Gen. Ndomba amrithi Shimbo

Status
Not open for further replies.
Huyu Ndomba hicho cheo amekipata baada ya kupikwa na kuiva kama kada mwaminifu wa CCM...tusitegemee mabadiliko yoyote katika utendaji jeshini.
 
Haya sasa mbona kimyaaa! Sijasikia la udini? Hii ina re assure imani yangu - pamoja na mapungufu kibao iliyonayo mkulu, sio mdini! Cheki wakuu wa TRA,PCCB, JWTZ, BoT, TSAF, P/Minister, Finance Minister, etc.

Mkulu hongra kwa hili nchi yetu inazidi kusonga mbele katika kuuzuka u-dini na u-kabila!
 
Ogah, Job K,

..Lt.Gen.Ndomba ana miaka 58.

..mtangulizi wake,Lt.Gen.Shimbo[rt], amestaafu akiwa na miaka 60.

..sasa hapa kuna maswali mengi naanza kujiuliza.

NB:

..Gen.Davis Mwamunyange anavunja rekodi ya kuwa Chief of Staff pekee aliyepanda cheo na kuwa Chief of Defence Forces.

..Gen.Tumainieli Kiwelu naye ndiye Generali pekee ambaye hakuwahi kushika nafasi ya Mkuu wa Majeshi. Alipandishwa cheo kuwa Jenerali baada ya kumaliza kipindi chake cha kuwa Mnadhimu Mkuu.

Huyu jamaa bado kajificha kule Kyaka baada ya kustaafu? He was one of very serious generals. Alikuwa hajui kukwepesha.
 
Asasi pekee nchini ambayo nahisi bado haijaingiliwa na uoza wa haya mawili ni jeshi, hasa katika ngazi za juu kama hii ya Unadhimu Mkuu wa Jeshi. Nasema hivi kwa sababu jeshi la ulinzi halishughuliki na [mambo ya ki] raia moja kwa moja tafauti na jeshi la polisi ambalo hupokea amri za wanansiasa.

Kuhusu udini jeshini ndio kabisa, hili halipo. Nahisi huwa ni sisi wenyewe tunaojenga mlima kutokana na kichuguu kwa tabia yetu ya Kitanzania ya kulalamikalalamika, kulialia ovyo na kukosa kila kitu, baada ya kuangalia mteuliwa anatoka dini gani. Imekuwa ni kawaida kwetu akiteuliwa Mkristo, Waislamu hulalamikia udini na akiteuliwa Muislamu Wakristo hulalamikia udini, kwa ubinafsi wetu wa kutaka tumuone mtu wetu akiongoza asasi hiyo, wakati masikini mteuliwa mwenyewe haendi kutoa misa kanisani wala hotba msikitini. Dini imekuwa ndio siasa zetu, na siaa zimekuwa ndio dini yetu.

Tuache hizo Watanzania, tujadili maendeleo!


Ninampongeza Jenerali S. A. Ndomba kwa kuteuliwa na ninamuombea ufanisi katika kazi yake.

unasema kwa mapenzi, hisia, au uhakika? Inabidi ukumbushwe saga la shimbo na mambo ya suma jkt na pawa tila zao za kilimo kwanza
 
Lets say they are being underutilised will that be okay with you?

Ukiangalia namba ya wanajeshi tulionayo na gharama tunazotumia kwenye jeshi unadhani ina justify ukilinganisha na umaskini huu? au ulifikiria kula nazungumziwa ugali tu?

Zaidi ya kwenda kwenye parade na kurudi home hebu nambie kazi nyingine kubwa zinazofanywa?

Umeamua kuwa mwana diplomasia, lol!
 
Nafuu kidogo uteuzi wa jeshini unafuata vigezo, sasa kwa nini uteuzi wa majaji unakuwa tatizo?
 
Aisee inaonekana lazima kwanza uongoze JKT. Wale JWTZ walokuwa na cheo kama cha huyo kabla hajapandishwa inakula kwao

Kuhusu kupandisha cheo mantiki yake ni kwamba kijeshi "The Leader is Always Right" mwenye cheo zaidi yako hakosei na hata akikosea tekeleza amri kwanza halafu malalamiko baadae.

Imenikumbusha mbali hii kitu.., ipo hivi..., "the general is never wrong" "and if he is wrong, refer to rule number one" hii philosophy ilianza kwa general patton wa marekani aliyepiganisha vita ya pili.., huyu general alikua "daredevil".., alikua anaweza kupeleka battallion kushambulia brigade(kwa kawaida battallion 3 zinatengeneza brigade moja)..., cha maana alichokua anafanya ni kuwapa morali wanajeshi wake na kuwaaminisha wapo better trained and better equiped than the enemy.., na hii iliwasaidia sana wamarekani kubeba visiwa kadhaa vya mjapan though japan alikua na nguvu kubwa ya wapiganaji....,na yeye alikua anaenda front line kufanya assesment..,
 
Aliwapeleka mahakamani makanali mafisadi wa SUMA JKT, alipokuwa bosi kule.
 
Nasisitiza Slaa hakuachishwa bali alikubali mwenyewe kuacha
Alifanya nini mpaka akatakiwa na "akakubali mwenyewe kuacha"?

Hakuvuliwa.Inasemekana aliamua yeye mwenyewe kuacha upadri na kuingia kwenye siasa
"Inasemekana"? Hujui, huwezi kusema "hakuvuliwa," wakati unakiri kwamba hujui.

"Inasemekana"? That's exactly my point, hakuna anaejua ni kwa nini, zaidi ya yule aliyempa barua ya kutengua utumishi wake.
 
Samwel Ndomba namfahamu akiwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara. Alikuwa mkali sana kwa maendeleo ya watu wa Ngara bila shaka zile powetiller pale Lugalo zitakwenda vijijini kufanya kazi yake ikiwa ni pamoja na kuanza kuiba sera ya Lowasa kulifanya jeshi kuwa moj aya wazalishaji wakuu wa chakula nchini.
 
Huyu hakuwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kama siyo Mkuu wa Wilaya? Kazi za hivyo vyeo vya wakuu wa mkoa au wilaya si ziko kwenye katiba ya CCM?
Mh Mizengo Pinda alilifafanua vyema kikao cha bunge kilichopita alipokuwa akijibu swali la mh Wenje. Unakumbuka kauli za Shimbo uchaguzi wa 2010?
 
unasema kwa mapenzi, hisia, au uhakika? Inabidi ukumbushwe saga la shimbo na mambo ya suma jkt na pawa tila zao za kilimo kwanza
@Raia Fulani Mkuu, hilo la siasa nimesema kwa hisia tukama nilivyoweka wazi tangu mwanzo kwenye bandiko langu. Ningefurahi, kwa faida yangu na wengine kama mimi kutukumbusha hiyo saga ya Shimbo hasa ikiwa tu saga hilo linahusu siasa.

Hilo la udini nimelisema kwa imani yangu ambayo bado ninaendelea kuwa nayo hadi nitakapothibitiwa vyenginevyo, kwamba Watanzania tunapenda kulalamikalalamika, kulialia ovyo na kukosoa kila kitu.
 
Basi tuwape wananchi sababu nyingi zaidi za kuwa proud na jeshi lao kwa kushirikisha hawa wanajeshi kwenye miradi ya maendeleo kama ujenzi wa miundombinu, kilimo cha kisasa nk sio kusubiri hadi maafa yatokee ndio waende kuokoa jahazi.

Kama unafuatilia vizuri kazi ambazo jeshi letu linafanya ni kuwa jeshi letu linafanya yote uliyoorodhesha kupitia JKT.

Haitakuwa busara iwapo tutawafanya wanajeshi wetu wote kuwa katika kujenga miradi ya maendeleo na kuacha kufanya kazi yao ya misingi ya kulinda mipaka ya nchi yetu na pia kufanya tafiti za kuendeleza mbinu za kisasa za ulinzi, sayansi na utawala bora!
 
Chief of staff mpya is not the right choice and in the matter of fact it is a snub to carrier commanders....within five years ....Ndomba amepanda cheo toka Mkuu wa Mkoa....,Kanali,brigedia jenerali ,(chief of personel), CN - chief of national service ,Maj general ..this year and yesterday Luteni Jenerali....
Ndomba is just a political commiser...Kama JK...bora Shimbo ni carrier.....,kozi stahiki za makamanda wa juu wa TPDF...Iitwayo ....NDC.....alipelekwa karibuni tu....wakati kuna wenzake wamefanyaa hiyo kozi toka wakiwa makanali....,wamepiganisha operesheni ..etc.....vitu ambavyo Ndomba hajafanya....... It's a blow kuweka wanasiasa kwenye kazi proffessional just kwa kuwa ni washkaji.......kuna makamanda KAma Wescesilous Kisampa,,hamad Kijuu,..Na Rioba...ambaye amepelekwa PMO kuratibu maafaa kwa kuwa in military seniority Ndomba asingeweza kuvaa...u Luteni general akawaruka yeye na Kisampa ....ambaye alipelekwa Dafur kupiganisha..majeshi ya Africa .........Ndomba hajaanza kufanya operesheni hata moja ya kijeshi Kama kamanda Mkuu ...so simply ni mwanasiasa na ni mweupe.

Very professional analysis!!!!
 
Ukitaka kupata uelewa wa Uteuzi huu soma thread yote hii alafu ndio uchangie hapa otherwise utakimbilia kusifia uteuzi alafu mwisho utafuta post zako zote za sifa kwa Gen Ndomba!
 
sikummbuki tarehe lakini ilikuwa ni mwezi may mwaka 2005.kulikuwa na mkutano wa wadau wa kilimo katika wilaya ya Ngara. Mgeni rasmi akiwa mkuu wa wilaya ya Ngara uteni Kanali Samwel Ndomba. Hadi muda wa kufungua ikoa unaanza mida ya saa 3 kamii asubuhi unafika, kulikuwa na wajumbe watatu pekee. Luteni kanali Ndomba aliwasubiri wafike, akafungue mkutano na kuagiza kuwa waliochelewa wote wasipewe posho. fedha hizo zipangiwe kazi nyingine.

Anakumbukwa Ngara kama mkuu wa wilaya amaye alisimamia miradi mingi ya maendeleo kwa kulisukuma UNHCR kutoa fedha z akufanya hivyo, hiyo ni pamoja na shule za sekondari Ndomba na Ngara kwa kutaja kwa uchache pamoja na kuboreshwa kwa kituo cha afya cha Nyamiaga( sasa ni hospitalikutokana na maboresho yaliyofanyika.

hata hivyo kuna baadhi ya ambo watu wengi hawaelewi hadi leo. Hatua yake ya kusukuma ujenzi wa soko la kimataifa karibu na iliyokuwa kambi ya wakimbizi ya Lukole, na baada ya kutoka wakimbizi soko hilo limebaki gofu kwani limejengwa mbali na makazi ya watu.

Anakumbukwa pia kwa kuwahi kuwaweka ndani Afisa kilimo na mifugo pamoja na mkuu wa polisi wa wilaya kwa kushindwa kusimamia maelekezo yake

Aidha mwaka 2006 katika kata ya kirushya wananchi walikumbwa na baa la njaa na kwa mujibu wa shirika la TCRS walikuwa wakiishi kwa maembe na wakati huo maembe hayo pia yalikuwa yameisha.

Luteni kanali Ndomba alikataa kukubali kwamba kuna njaa, hadi zilizopigwa kelele za vyombo vya habari na baadaya siu kadhaa aliamuru halmashauri ya wilaya iepeleke tai 10 za chakula cha msaada

kilichofuata baadaye ni Historia, alipadishwa cheo kuwa Kanali, akateuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha etc, etc

huyu ndiye ndomba ninayemfahamu ambaye ni mkatoliki mzuri
 
Kwani kupewa hvyo vyeo mpaka wapandishwe kuwa sijui ma luten, na kama ni hivyo kwani hakuna waliofikia huo u luten wapewe hizo nyazifa? naomba kujuzwa bandugu
Ndugu maguguniga vyeo ndani ya jeshi hasa vya Mnadhimu mkuu na mkuu wa jeshi la ulinzi ni kinashikwa na mtu mmoja aliye madarakani kwa wakati huo ndio mana hatuwezi kuwa na Ma-luteni Jenerali wawili ndani ya jeshi ama Mkuu wa jeshi (CDF) hivyo lazima mmoja astaafu ndio uteuzi hutolewa na kuchaguliwa mwenye cheo kinachokaribia Uluteni generali ambao huwa Meja-jenerali ama Brigedia generali kushika wadhifa tajwa hapo juu kama ilivyotokea kwa Meja -jenerali ndomba na kuwa Luteni jenerali.
 
Wote ni walewale tu. Subiri utaona. Mtu dhaifu huangaza kuona kama atapata watu dhaifu wamsaidie kuudumisha udhaifu uliopo usianikwe kiudhaifu. Ukisikia jogoo linawila saa 12 jioni ujue sio kawaida kwani kawaida ni kama sheria.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom