GEITA: Mkuu wa Mkoa amzuia Naibu Waziri kuzindua filamu ya 'Magwangala'

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,395
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amemzuia Naibu Waziri wa Habari, Anastazia Wambura kuzindua Filamu ya 'Magwangala' kwa madai ya filamu hiyo kuwa na maudhui yanayoutia doa Mgodi wa Geita Gold Mine(GGM).

Lakini cha kushangaza zaidi ni kuwa Mkuu wa Mkoa na Naibu Waziri Wote ni Presidential appointees(Wateule wa Rais) hii inazua maswali juu ya mawasiliano ya viongozi Serikalini.

Pia kwa siku na miezi ya hivi karibuni Wateule wa Rais hasa Wakuu wa Wilaya na Mikoa wamekuwa wakilalamikiwa kutumia maguvu hasa kwa wapinzani na sasa imeenda kwa wateule wenzao.

Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini, Constantine Kanyasu amesema kuwa serikali ya Mkoa imelalamikiwa na baadhi ya wadau wa madini na kusema waliolalamika hawajalalamika kwa maandishi na hakuna maeneo husika waliyoyalalamikia na pia ameongeza kuwa kwa mujibu wa Naibu Waziri ametoa maelekezo ikiwemo kugharamikia marekebisho yatakayoonekana ni ya lazima.

Meneja mahusiano wa GGM anayehusika na masuala ya jamii alisema sio lengo la GGM kuzuia filamu hiyo na wako bega kwa bega kuwasaidia wasanii kufikia malengo yao lakini kwa filamu ya Magwangala imeonekana kuna maeneo ambayo yanaeleza mgodi kuua, kunyanyasa watu jambo ambalo sio la kweli.

Filamu hiyo ambayo imechezwa na watu mbalimbali akiwemo mbunge wa jimbo la Geita Constantine Kanyasu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Geita, Leonard Bugomola na wasanii mbalimbali inaelezea maisha ya wachimbaji wadogo nchini wanavyotegemea magwangala.

Pamoja ya hayo, filamu hii ya Magwangala imesajiliwa na Bodi ya Filamu nchini na kupewa daraja 16.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom