Mbunge Rose Busiga akabidhi Tuzo ya Pongezi kwa Naibu Waziri Mkuu Dkt. Doto Biteko

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MBUNGE ROSE BUSIGA AKABIDHI TUZO YA PONGEZI KWA NAIBU WAZIRI MKUU, MHE. DKT. DOTTO BITEKO

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Geita, Mhe. Rose Vicent Busiga ametoa Tuzo ya Pongezi kwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Mashaka Biteko kwa niaba ya Wanawake wa Mkoa wa Geita na tuzo imekabidhiwa na Uongozi wa UWT Taifa kwa Naibu Waziri Mkuu kumpongeza kwa kuaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Vilevile, Mhe. Rose Vicent Busiga amekabidhi Tuzo ya Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martine Shigela kwa niaba ya Wanawake wa Mkoa wa Geita. Tuzo imekabidhiwa na Uongozi wa UWT Taifa kwa kutambua mchango wake kwa Wanawake wa Mkoa wa Geita kwa kuwa mtu muhimu katika kusikiliza na kutatua changamoto zao mara tu anapohitajika.

Aidha, kupitia Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Geita, Mhe. Rose Busiga, Wanawake wa Mkoa wa Geita wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya kwa Mkoa wa Geita na Tanzania kupitia Elimu, Maji, Afya, Umeme na Miundombinu ya barabara na kusema Wapo tayari kumpa miaka mingine Mitano ili aendelee kuwatumikia watanzania.

WhatsApp Image 2023-09-24 at 22.09.55.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-24 at 22.09.54(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-24 at 22.09.54.jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-09-24 at 22.09.51.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-24 at 22.09.51.jpeg
    44.9 KB · Views: 1
Back
Top Bottom