GEITA: Mkuu wa Mkoa amzuia Naibu Waziri kuzindua filamu ya 'Magwangala'

Kuna RAS mmoja rafiki yangu alinambia hawa maDC na maDED wengi mkoani kwake ni shida. Wana tuviburi flani hivi na amesikia wengine wakijitamba kwamba wote ni wateuliwa wa Mkulu hivyo "waheshimiane":). Kuna haja uteuzi wa hawa wengine urudishwe ofisi ya PM. Rais asiwe anateua tu kila mtu.
 
Serikali ya kiki hii kila MTU anataka kuonekana anafanya kazi hata kama hiyo kazi haina tija
 
Pole ndugu Pythagoras,

Sijawahi kuwa mwanachama Wa chama chochote Bali napenda kuongelea facts za vitu. Ninajua ninachoongea na ninajua kitaalamu hayo magwangala, kwa jinsi zoezi na matamko yalivyokuwa na mpaka sasa kimya maana nadhani walibaini ukweli wake na hivyo kuipotezea kimyakimya kama maswala mengine ya maana nchini yanavyoenda.

Sasa kwa kuibuka hiyo filamu nadhani itawaweka njia panda na kuibuka maswali yasiyo na majibu na maamuzi yao ya mwanzo yatakuwa ya hovyo na aibu kwa wakubwa.

Ni logic tu, kwa wanaoelewa haya maswala yanavyoenda, otherwise nawe utakuwa mkumbo mmoja.
 
Kuna RAS mmoja rafiki yangu alinambia hawa maDC na maDED wengi mkoani kwake ni shida. Wana tuviburi flani hivi na amesikia wengine wakijitamba kwamba wote ni wateuliwa wa Mkulu hivyo "waheshimiane":). Kuna haja uteuzi wa hawa wengine urudishwe ofisi ya PM. Rais asiwe anateua tu kila mtu.

Kama umegundua, basi utafahamu kuwa mkakati muhimu wa madikteta duniani ni kuhodhi madaraka ya maamuzi na uteuzi. Fikiria, serikali za mitaa kuwa chini ya rais moja kwa moja - a great contradiction.

Lengo ni kuhakikisha wateule wote wanategemea fadhila za kiongozi mkuu (rais) huku hawana uhakika wa nafasi zao wala mipaka ya madaraka yao bali salama yao ni kufuatilia na kutenda kwa kadiri hisia za rais zinavyotaka bila kujali matakwa ya sheria na mifumo/miundo rasmi iliyopo.

Hakuna cha hierarchy wala cha mashauriano hapo. Ukubwa wa madaraka na/au sauti ya mtendaji hutegemea "ukaribu wake kwa rais". Hivyo, haishangazi kuona mkuu wa mkoa "anatisha" kuliko hata VP au PM. Unaweza kuta ndani ya taasisi ya umma, maamuzi ya mwisho yanafanywa na naibu mtendaji mkuu (deputy CEO) huku CEO mwenyewe akiwepo na "akipiga wino na muhuri" bila kuhoji. Ndio mfumo wa nchi zinazoendeshwa kwa utashi wa mtu/kikundi.
 
Pole ndugu, sijawahi kuwa mwanachama Wa chama chochote Bali napenda kuongelea facts za vitu. Ninajua ninachoongea na ninajua kitaalamu hayo magwangala, kwa jinsi zoezi na matamko yalivyokuwa na mpaka sasa kimya maana nadhani walibaini ukweli wake na hivyo kuipotezea kimyakimya kama maswala mengine ya maana nchini yanavyoenda. Sasa kwa kuibuka hiyo filamu nadhani itawaweka njia panda na kuibuka maswali yasiyo na majibu na maamzi yao ya mwanzo yatakuwa ya hovyo na aibu kwa wakubwa. Ni logic tuu kwa wanaoelewa haya maswala yanavyoenda, otherwise nawe utakuwa mkumbo mmoja.
Mkuu uko sahihi kuhusu magwangala,ni uamuzi wa hovyo kuwahi kutokea!
 
Kama Mkuu wa Mkoa kashauri na Mkuu wa Wilaya Kapufi basi hilo litakuwa sahihi kuwa hiyo filamu imezuiwa.Kapufi ni mpenda pesa na mjanja mjanja sana. Anampelekesha Mkuu wa Mkoa bila yeye kujielewa.

GGM wamekuwa wakimtumia Mkuu wa wilaya kufunika mambo yao machafu hapa Geita.
Ikumbukwe kuwa huu mgodi mkubwa zaidi hapa Tanzania unatulipa sisi wafanyakazi mshahara mdogo sana.

Pia malalamiko ya Musukuma kuwa GGM hawajasambaza maji kwenye jamii inayozunguka mgodi kama walivyomuahidi Makamu wa Rais ni ya kweli.Lakini Mkuu wa Wilaya alijifanya kufuatilia wakati anafika Baadaye akawa kimya.

Kuna malalamiko mengi sana dhidi ya mgodi huu lakini Mkuu wa Wilaya kanyamaza kwa sababu anahongwa na GGM.
 
Mgodi wa ggm haumilimiwi na accacia, accacia inamiliki North mara

Sent using Jamii Forums mobile app
Habari tatanishi! Tuliambiwa ACACIA inamiliki migodi mitatu GGM, Bulyanhulu na North Mara sasa imebaki North Mara pekee basi kuna dalili hata zile kontena zikapungua kwa kasi ya supersonic kama wale wabunge wa kutenguliwa na kuteuliwa! (pia inawezekana hiyo "accacia" haimiliki mgodi wowote nchi hii!)
 
duu serikali ya kusadikika , eti leo katika serikali ya kusadikika rc ana mamlaka ya kumzuia waziri asifanye jambo ?
kupata vichekesho kama hivi tuma nano UKUKU kwenda 1556;);););):D:D:D:D
 
Hapo mkuu wa mkoa atakuwa na mipango fulani na ggm haiwezekani uzuie filamu tu hvhv na ggm hawataki kabisa kusikia neno magwangwala wakati mji wa geita unategemea sana magwangwala kama mojawapo ya kufanya mzunguko wa pesa kuwa mzuri
 
Back
Top Bottom