Gen. Ndomba amrithi Shimbo

Status
Not open for further replies.

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,230
13,415
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Meja Jenerali Samuel Albert Ndomba kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Aidha, Rais Kikwete amempandisha cheo Meja Jenerali Ndomba kuwa Luteni Jenerali.

Taarifa iliyotolewa leo, Ijumaa, Septemba 21, 2012, mjini Dar Es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu, imesema kuwa uteuzi huo unaanza leo.

Taarifa hiyo ya Balozi Sefue imesema kuwa kabla ya uteuzi wake, Meja Jenerali Ndomba alikuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Jenerali Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Abdulrahman A. Shimbo ambaye amestaafu Jeshi kwa mujibu wa sheria baada ya kufikisha umri wa miaka 60.

​Taarifa ya Balozi Sefue pia imesema kuwa Rais Kikwete amemteua Brigedia Jenerali Raphael Mugoya Muhuga kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa kuanzia leo, Ijumaa, Septemba 21, 2012.

Aidha, Rais Kikwete amempandisha cheo Brigedia Jenerali Muhuga kuwa Meja Jenerali.

Kabla ya uteuzi wake, Brigedia Jenerali Muhuga alikuwa Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
21 Septemba, 2012

 
Hongera JK kwa uteuzi huu makini ila tunataka fisadi Shimbo afikishwe mahakamani soon.
 
Katika vitu ambavyo sijawahi kuviamini hata chembe ni kashfa ya mzee aliyestaafu huyu kuwa alikuwa na trilion 3 south. Wabongo tunapenda sana umbeya kuliko taarifa zilizofanyiwa utafiti wa kina. Huyu mzee maskini kutoa lile tamko kwa niaba ya vyombo vya ulinzi na Usalama imekula kwake mpaka keshokutwa. Ila kwa kuwa sasa amestaafu embu sasa kwa ushahidi anikeni ukwasi alionao huyu mzee. Huyu aliyechukua nafasi yake kwasasa no comment ila kila anayeteuliwa na JK kuna vitu wanafanana sasa hatujui huyu wanafanana kwa lipi
 
Ndugu yetu Ndomba, tunakusihi Jeshi la WANANCHI Tanzania liendelee kubakia kuwa mali ya WANANCHI na wala si mali ya CCM tena kwa kipindi chochote kile hasa wa uchaguzi.

Ziara ya kwanza nenda ukatembelee Ziwa Nyasa na ukanywe chai pale Domira Bay nchini Malawi, ukale chakula cha mchana pale Olivenca nchini Msumbiji kabla ya kuja kusuuzia na wali manukato wa pale Kyema na kulala huko huko hadi kesho yake.

Matumaini yetu ni kwamba Kaka Denisi Mwamnyange atakua amepata msaidizi wa kutumainika na wala si kuendeleza tu siasa za ma-ofisini.

Jicho letu liko nje mkuu hadi siku ya kuvishwa kwako wewe taji kwa 'kazi nzuri' wakati wa kustaafu kwako na wewe.
 
Mmatengo huyu wa Mkumbi huko Mbinga nadhan ataacha unazi wa CCM na kufanya kazi kiweledi zaid.
 
Hongera Ndomba kwa kula shavu jk atampa shimbo kazi ingine
 
Ni rafiki mkubwa wa JK sababu ya utendaji wake na msimamo wake!!alishapendekezwa hapo nyuma kumrithi Dr Hosea pale Takukuru!iliposhindikana akapewa utumishi jeshini,baadae akaenda JKT,,,ni mchapakazi sana na hodari!Hongera JK kwa hilo!
 
Tunawaombea wateuliwa wote utumishi uliotukuka. Tunaamini hawatamwangusha Rais katika kutekeleza majukumu yake ya kikazi.
 
Tatizo lililokuwa limelikumba jeshi letu la ulinzi ni madai ya uingizaji wa siasa jeshini, na chembe za udini kushamiri ndani ya jeshi.

Simujui kwa undani Jenerali Ndomba, lakini kwakifupi inatajwa kuwa huyo ni moja ya masalia imara ya vijana wa Mwalimu Nyerere walioamini katika UZALENDO.

Nimtu mashuhuri mwenye uso wa kijana akijitunuku tabasamu la nidhamu ya kijeshi, wadadisi ndani ya SIASA za kijeshi wanamtaja kuwa ndie mrithi stahiki wa Mkuu wa Majeshi Aden Mwamunyange.

Anatajwa kuwa ni kijana na tokezo la akina Jen Waitara, Jen Mboma na Jen Mwamunyange.

Naamini katika safari hii iliyo ndefu na inayokaribia ukingoni yakulikomboa Taifa letu, General Ndomba asiwe kikwazo wa mageuzi haya ya kiraia yenye kuongozwa na alama za nyakati ambazo kihistoria na kimaandiko hazijawahi kupingwa kwa mtutu wala kombora.
 
Shimbo fedha za south Africa ni kweli zako?mbona unaondoka kimya kimya na boss wako JK akikuaga kimya kimya?duh!hali hii mpaka lini?na wewe afande Ndomba pokea cheo hicho kwa uangalifu maana bado muda mfupi tuingie kwenye uchaguzi usifanye ya Shimbo tafadhali.Ndomba nakutakia kazi njema afande
 
Kwani kupewa hvyo vyeo mpaka wapandishwe kuwa sijui ma luten, na kama ni hivyo kwani hakuna waliofikia huo u luten wapewe hizo nyazifa? naomba kujuzwa bandugu

Jeshi linafanya shughuli zake kwa amri. Mtu mwenye cheo kikubwa hutoa amri na mwenye sheo kidogo analazimika kuipokea hiyo amri. Cheo kikubwa kabisa ni general kinafuatiwa na luten general halafu major general then brigedia, colonel, luten colonel, Major, Captain etc.

Kila wakati jeshi huwa na general mmoja na luten general mmoja. vyeo vingine vinaweza kuwa zaidi ya mmoja. Kwa hiyo kustaafu kwa huyu kunampa nafasi yule anayefuatia kupandoshwa cheo ili kushika nafasi ile na kumpa uwezo wa kutoa amri kwa walio chini yake.

Kwa mfano, Brig. Muhuga angewekwa kuwa mkuu wa JKT bila kupandishwa kuwa Maj. Gen. angepata vikwazo katika kutoa amri kwa mabrigedia wengine waliokuwepo JKT hasahasa kama walijiunga jeshi au kuupata ubrigedia kabla yake.

Hiyo ndiyo sababu ya kupandishwa vyeo wateule hawa wa leo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom