule wa juzi hapa eti Raisi anasema mhasibu mmoja alifanya kosa katika ununuzi wa rada, eti mhasibu alikosea. Tafadhali sana sababu dhaifu kama hizi zisiletwe humu. Au wale waliotaka kuhamisha mabilioni kutoka hazina eti kwenye lori kwenda wizara ya mambo ya nje, eti walijiwekea saini na kuidhinisha kuondoa kiasi hicho bila kuwa na authority ya kufanya hivyo. Huu ni upuuzi wa hali ya juu. Serikali makini haiwezi kuwa inawapa wananchi wake sababu za kijinga jinga namna hii. Tunakuwa kama tunaongozwa na wapiga ramli na wacheza kamari?
Hivi visingizio uchwara lazima vikomeshwe na njia mahsusi ya kwanza ni kuhakikisha CCM inakaa benchi kwanza kwa miaka kadhaa, maana kwao limezoeleka ni kama utamaduni wa chama.
 
Mkuu MVUMBUZI ni kweli wafanyakazi wengi wameathirika sana.Nianze na rafiki yangu Mwetta amekimbia mji wa Arusha kahamia Singida anauza tairi mbili kwa mwezi.Yupo rafiki yangu mwingine Uncle anauza chumvi na binzari maeneo ya Ngulelo ukimtazama lazima machozi yakutoke.Wafanyakazi waliotangulia mbele ya haki ni wengi nianze na Security Auditor Nyagori,Quality Controller MC Lema,Receiving Supervisor Piniel King'ori huyu alikufa kwa Babu wa Kikombe huko Samunge.Dereva Msuya,wafanyakazi wa Production waliotangulia mbele ya haki ni wengi sana.

Kaka Ngongo nakuaminia. Naomba kifufuke kwani nina jirani yangu aliyekuwa mfanyakazi humo anateseka sana na pia rafiki yangu mwingine yeye ameamua kufundisha na pia sitamsahau Quality Controller R.I.P MC PAP au MC Lema aliyefariki tarehe 2/01/2010 huko Castle Hotel Moshi ambaye alikuwa mfanyakazi pale. Sitamsahau mama yangu Mrs K aliyepoteza kazi ya kutoa huduma ya chakula kwa wafanyakazi pale General tyre. List ya walioathirika ni ndefu naomba wawe hai hadi kitakapoanza kazi nikijua wale waliokuwepo haswa wenye special skills watapewa kipaumbele!!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu MVUMBUZI ni kweli wafanyakazi wengi wameathirika sana.Nianze na rafiki yangu Mwetta amekimbia mji wa Arusha kahamia Singida anauza tairi mbili kwa mwezi.Yupo rafiki yangu mwingine Uncle anauza chumvi na binzari maeneo ya Ngulelo ukimtazama lazima machozi yakutoke.Wafanyakazi waliotangulia mbele ya haki ni wengi nianze na Security Auditor Nyagori,Quality Controller MC Lema,Receiving Supervisor Piniel King'ori huyu alikufa kwa Babu wa Kikombe huko Samunge.Dereva Msuya,wafanyakazi wa Production waliotangulia mbele ya haki ni wengi sana.

Kifupi nishukuru Mungu kwa uelewa wa michango ya wana Arusha kwa kuguswa na hili jambo. Natumaini moyo huu utasikika na ndugu zetu waliopata madhira, watakusanya ujasiri na kusonga mbele kama mashuhuda wa linalowezekana kwa Mungu mwanadamu atachelewesha tu.

Sisi wengine tunaamini unaokufa ni mwili tu kwa hiyo waliotangulia mbele ya haki bado roho zao zitapata faraja na hili jambo.

BRAVO ARUSHA SPIRIT ON GTEA.

Ahsante Ngongo kwa taarifa hii muhimu.
 
Back
Top Bottom