Gen. Mboma ajaribu kugombea, aangushwa!

Gen. Mboma ajaribu kugombea, aangushwa!

Huyu mtu ana uwezo mkubwa sana ki akili na na vilevle ana busara si za kawaida, nafikiri kwa kupata ubunge atasaidia watu wengi sana, huko Mbeya, Bungeni, serikalini hata Nchi nzima , lazima tukumbuke bila wazee wenye vipaji na busara nzito kama za huu mzee tunaweza kupoteza mengi.[/QUOTE]

- Makubwa haya, walete walete hao saafi sana!
 
Huyu mtu ana uwezo mkubwa sana ki akili na na vilevle ana busara si za kawaida, nafikiri kwa kupata ubunge atasaidia watu wengi sana, huko Mbeya, Bungeni, serikalini hata Nchi nzima , lazima tukumbuke bila wazee wenye vipaji na busara nzito kama za huu mzee tunaweza kupoteza mengi.

Alisubiri aliyetangulia afe ndio aje kuonesha busara, vipaji na kusaidia siyo? Una akili sana wewe gggggggggggrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrhhhhh!!!!
 
ha ha ha ha ha ha

nimeamua kucheka mawazo ya R. Mboma na wastaafu wengine kwani yanahitajika tena??????? hata watafiti wa mambo wanasema ana weza tu kuwa mshauri wa mambo aliyoyafanya akiwa na uwezo wa kuwa mfanyakazi kweli bunge linaweza kuwa sehemu ya wastaafu kwa kuwa GANDA LA MUA LA JANA CHUNGU KIVUNO
 
inabidid watanzania tuwe makini tunapochagua wabunge wetu. Huyu Mboma alikuwa mkuu wa jeshi na bado ni mshauri mkuu wa jeshi, sasa yeye kujiunga na siasa tutamwambini vipi kwamba atatoa ushauri kwa jeshi ambao upo neutral? hii kweli ni mambo ya mugabe and mseveni.... uwiiiiiiiiiiiiii

tupe story wajameni.. leteni ufisadi wake huyu jamaaaa
 
Huyu mtu ana uwezo mkubwa sana ki akili na na vilevle ana busara si za kawaida, nafikiri kwa kupata ubunge atasaidia watu wengi sana, huko Mbeya, Bungeni, serikalini hata Nchi nzima , lazima tukumbuke bila wazee wenye vipaji na busara nzito kama za huu mzee tunaweza kupoteza mengi.

MHH wewe byabusha... i hope you are not serious mzee wangu!! this is new country, mambo ya busara kwa ajili ya umri umepitwa na wakati, kama ni mtu wabusara akae awe anashauri serikali na awaache young generation watende kazi

Kwanini watu hawamuuigi late J.K.Nyerere and mzee mandela? awa ndio wanabusara na wakaona kwamba inabidi wapass their abilities kwa muda uliobaki wa maisha yao kufundisha uongozi bora kwa generation iliyobaki, mbona na ndugu zake wa ccm wote wanatamaa ya uongozi
 
Huyu mtu ana uwezo mkubwa sana ki akili na na vilevle ana busara si za kawaida, nafikiri kwa kupata ubunge atasaidia watu wengi sana, huko Mbeya, Bungeni, serikalini hata Nchi nzima , lazima tukumbuke bila wazee wenye vipaji na busara nzito kama za huu mzee tunaweza kupoteza mengi.

Duh! Post ya kwanza tu, shombo baraza zima! kazi kweli kweli.
 
Bw Byabusha
Ulisikia wapi CDFs wanawekwa kwenye list ya matajiri duniani? Uliza kati ya MaCDF wa enzi zake yeye alikuwa wa ngapi, then ulinganishe na mapato yake na utuambie kama vina uwiano. By the way ule mgodi wake vipi?
 
Huyu mtu ana uwezo mkubwa sana ki akili na na vilevle ana busara si za kawaida, nafikiri kwa kupata ubunge atasaidia watu wengi sana, huko Mbeya, Bungeni, serikalini hata Nchi nzima , lazima tukumbuke bila wazee wenye vipaji na busara nzito kama za huu mzee tunaweza kupoteza mengi.

Upu'zi mtupu....
 
Gen. Mboma anadai yeye kalipwa kiinua mgongo kizuri hivyo haitaji kujinufaisha zaidi ya kuwaletea wananchi wa Mbeya maendeleo. Bull*&#$t. Mbona hazungumzii juu ya Meremeta na upuuzi wote huo. Kuwaletea wananchi maendeleo si lazima uwe Mbunge. Kuna watu wengi wamepeleka maendeleo kwa wananchi bila ya kuwa na Ubunge. Sipendi kuwataja majina maana watu wengine wanaweza kusema ninawafagilia hapa.
Hizo pesa alizoibia Taifa anatakiwa azirudishe kwa wananchi ili zisaidie maendeleo yao. Yaani hana hata aibu kuzungumzia kiinua mgongo, ni haki yake kupata kiinua mgongo chake lakini kama angekuwa mzalendo kweli angeachana na kiinua mgongo kulingana na pesa aliyoiibia Taifa la Tanzania na wananchi wake kwa ujumla. Huu ni Uroho, Ulishastaafu pumzika ukisuburi zamu yako kwenda KISUTU.
 
Mkuu by a Busha by JF....People don't buy cheap arguments..Ni lazima uje na fact la sivyo you'll be by a.....
 
Gen. Mboma anadai yeye kalipwa kiinua mgongo kizuri hivyo haitaji kujinufaisha zaidi ya kuwaletea wananchi wa Mbeya maendeleo. Bull*&#$t. Mbona hazungumzii juu ya Meremeta na upuuzi wote huo. Kuwaletea wananchi maendeleo si lazima uwe Mbunge. Kuna watu wengi wamepeleka maendeleo kwa wananchi bila ya kuwa na Ubunge. Sipendi kuwataja majina maana watu wengine wanaweza kusema ninawafagilia hapa.
Hizo pesa alizoibia Taifa anatakiwa azirudishe kwa wananchi ili zisaidie maendeleo yao. Yaani hana hata aibu kuzungumzia kiinua mgongo, ni haki yake kupata kiinua mgongo chake lakini kama angekuwa mzalendo kweli angeachana na kiinua mgongo kulingana na pesa aliyoiibia Taifa la Tanzania na wananchi wake kwa ujumla. Huu ni Uroho, Ulishastaafu pumzika ukisuburi zamu yako kwenda KISUTU.

Ni lazima atueleze Jeshi lilihusika vipi na kashfa ya Meremeta ambayo mabilioni ya pesa toka BoT yaliingia katika kampuni hiyo kinyemela. Je, alinufaika na wizi huo, Je anajua chochote kuhusian ana jeshi kuhusika na machimbo ya Meremeta?
 
Next time, msishangae kusikia Jaji mkuu mstaafu Barnabas Samata naye amejitosa kwenye ubunge kupitia CCM. Then, mwenyekiti mstaafu wa tume ya uchaguzi, former msajili wa vyama vya kisiasa, the list goes on and on and on........This recycling is too much.

UMESHAHU KAMA ALIYEKUWA MSAJIRI WA KWANZA GEORGE LIUNDI ALISHINDWA KTK KURA ZA MAONI MARA TU BAADA YA KUACHIA KITI HICHO?

NAOMBA TUAMINI KUWA FORMER CDF ANA SABABU ZA MSINGI ZA KUINGIA HUKO ANAKOTAKA AINGIE, SWALI NI CCM WENYEWE NA MFUMO WAKE, WAKO TAYARI KUWA NA GIANT HUYU KTK JUMBA LA SPIKA SITTA?

LEO NIMEISIKILIZA RADIO MOJA KTK USOMAJI WA MAGAZETI YA BONGO, WAMENG'ANG'ANA NA UJESHI WA MBOMA, HOJA YAO KUU NI ILE YA ZITO, WANASAHAU 1995-00 MEJA JENERALI MARWA ALIINGIA KILINGENI LAKINI PIA KUMBUKENI KUWA KALEMBO NA WENGINEO KTK SIASA ZETU, NASEMA HIVI NIKIFAHAMU KUWA UKIFIKIA LEVEL YA JENERAL(Brigedia,Meja,Luteni) UNAISHI KWA KODI ZETU MPAKA UNAKUFA, TOFAUTI NI NDOGO SANA KWAO KULINGANA NA RANKS ZAO.

GENERAL MBONA YUKO NJE YA MEDANI ZA JESHI TANGU 2002, MORE THAN 6YRS NOW, CCM WANASEMA NI LAZIMA UWE MWANACHAMA HAI KWA KIPINDI KISICHOPUNGUA MIAKA MITANO, TATIZO LIKO WAPI?

REJEENI MAREKANI PALE GENERAL COLLIN POWEL ALIPOINGIA KTK SAISA ZA KI REPUBLICAN NA KUTEULIWA KUWA 1ST BLACK SS AKIWA NA HESHIMA YA MKUU WA MAJESHI MSTAAFU.

MBOMA KUINGIA HUKO ANAJUA HATARI YA SIASA, MAKUNDI KTK SIASA ZA CCM, NA ZAIDI HALI YA NCHI KWA SASA, NARUDIA TENA, GENERAL MBOMA YUKO TAYARI KWA LOLOTE NA NDIO MAANA YA YEYE KUOMBA KUINGIA HUKO MJENGONI.
 
ukisha kula nyama ya mtu utaendelea kula tu, ukiacha ujue umekufa tayari.
Watu wanaotamani madaraka kwa uchu kama huu ni kama waliokula nyama ya mtu.
Mh mboma bado anakumbuka radha na utamu wa madaraka.
Pamoja na kukusanya mabilioni ya wizi, haoni raha kukaa na kuyatafuna kwani hakuna mtu anamwita mh au afande.
Akiukwaa amejianika mwenyewe, uchafu wake wote alofanya akiwa jeshini utawekwa wazi hapa.
Amshauri na afande defao(mahita) naye agombee ubunge ili idadi ya mishushu, mimwera na mijeshi izidi kuongezeka kwenye kilinge cha bunge.

ni heri tu wakuu, wacha wajeshi wajichukulie nchi yao taratibu, mzee apson itwae mbozi mashariki na igp mahita tusaidie kumdhibiti mwarabu abood hapo morogoro.

Siasa ni medani huru kwa kila anayeiona fursa hiyo na kuwa tayari kuitumia, tujenge hoja hapa na si kumtishia mboma eti atavuliwa nguo za ndani, ni nani aliyemsafi kati hao tunaowaamini mpaka tumtishie mboma kwa uchafu.

Siasa yetu inakuwa na ni wasaa sasa wa kujichuja
 
Mkuu FMES na Wakulu wengine,

Siasa za mbeya ziko tofauti sana na hata mambo ya Operesheni sangara yalileta matatizo.sababu Sangara siyo neno la asili yao na wananchi ndiyo walileta malalamiko hayo.

Tatizo la Mbeya siyo CCM.Ila Ukabila tu ..unaweza ukawa fisadi ila kama wewe ni mkabila basi Mbeya ni kwako.wewe unazani kazi anayo fanya Mwandosya ya kuwasaidia watu wa South Line mchezo.

siasa za huko Mie huwa siziongelei na nilisahaacha
 
Mbwembwe za Mboma

Wakati wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Mbeya Vijijini wanakutana kesho kupiga kura za maoni, aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Mstaafu Robert Mboma, amerudisha fomu za kuwania ubunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini kwa staili ya kipekee, huku akisindikizwa na viongozi wa mila (machifu).

Jeneral Mboma anawania kiti hicho kilichobaki wazi, kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Ruichard Nyaulawa, kilichotokea usiku wa kuamkia Novemba 9,mwaka huu.

Mboma ambaye alichukua fomu hizo juzi, alirejesha fomu hiyo jana saa 3 asubuhi akiwa na machifu ambao walimtanguliza kuingia ndani ya ofisi za CCM Wilaya ya Mbeya na kukabidhi fomu hizo kwa Katibu wa CCM Mbeya Vijijini, Hassan Dumwali.

Mbali na machifu hao, Jenerali Mboma pia alisindikizwa na baadhi ya ndugu zake akiwemo mkewe, Ajira Mboma.

Machifu hao ni Chifu Mwaluvanda wa kata ya Santilya na Chifu Fredy wa kata ya Ilungu, mwasisi wa CCM Mzee Aron Mwankina ambapo mmoja wao alikuwa ameshikilia bakora za kimila huku wakiwa wamemtanguliza Jenerali Mboma kuingia ofisi za CCM.

Mara baada ya kukabidhi fomu hizo, Jenerali Mboma alielezwa na Katibu wa CCM Mbeya Vijijini, Dumwali kuhudhuria mkutano mkuu wa CCM wa wilaya hiyo kwa ajili ya kupiga kura za maoni kwa wagombea utakaofanyika kesho.

Katibu wa CCM Wilaya ya Mbeya Vijijini, akizungumza na Nipashe Jumapili alisema wagombea wote tisa walioomba nafasi hiyo wamerejesha fomu na sasa kilichobaki ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kuwapigia kura za maoni.

Juzi akizungumza baada ya kuchukua fomu, alisema hagombei ubunge kwa ajili ya kufuata maslahi bora bungeni kwa sababu amelipwa kiinua mgongo kizuri, lakini lengo lake ni kuwasaidia kimaendeleo wananchi wa Jimbo la Mbeya Vijijini.

Mbali na Jenerali Mboma, wanachama wengine wa CCM waliokwisha chukua fomu ni Djovita Diame ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Mbeya Vijijini, Mchungaji Luckson Mwanjali (Katibu wa fedha na Uchumi), Aran Mwaigaga (Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Taifa).

Wengine ni Flora Mwalyambi (Mjumbe wa Halmashauri CCM Mbeya vijijini) Michael Mponzi ambaye ni mtoza ushuru kituo cha Igoma katika Halmashauri ya Mbeya vijijini, Petro Mwashusa (Afisa Elimu wilaya ya Chunya),Mariam Mwambanga, na Andrew Sayila .

Wakati huo huo,Wakili wa kujitegemea na ambaye pia ni askari mstaaf, Sambwe Shitambala, amechukua fomu za kuwania ubunge wa jimbo la Mbeya Vijijini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

SOURCE: Nipashe
 
Mboma ni mtu ambaye anafaa kuwania uongozi. Anayo haki,siyo kama anavyosema Zitto kwamba Mboma hana haki kugombea. Mboma has a right and a left. Kwa wale wasio elewa hiyo expression,it was used in the Wild West,the cowboys,who used to say,whenever asked what right have you got,they would say,I have a right and a left.
I am not suggesting the General is a wild man. Alikuwa Commanding Officer,CO katika kambi nilipokuwa Jeshini,kwa hiyo I know he is a reasonable person.
Kuhusu wale wengine waliojitokeza kuchukua fomu,siwafahamu,labda because they are University lecturers,au maybe they have not done anything for this Nation.
 
Mh jamani maana ya kustaafu mimi siielewi tena.............. Kwa heri
 
Mboma ni mtu ambaye anafaa kuwania uongozi. Anayo haki,siyo kama anavyosema Zitto kwamba Mboma hana haki kugombea. Mboma has a right and a left. Kwa wale wasio elewa hiyo expression,it was used in the Wild West,the cowboys,who used to say,whenever asked what right have you got,they would say,I have a right and a left.
I am not suggesting the General is a wild man. Alikuwa Commanding Officer,CO katika kambi nilipokuwa Jeshini,kwa hiyo I know he is a reasonable person.
Kuhusu wale wengine waliojitokeza kuchukua fomu,siwafahamu,labda because they are University lecturers,au maybe they have not done anything for this Nation.

Hivi kuna lecturers humo?

Kuwa CO resonable does not make him a good politician. Siasa za bongo ni kinganganizi tu cha madaraka hakuna kusaidia wananchi. Tatizo hawa jamaa wamezoea kuogopwa sasa wakitoka madarakani wanjikuta ni watu wa kawaida wanachanganyikiwa. Ndiyo sababu kila mmoja akiretire anakimbilia siasa. Si ulisikia hata Mahita anajaribu siasa????
 
Wakuu Mlekwa & Ngongo
Nakubaliana na hoja zenu za umoja ni nguvu.Lakini katika umoja huo, tukubaliane kuwa wakati mwingine tupanue wigo wa uchaguzi wa sera badala ya personalities au itikadi za vyama.Najua watz wengi wapenda demokrasia mna hamu sana ya kuona opposition inaongeza idadi ya viti bungeni.Mimi kwa upande wangu napenda tuwafundishe na kuwazoesha wapiga kura kuchagua ubora wa sera na mgombea.Naunga mkono CHADEMA wagombee, ili sera zao zitambulike kwa wapiga kura wa Tanzania hiyo ndio nafasi pekee ya kujitangaza.Ninachotaka kushauri hapa si vizuri,incase mgombea wao hauziki waanze kumkandia mgombea wa chama kingine cha upinzani.
Tofauti ya uchaguzi wa Tarime vyama vingine vya upinzani vilikuwa vinaonyesha kukipiga vita vya wazi CHADEMA.Hali hiyo isirudiwe,chama kishiriki kueleza sera na mikakati yake ya kuboresha na kutetea walipa kodi wa Taifa letu.
Mkuu Gembe, si kweli kuwa sisi watu wa Mbeya tuna ukabila.Nitakupa mfano wa madiwani wawili wa kyela na nitaonyesha mabano ya kata wanazowakilisha.Kuna Visky Mahenge ambaye ni mkinga(Kyela) na Mh.Chrissy ambaye ni mkulya(Ipinda).Vilevile kule mbozi wenyeji wa wilaya ni Wanyiha na Wanyamwanga, lakini Mwenyekiti wa Council ni mnyakyusa.Huyu marehemu Nyaulawa,alikuwa mkinga ambao kule Mbeya vijijini ni wachache na walio wengi ni Wasafwa na Wamalila(kabila la Mboma).Huu mkoa wa Mbeya sasa hivi una wahamiaji wengi kutoka sehemu mbalimbali ya nchi yetu na nchi jirani na wanaishi vizuri na kushiriki kwenye chaguzi mbalimbali za uongozi.Nakumbuka hata uchaguzi mkuu wa 2005,NCCR-Mageuzi walimsimamisha Temigunga Kisonga(mhehe) na alivutia wapiga kura wengi licha ya kwamba matokeo yalitoka kinyume na ilivyotegemewa.Mimi kama mchunguzi kilichowaangusha wapinzani ni kukosa network ya mawakala wa dhati kama wale wa Tarime.Kipindi kile mchuano ulikuwa mkali kati ya Mwakagenda(CHADEMA) na Kisonga(NCCR-Mageuzi),lakini matokeo yakawa landslide victory kwa mgombea wa CCM akisaidiwa na nguvu ya EPA.
Ninachokijua mimi ni kwamba wananchi wa Mbeya wana permanent interest,wanataka miundo-mbinu kama vile International Airport,Tarmac road mbeya-chunya-itigi,Chuo Kikuu cha sayansi na Teknolojia n.k.Mbeya hawana chuki na mtu yeyote anayejali maslahi yao na wala hawawezi kulambishwa pipi ya kupewa vyeo kwa sababu vyeo hivyo vinakuwa kwa waliopewa sio mkoa wote.Hawapendi kuzugwa!
 
Back
Top Bottom