Serikali isimsikilize ‘mfanyabiasiasa’ Godbless Lema kuhusu kiwanda cha General Tyre

Rich Hash

Senior Member
Mar 7, 2017
148
250
Na Samson Mwigamba....

WAKATI nikiwa bado ni mwanachama na kiongozi wa CHADEMA Arusha, kuna siku nilikuwa naongea na viongozi wa chama hicho wilaya ya Arusha mjini. Tukimzungumzia Godbless Lema, aliyeonekana kupania sana kugombea ubunge kupitia CHADEMA kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Viongozi wa wilaya ya Arusha mjini walikuwa wakipinga kwa nguvu zao zote Lema kugombea ubunge wa Arusha mjini kupitia CHADEMA. Baada ya kuwahoji sana Mwenyekiti wa wilaya akaniambia huyo ni ‘mfanyabiasiasa’.

Nilivutiwa kujua mfanyabiasiasa ni mtu wa aina gani. Yule mwenyekiti akaniambia ni mtu anayefanya biashara kwenye siasa. Anayetumia siasa kama biashara ya kujipatia pesa kwa ujanja ujanja. Huo ni wakati ambao Godbless Lema aliyekuwa katibu mwenezi wa TLP Mkoa wa Arusha alijitokeza kwenye vyombo vya habari akiwa na aliyekuwa diwani wa kata ya Sombetini Arusha mjini kupitia TLP, Alphonce Mawazo (sasa marehemu). Akatangaza kwamba yeye na Mawazo wameamua kuhama TLP na kuhamia CHADEMA.

Uchaguzi mdogo ulipoitishwa kwenye kata ya Sombetini iliyoachwa wazi na Alphonce Mawazo, watu wakashangaa Mawazo akiwa ameongozana na Lema akitangaza kugombea tena udiwani kwenye kata hiyo kupitia CCM. Na hata baada ya tukio hilo Lema aliendelea kujitambulisha kwamba yeye ni mwana CHADEMA. Lakini kwenye kampeni hizo alipanda kwenye majukwaa ya CCM kumpigia debe Alphonce Mawazo achaguliwe tena kuwa diwani kupitia CCM. Ndiyo maana viongozi wa CHADEMA wilaya ya Arusha mjini walikuwa hamwelewi yeyote aliyeunga mkono Lema kugombea ubunge kupitia chama chao kwenye uchaguzi wa 2010.

Nimeshtushwa sana na maneno ya ‘mfanyabisiasa’ hivi karibuni akichangia bungeni taarifa ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda na biashara. Lema akichangia taarifa hiyo alizungumzia kiwanda cha General Tyre, kiwanda cha kutengeneza matairi kilichoko mjini Arusha. Lema aliongea vema kabisa juu ya umuhimu wa kiwanda hicho kwa ukanda huu wa Afrika mashariki na kati. Ni kweli kwamba kiwanda hiki ni muhimu sana. Ni kiwanda kilichokuwa kinasambaza matairi Afrika mashariki na kati na kilikuwa hakitoshelezi soko hilo.

Niliwahi kutembelea kiwanda cha matairi Arusha. Kiwanda hiki kilikuwa kikitumia teknolojia ya Continental ya Ujerumani na kuzalisha matairi bora kabisa katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kati. Matairi yake yalikuwa yakiiuzwa na hayakutosheleza soko. Maana yake ni kiwanda ambacho hakikutakiwa kufa badala yake kilitakiwa kupanuliwa ili kuongeza uzalishaji kutosheleza soko la Afrika mashariki na kati na baadaye kufikiria kwenda Afrika nzima.

General tyre walikuwa wamepiga hatua kubwa sana. Kwa sababu malighafi kubwa ya kutengeneza matairi ni mpira. Na kiwanda hiki kilikuwa kikiagiza malighafi hiyo kutoka Malaysia kwa gharama kubwa. Ikabidi wafanye utafiti kuona ni wapi Tanzania kuna aina ya hali ya hewa na udongo unaohitajika kwa kilimo cha mpira kama Malaysia. Wakapata kwamba ni Mkoa wa Tanga. Wakaenda Tanga na kununua mashamba makubwa kwa ajili ya kilimo cha mpira kama ule wa Malaysia ili baada ya miaka michache waanze kuvuna malighafi hapa hapa Tanzania na kupunguza gharama ya kutengeneza matairi. Mipango murua kabisa kwa kiwanda kilichokuwa na chango mkubwa kwenye uchumi wa taifa na kuajiri watu zaidi ya 1,000 kikifanya kazi saa 24.

