Gen. Mboma ajaribu kugombea, aangushwa!

MKUU WA MAJESHI NA MNADHIMU NI KAMA MARAIS WASTAAFU WANALELEWA HADI WANAKUFA....LAKINI PIA KITENDO CHA MBOMA KUGOMBEA NI FUNZO KWA SERIKALI....INAWASAHAU SANA HAWA WAKUU WANAKUWA IDLE.....IWATAFUTIE ACTIVITIES.....MBALI YA ZILE WANAZOFANYA MASHAMBANI MWAO...

Mwanzoni mwa thread hii nilichangia kwa kusema ni AIBU kwa Mboma kudai kuwa alilipwa kiinua mgongo kizuri hivyo atakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuleta maendeleo kwa wananchi bila ya kuwa na tamaa ya kujitajirisha. Hiyo ilikuwa ni hoja ya KIPUUZI. Kuleta maendeleo kwa wananchi si lazima uwe Mbunge, kama yeye anafikiri kuwa yuko idle sana kwa nini asianzishe hata foundation ya kusaidia KUWALINDA MAALBINO?Kilio cha Maalbino Tanzania kimesikika kila pembe ya DUNIA, kwa nini yeye Mboma kwa kutumia QUALIFICATIONS zake alitumikie Taifa kwa kuhudumia MAALBINO. It's time for him to pay back to Tanzanians huku akiendelea kulelewa kwa KODI ya Watanzania.
AGAIN, MAENDELEO HAYALETWI KWA KUPITIA UBUNGE TU. Askofu, mhubiri maarufu nchini Marekani ambaye vilevile ni mtunzi wa Vitabu Thomas Dexter Sr. (Bis. T.D Jakes) anatumia talent na utajiri wake kutoa misaada kwa ajili ya Maendeleo ya baadhi ya nchi za Afrika kama vile Kenya, Uganda na Afrika Kusini. Amesaidia kujenga baadhi ya visima nchini Kenya. Hiyo inawarahisishia wanawake nchini humo kutembea mwendo mfupi kwenda kuchota maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Vilevile jamii inapata maji safi. Lakini yeye si muajiriwa wa serikali yoyote ile lakini anaona umuhimu wa kuhudumia wananchi wenye shida. Wapo watu wengi wenye moyo huo hata hapa nyumbani na mojawapo ni Bw. Mengi na wengineo.

Kama kweli Mboma anataka kueleta maendeleo kwa wananchi huko Mbeya bado ana nafasi hiyo nje ya Ubunge. Maana kipindi chote amekuwa kimya hadi ulipowadia wakati wa kuchukuwa fomu za kugombea jimboni mwake. Miaka 6 yote alikuwa wapi? Watu wataendelea kum-judge kwa matendo yake hasa baada ya kuangushwa kwenye kura za maoni. Wengine wakishaanguka kwenye kura basi hawaonekani tena. Anatakiwa kudhihirisha kwa Wananchi wote kuwa aliyokuwa akisema kuhusu maendeleo ya wananchi ni ya kweli. Aanze kuwahudumia wananchi huku akiendelea kuishi kwa pensheni inayolipwa kwa kodi ya walala puu..
 
Ndugu wa Mgonja wahaha
Mwandishi Wetu
Daily News; Tuesday,December 16, 2008 @21:15

Ndugu pamoja na watu wa karibu wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja, wanatafuta fedha kwa ajili ya kufanikisha dhamana ya ndugu yao ambaye juzi alifikishwa mahakamani akituhumiwa kutumia vibaya madaraka yake na kuisababishia serikali hasara.

Mgonja aliyekuwa Katibu Mkuu Mwandamizi wa Hazina hadi wiki mbili zilizopita, alipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka yake na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 11.

Mmoja wa mawakili wanaomtetea Mgonja, Dk. Alex Nguluma alisema kwa simu jana Dar es Salaam kuwa ndugu pamoja na watu wa karibu wa mtuhumiwa wanaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kumdhamini ndugu yao.

Wakili huyo alisema kutokana na upande wa mashitaka kukataa kumuunganisha mshitakiwa pamoja na washitakiwa wengine Daniel Yona na Basil Mramba, ambao kesi yao inalandana na ya mteja wao, hawatapeleka shauri hilo Mahakama Kuu kwa sababu itachukua muda mrefu na mtuhumiwa ataendelea kusota rumande.
Alisema kutokana na kutounganishwa huko, fedha anazotakiwa kujidhamini Mgonja ni nyingi kwa hiyo inamwia vigumu kulipa dhamana kwa kutumia mali zake mwenyewe.

Hakimu Mkazi Henzron Mwankenja, baada ya kusikiliza kesi hiyo juzi, alitoa masharti manne ambayo kama Mgonja atayatimiza, atakuwa nje kwa dhamana. Aliyataja masharti hayo kuwa ni ajidhamini kwa kuwasilisha fedha taslimu au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh bilioni 5.9 ambayo ni nusu ya fedha anazodaiwa kuipatia hasara serikali.

Sharti la pili ni mshitakiwa kutakiwa kukabidhi mahakamani hati za kusafiria na asisafiri nje ya Mkoa wa Dar es Salaam hadi kwa kibali maalumu cha mahakama. Pia alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika ambao watasaini hati ya dhamana. Mshitakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo na alipelekwa mahabusu ya Keko hadi Desemba 29, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.

Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Hazina ambaye alistaafu wiki mbili zilizopita, alisomewa mashitaka manane yakiwamo ya kuipa upendeleo Kampuni ya Alex Stewart (ASSAYERS) ya Uingereza iliyoingia mkataba wa kukagua kampuni za madini nchini ambapo kwa kupitia kampuni tanzu ya Alex Stewart (ASSAYERS) Government Business Corporation, waliingia mkataba na kampuni tanzu kuzalisha madini ya dhahabu kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma.
 
Mkuu PM,

Nakubaliana na mengi uliyoandika hapo. Ningeongezea hata Jaji mkuu kwenye hilo kundi.

Mkuu wa majeshi ana network kubwa sana, hivi kweli anaweza kukosa cha kufanya kwenye nchi maskini kama Tanzani? Kwa kushirikiana na NGO anaweza kutoa contributions nyingi sana kwenye jamii.

Hii ya kupewa majukumu mengine na serikali naona haifai. Mbona kuna mambo mengi sana ya maana ya kufanya Tanzania kwa mtu asiye na njaa?


kabisa lazima tuweke standards kwenye nchi...kwa mkuu wa majeshi ubbunge ni kama udiwani.......ni kitu kidogo sana......lazima tuweke wazi kuwa hawa wakishastaafu basi....wabakie washauri tu!....along umeongeza na jaji mkuu...nakubali..!!

tuangalie namna bora ya kuwafanya wastaafu wetu nyeti kuwa busy...waandike vitabu...watoe mihadhara vyuo vikuu ..,waazishe NGO...,tena kama mboma wala hawezi lalamika kuwa idle kwani mara kadhaa ameteuliwa kwenye boards na kamati.......

pia kuna tabia kwa majaji imetokea ..wanastaafu wanaomba kuwa mawakili....hapa kuna udhaifu ..je wanapewa kiinua mgongo kidogo?????...juzi nimekutana na jaji mmoja mstaafu anakanyaga mguu..amebakia na suti tu ....maana huwa hawaachi kuvaa suti hata wachoke vipi!....watu kama hawa kuadhirika wanapostaafu ni aibu kwa taifa!..inatoa mfano mbaya kwa wanaobakia kwenye huduma!
 
Date::12/16/2008
Wastaafu Afrika Mashariki wafurahia Mgonja kufikishwa kortini

Na Fidelis Butahe
Mwananchi

WASTAAFU wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) wamepongeza hatua ya serikali kumfikisha Mahakamani aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi na Mipango, Gray Mgonja.

Mgonja alifikishwa Mahakamani juzi kwa tuhuma ya kutumia vibaya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh 11 bilioni.

Katibu Mkuu huyo mstaaafu wa hazina, anadaiwa kuwa Desemba 18 mwaka 2003 na Novemba 15 mwaka 2005 akiwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, alitoa taarifa za serikali (government notice) ambayo aliipa msamaha na unafuu wa kodi kampuni ya M/S Alex Stewart kinyume na ushauri uliotolewa na Mamlaka ya Mapato (TRA).

Akizungumza na Mwananchi mjumbe wa jumuiya hiyo, Ramadhani Makinga alisema wamefurahishwa na hatua hiyo kwa madai kuwa Mgonja alikuwa ni mmoja kati viongozi wa wizara hiyo waliokuwa wakikwamisha malipo ya wastaafu wa Jumuiya ya Afriak Mashariki (EAC).

“Tumefurahi sana Mgonja kuhusishwa na tuhuma hizo. Alipokuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi alikuwa ni moja ya watu waliosababisha wazee wasilipwe fedha zao. Tulipokuwa tukienda wizarani alikuwa hataki kabisa kusikiliza shida zetu kwa madai kuwa ana kazi nyingi. Sasa tuone hizo kazi atazifanyia wapi?” alisema Makingi na kuongeza kuwa

“Hata siku ile tulipokaa katikati ya barabara ya kuingilia Hazina, Mgonja hakuja kabisa kutusikiliza badala yake alikuja kutusikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Omary Yusuf Mzee, kwa hali hiyo sisi tumefurahishwa sana, dua tunazoomba kwa ajili ya wote wanaowatakia mabaya wastaafu wa EAC zimeanza kufanya kazi.”

Wastaafu hao wamemwomba katibu mkuu wa sasa wa wizara hiyo, Alhaj Ramadhani Kijja kuwa mstari wa mbele kusikiliza matatizo ya wastaafu wa Jumuiya hiyo na kuyafanyia kazi.

Alisema dua wanazoomba kila wanapokutana katika vikao vyao zimeanza kuzaa matunda na kwamba viongozi wote ambao wana nia ya kuzitafuna fedha za jumuiya ya Afrika Mashariki nao watafikisha mahakamani.

Naye Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Nathaniel Mlaki amewataka watu mbalimbali jijini Dar es Salaam, kujitokeza kwa wingi katika matembezi ya hiari yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwalipa mawakili wanaowatetea wazee hao katika kesi inayowakabili baadhi ya viongozi wao.

Alisema kuwa yatafanyika Desemba 23 yataanzia viwanja vya Kidongo Chekundu na kumalizikia Jangwani.
 
Aanze kuwahudumia wananchi huku akiendelea kuishi kwa pensheni inayolipwa kwa kodi ya walala puu..

- Lakini Mboma si mbia wa Kiwira, na amekua akisafiri kila kona ya dunia kwa ajili ya biashara ya Kiwira, kwa hiyo mkuu PM huyu hakuwa idle, maana mstaafu aliye idle hawezi kwenda New York, kutafuta wawekezaji wa mgodi wa Kiwira, mimi ninaamini kuwa ameamua kufuata nyayo za kujikinga mapema na kamata kamata, maana believe me inaelekea Kiiwra hii, watch!

- Behind kukamatwa kwa Yona na Mramba, kuna kitendawili kikubwa sana!
 
Kuendelea kuuhusisha mkoa wa Mbeya na ukabila ni kutoutendea haki, na mara zote madai haya huibuka wakati wa chaguzi za kisiasa na wananchi wanapolalamikia wizi unaofanywa kwenye halmashauri. Iwapo Thom angepita ni wazi tusingesikia kelele za ufisadi, kina bubelwa aliyewahi kuwa city tresurer wa jiji la Mbeya walipoiba na watu kukaa kimya hapakuwepo na kelele za ukabila.

Pale Kyela walipomkatalia Vicks Mahenge kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo kwa sababu ya kukosa elimu, zikaibuka kelele za ukabila na kusahau kuwa ni hao hao waliompa udiwani wa kata ya mjini!

Mbeya haina ukabila bali ni njaa za wanasiasa uchwara na wezi, sina haja ya kutoa mifano zaidi kwani Nsaji Mpoki amefanya hivyo.

Madai ya ukabila ni upomkubwa, wako mababila mvbali mbali mkoani humo ambao wanamiliki ardhi na uchumi mkubwa kuliko wenyeji na wala wenyeji hawalalalamiki.

Wenyeji wa Mbeya hawaendi kunywa kwenye baa kwa sababu ni mnyakyusa mwenzao, au mmalila au msafywa, au mnyamwanga au mdali kama ilivyo kwa baadhi ya makabila hapa ambapo wachaga hunywa baa za wachaga wenzao

Mzee umejieleza vizuri mpaka raha, halafu mwisho ni kama ukalikoroga vile kwa kuchomeka jungu.

Mimi nina rafiki zangu wachaga na wanakunywa pombe, na tukitoka sisikiagi tutafute baa ya mchaga. Labda kama ulitaka kusema "wachaga wote ninaowajua wanakunywa kwenye baa za wachaga wenzao". Na pengine ungeieka hivyo isinge-sound kama jungu tu. :)

Yaani hao unaowalaumu kwamba wanasema watu wambeya wakabila huwa wanatumia logic hiyo hiyo uliyoitumia wewe kusema wenzako ni wakabila. Kama unadhani hiyo logic ni sawa, basi kuwa mpole usikasirike wala usitee kwamba wambeya si wakabila. Kama unadhani hiyo logic siyo sawa, basi jitahidi kuifanya busara yako itawale munkari wako.

Au labda ni mkuki kwa nguruwe, ukikuchoma wewe jinai?
 
Wakuu Mlekwa & Ngongo
Nakubaliana na hoja zenu za umoja ni nguvu.Lakini katika umoja huo, tukubaliane kuwa wakati mwingine tupanue wigo wa uchaguzi wa sera badala ya personalities au itikadi za vyama.Najua watz wengi wapenda demokrasia mna hamu sana ya kuona opposition inaongeza idadi ya viti bungeni.Mimi kwa upande wangu napenda tuwafundishe na kuwazoesha wapiga kura kuchagua ubora wa sera na mgombea.Naunga mkono CHADEMA wagombee, ili sera zao zitambulike kwa wapiga kura wa Tanzania hiyo ndio nafasi pekee ya kujitangaza.Ninachotaka kushauri hapa si vizuri,incase mgombea wao hauziki waanze kumkandia mgombea wa chama kingine cha upinzani.
Tofauti ya uchaguzi wa Tarime vyama vingine vya upinzani vilikuwa vinaonyesha kukipiga vita vya wazi CHADEMA.Hali hiyo isirudiwe,chama kishiriki kueleza sera na mikakati yake ya kuboresha na kutetea walipa kodi wa Taifa letu.
Mkuu Gembe, si kweli kuwa sisi watu wa Mbeya tuna ukabila.Nitakupa mfano wa madiwani wawili wa kyela na nitaonyesha mabano ya kata wanazowakilisha.Kuna Visky Mahenge ambaye ni mkinga(Kyela) na Mh.Chrissy ambaye ni mkulya(Ipinda).Vilevile kule mbozi wenyeji wa wilaya ni Wanyiha na Wanyamwanga, lakini Mwenyekiti wa Council ni mnyakyusa.Huyu marehemu Nyaulawa,alikuwa mkinga ambao kule Mbeya vijijini ni wachache na walio wengi ni Wasafwa na Wamalila(kabila la Mboma).Huu mkoa wa Mbeya sasa hivi una wahamiaji wengi kutoka sehemu mbalimbali ya nchi yetu na nchi jirani na wanaishi vizuri na kushiriki kwenye chaguzi mbalimbali za uongozi.Nakumbuka hata uchaguzi mkuu wa 2005,NCCR-Mageuzi walimsimamisha Temigunga Kisonga(mhehe) na alivutia wapiga kura wengi licha ya kwamba matokeo yalitoka kinyume na ilivyotegemewa.Mimi kama mchunguzi kilichowaangusha wapinzani ni kukosa network ya mawakala wa dhati kama wale wa Tarime.Kipindi kile mchuano ulikuwa mkali kati ya Mwakagenda(CHADEMA) na Kisonga(NCCR-Mageuzi),lakini matokeo yakawa landslide victory kwa mgombea wa CCM akisaidiwa na nguvu ya EPA.
Ninachokijua mimi ni kwamba wananchi wa Mbeya wana permanent interest,wanataka miundo-mbinu kama vile International Airport,Tarmac road mbeya-chunya-itigi,Chuo Kikuu cha sayansi na Teknolojia n.k.Mbeya hawana chuki na mtu yeyote anayejali maslahi yao na wala hawawezi kulambishwa pipi ya kupewa vyeo kwa sababu vyeo hivyo vinakuwa kwa waliopewa sio mkoa wote.Hawapendi kuzugwa!

Nsaji,

Hata huyo mwenyekiti wa CCM wa mkoa, ingelikuwa sehemu zingine isingeliwezekana lakini kwa Mbeya kashinda bila matatizo.

Kuna watu wanashindwa kutofautisha kati ya kupenda kwenu na ukabila. Watu wa Mbeya walio wengi wanapenda kwao ingawaje hawajawafikia Wachaga.

Hata kwenye ubunge 2005 Kyela kuliingizwa swala la kwamba mbona huyu anatoka Rungwe nk. Lakini wananchi walijua wanamtaka nani na bado wakamchagua.

Ila Mbeya na sisi tunaongoza kwa siasa za makundi, kwanini tusiunganishe nguvu zetu kusukuma maendeleo? Ikifika mwaka 2010 kila mtu anaweza kufanya atakacho lakini kwasasa ni muhimu kuweka nguvu zote kwenye kusaidia maendeleo ya mkoa kwa faida za mkoa na nchi kwa ujumla.

Watu wanatumia ujinga na njaa za baadhi ya watu kupandikiza chuki. Ukionekana na mtu fulani tayari shida, kwanini tuchaguliwe maadui au marafiki?

Kuna watu mpaka wanadiriki kukwamisha miradi ya watu, kisa wanaogopa 2010. Tutaendeleza ujinga huo mpaka lini?

Aliyesema mtu hachagui jirani yake, hakukosea, inabidi viongozi wetu wawe tayari kufanya kazi na mtu yeyote.
 
Mkuu Mtanzania,
Tuko pamoja kwa hili,nilichokishuhudia katika maisha yangu kuhusu mikoa hii ya nyanda za juu kusini ni ubinafsi.Watu wa kanda hii wako tayari hata kuhujumu mwenzao asifanikiwe na kuharibu kabisa ukuzaji wa uchumi wa kanda hii.Mimi naombea serikali iwekeze kwenye miundombinu ya barabara,umeme wa uhakika na kiwanja cha ndege.Miundombinu ikiwepo na kwa kuwa wakaazi hawana ushirikiano,wawekezaji kutoka sehemu nyingine watakuja na kufaidika na rasilimali zilizopo huku na kupanua wigo wa kipato kwa wananchi.Kanda hii wanaogopa sana mwenyeji kufanikiwa kwa sababu viongozi wetu wanaogopa kupoteza maslahi yao ya kisiasa.
 
Kwa cheo alichokuwanacho Ubunge ni kujishusha,pia kuingia kwenye siasa kwa mwanajeshi kunampunguzia sifa zake za awali kama mlinzi wa nchi bila chama hasa kwa cheo chake cha ukuu wa majeshi.
 
bubu unaboa...hii thread ni ya mboma wewe hizo habari za mgonja ka wataka tuzisome si uzipe thread yake???
ndo maana kwenye taarabu waliwahi imba jitu zima ovyooo
usilazimishe watu wakuongelee wewe bana
 
MATOKEO JIMBO LA MBEYA,

Mboma kabwagwa na na Mchungaji wa Kanisa ka Uinjilisti maarufu kama Kanisa la Leiner hapa Mbeya.

Mchungaji Manjali ameibuka mshindi kwa kura 435, Alan Mwaigaga kura 259, Andrew Saile kura 229 na Mboma kura 164

yametangazwa nusu saa iliyopita

Kazi inaanza...tusubiri kina Sheikh Ponda soon....

Ni hatari lakini ni wazi kuwa baada ya muda mrefu wa siasa chafu na uozo wa kimaadili miongoni mwa wanasiasa wetu watanzania wanarudi katika uongozi wa kiimani. Tusubiri Karl Rove wetu aje na movement yake...

Tanzanianjema
 
- Mboma ameshindwa kwa sababu sio Mnyakyusa, hili somo liliibuliwa kwenye uchaguzi wa Tom na Mwandosya, kwamba hawa kina Mbomba na mstaafu wa idara ni wahamiaji sio wenyeji,

- Hii ni kutokana na matusi aliyokuwa akiporomosha kijana Tom against Mtumzima Mwandosya, wenyeji wa huko Mbeya yaani Wanyakyusa walianza kujiuliza maswali mengi sana, lakini makubwa yalikuwa mawili:- (1). Kama Tom na wanaomuunga mkono ni wenyeji?, (2). Tom kijana mdogo sana anaitoa wapi jeuri ya kumtukana mtuzima kama Mwandosya?

Jawabu likawa ni Wa-Zambia watu wa kuja huko Mbeya, na pili jeuri yake Tom anaitoa kwa muungwana na mtandao wake, nasikia ndio hasa kisa na mkasa wa yale mawe kwa muungwana, unafikiri mkulu anataka mawe tena huko? Ndio maana Mboma amekula chuya angeuliza kwanza kabla ya kukurupuka, maana Mkuu wa Majeshi kushindwa na Mchungaji, haiweki mwongozo kwa the future na ni matusi makubwa sana kwa walinzi wetu wa taifa!
 
Sishangai.

Hali ya uchumi ikiwa mbaya, wote tunamrudia Mungu pia tunashika mila zetu kwa nguvu zaidi.
Mchungaji kumshinda Mboma ni sawa kabisa ni ushahidi kwamba watu wamegeuzia uelekeo wao kwenye imani yao kuliko ujiko mwingine wowote.
 
Mkuu Mtanzania,
Tuko pamoja kwa hili,nilichokishuhudia katika maisha yangu kuhusu mikoa hii ya nyanda za juu kusini ni ubinafsi.Watu wa kanda hii wako tayari hata kuhujumu mwenzao asifanikiwe na kuharibu kabisa ukuzaji wa uchumi wa kanda hii.Mimi naombea serikali iwekeze kwenye miundombinu ya barabara,umeme wa uhakika na kiwanja cha ndege.Miundombinu ikiwepo na kwa kuwa wakaazi hawana ushirikiano,wawekezaji kutoka sehemu nyingine watakuja na kufaidika na rasilimali zilizopo huku na kupanua wigo wa kipato kwa wananchi.Kanda hii wanaogopa sana mwenyeji kufanikiwa kwa sababu viongozi wetu wanaogopa kupoteza maslahi yao ya kisiasa.
Very true
 
Back
Top Bottom