Lakini kilichotokea ni kwamba vigogo waliokuwa wanaagiza matairi kutoka nje walitaka kupata faida ya haraka kwa ajili yao na faimilia zao. Wakakiua kiwanda kile ili matairi wanayoleta kutoka nje yapate soko na wao wanufaike zaidi kibinafsi. Hiyo ndiyo Tanzania ya kabla ya Magufuli kuingia madarakani. Kila mtu alifanya alilotaka kulingana na ‘urefu wa kamba yake’.

Bunge la kumi la Tanzania (2010 – 2015) liliunda Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC). Katika kipindi hicho, kamati hiyo iligundua kwamba Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lilikuwa linakidai kiwanda hicho bilioni kadhaa lilizokikopesha na kwamba NSSF ilitaka kiwanda kiuzwe ili kurejesha fedha zake. Ndipo POAC katika kujifaragua kukiokoa kiwanda cha General Tyre iliunda kamati ndogo ya kufuatilia na kushauri namna ya kuifufua general tyre. Kwenye kamati hiyo ndogo waliomba baadhi ya wajumbe watoke kamati ya Viwanda na biashara na pia waliomba Godbless Lema, mbunge wa Arusha mjini, aingie kwenye kamati hiyo ndogo kama mbunge mwenyeji wa jimbo la Arusha mjini kilipo kiwanda hicho.

Lakini kabla hata kamati hiyo ndogo haijaanza kazi, kukawa na kikao cha kambi rasmi ya upinzani bungeni, kikao ambacho kilipoanza Zitto Kabwe hakuwepo. Zitto wakati huo alikuwa ndiye mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC). Kwenye kikao hicho Godbless Lema akamlalamikia Zitto kwa kuunda kamati ndogo ya kwenda kuchunguza general tyre bila kumhusisha yeye mbunge mwenyeji. Mungu saidia, Zitto akatokea kabla kikao hakijaisha na ndipo baadhi ya wabunge wakamwomba atoe ufafanuzi juu ya madai ya Lema. Kwa mshangao wa wengi, Zitto akasea alimhusisha Lema na kwamba Lema ni mmoja wa wajumbe kwenye kamati hiyo ndogo.

Kamati ikaja Arusha na kufanya kazi yake. Zitto Kabwe alikuwa amemwomba Esther Matiko awe anampa taarifa zote za kitakachoendelea. Baada ya kazi ile Esther Matiko akamtaarifu Zitto kwamba walipofika Arusha Lema alizungumza na baadhi ya wafanyabiashara mjini Arusha na wamemhakikishia kwamba wako tayari kulinunua eneo kilipo kiwanda cha General Tyre kwa bei nzuri.

Sasa Lema akaja kuwashawishi wabunge wenzake kwenye kamati ile ndogo kwamba kwenye mapendekezo yao waandike kwamba eneo kilipo kiwanda pameshakuwa mjini mno. Kwa hiyo washauri kwamba eneo hilo liuzwe, kisha litafutwe eneo lingine nje ya mji ndiko kihamishiwe kiwanda hicho. Halafu akawa anawaahidi wabunge hao kwamba kila mmoja atapata kiwanja kwenye eneo hilo na linalobaki litakuwa la wafanyabiashara hao watakaolinunua.

Hakuishia kwa hao aliokuwa nao kwenye kamati hiyo ndogo. Akaamua kumfuata Mwenyekiti wa POAC na kumwambia hayo hayo. Tena akamuuliza kwamba yeye hataki kuwa na estate kwenye jiji kama Arusha? Bahati nzuri mwenyekiti alimkatalia. Taarifa ya kamati ile ilipojadiliwa kwenye POAC, ikakubaliwa kwamba kiwanda hicho kifufuliwe na kimilikiwe kwa ubia kati ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambayo ilikuwa inakidai kiwanda hicho. Maazimio hayo hayakuwahi kufanyiwa kazi mpaka serikali ya awamu ya nne inaondoka madarakani.

Nimeshtushwa sana na Lema kurudi bungeni na kauli zile zile hivi majuzi akichangia taarifa ya kamati ya bunge ya viwanda na biashara. Lema alisema, “Pale kilipo kiwanda cha general tyre ni katikati ya makazi ambayo ni elites. Ni karibu ekari 70. Ukiweza kuuza ekari moja pale ni karibu shilingi milioni 300 au milioni 400 kwa mnada. Kwa sababu ni eneo prime. Kwa hiyo general tyre ukiithamanisha leo ni zaidi ya bilioni 28 mpaka 30.
Kiwanda cha matairi mheshimiwa mwenyekiti, hakihitaji zaidi ya dola bilioni 15 bilioni 20. Maana yake nini, mtaji ni eneo lile kuligeuza kuwa pesa. Nendeni kwenye maeneo ya EPZ yaliyoko katika mkoa wa Arusha, chukueni zaidi ya eka 100. Tafuteni mwekezaji atawakuta na ardhi na atawakuta na pesa. Kiwanda tayari kitafunguliwa".

Serikali isimsikilize huyu mfanyabiasiasa Godbless Lema kuhusu kiwanda cha General Tyre. Hana lingine zaidi ya kutaka ‘kupiga’ pesa. Serikali ikitekeleza hicho anachokisema Lema, atakwenda kuwaambia matajiri wake kwamba ni yeye aliyepigania ‘dili’ hilo mpaka kulifanikisha. Kisha watanunua eneo hilo kwa bei chee na kumpa yeye mgawo wake. Tunaomfahamu tunajua namna baada ya kuwa mbunge alivyopata kiwanja alichojenga nyumba yake anayoishi sasa. Tunajua ‘dili’ zote alizopiga mjini.

Tunakumbuka alivyosuguana na aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Arusha mjini akimtuhumu Lema kwamba alikuwa anachangisha mamilioni ya pesa toka kwa wafanyabiashara wilayani Arusha mjini kwa jina la chama lakini pesa hizo alizipiga zote hakuna hata senti iliyoingia kwenye chama. Tunajua alivyokuwa mwenyekiti wa kamati ya fedha kwenye kushughulikia madhara yaliyotokana na maandamano ya Januari 5, 2011 mjini Arusha. Akakusanya pesa kwa ajili ya majeruhi na wafiwa na hazikuonekana wala hakuwahi kuleta taarifa kwenye chama.

Serikali inajua kwamba kiwanda cha General Tyre kimejengwa kwenye eneo la viwanda huko Njiro jijini Arusha. Chini ya kiwanda ya General Tyre utakuta kiwanda cha madawa, kiwanda cha nguo, kiwanda cha mafuta na vingine vingi. Ukiwa unatoka mjini kuelekea Njiro, kabla ya kiwanda cha General Tyre utakuwa umepita kiwanda cha bia kilicho karibu na viwanda vilivyokufa vya kiko na cha nguo cha Kiltex. Kisha utapita kiwanda cha soda za pepsi.

Ukifika kwenye kiwanda cha General Tyre, utaona kinatazamana na Carmatec ambacho pia ni kiwanda kwa namna fulani. Baada ya kiwanda cha General Tyre ukiendelea mbele na barabara ya Njiro, utakuta kituo cha mafuta cha Puma na baada ya hicho kituo cha mafuta unafuata mfululizo wa viwanda kikiwemo cha mbao (Fibrewood) na cha vyakula (superfood) pamoja na cha mikate.

Kwa hiyo kauli ya Lema kwamba kiwanda cha General Tyre kimejengwa kwenye makazi ya watu ‘elites’ ni ya kupuuzwa kabisa. Kiwanda hicho kiko kwenye eneo la viwanda na miaka yote kimefanya kazi bila bughudha yoyote. Kwenye eneo hilo la viwanda hakuna ekari inayouzwa milioni 400. Nilifanya kazi kwenye kiwanda kimojawapo cha vyakula kilichojengwa eneo la viwanda la Njiro na wakati wa ujenzi wa kiwanda hicho miaka kadhaa tu iliyopita eneo la zaidi ya ekari moja lilinunuliwa kwa milioni 75. Hizo milioni 300 – 400 anazozitaja Lema ni uongo wa mchana wa kutaka kufanikisha anachokitaka kwa maslahi binafsi.

Kiwanda kile kina majengo yaliyokamilika ya kiwanda na hata ya utawala. Kina mashine zilizosimikwa, kina fence nzuri, kina rasilimali nyinginezo ukiwemo uwanja wa michezo. Na kina eneo la ziada la kutosha kwa ajili ya upanuzi. Tukiamua kuuza eneo hilo tutapata hela kidogo ambayo haitaweza kukihamisha tu kama kilivyo pale na kukipeleka eneo lingine. Halafu kuna suala la muda na urahisi wa kupata mwekezaji. Kukiwa na kiwanda kinachotakiwa kufanyiwa matengenezo tu na kuanza tena uzalishaji ni rahisi kupata uwekezaji au hata taasisi za umma kuwekeza kuliko kutafuta mwekezaji wa kwenda kuanza upya kujenga kiwanda ili tu wachache wafaidike.

Wafanyakazi wa General Tyre wametapakaa mjini Arusha wengine maisha yamewapiga wamekimbilia nje ya Arusha. Wameishi kwa matumaini ya kurudi kazini miaka yote, halafu leo tuwaache waendelee kusota mpaka tujenge kiwanda kipya. Haya ni mawazo yanayoweza kutoka kwenye kinywa cha fisadi tu na si vinginevyo.

Lakini juu ya yote namalizia kwa kusema kwamba serikali ya awamu ya tano imenuia kuifanya nchi hii ya viwanda. Haiingii akilini kwa nini mawaziri wote wa viwanda hawajafanya juhudi za kuwezesha kufufuka kwa kiwanda hiki muhimu. Hiki kiwanda kikianza leo, leo leo kinaanza kuunza matairi Tanzania yote bara na visiwani, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Malawi, na kwingineko. Waziri wa viwanda chukua hatua za haraka kiwanda hiki kianze. Ni cha pekee na kitatuweka kwenye ramani nzuri sana ya uzalishaji matairi. Mashamba ya Tanga yaendelezwe ili tufikie kutumia mpira wetu na si kuagiza Malaysia.
 
Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
9,320
2,000
Nyumbulism hamuwezi soma vitu vigumu kama hivi zaidi ya kuhisi tu na ku-comment heading bila kujua content
Rudi shule ukajifunze kuunda sentensi ya Kiingereza wewe:

Nyumbulism ni abstract noun na Nyumbu ni proper noun,huwezi kutumia abstract noun kuwakilisha watu!

Andika Kiswahili tu!Yanini kumuiga tembo kunya wewe?
 
Content nimesoma na ninaona contradictions throughout!

Ndio maana ni Pile of Shit!

Samson Mwigamba is a walking contradiction!
 
stella1975

JF-Expert Member
Nov 25, 2018
874
1,000

Wewe ni mjinga tena ni jinga kuna kitu unanufaika na huu upuuuzi, huyu alieandika hiii kitu ni mbunge au mfanyabiashara maarufu, sasa anatetea maslahi jinga kabisaaa hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
32,010

Hawa kina lema wanaishi enzi zile za upiga dili
 
Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
9,320
2,000
Ungeweka hizo contradictions ingependeza zaidi ili kupanua watu mawazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Niweke za nini?

Pitia mwenyewe utaziona....unajua kusoma,mpaka usomewe?

Kama umesoma na huoni contradictions ni wewe,mimi na yule tunatumia miwani tofauti,tunaona kwa mrengo wa tofauti na ni haki yetu pia!

Wewe hujaona,mimi nimeona,nani wa kumsema mwenzie?None!
 
kantalambaz

JF-Expert Member
Dec 24, 2017
1,647
2,000
Unajificha kwenye kichaka cha ujumbe huh.....

Shule tulikupeleka, halafu mpaka leo hujui kuumba sentensi ya Kiingereza,halafu unajificha kwenye kichaka cha ujumbe?

Hivi lini Watanzania tutakubali tunapokosea na kujirekebisha?
Hapa hatuko kwenye somo la linguistics tafadhali tujikite kwenye hoja ya msingi. Kama wewe ni mahiri sana wa lugha nakuashauri uanzishe uzi wa mambo hayo itapendeza zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
9,320
2,000
Hapa hatuko kwenye somo la linguistics tafadhali tujikite kwenye hoja ya msingi. Kama wewe ni mahiri sana wa lugha nakuashauri uanzishe uzi wa mambo hayo itapendeza zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nani amekwambia tuko kwenye somo la Linguistics?

Umejenga sentensi vibaya inaleta meaning tofauti kabisa na ile uliyokua unaitaka,umeambiwa,bado unajishebedua,sasa sijui unataka tukufanyeje?

Tusikwambie ukikosea kuandika sentensi kwa lugha uliyosoma darasani kwa miaka zaidi ya 14 na ada na resources zaidi ya mamilioni ya fedha?

Nyie ndio tunawachagua marais wetu mikataba inakuja mnasaini kama majuha!

Sijui Tanzania tutakuja kupata mwenye akili lini!
 
Rich Hash

Senior Member
Mar 7, 2017
148
250
Unachosha daaaah

Sent using Jamii Forums mobile app
Pile of shit!
Nyumbulism hamuwezi soma vitu vigumu kama hivi zaidi ya kuhisi tu na ku-comment heading bila kujua content
Rudi shule ukajifunze kuunda sentensi ya Kiingereza wewe:

Nyumbulism ni abstract noun na Nyumbu ni proper noun,huwezi kutumia abstract noun kuwakilisha watu!

Andika Kiswahili tu!Yanini kumuiga tembo kunya wewe?
Endelea ku-google uendelee kuleta matango pori
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom